Mafundisho ya Kristo
Mafundisho ya Kristo yanaturuhusu kupata uwezo wa kiroho ambao utatuinua kutoka kwa hali yetu ya sasa ya kiroho mpaka kwa hali ambapo tunaweza kuwa wakamilifu.
Ziara ya Yesu kwa Wanefi baada ya ufufuo Wake ilipangwa kwa makini ili kutufundisha mambo ya umuhimu mkubwa. Ilianza na Baba akiwashuhudia watu kwamba Yesu alikuwa ndiye “Mwanawe Mpendwa, [Yeye] anapendezwa Naye.”1 Kisha Yesu Mwenyewe akashuka na kushuhudia juu ya dhabihu Yake ya upatanisho,2 akiwaalika watu “kujua hakika ya” kwamba Yeye ndiye Kristo kwa kuja na kuhisi alama za jeraha kwenye upande Wake na alama za misumari katika mikono yake na miguu.3 Shuhuda hizi zinathibitisha bila shaka kwamba Upatanisho wa Yesu ulikuwa kamili na kwamba Baba alitimiza ahadi Yake ya kumtoa Mwokozi. Kisha Yesu akawafundisha Wanefi jinsi ya kupata baraka zote za mpango wa furaha wa Baba, ambazo tumeandaliwa kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, kwa kuwafundisha mafundisho ya Kristo.4
Ujumbe wangu leo unalenga juu ya mafundisho ya Kristo. Maandiko yanafafanua mafundisho ya Yesu Kristo kama kufanya imani katika Kristo na Upatanisho Wake, kutubu, kubatizwa, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho5
Mafundisho ya Kristo Yanaturuhusu Kupata Baraka za Upatanisho wa Kristo.
Upatanisho wa Kristo unajenga mazingira ambayo kwayo tunaweza kutegemea “uhalali, na rehema, na neema ya Masiya Mtakatifu,”6 “kukamilika katika [Kristo],”7 kupata kila kitu kizuri,8 na kupokea uzima wa milele.9
Mafundisho ya Kristo kwa upande mwingine ni njia—ile njia pekee—ambayo kwayo sisi tunaweza kupata baraka zote tulizowekewa kupitia kwa Upatanisho wa Yesu. Ni mafundisho ya Kristo ambayo yanaturuhusu kupata uwezo wa kiroho ambao utatuinua kutoka kwa hali yetu ya sasa ya kiroho mpaka kwa hali ambapo tunaweza kuwa wakamilifu kama Mwokozi.10 Kuhusu mchakato huu wa kuzaliwa upya, Mzee D. Todd Christofferson amefundisha: “Kuzaliwa mara ya pili, tofauti na kuzaliwa kwetu kimwili, ni zaidi mchakato kuliko ilivyo tukio. Na kujihusisha katika mchakato huo ndio lengo kuu la maisha.”11
Hebu tuchunguze kila kipengele cha mafundisho ya Kristo.
Kwanza, imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake. Manabii wamefundisha kwamba imani huanza kwa kusikia neno la Kristo.12 Maneno ya Kristo yanashuhudia dhabihu Yake ya upatanisho na kutuambia jinsi tunaweza kupata msamaha, baraka na kuinuliwa.13
Baada ya kusikia maneno ya Kristo, tunafanya imani kwa kuchagua kufuata mafundisho na mfano wa Mwokozi.14 Ili kufanya hivyo, Nefi alifundisha kwamba ni sharti “tutegemee kabisa ustahili wa yule [Kristo,] aliye mkuu kuokoa.”15 Kwa kuwa Yesu alikuwa Mungu katika maisha kabla ya maisha ya duniani,16 aliishi maisha yasiyo na dhambi,17 na wakati wa Upatanisho Wake aliridhisha mahitaji yote ya haki kwa ajili yako na mimi,18 Ana uwezo na ufunguo wa kuleta ufufuo wa watu wote,19 na aliwezesha rehema kuipita haki juu ya masharti ya toba.20 Mara tunapoelewa kwamba tunaweza kupata huruma kutokana na wema wa Kristo, tunakuwa na uwezo wa “kuwa na imani hata toba.”21 Kutegemea kabisa wema wa Kristo basi ni kuamini kwamba alifanya kile cha muhimu ili atuokoe na kisha kutenda kwa imani yetu.22
Imani pia inatufanya kuacha hofu kabisa kuhusu kile wengine wanadhani kutuhusu na kuanza kujali zaidi juu ya kile Mungu anafikiria kwetu.
Pili, Toba Samweli Mlamani alifundisha, “Ikiwa mtaamini katika jina la [Kristo] mtatubu dhambi zenu zote.”23 Toba ni zawadi yenye thamani kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni ambayo imewezeshwa kupitia kwa dhabihu ya Mwanawe Mzaliwa wa Pekee. Ndio njia ambayo Baba ametupa ambayo kwayo tunabadilika, au kugeuza, mawazo yetu, matendo, na uhai wetu ili tuweze kuwa zaidi na zaidi kama Mwokozi alivyo.24 Si tu kwa ajili ya dhambi kubwa lakini ni njia ya kila siku ya utathmini wa binafsi na uboreshaji25 ambayo hutusaidia kushinda dhambi zetu, hali yetu ya kutokamilika, udhaifu wetu, na mapungufu yetu.26 Toba inatufanya kuwa “wafuasi wa kweli” wa Kristo, ambayo hutujaza kwa upendo27 na kuondoa woga wetu.28 Toba sio mpango mbadala kwa mpango wetu wa kuishi kikamilifu ukishindikana.29 Toba ya kila wakati ni njia pekee ambayo inaweza kutuletea shangwe ya kudumu na kutuwezesha kurudi kuishi na Baba yetu wa Mbinguni.
Kupitia kwa toba tunakuwa watiifu kwa mapenzi ya Mungu. Sasa hili halitafanyika peke yake. Kutambua wema wa Mungu na utupu wetu,30 ikiwemo ni pamoja na jitihada zetu bora ili kuwianisha tabia zetu na mapenzi ya Mungu,31 huleta neema katika maisha yetu.32 Neema “ni njia takatifu ya Mungu ya msaada au nguvu, iliotolewa kwa njia ya huruma karimu na upendo wa Yesu Kristo … Ili kufanya matendo mema ambayo [sisi] kwa vinginevyo hatuwezi kudumisha tukiachwa pekee yetu.”33 Kwa sababu toba hakika ni kuhusu kuwa kama Mwokozi, ambayo ni vigumu kwetu wenyewe, hakika tunahitaji neema ya Mwokozi ili kufanya mabadiliko yanayohitajika katika maisha yetu.
Tunapotubu, tunageuza tabia zetu za kitambo, zisizokuwa takatifu, udhaifu, mapungufu, na hofu kwa tabia geni na imani zinazotuleta karibu na Mwokozi na kutusaidia kuwa kama Yeye alivyo.
Tatu, ubatizo na sakramenti. Nabii Mormoni alifundisha kwamba “matunda ya kwanza ya toba ni ubatizo.”3 Ili kuwa kamili, toba sharti iunganishwe pamoja na agizo la ubatizo lililofanywa na mtu anayeshikilia mamlaka ya ukuhani wa Mungu. Kwa waumini wa Kanisa, maagano yailiyofanywa wakati wa ubatizo na matukio mengine yanawekwa upya tunapopokea sakramenti.35
Katika maagizo ya ubatizo na sakramenti, tunaweka ahadi ili kushika amri za Baba na Mwana, daima kumkumbuka Kristo, na kuwa tayari kuchukua jina la Kristo (au kazi Yake na sifa36) juu yetu.37 Mwokozi, badala yake, anaahidi kusamehe, au kuondoa, dhambi zetu38 na “kumimina Roho Yake kwa wingi juu yetu.”39 Kristo pia anaahidi kutuandaa kwa ajili ya uzima wa milele kwa kutusaidia kuwa kama Yeye.40
Douglas D. Holmes, Mshauri wa Kwanza katika Urais Mkuu wa Vijana, ameandika: “Maagizo ya ubatizo na sakramenti yanaashiria matokeo yote ya mwisho na njia ya kuzaliwa mara ya pili. Katika ubatizo, tunazika mtu wa kale wa mwili na kuinuka katika maisha mapya.41 Katika sakramenti, tunajifunza kuwa mabadiliko haya ni mchakato wa hatua kwa hatua, [ambapo] kidogo kidogo, wiki kwa wiki, tunabadilishwa tunapotubu, kuweka maagano, na kupitia kwa endaumenti zaidi za Roho [kuwa kama Mwokozi].”42
Maagizo na maagano ni muhimu ndani ya mafundisho ya Kristo. Ni kwa kupokea maagizo ya ukuhani na kuweka maagano husika ambapo nguvu ya utauwa inadhihirishwa katika maisha yetu.43 Mzee D. Todd Christofferson alieleza kuwa hii ‘nguvu ya utauwa’ huja ndani ya mtu na kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu.”44
Nne, kipawa cha Roho Mtakatifu. Baada ya ubatizo tunapewa kipawa cha Roho Mtakatifu kupitia kwa agizo la uthibitisho.45 Kipawa hiki, tukikipokea, kinaturuhusu kupata uenzi wa kila mara wa Mungu46 na upatikanaji daima wa neema ambayo kiasili huja kupitia kwa ushawishi Wake.
Kama mwenza wetu, kila mara, Roho Mtakatifu anatupa uwezo wa ziada au nguvu za kuweka maagano yetu.47 Pia anatusafisha,48 ambayo inamaanaisha kutufanya “huru kutokana na dhambi, safi, na takatifu kwa njia ya upatanisho wa Yesu Kristo.”49 Mchakato wa utakaso hautusafishi tu, lakini pia unatubariki na vipawa vinavyohitajika vya kiroho au sifa takatifu za Mwokozi50 na kubadilisha hali yetu asili,51 kiasi “kwamba hatuna hamu tena ya kutenda mabaya.”52 Kila wakati tunapopokea Roho Mtakatifu katika maisha yetu kwa njia ya imani, toba, maagizo, huduma ya Kristo, na juhudi zingine njema, tunabadilishwa hadi hatua kwa hatua, kidogo kidogo tunakuwa kama Kristo.53
Tano, kuvumilia hadi mwisho. Nabii Nefi alifundisha kwamba baada ya kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu ni lazima kuvumilia hadi mwisho,“kwa kufuata mfano wa Mwana wa Mungu aliye hai.”54 Mzee Dale G. Renlund ameelezea mchakato wa kudumu mpaka mwisho kama ifuatavyo “Tunaweza kukamilishwa kwa kuonyesha … imani kwa Kristo kwa kurudia na mara kwa mara kutubu, kushiriki sakramenti kuweka upya maagano na baraka za ubatizo, na kupokea Roho Mtakatifu kama rafiki wa kila mara kwa kiwango kikubwa. Tunapofanya hivyo, tunakuwa zaidi kama Kristo alivyo na tunakuwa na uwezo wa kuvumilia hadi mwisho, kwa kila kitu husika.”55
Kwa maneno mengine, upokeaji wa Roho Mtakatifu na mabadiliko ambayo mapokezi hayo huleta ndani yetu na zaidi hujenga imani yetu. Imani zaidi inaelekeza kwa toba zaidi. Kwa mfano tukijitolea mioyo yetu na dhambi zetu juu ya madhabahu ya sakramenti, tunapokea Roho Mtakatifu kwa kiwango kikubwa. Kupokea Roho Mtakatifu kwa kiwango kikubwa zaidi hutusongeza katika njia ya kuzaliwa mara ya pili. Tunapoendelea katika mchakato huu na kupokea maagizo na maagano yote ya injili, tunapokea “neema juu ya neema” mpaka tupokee ukamilifu.56
Ni Lazima Tutumie Mafundisho ya Kristo katika Maisha Yetu
Kina ndugu na dada, tunapotumia mafundisho ya Kristo katika maisha yetu, tunabarikiwa kiroho na kimwili, hata katika majaribu. Hatimaye tuna uwezo wa “kushikilia kila kitu kizuri.”57 Nashuhudia kwamba mchakato huu umetokea na huendelea kutokea katika maisha yangu mwenyewe, hatua kwa hatua, kidogo kidogo.
Lakini cha muhimu zaidi, ni lazima tutumie mafundisho ya Kristo katika maisha yetu kwa sababu yanatupa njia pekee ya kurudi kwa Baba wetu wa Mbinguni. Ni njia pekee ya kumpokea Mwokozi na kuwa wana na mabinti Zake.58 Hakika, njia pekee ya kukombolewa kutoka katika dhambi na kuendelea kiroho ni kutumia mafundisho ya Kristo katika maisha yetu.59 Vinginevyo, Mtume Yohana alifundisha kwamba “yeye … adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.”60 Na Yesu mwenyewe aliwaambia Wanefi Kumi na Wawili kwamba tukishindwa kufanya imani katika Kristo, kutubu, kubatizwa, na kuvumilia hadi mwisho, “tutaangushwa chini na kutupwa kwenye moto, mahali ambapo [sisi] hatuwezi kurudi nyuma.”61
Basi ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia mafundisho ya Kristo kikamilifu zaidi katika maisha yetu? Njia mojawapo ni kufanya juhudi bora kila wiki ili kujiandaa kwa ajili ya sakramenti kwa kuchukua muda kiasi ili kufikiria kwa maombi mahali ambapo tunahitaji kuboresha zaidi. Kisha tunaweza kuleta dhabihu ya angalau jambo moja ambalo linatuzuia kuwa kama Yesu Kristo mbele ya madhabahu ya sakramenti, tukiomba msaada kwa imani, tukiomba vipawa muhimu vya kiroho, na kuahidi kuboreka wakati wa wiki ijayo.62 Tunapofanya hivyo, Roho Mtakatifu ataingia katika maisha yetu kwa kiwango kikubwa, na tutakuwa na nguvu zaidi za kushinda mapungufu yetu.
Nashuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu na kwamba jina Lake ndilo jina pekee ambalo tunaweza kuokolewa.63 Mambo yote ambayo ni mazuri yanawezeshwa tu kwa njia Yake.64 Lakini kwa kweli “kushikilia kila kitu kizuri,”65 ikiwemo uzima wa milele, ni lazima tuendelee kutumia mafundisho ya Kristo katika maisha Yetu. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.