“Kama Mgenijua”
Je, tunajua tu kuhusu Mwokozi, au tunazidi kumjua? Je, tunaweza kumjua Bwana vipi?
Mwokozi alipokuwa akihitimisha Mahubiri ya Mlimani, Alisisitiza ukweli wa milele kwamba “ni kwa kufanya mapenzi ya Baba peke yake ndipo inapatikana neema Mwana wa Mungu ya wokovu.”1
Alitangaza:
“Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana atakayeingia kwenye ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi watasema kwangu siku ile: Bwana, Bwana, si tulifanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako si tumetoa pepo chafu, na katika jina lako kufanya miujiza mingi?
“Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.”2
Uelewa wetu kwenye mfululizo wa matukio unakuzwa tunapotafakari juu ya uhariri wenye maongozi wa maandishi. Cha muhimu, kishazi cha Bwana kilichotolewa kwenye toleo la Biblia la King James, “Sikuwajua ninyi kamwe,” ilibadilishwa na tafsiri ya Joseph Smith kuwa “hamkunijua.”3
Fikiria pia fumbo la wanawali kumi. Kumbuka wale wanawali watano wapumbavu na ambao hawakujiandaa walienda kuchukua mafuta kwa ajili ya taa yao baada ya kusikia vigelegele vya kwenda na kukutana na bwana harusi.
“Na hao walikuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa.
“Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie.
“Akajibu akasema, Amin nawaambia, siwajui ninyi.”4
Matokeo ya fumbo hili kwa kila mmoja wetu yamefafanuliwa na rejeo lingine la kuinua. Cha Muhimu zaidi, neno “Siwajui ninyi” kama lilivyoandikwa katika toleo la Biblia la King James lilitafsiriwa katika tafsiri ya Joseph Smith kuwa “hamnijui.”5
Maneno “hamkunijua” na “hamnijui” sharti iwe ni sababu ya kujichunguza kwa kina kiroho kwa kila mmoja wetu. Je ,tunajua tu kuhusu Mwokozi, au tunazidi kumjua? Je, tunaweza kumjua Bwana vipi? Maswali haya ya moyo ni kiini cha ujumbe wangu. Kwa umakini naalika usaidizi wa Roho Mtakatifu tunapofikiria pamoja somo hili muhimu.
Kuja Kujua
Yesu alisema:
“Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima: mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi .
“Kama umenijua mimi, umengemjua Baba yangu pia.”6
Tunamjua Baba kama tunavyomjua Mwanawe Mpendwa.
Lengo kubwa la maisha si tu kujifunza kuhusu Mzaliwa Pekee wa Baba lakini pia kujitahidi kumjua Yeye. Njia kuu nne za muhimu ambazo zinaweza kutusaidia kumjua Bwana ni kuifanyia kazi imani yetu kwake, kumfuata, kumtumikia, na kumwamini.
Kuifanyia Kazi Imani Kwake
Kufanyia kazi imani katika Yesu Kristo inategemea sana kwenye faida, rehema, na neema Zake.7 Tunaanza kwa kumjua Mwokozi ikiwa tutaamsha na kuziwasha akili zetu hata kwenye kujaribu maneno yake, hata kwa njia ambayo tutatoa nafasi katika nafsi zetu kwa sehemu ya maneno Yake.8 Imani yetu katika Bwana inapoongezeka, tunamwamini na kuwa na ujasiri katika nguvu Zake katika kukomboa, kuponya, na kutuimarisha.
Imani ya kweli inalenga ndani na katika Bwana na kila mara hutuongoza kwenye matendo ya haki. “Imani katika Kristo ni Kanuni ya kwanza katika dini iliyofunuliwa … na kanuni ya matendo katika viumbe wote wenye akili.”9 Kwa sababu kutenda kulingana na kanuni sahihi Mkombozi alitangaza kwamba ni kiini cha kupokea na kujaribu imani ya kweli, “imani bila matendo imekufa.”10 Tunatakiwa kuwa “watendaji wa neno, na siyo wasikiaji tu.”11
Kusikia neno la Mungu na kupokea karama za kiroho katika Mwokozi vinashabihiana, kwani “imani huja kwa kusikia, na kusikia kwa neno la Mungu.”12 Tunajifahamishana na Yeye na sauti Yake tunaposoma na kusherehekea neno lake katika maandiko,13 tunaomba kwa Baba katika jina Lake kwa nia ya kweli14 na kutafuta kuwa na uenzi wa Roho Mtakatifu daima.15 Kujifunza na kuyatumia katika maisha yetu mafundisho ya Kristo ni hitaji la msingi katika kupokea karama ya imani katika Yeye.16
Kuifanyia kazi imani katika Bwana ni maandalizi muhimu kwa ajili ya kumfuata Yeye.
Kumfuata Yeye
“Na Yesu, alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini kwa maana walikuwa wavuvi.
“Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.|
“Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.”17
Petro na Andrea walikuwa mifano mizuri ya kusikiliza na kumfuata Bwana.
Mwokozi vivyo hivyo anatuagiza mimi na wewe: “Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalama wake, anifuate.”18 Kujitwika msalaba wake ni kujikana kwa vitu visivyo vya uungu na kila tamanio la kidunia na kutii amri za Bwana.19
Mwokozi ametuasa tuwe kama Yeye alivyo.20 Basi, kumfuata Bwana inajumuisha na kumuiga Yeye. Tunaendelea kumjua Bwana tunapomtafuta kupitia kwa nguvu ya Upatanisho Wake kuwa kama alivyo Yeye.
Katika huduma Yake hapa duniani, Yesu aliwekea alama njia, akaongoza njia, ana akaweka mfano mkamilifu. “Wazo sahihi la hulka, ukamilifu, na sifa Zake”21 hutupa madhumuni endelevu na mwelekeo dhahiri tunapomfuata katika njia ya ufuasi wa kujitolea.
Kumfuata Mwokozi pia kunatuwezesha kupokea “uelewa halisi kwamba mwenendo wa maisha ambao tunafuatana”22 nao ni kulingana na mapenzi ya Mungu. Uelewa huu siyo muujiza uliofichika na unalenga kimsingi katika utafutaji wetu wa muda au shughuli za kawaida za dunia. Badala yake, maendeleo thabiti na endelevu katika njia ya maagano ni sehemu ya maisha ambayo inampendeza Yeye.
Ndoto ya Lehi katika Kitabu cha Mormoni inatambua njia tunayotakiwa kuifuata, changamoto tutakazokumbana nazo, na mahitaji ya kiroho yaliyopo kutusaidia katika kumfuata na kuwa kama Mwokozi. Kwenda mbele kwenye njia nyoofu na nyembamba ndio kitu ambacho Yeye angetutaka tufanye. Kuonja tunda la mti na kuwa “waongofu katika Bwana”23 ni baraka Yeye anatamani tupokee. Hivyo, Yeye anatuita, “Njooni, mnifuate.”24
Pamoja kuifanyia kazi imani na kumfuata Yesu Kristo ni maandalizi muhimu kwa ajili ya kumtumikia Yeye.
Kumtumikia Yeye
“Kwani ni vipi mtu atamjua yule bwana ambaye hajamtumikia , na aliye mgeni kwake, na yuko mbali katika mawazo na nia za moyo wake?25
Tunamjua Mungu zaidi tunapomtumikia na kufanya kazi katika ufalme Wake. Tunapofanya hivyo, anatubariki zaidi kwa msaada wa mbinguni, karama za kiroho, na ongezeko la uwezo. Hatuachwi peke yetu kamwe tunapofanya kazi katika shamba Lake la mzabibu.
Yeye alitangaza: “Kwani nitawatangulieni. Nitakuwa mkono wenu wa kuume na wa kushoto, na Roho wangu atakuwa mioyoni mwenu, na malaika zangu watawazingira, ili kuwabeba juu.”26
Tunamjua Mwokozi tunapojitahidi kwenda pale anapotutaka twende, tunavyojitahidi kusema kile Yeye anataka tuseme, na tunavyokuwa kile anachokitaka tuwe.27 Tunapojinyenyekeza na kuonyesha utegemezi wetu Kwake, anatuongezea uwezo wetu wa kumtumikia kwa umakini zaidi. Taratibu, matamanio yetu yanalingana kikamilifu na matakwa Yake, na madhumuni Yake yanakuwa madhumuni yetu, kiasi kwamba hatuwezi kuomba kile kilicho kinyume na mapenzi Yake.”28
Kumtumikia kunahitaji moyo wetu wote, uwezo, akili, na nguvu.29 Kutokana na haya, kuwatumikia wengine bila uchoyo kunakinzana na uchoyo na tabia za ubinafsi za mwanadamu wa kawaida. Tunaelekea kuwapenda wale tuaowatumikia. Na kwa sababu kuwatumikia wengine ni kumtumikia Mungu, tunampenda Yeye na kaka na dada zetu kwa undani zaidi Upendo kama huu ni dhihirisho la karama za kiroho za upendo, hata upendo msafi wa Kristo.30
“Ombeni kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, kwamba mjazwe na upendo huu, ambao ametoa kwa wote ambao ni wafuasi wa kweli wa Mwanawe, Yesu Kristo; ili muwe wana wa Mungu; kwamba wakati atakapoonekana tutakuwa kama Yeye. Kwani tutamwona vile alivyo; ili tuwe na tumaini hili; ili tutakaswe hata vile alivyo mtakatifu.”31
Tunamjua Bwana tunapojazwa na upendo Wake.
Kumwamini Yeye
Je, inawezekana kuifanyia kazi imani katika Yeye, kumfuata, kumtumikia, na usimwamini?
Nimekuwa karibu na waumini wa Kanisa wanaokubali kama mafundisho na kanuni ni kweli zilizopo kwenye maandiko na zinazohubiriwa kwenye mimbari. Na bado wana wakati mgumu kuamini kweli za injili zinazofanya kazi mahususi katika maisha yao na katika hali zao. Wanaonekana kuwa na imani katika Mwokozi, lakini hawaamini ahadi za baraka Zake zipo kwa ajili yao au zinaweza kufanya kazi katika maisha yao. Vilevile nimekutana na kina kaka na dada ambao wanahudumu vyema lakini injili ya urejesho haijakuwa uhalisia wa maisha na mabadiliko katika maisha yao. Tunakuja kumjua Bwana si kwa kuamini tu lakini pia kwa kumwamini Yeye na uhakika Wake.
Katika Agano Jipya, baba mmoja alimwomba Mwokozi kumponya mtoto wake. Yesu akajibu:
“Ukiweza, yote yawezekana kwake aaminiye.”
“Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema akilia, Bwana, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.”32
Nimefikiria mara nyingi kwenye ombi la huyu baba: “Nisaidie kutoamini kwangu.” Nina shaka kama haja ya ombi la huyu mwanaume kimsingi ilikuwa kumsaidia kuamini katika Yesu kama Mkombozi na katika nguvu Zake za uponyaji. Inawazekana tayari amemkiri Kristo kama Mwana wa Mungu. Lakini labda alihitaji msaada kuamini katika nguvu ya uponyaji ya Bwana kwamba ingekuwa ya kulenga mtu mmoja mmoja na ya kipekee kwamba ingembariki mwanawe mpendwa pekee. Angeweza kuwa ameanimi katika Kristo kwa ujumla lakini sio kuamini Kristo mahususi na kibinafsi.
Mara nyingi tunashuhudia kwa kile tunachojua kuwa ni cha kweli, lakini labda swala la msingi kabisa kwa kila mmoja wetu ni kama tunaamini kile tunachokijua.
Ibada takatifu zinazofanywa na wenye mamlaka sahihi ya ukuhani ni muhimu katika kuamini Mwokozi, kumjua, na mwishowe, kuamini kile tunachokijua.
“Na ukuhani [Melkizedeki] huhudumia injili na hushikilia ufunguo wa siri za ufalme, hata ufunguo wa ufahamu wa Mungu.
“Kwa hiyo, katika ibada hizo, nguvu ya uchamungu hujidhihirisha.”33
Tunaamini na tunakuja kujua kwamba Bwana kama ufunguo wa ufahamu wa Mungu ambao hutolewa kupitia ukuhani wa Melkizedeki unafungua milango na kutufanya kila mmoja wetu kupokea nguvu ya uungu katika maisha yetu. Tunaamini na kuja kumjua Mwokozi tunapomfuata kwa kupokea na kwa heshima kutukuza ibada takatifu na kuongozeka kuwa na mfano Wake katika taswira nyuso zetu.34 Tuanaamini na kuja kumjua Kristo tunapopata mabadiliko binafsi, uponyaji, nguvu, na nguvu ya utakaso ya Upatanisho Wake. Tuanaamini na kumjua Bwana kama “nguvu ya neno lake linakita mizizi ndani yetu,”35 limeandikwa katika akili zetu na mioyo yetu,36 na sisi “tunapotoa dhambi zetu zote ili kumjua [Yeye].”37
Kumwamini yeye na kuamini kuwa baraka Zake nyingi zipo na zinafanya kazi katika maisha yetu binafsi na katika familia zetu. Kumwamini Yeye kwa mioyo yetu yote38 hutokea pale tunaposonga mbele kwenye njia ya agano, tukisalimisha matakwa yetu Kwake, na tukiweka vipaumbele Vyake na muda Wake kwetu. Kumwamini Yeye—kukubali kama kweli nguvu Yake na ahadi Zake—hualika mtazamo na amani katika maisha yetu.
Ahadi na Ushuhuda
Katika siku ya uzoni, “kila goti litapigwa na kila ulimi utakukiri”39 kuwa Yesu ndiye Kristo. Katika siku hiyo iliyobarikiwa, tutajua kwamba anamjua kila mmoja wetu kwa jina. Na ninaahidi hatuwezi kujua kuhusu Bwana tu bali pia tunaweza kuja kumjua Yeye tunapoifanyia kazi imani, kumfuata, kumtumikia, na kumwamini Yeye. Ninashuhudia katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina