2010–2019
Hudumu
Oktoba 2016


10:58

Hudumu

Kila muumini anahitajika, na kila muumini anahitaji nafasi ya kuhudumu.

Nikiwa kijana nilifurahia kufanyakazi na mjomba wangu Lyman na shangazi yangu Dorothy kwenye shamba lao. Mjomba Lyman mara nyingi aliongoza miradi yetu, na Shangazi Dorothy mara nyingi alisaidia na aliendesha gari ya zamani aina ya Dodge. Ninakumbuka hali ya wasiwasi wakati tulipokwama kwenye tope au kujaribu kupanda mlima mkali. Mjomba Lyman alipiga kelele, “Weka gia kubwa, Dorothy!” Hapo ndipo nilipoanza kuomba. Kwa namna fulani, kwa msaada wa Bwana na baada ya kusagika kwa gia, Shangazi Dorothy aliingiza gia kubwa. Magurudumu yote yakiwa yanafanya kazi, gari likatoka na kazi yetu ikaendelea.

“Kuweka gia kubwa” inamaanisha kubadilisha kwenye gia maalum ambapo idadi ya gia zimepangwa kufanyakazi pamoja ili kutoa nguvu zaidi.1 Gia kubwa, pamoja na mwendo magurudumu mane, inakusaidia kuweka gia chini, kutoa nguvu zaidi, na kwenda.

Gia kubwa

Ninataka kufikiri kila mmoja wetu kuwa sehemu ya gia kubwa pale tunapohudumu pamoja Kanisani—katika kata na matawi, katika akidi na vikundi usaidizi. Kama vile gia zinavyoungana ili kuleta nguvu, tuna nguvu kubwa tunapoungana pamoja. Tunapoungana ili kutumikiana, tunafanikisha mambo mengi pamoja kuliko kufanya peke yetu. Inasisimua kujihusisha na kuungana tunapohudumu na kusaidia katika kazi ya Bwana.

Kuhudumu ni Baraka

Nafasi ya kuhudumu ni moja ya baraka kubwa ya uumini katika Kanisa.2 Na Bwana alisema, “Kama wanipenda utanitumikia“3 na tunamtumikia Yeye kwa kuwatumikia wengine.4

Tunapohudumiana, tunakuwa karibu na Mungu.5 Tunakuja kumjua Yeye katika njia ambazo wakati mwingine hatuwezi. Imani yetu Kwake inaongezeka. Matatizo yetu yanawekwa kwenye taswira. Maisha yanakuwa ya kuridhisha. Upendo wetu kwa wengine unaongezeka, na pia matamanio ya kuhudumu. Kupitia kwa mchakato huu wa baraka, tunakuwa kama Mungu alivyo, na tunakuwa tumejiandaa vizuri kurudi Kwake.6

Kama vile Rais Marion G. Romney alivyofundisha: “Huduma siyo kitu kinachoendelea katika dunia hii hivyo tunapata haki ya kuishi katika ufalme wa selestia. Huduma ni uzi ambao maisha yaliyotukuka ambao kwao ufalme wa selestia umetengenezwa.”7

Kuhudumu Kunaweza Kuwa Changamoto

Kuhudumu katika Kanisa, hata hivyo, kunaweza kuwa changamoto kama tukiulizwa kufanya kitu ambacho kinatutisha, kama tunachoka kuhudumu, au kama tunaitwa kufanya kitu ambacho hakituvutii.

Hivi karibuni nilipata jukumu jipya. Nilikuwa ninaahudumu katika Eneo la Afrika Kusini Mashariki. Ilikuwa ni msisimko kuhudumu katika sehemu ambayo Kanisa ni changa na likiwa limeanzishwa, na tuliwapenda Watakatifu. Kisha nikaitwa nirudi makao makuu ya Kanisa, na niwe mkweli, sikuwa hamu sana. Mabadiliko ya majukumu yalileta yasiyojulikana.

Usiku mmoja nikitafakari mabadiliko yanayokuja, niliota kuhusu babu yangu Joseph Skeen. Nilijua kutoka katika shajara yake kwamba wakati yeye na mke wake, Maria, walipohamia Nauvoo, alitamani kuhudumu, hivyo alimtafuta Nabii Joseph Smith na kuuliza jinsi ya kusaidia. Nabii alimtuma akafanye kazi kwenye shamba na akamwambia akafanye kwa juhudi zake zote, hivyo akafanya. Alifanya kazi katika shamba la Smith.8

Nilitafakari nafasi ambayo Joseph Skeen alikuwa nayo katika kupokea wito wake kwa njia ile. Mara nikagundua kwamba nina nafasi kama hiyo, ambayo wote tunafanya. Miito yote ya Kanisa inatoka kwa Mungu—kupitia watumishi Wake waliochaguliwa.9

Nilihisi uthibitisho halisi wa kiroho uliohakikisha kwamba na wito wangu mpya ulikuwa wa maongozi. Ni muhimu kwamba tuweke muunganiko huo—kwamba miito yetu huja kwetu kutoka kwa Mungu kupitia viongozi wetu wa ukuhani. Baada ya uzoefu huu, mtazamo wangu ulibadilika, na nilijawa na hamu ya kina ya kuhudumu. Nina shukrani kwa ajili ya baraka ya toba na kwa moyo wangu uliobadilika. Ninapenda majukumu yangu mapya.

Hata kama tunafikiri kwamba wito wetu wa Kanisa yalikuwa ni mawazo ya viongozi wa ukuhani, kwamba ilikuwa sehemu ya mkondo wa mzunguko, au kwamba ulikuja kwetu kwa sababu hakuna mtu aliyekubali, tutabarikiwa tutakapohudumu. Bali kama tunagundua mkono wa Mungu katika wito wetu na kuhudumu kwa moyo wetu wote, nguvu za nyongeza zitakuja kwenye kuhudumu kwetu, na tunakuwa watumishi wa kweli wa Yesu Kristo.

Kuhudumu Kunahitaji Imani

Kutimiza miito kunahitaji imani. Mara baada ya Joseph alipoanza kufanya kazi kwenye shamba, yeye na maria wakawa wagonjwa sana Hawakuwa na fedha na walikuwa miongoni mwa wageni. Ulikuwa ni wakati mgumu kwao. Katika jarida lake, Joseph aliandika, “Tulifanyakazi pamoja [na] kubaki Kanisani pamoja na imani yetu ndogo tuliyokuwa nayo, ijapokuwa shetani alijaribu kutuangamiza na kuturudisha nyuma.”10

Mimi, pamoja na mamia ya vizazi, tutakuwa na shukrani ya milele kwamba Joseph na Maria hawakurudi nyuma. Baraka zinakuja tunapovumilia katika wito wetu na majukumu yetu na kung’ang’ania kwa imani yote tuliyonayo.

Ninamjua mwalimu mzuri wa Mafundisho ya Injili anayewainua washiriki wa darasa akiwa anafundisha na kusimamia majadiliano, lakini haikuwa hivyo kila mara. Baada ya kujiunga na Kanisa, alipokea wito kufundisha katika Msingi. Alihisi hakuwa na ujuzi wa kufundisha, lakini kwa sababu alijua umuhimu wa kuhudumu, alikubali. Mara woga ukamshika, na akaacha kuhudhuria ili asiweze kufundisha. Shukrani kwa mwalimu wa nyumbani aliyegundua kutokuwepo kwake, alimtembelea, na alimwalika tena. Askofu na waumini wa kata walimsaidia. Hatimaye, kuongezeka kwa imani, alianza kufundisha darasa. Akiwa anatumia kanuni ambazo sasa zinafundishwa kwenye Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, Bwana akabariki juhudi zake, na akawa mwalimu mwenye kipawa.11

Mwanaume au mwanamke wa asili katika sisi wote anapelekea kujizuia kuhudumu kwa sababu kama vile “Siko tayari kuhudumu; Bado nina mengi ya kujifunza, Nimehudumu kwenye wito huo wakati uliopita, nimechoka na nahitaji kupumzika,” “Nina umri mkubwa—ni zamu ya mtu mwingine,” au “Nina kazi nyingi.”

Akina kaka na dada, kukubali na kutimiza wito ni tendo la imani. Tunaweza kuamini katika yale ambayo nabii wetu, Rais Thomas S. Monson anafundisha: “Yule Bwana huita, Bwana humhitimisha” na “Wakati tunapokuwa katika kazi ya Bwana, tuna haki ya usaidizi wa Bwana.”12 Tunapokuwa tumezidiwa au hatujazidiwa, tuwe na woga hata kifo au kuchoka hata kifo, Bwana anatutaka tuingize gia, kuwasha, na kuhudumu.

Sioni dalili kwamba Rais Monson na washiriki wake katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama wana shughuli nyingi au wamechoka sana. Wao ni mfano wa namna msukumo wa nguvu huja katika maisha yetu kama tuna imani, kukubali kazi, na kutimiza kwa kujitolea na kujituma. Wao “waliweka [mabega yao] kwenye sukani”13 miaka mingi iliyopita, na wanaendelea kusukuma mbele, kusonga mbele, na juu.

Ndiyo, wanahudumu kwenye wito muhimu, lakini kila wito au uteuzi ni muhimu. Rais Gordon B. Hinckley, nabii wa wakati uliopita na Rais wa Kanisa, alisema: “Sisi wote tupo katika jitihada hii ya pamoja. … Wajibu wako ni mkubwa katika nyanja yako ya majukumu kama ulivyo wajibu wangu katika nyanja yangu. Hakuna wito katika Kanisa ulio mdogo au una matokeo madogo.”14 Kila wito ni muhimu.15

Acha Sisi Tuhudumu

Acheni tusimame katika imani, “tuweke [mabega yetu] kwenye sukani,” na kuisogeza “kazi takatifu mbele.”16 Acheni tuweke “kwenye gia kubwa,” pamoja na Shangazi mwema Dorothy. Kaka na dada zetu, acha tuhudumu.

Kama unataka kumfanikisha askofu au rais wako wa tawi, mwulize swali “Nawezaje Kusaidia?” “Ni wapi ambapo Bwana angependa mimi nihudumu?” Atakapoomba na kufikiria juu yako, familia, na majukumu ya ajira, ataongozwa kutoa wito sahihi. Utakaposimikwa, utapokea baraka za ukuhani ili zikusaidie kufanikiwa. Wewe utabarikiwa ! Kila muumini anahitajika, na kila muumini anahitaji nafasi ya kuhudumu.17

Yesu Kristo ni Mfano Wetu

Yesu Kristo, mfano wetu mkubwa, alitoa maisha Yake kwa ajili ya kazi ya Baba Yake. Katika Baraza Kuu kabla ya ulimwengu huu haujaanzishwa, Yesu, alichaguliwa na kupakwa mafuta toka mwanzo, alijitolea, “Nipo hapa, nitume mimi.”18 Kwa kufanya hivi, Akawa mtumishi wetu sisi wote Kupitia kwa Yesu Kristo na uwezo tunaoupokea kupitia Upatanisho Wake, pia tunaweza kuhudumu. Atatusaidia sisi.19

Ninatoa upendo wangu wa moyo kwa wale ambao hawawezi kuhudumu katika Kanisa katika njia ya kawaida kwa sababu ya shida binafsi lakini anayeishi maisha yako katika roho ya utumishi. Ninaomba kwamba utabarikiwa katika juhudi zako. Pia ninatoa shukrani kwa wale wanaotii wito wao wiki hadi wiki, pia na wale ambao hivi karibuni watakubali wito wa kuhudumu. Matoleo yote na dhabihu zinathaminiwa, hususani na Yeye ambaye tunamtumikia. Wote wanaohudumu watapata neema ya Mungu.20

Bila kujali umri wetu au shida zetu, acheni huduma iwe “kauli mbiu.”21 Hudumu katika wito wako. Hudumu misheni. Mhudumie mama yako. Mhudumie mgeni. Mhudumie jirani yako. Hudumu tu.

Naomba Bwana ambariki kila mmoja wetu katika juhudi zetu kuhudumu na kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo.22 Ninashuhudia kwamba Yesu Kristo yu hai na anaongoza kazi hii. Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona “Compound Gears,” technologystudent.com/gears1/gears3.htm; “Compound Gear Reduction,” curriculum.vexrobotics.com.

  2. Ona Preach My Gospel: A Guide to Missionary Service (2004), 87.

  3. Mafundisho na Maagano 42:29; ona pia Mafundisho na Maagano 59:5.

  4. Ona Mathayo 25:40; Mosia 2:17.

  5. Ona Yohana 12:26.

  6. Ona Mafundisho na Maagano 81:4–6.

  7. Marion G. Romney, “The Book of Mormon,” Ensign, May 1982, 93.

  8. Ona Joseph Skeen, reminiscences and diary, 7, Church History Library, Salt Lake City; ona pia Journal and History of Joseph Skeen, ed. Greg S. Montgomery and Mark R. Montgomery (1996), 23.

  9. Ona Mafundisho na Maagano 1:38; Makala ya Imani 1:5.

  10. Skeen, reminiscences and diary, 8, spelling and punctuation standardized; ona pia Journal and History of Joseph Skeen, 23; Luke 22:31; 2 Nephi 28:19–24; Alma 30:60; Doctrine and Covenants 10:22–27.

  11. Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi (2016), 37–38; Handbook 2: Administering the Church (2010), 5.3, 5.5.4.

  12. Thomas S. Monson, “Duty Calls,” Ensign, May 1996, 44.

  13. “Put Your Shoulder to the Wheel,” Hymns, no. 252.

  14. Gordon B. Hinckley, “The Empty Tomb Bore Testimony,” Ensign, May 1995, 71.

    Rais Hinckley pia alisema: “Mna nafasi kubwa ya kutimiza wajibu wa kazi yako kama mimi nifanyavyo kazi yangu. Kuendelea kwa kazi hii kutategemea muungano wa juhudi zetu. Bila kujali wito wako, yatishia kama vile nafasi ya kufanikisha mambo mazuri kama yangu. Kilicho muhimu zaidi ni kwamba hii ni kazi ya Bwana. Kazi yetu ni kwenda kutenda mema kama Alivyofanya” (“This Is the Work of the Master,” 71).

    President Thomas S. Monson alisema: “Jinsi gani mtu anaweza kuutukuza wito wake? Ni kwa kufanya huduma inayohusiana nayo”” (“Duty Calls,” 43).

  15. Ona Alma 37:6.

  16. “Put Your Shoulder to the Wheel,” Hymns, no. 252.

  17. Ona Handbook 2, 3.3.1, 3.3.3, 19.1.1, 19.4. “Through the service of men and women and boys and girls, God’s work is done” (Gospel Principles [2009], 163).

  18. Ibrahimu 3:27.

  19. Ona Mafundisho na Maagano 76:5.

  20. OnaMosia 18:26.

  21. “They, the Builders of the Nation,” Hymns, no. 36.

  22. Ona Moroni 7:48.