2010–2019
Ghorofa ya Nne, Mlango wa Mwisho
Oktoba 2016


21:33

Ghorofa ya Nne, Mlango wa Mwisho

Mungu “huwazawadia wale wanaomtafuta yeye kwa bidii,” kwa hiyo endeleenikubisha. Kina dada msikate tamaa. Mtafuteni Mungu kwa moyo yenu yote.

Dada zabfu wapendwa, marafiki wapendwa, tumebarikiwa jinsi gani kukusanyika tena katika huu mkutano mkuu wa ulimwenguni kote chini ya maelekezo na uongozi wa nabii wetu mpendwa na Rais, Thomas S. Monson. Rais, sisi tunakupenda na tunakukubali! Tunajua unawapenda kina dada wa Kanisa.

Mimi napenda kuhudhuria kikao hiki cha mkutano mkuu maalum wa kina dada wa Kanisa.

Kina dada, ninapowaona, sina budi kuwafikiria wanawake ambao wamekuwa na ushawishi mkubwa katika maisha yangu, bibi yangu, mama yangu, ambao walikubali mwaliko wa kuja na kuona Kanisa na mafundisho yake.1 Kuna mke wangu mpendwa, Harriet, ambaye nilimpenda mara ya kwanza nilipomuona. Kuna mama Harriet, ambaye alijiunga na Kanisa muda mfupi baada ya kumpoteza mume wake kutokana na saratani. Kisha kuna dada yangu, binti yangu, binti mjukuu wangu, na binti kitukuu changu—wote hawa wamekuwa na ushawishi mzuri sana kwangu. Wao kwa kweli huleta uchangamfu katika maisha yangu. Wao hunipa motisha kuwa mtu bora na kiongozi wa Kanisa mwenye utambuzi. Jinsi gani maisha yangu yangekuwa tofauti bila wao!

Labda kile kinachoninyenyekeza sana ni kujua kwamba ushawishi kama huu huakisiwa mara milioni kote katika Kanisa kupitia uwezo, talanta, akili, na ushuhuda wa wanawake wenye imani kama ninyi.

Sasa, baadhi yenu mnaweza kuhisi kutosahili kuwa na sifa hii kuu. Mnaweza kujihisi kuwa ninyi si kitu hata kuwa na ushawishi wa maana kwa wengine. Labda hata haujifikirii wenyewe kama “mwanamke mwenye imani” kwa sababu wakati fulani unahangaika na shaka au hofu.

Leo, mimi ningependa kuongea na mtu yeyote ambaye ameshajisikia hivi—na hiyo labda inamjumuisha kila mmoja wetu wakati mmoja au mwingine. Mimi ningependa kunena juu ya imani—ni nini, kile inaweza kufanya na kile haiwezi kufanya, na kile sharti sisi tufanye ili kuamsha nguvu za imani katika maisha yetu.

Imani Ni Nini

Imani ni ushawishi wa nguvu kuhusu kitu fulani tunachoamini—ushawishi wenye nguvu hata kwamba unatusukuma kutenda vitu ambayo pengine hatungeweza kutenda. “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”2

Ingawa hili lina maana kwa Wakristo waaminio, mara nyingi linawakanganya wasioamini. Wao hutikisa vichwa vyao na kuuliza, Je! Mtu anaweza kuwa na uhakika wa kitu ambacho hawezi kukiona? Kwa wao, huu ni ushahidi wa ukosefu wa mantiki wa dini.

Kile wanachokosa kuelewa ni kwamba kuna njia nyingi za kuiona kuliko kuona kwa macho tu. Kuna njia nyingi za kuhisi kuliko kuhisi kwa mikono yetu, njia nyingi za kusikia kuliko kwa masikio yetu.

Ni kitu kama vile tukio la msichana mdogo aliyekuwa matembezini na bibi yake. Wimbo wa ndege ulikuwa mtukufu kwa yule msichana mdogo, na akamweleza bibi yake kila sauti.

“Umesikia hiyo?” msichana mdogo aliuliza tena na tena. Lakini bibi yake alikuwa hasikii vizuri na hangeweza kutofautisha sauti hizo.

Mwishowe, bibi alipiga magoti na kusema, “Samahani, mpendwa. Bibi hawezi kusikia vizuri,”

Kwa ghadhabu, yule msichana mdogo alimshika bibi yake usoni kwa mikono yake, akumtamaza machoni mwake, na kusema, “Bibi, sikiliza vyema!”

Kuna masomo katika hadithi hii kwa wote wasioamini na waaminio. Kwa sababu tu vile sisi hatuwezi kusikia haimaanishi kuwa hakuna cha kisikia. Watu wanaweza kusikiliza ujumbe mmoja au kusoma maandiko sawa, na mmoja anaweza kuhisi ushahidi wa Roho, hali yule mwingine hasihisi.

Kwa upande mwingine, katika juhudi zetu za kuwasaidia wapendwa wetu wapate uzoefu wa sauti ya Roho na uzuri wake, umilele na uzuri wa kina wa injili ya Yesu Kristo, ukiwaambia wao “sikilizeni vyema” huenda isiwe njia nzuri.

Labda ushauri bora—kwa mtu yeyote anayetaka kuongeza imani—ni kusikiliza kwa njia tofauti. Mtume Paulo alituhimiza tutafute sauti ambayo huongea na roho zetu wala si masikio yetu tu. Alifundisha, “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.”3 Au tunapaswa kuyazingatia maneno ya Mwanamfalme Mdogo wa Saint-Exupéry, ambaye alisema: “Mtu huona wazi tu kwa moyo wake. Chochote muhimu ni fiche kwa macho.”4

Nguvu na Mipaka ya Imani

Wakati mwingine si rahisi kukuza imani katika vitu vya kiroho unapoishi katika ulimwengu wa kimwili. Lakini inastahili juhudi, kwa sababu nguvu za imani katika maisha yetu zinaweza kuwa za kina sana. Maandiko yanatufundisha kwamba kupitia imani dunia ziliumbwa, maji yakatawanywa, wafu wakafufuliwa, mito na milima ikaondolewa kutoka kwenye njia zao.5

Bado baadhi wanaweza kuuliza, “Ikiwa imani ina nguvu sana, basi kwa nini siwezi kupokea jibu la sala za dhati? Mimi sihitaji bahari itawanywe au mlima uondoshwe. Mimi nahitaji ugonjwa wangu uondolewe au wazazi wangu wasameheane au mwenzi wa milele atokee mlangoni mwangu na shada la maua mkono mmoja na pete ya posa ule mkono mwingine. Kwa nini imani yangu haiwezi kutimiza hilo?”

Imani ina nguvu sana, na kila mara ina matokeo ya miujiza. Lakini bila kujali tuna imani kiasi gani, kuna vitu viwili ambavyo imani haiwezi kufanya. Kwani, haiwezi kukiuka haki ya kujiamulia ya mtu mwingine.

Mwanamke mmoja aliomba kwa miaka mingi kwamba bintiye mpotovu angerudi kwenye zizi la Kristo na akahisi kuvunjika moyo kwamba maombi yake yalionekana kutojibiwa. Hii hasa ilikuwa ni uchungu sana wakati aliposikia hadithi za watoto wengine wapotovu ambao walikuwa wametubu dhambi zao.

Shida haikuwa uchache wa maombi au ukosefu wa imani. Alihitaji tu kuelewa kwamba, hata uchungu jinsi gani ilivyo kwa Baba yetu aliye Mbinguni, Yeye hatamlazimisha mtu yeyote kuchagua njia ya haki. Mungu hakuwalazimisha watoto Wake kumfuata katika maisha ya kabla kuzaliwa. Iweje sasa atulazimishe tunaposafiri kupitia haya maisha ya ulimwenguni?

Mungu ataalika, atashawishi. Mungu atatufikia bila kuchoka kwa upendo na maongozi na hamasa. Lakini kamwe Mungu hatashurutisha—hiyo itakinzana na mpango Wake mkuu kwa ukuaji wetu wa milele.

Jambo la pili ambalo imani haiwezi kufanya ni kulazimisha mapenzi yetu kwa Mungu. Sisi hatuwezi kumlazimisha Mungu kukubaliana na hamu zetu—bila kujali jinsi tulivyo sahihi au jinsi tunavyoomba kwa dhati. Fikiria uzoefu wa Paulo, ambaye alimsihi Bwana mara nyingi sana apate afueni kwa ajili ya jaribio la kibinafsi—alilokuwa nalo ambalo aliliita “mwiba mwilini.” Lakini hayo hayakuwa mapenzi ya Mungu. Hatimaye, Paulo alitambua kwamba majaribu yake yalikuwa baraka, na alimshukuru Mungu kwa kutojibu maombi yake katika njia ile aliyotarajia.6

Amini na Imani

La, madhumuni ya imani sio kubadilisha mapenzi ya Mungu bali ni kutuwezesha sisi kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu. Imani ni amini—kuamini kwamba Mungu huona kile ambacho hatuwezi kuona na kwamba Yeye anajua kile sisi hatujui.7 Wakati mwingine kuamini ono letu na hukumu yetu haitoshi.

Nilijifunza hayo kama rubani wa ndege, katika zile siku ambazo ilinibidi niendeshe ndege katika ukungu mzito au mawingu na ningeweza kuona tu futi chache mbele. Ilinibidi nitegemee vifaa ambavyo vingenijulisha pale nilipo na pale nilipokuwa naelekea. Ilinibidi nisikilize sauti ya mthibiti wa safari za angani. Ilinibidi nifuate mwongozo wa mtu aliyekuwa na taarifa sahihi kusinda nilizokuwa nazo. Mtu ambaye nisingeweza kumwona lakini ambaye nilikuwa nimejifunza kumwamini. Mtu ambaye angeweza kuona kile ambacho nisingeweza kuona. Ilinibidi niamini na kutenda vilivyo, ili nifike mwisho wa safari yangu salama.

Imani inamaanisha kwamba tusiamini tu katika hekima ya Mungu bali pia katika upendo Wake. Inamaanisha kuamini kwamba Mungu anatupenda kikamilifu, kwamba chochote afanyacho—kila baraka Yeye hutoa na kila baraka ambayo, huzuia—ni kwa ajili ya furaha yetu ya milele.8

Kwa aina hii ya imani, ingawa tunaweza kukosa kuelewa kwa nini vitu fulani vinatokea au kwa nini maombi fulani hayajabiwi, tunaweza kujua kwamba mwishowe  kila kitu kitapata maana. Mambo yote [yatafanya] kazi pamoja na wale wampendao [Mungu].”9

Yote yatasawazishwa. Yote yakuwa sawa.

Tunaweza kuwa na hakika majibu yatakuja, na tunaweza kuwa na imani siyo tu kuwa tutaridhika na majibu, bali pia tutazidiwa na neema, rehema, ukarimu na upendo wa Baba yetu wa Mbinguni alionao kwa ajili yetu, watoto Wake.

Endelea Tu Kubisha Mlango

Mpaka hapo, tunatembea kwa imani yoyote ile tulionayo,10 tukitafuta daima kuongeza imani yetu. Wakati mwingine, hili si jambo rahisi. Wale ambao si wavumilivu, wasio na sharti, au wazembe wanaweza kuona imani inatatiza. Wale ambao huvunjika moyo  upesi au kukanganyika inawezekana wasiipate. Imani huja kwa wanyenyekevu, wenye bidii, wastahamilifu.

Huja kwa wale ambao wanaolipia gharama ya uaminifu.

Ukweli huu unaonyeshwa katika tukio la wamisioanri wawili vijana wakihudumu katika enao ambalo kulikuwa na ubatizo wa waongofu mchache. Nadhani ingeeleweka kwao kufikiria kile walichokifanya hakingeleta tofauti sana.

Lakini hawa wamisionari wawili walikuwa na imani, na walikuwa na sharti. Walikuwa na mtazamo ambao kama hakuna mtu angesikiliza ujumbe wao, isingekuwa ni kwa sababu walikuwa wamefanya juhudi kwa uzembe.

Siku moja, walipata hisia ya kwenda kwa wakazi walioishi katika jengo la nyumba za kukodi la ghorofa nne maridadi. Walianza ghorofa ya kwanza na kubisha kila mlango, waliwasilisha ujumbe wa kuokoa wa Yesu Kristo na Kanisa Lake la Urejesho.

Jengo la ghorofa ya utotoni wa Dada Uchtdorf

Hakuna yeyote katika ghorofa ya kwanza aliyetaka kuwasikiliza.

Ingekuwa rahisi jinsi gani kusema, “Tumechoka. Acha tukomee hapa. Acha twende na kujaribu jumba lingine.”

Lakini hawa wamisionari wawili walikuwa na imani na walikuwa tayari kufanya kazi, na kwa hivyo walibisha kila mlango katika ghorofa ya pili.

Pia, hakuna yeyote ambaye angewasikiliza.

Ghorofa ya tatu ikawa vivyo hivyo. Na ghorofa ya nne vivyo hivyo—na, ni mpaka walipobisha mlango wa mwisho wa ghorofa ya nne.

Mlango ulipofunguliwa, msichana mdogo akitabasamu kwao na kuwaomba wangojee aongee na mama yake.

Mama yake, ambaye alikuwa na umri wa miaka 36, ambaye karibuni alikuwa amempoteza mume wake, hakuwa na hamu ya kuongea na wamisionari Wamormoni. Kwa hiyo alimwambia binti awaambie waende zao.

Lakini yule binti akamsihi. Hawa vijana ni wazuri sana, alisema. Na ingekuwa dakika chache tu.

Kwa hiyo, akisitasita, mama akakubali. Wamisionari waliwasilisha ujumbe wao na kumpatia yule mama kitabu cha kusoma—Kitabu cha Mormoni.

Baada ya wao kuondoka, yule mama aliamua kusoma kurasa chache tu.

Alimaliza kusoma kitabu chote katika siku chache.

Familia na Dada Uchtdorf na wamisionari

Muda mfupi baadaye, familia hii ya ajabu ya mzazi mmoja iliingia katika maji ya ubatizo.

Wakati familia hii ndogo ilihudhuria tawi la sehemu yao katika Frankfurt, Ujerumani, shemasi mdogo akaona urembo wa mmoja wao na kufikiria, “Hawa wamisionari walikuwa wanafanya kazi nzuri sana!”

Jina la huyo shemasi lilikuwa Dieter Uchtdorf. Na msichana mwenye haiba—ambaye alikuwa amemsihi mama yake awasikilize wamisionari—alikuwa na jina maridadi la Harriet. Anapendwa na wote ambao hukutana naye anapoandamana nami katika safari zangu. Amebariki maisha ya watu wengi kupitia upendo wake kwa injili na hulka yake ya msisimko. Yeye kwa kweli ni uchangamfu wa maisha yangu.

Dada Uchtdorf alkitoa hutoba huko Norway

Ni mara nyingi kiasi gani nimeinua moyo kwa shukrani kwa ajili ya hawa wamisionari wawili ambao hawakukomea ghorofa ya kwanza! Ni mara nyingi kiasi gani moyo wangu umefikia kwa shukrani kwa ajili ya imani yao na kaziyao. Ni mara nyingi kiasi gani nimetoa shukrani kwamba waliendelea—hata ghorofa ya nne, mlango wa mwisho.

Itafunguliwa Kwako

Katika kutafuta kwetu kwa imani ya kudumu, katika juhudi zetu za kumpata Mungu na madhumuni Yake, acha tukumbuke ahadi ya Bwana. “Bisheni, nanyi mtafunguliwa.”11

Je, tutakoma baada ya kubisha mlango mmoja au miwili? Ghorofa moja au mbili?

Au tutaendelea kutafuta mpaka tufike ghorofa ya nne, mlango wa mwisho?

Mungu “huwapa thawabu wale wamtafutao,”12 lakini hiyo thawabu haipo nyuma ya mlango wa kwanza. Kwa hiyo tunahitaji kuendelea kubisha. Kina dada msikate tamaa. Mtafuteni Mungu kwa moyo yenu yote. Fanyeni imani. Tembeeni katika haki.

Mimi naahidi kwamba kama mtafanya hivyo—hata mpaka ile ghorofa ya nne, mlango wa mwisho—mtapokea majibu mnayotafuta. Mtapata imani. Na siku moja mtajawa na nuru ambayo hung’aa “hizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.”13

Dada zangu wapendwa katika Kristo, Mungu ni halisi.

Yeye yu Hai

Anawapenda.

Anawajua.

Anawaelewa.

Anajua kusihi kwenu kwa kimya kimya kwa mioyo yenu. Hatawatelekeza. Hatawasahau.

Huu ni ushuhuda wangu na baraka za kitume kwa kila mmoja ambaye atasikia katika moyo na akili yake huu ukweli mtukufu. Ishini kwa imani, marafiki zangu wapendwa, dada zangu wapendwa, na “Bwana Mungu wetu, atawaongezea mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!”14

Nawaachieni imani yangu, msimamo wangu, ushahidi wangu wa hakika usiotikisika kwamba hii ni kazi ya Mungu Katika jina takatifu la Mwokozi wetu mpendwa, katika jina la Yesu Kristo, amina