Nitaleta Nuru ya Injili ndani ya Nyumba Yangu
Tunaweza kuleta nuru ya injili ndani ya nyumba zetu, shule, na sehemu zetu za kazi kama tutatafuta na kushiriki mambo chanya kuhusu wengine.
Kama mjibizo wa mwaliko wa Linda K. Burton kwenye Mkutano Mkuu wa Aprili,1 wengi wenu mmehusika kimawazo na matendo ya ukarimu ya upendo yanayozingatia katika kufanikisha mahitaji ya wakimbizi katika maeneo yenu. Kutoka mambo ya kawaida, juhudi za mmoja mmoja mpaka mipango ya jumuiya yote, matendo hayo ni matokeo ya upendo. Mliposhiriki muda wenu,vipaji na rasilimali zenu—na wakimbizi —mioyo yenu imefanywa miyepesi. Ujenzi wa matumaini na imani na hata upendo mkuu kati ya mpokeaji na mtoaji ni matokeo yasiyozuilika ya upendo wa kweli
Nabii Moroni anatuambia kwamba upendo ni tabia muhimu kwa wale watakaoishi na Baba wa Mbinguni katika ufalme wa selestia. Anaandika, “Usipokuwa na upendo huwezi kabisa kuokolewa katika ufalme wa Mungu.”2
Bila shaka,Yesu Kristo ni mfano kamili wa upendo. Kujitoa kwake kabla ya kuja duniani kuwa Mwokozi wetu, matendo Yake katika maisha Yake yote duniani, zawadi Yake kutoka mbinguni ya Upatanisho, na juhudi Zake zinazoendelea kuturudisha kwa Baba yetu wa Mbinguni ni upendo wa mwisho usioelezeka. Anafanya kazi na umakini wa ajabu: upendo kwa Baba Yake wadhahirisha kupitia upendo Wake kwa kila mmoja wetu. Alipoulizwa kuhusu amri iliyo kuu,Yesu alijibu:
“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
“Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
“Na ya pili yafanana nayo, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”3
Mojawapo ya njia za maana sana tunaweza kukuza na kuonyesha upendo kwa jirani yetu ni kwa kuwa wakarimu katika mawazo na maneno yetu. Miaka michache iliyopita, rafiki mpendwa alisema, “Sura kubwa ya upendo inaweza kuwa kuzuia hukumu.”4 Hiyo bado ni kweli leo.
Hivi karibuni,wakati Alyssa mwenye umri wa miaka mitatu alipoangalia filamu pamoja na ndugu zake, alisema kwa fumbo la wazi, “Mama, yule kuku sio wa kawaida!”
Mama yake aliangalia skrini na akajibu kwa tabasamu,”Mpenzi, yule ni tausi.”
Kama yule mtoto wa miaka mitatu asiyejua, wakati mwingine hata sisi tunawatazama wengine kwa uelewa usio kamili au usio sahihi. Tunaweza kuzingatia kwenye tofauti na kuona dosari kwa wale wanaotuzunguka ambako Baba yetu wa Mbinguni, anawaona watoto Wake, walioumbwa katika mfano Wake wa milele, pamoja na utukufu na uwezekano wa uzuri.
Rais James E. Faust anakumbukwa kwa kusema, “Ninavyozidi kukomaa, ndivyo ninaacha kuhukumu sana.”5 Hiyo inanikumbusha uchunguzi wa Mtume Paulo:
Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
“Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.”6
Tunapoona kutokamilika kwetu kwa uwazi sana, hatutapendelea kiasi kuwaangalia wengine kupitia “glasi, kwa giza.” Tunataka kutumia nuru ya injili kuwaangalia wengine kama Mwokozi anavyofanya—kwa huruma, tumaini, na upendo. Siku itakuja wakati tutakapokuwa na uelewa kamili wa mioyo ya na tutakuwa na shukrani kuwa na huruma iliyoelekezwa kwetu—kama vile tunavyoelekeza mawazo ya upendo na maneno kwa wengine wakati wa maisha haya.
Miaka michache iliyopita, nilikwenda katika mtumbwi pamoja na kundi la wasichana. Maziwa ya bluu yenye kina yaliyozungukwa na kijani kibichi, vilima vyenye misitu minene na miamba ya mawe ilikuwa mizuri ya kustaajabisha. Maji yaling’ara kwenye makasia yetu tulipoyatumbukiza ndani ya maji meupe, na jua liling’ara kwa mfukuto wakati tukienda kilaini ng’ambo ya pili ya ziwa.
Hata hivyo, mawingu hatimaye yalitanda angani na upepo mkali ulianza kuvuma. Ili kuendelea kwa vyovyote vile, ilibidi kupiga makasia kwa nguvu zaidi ndani ya maji, kupiga makasia bila kupumzika katikati ya mapigo. Baada ya masaa machache ya kuchosha ya kazi, na kuvunja mgongo, hatimaye tulipinda kona kwenye ziwa kubwa na kungundua kwa mshangao wetu na furaha kwamba upepo ulikuwa ukivuma kwenye mwelekeo tuliotaka kwenda.
Kwa haraka tulijinufaisha na zawadi hii. Tulitoa kipande kidogo cha nguo, na tukafunga pembe zake mbili kwenye mipini ya kasia na pembe zingine mbili kwenye miguu ya mume wangu, ambayo aliipanua hata kwenye ukingo wa juu wa mtumbwi. Upepo ulijaza matanga ya ubunifu, na tukaondoka!
Wasichana katika mtumbwi mingine walipoona jinsi tulivyokuwa tunaenda kiurahisi katika maji, kwa haraka walitengeneza papo hapo matanga yao. Mioyo yetu ilijawa na kicheko na faraja, shukrani kwa ajili ya kupungua kwa changamoto za siku.
Jinsi gani kama upepo ule mtukufu unaweza kuwa sifa ya kweli ya rafiki, maamkizi ya furaha ya mzazi, kuthibitisha kwa kichwa na ndugu, au tabasamu ya msaada ya mfanyakazi mwenza au mwanafunzi mwenza, wote wakitoa “upepo mzuri katika matanga yetu” tunapopambana na changamoto za maisha! Rais Thomas S. Monson alisema hivi: “Hatuwezi kuuongoza upepo, lakini tunaweza kurekebisha matanga. Kwa furaha tele, amani, na kuridhika, acha tuweze kuchagua mtazamo chanya.”7
Maneno yana nguvu za kushangaza, yote kujenga na kubomboa. Mnaweza wote labda kukumbuka maneno hasi ambayo yalitushusha chini na maneno mengine yaliyosemwa kwa upendo ambao yalifanya roho zetu zipae. Kutafuta kusema tu yale ambayo ni chanya kuhusu—na kwa—wengine huinua na kuimarisha wale wanaotuzunguka na kuwasaidia wengine kufuata katika njia za Mwokozi.
Kama msichana mdogo wa Msingi, nilifanya kazi kwa bidii kushona kingamo za msemo rahisi uliosema,“Nitaleta nuru ya injili katika nyumba yangu.” Mchana wa siku moja ya wiki,wakati sisi wasichana tukishona nguo, mwalimu wetu alituambia hadithi ya msichana aliyeishi mlimani upande mmoja wa bonde. Kila jioni sana, aliona kwenye mlima upande mkabala wa bonde nyumba ambayo ilikuwa na madirisha ya dhahabu yanayong’ara. Nyumba yake ilikuwa ndogo na kiasi chakavu, na msichana alikuwa na ndoto ya kuishi katika nyumba ile nzuri yenye madirisha ya dhahabu.
Siku moja yule msichana aliruhusiwa kuendesha baisikeli yake kuvuka bonde. Kwa shauku aliendesha mpaka akaiifikia ile nyumba yenye madirisha ya dhahabu ambayo ameistaajabia kwa muda mrefu. Lakini alipoteremka kutoka kwenye baiskeli yake, aliona kwamba ile nyumba ilikuwa imetelekezwa na ni gofu, lenye majani marefu katika ua na madirisha ambayo yalikuwa ya kawaida na machafu. Kwa masikitiko, msichana aliinamisha kichwa chake kuelekea nyumbani. Kwa mshangao wake, aliona nyumba yenye madirisha ya dhahabu inayong’aa juu ya mlima kuvuka bonde, na mara alitambua ilikuwa ni nyumba yake mwenyewe!8
Wakati mwingine, kama msichana huyu mdogo, tunaangalia kile wengine wanaweza kuwa nacho au kuwa na kujiona sisi tumepungukiwa. Tunakuwa tumezingatia mfano wa maisha ya Pinterest au Instagram au tumenaswa katika mashindano mashuleni na sehemu za kazi. Hata hivyo,wakati tunapochukuwa muda “kuhesabu baraka [zetu] nyingi.”9 tunaona kwa taswira ya kweli na kugundua uzuri wa Mungu kwa watoto Wake wote .
Haijalishi kama tupo 8 au 108, tunaweza kuleta nuru ya injili ndani ya mazingira yetu, iwe ni majengo marefu ya Manhattan, nyumba za nguzo Malaysia, au yurt Mongolia. Tunaweza kuamua kutafuta mazuri kwa wengine na katika mazingira yanayotuzunguka. Wasichana na wasio wasichana kila sehemu wanaweza kuonyesha upendo wanapochagua kutumia maneno ambayo yanajenga kujiamini na imani kwa wengine.
Mzee Jeffrey R. Holland alielezea kuhusu kijana aliyekuwa anataniwa na vijana wenzake wakati wakiwa shuleni. Miaka kadha baadaye, aliondoka kwenda mbali, akajiunga na jeshi, akapata elimu, na akawa muumini hai katika Kanisa. Wakati huu wa maisha yake ulikuwa na kiwango cha juu cha mafanikio ya ajabu.
Baada ya miaka michache, alirudi nyumbani. Hata hivyo, watu walikataa kukubali ukuaji na maendeleo yake. Kwao, alikuwa bado yule yule, na walimchukulia vile vile. Hatimaye, huyu mtu mzuri alififia kwenye kuvuli cha mafanikio yake ya zamani bila kuweza kutumia maendeleo ya vipaji vyake vya ajabu kuwabariki wale waliomdhihaki na walimkataa tena.10 Ni hasara jinsi gani, kote, kwake na jumuiya yake!
Mtume Petro alifundisha, “Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.”11 Hamasa ya upendo, maana yake “kwa moyo wote,” inaonyeshwa na kusahau makosa na vikwazo vya mwingine kuliko kuweka visasi au kujikumbusha wenyewe na wengine mapungufu ya zamani.
Wajibu wetu na fadhila ni kukumbatia maendeleo katika kila mmoja tunapojitahidi kuwa zaidi kama Mwokozi wetu,Yesu Kristo. Ni msisimko jinsi gani unakuwa kuona nuru katika macho ya aliyeweza kuelewa Upatanisho wa Yesu Kristo na anafanya mabadiliko ya kweli katika maisha yake! Wamisionari waliopata uzoefu wa furaha wa kumwona muumini mpya akiingia katika maji ya ubatizo na kisha kuingia milango ya hekalu ni mashahidi wa baraka za kuwaruhusu—na kuwatia moyo—wengine kubadilika. Waumini wanaokaribisha waumini wapya ambao wangeweza kufikiriwa watarajiwa wasioelekea kuwa wa ufalme wanapata furaha kuu katika kuwasaidia wahisi upendo wa Bwana. Uzuri mkuu wa injili ya Yesu Kristo ni ukweli wa kuendelea mbele milele—sio tu tumeruhusiwa tubadilike na kuwa wazuri zaidi bali tutiwe moyo,na hata tumeamriwa , tuendelee katika kutafuta maendeleo na hatimaye, utimilifu.
Rais Thomas S. Monson alielezea: “Katika njia ndogo mia moja, nyinyi wote mnavaa joho la upendo. … Kuliko kuwa mtu wa kuhukumu au mkosoaji wa wenzako, na tuwe na upendo safi wa Kristo kwa wasafiri wenzetu katika safari hii kupitia maisha. Na tutambue kwamba kila mmoja anafanya [kwa uwezo wake] kushughulikia changamoto ambazo zinakuja kwenye njia [zao], na tujitahidi kufanya kwa uwezo wetu mkubwa kusaidia.”12
Upendo, katika masharti chanya, ni subira, na kuridhika. Upendo unaweka wengine kwanza, ni myenyekevu, unatumia kujizuia, unatafuta mazuri kwa wengine, na unashangilia wakati mtu fulani anafanya vizuri.13
Kama akina dada (na akina kaka) katika Sayuni, tutaweka sharti kwa “wote kufanya kazi pamoja … kufanya chochote kile ambacho ni cha upole na ubinadamu, kufurahisha na kubariki katika jina [la Mwokozi]”?14 Tunaweza, kwa upendo na matumaini makubwa, tutafute na tukumbatie uzuri kwa wengine, tukiruhusu na kutia moyo maendeleo? Tunaweza kufurahia katika ufanisi wa wengine wakati tukifanya kazi kwa uboreshaji wetu wenyewe?
Ndiyo, sisi tunaweza kuleta nuru ya injili ndani ya nyumba zetu, shule, na sehemu zetu za kazi kama tutatafuta na kushiriki mambo chanya kuhusu wengine na kuyaacha yasio kamili yatokomee mbali. Ni shukrani kiasi gani ijazayo moyo wangu ninapofikiri kuhusu toba ambayo Mwokozi wetu,Yesu Kristo, amefanya iwezekane kwetu sisi wote ambao bila kutarajia tumetenda dhambi katika ulimwengu huu usio kamili na wakati mwingine mgumu!
Ninatoa ushuhuda wangu kwamba tunapofuata mpango Wake mkamilifu, tunaweza kupokea zawadi ya upendo, ambayo itatuletea furaha kuu katika maisha haya na baraka iliyoahidiwa ya maisha ya milele pamoja na Baba yetu wa Mbinguni. Katika jina la Yesu Kristo, amina.