Kanuni na Ahadi
Na tuweze kutunza miile yetu na akili zetu kwa kushika kanuni zilizowekwa katika Neno la Hekima, mpango mtakatifu uliotolewa.
Usiku wa leo, ndugu zangu, naomba uongozi wa Baba yetu wa Mbinguni ninaposhiriki ujumbe wangu na ninyi.
Mnamo 1833 Bwana alimfunulia Nabii Joseph Smith mpango wa maisha yenye afya. Mpango ambao unapatikana katika sehemu ya 89 ya Mafundisho na Maagano na unajulikana kama Neno la Hekima. Unatoa mwelekeo maalum kuhusu chakula tunachokula, na unaharamisha matumizi ya vitu ambavyo ni hatari kwa miili yetu.
Wale wanaotii amri za Bwana na ambao wanatii Neno la Hekima wameahidiwa baraka fulani, ambazo ni afya njema na nguvu zaidi ya kimwili.1
Hivi majuzi nilisoma maelezo ya kweli ya udhihirisho makubwa kuhusu ahadi hii. Muumini mwaminifu wa Kanisa, John A. Larsen alihudumu wakati wa Vita vya Dunia vya II hkatika Walinzi wa Pwani wa Marekani kwenye meli ya USS Cambria. Wakati wa vita huko Ufilipino, neno lililetwa kuhusu kikosi kilichokaribia cha kamikaze za ndege za kivita za bomu. Amri ilitolewa ya uokoaji wa mara moja Kwa kuwa USS Cambria ilikuwa tayari imeenda, John na wenzake watatu walikusanya vifaa vyao na kwa haraka wakaelekea pwani, wakitarajia kubebwa hadi kwa meli zilizokuwa zikiondoka. Kwa bahati nzuri, chombo kiliwachukua na kuelekea kwa kasi hadi kwenye meli ya mwisho iliyokuwa ikitoka ufuoni. Watu kwenye meli hiyo iliyokuwa ikiondoka, katika jitihada za kuokoa kwa haraka iwezekanavyo, walishughulika ndani ya staha na walikuwa na muda tu wa kutupa kamba kwa wale watu wanne, ili pengine waweze kupanda ndani ya staha.
John, na radio nzito iliyofungiwa mgongoni mwake, alijipata akining’inia kwenye sehemu ya mwisho ya kamba yenye futi arobaini (12 m), katika upande wa meli inayoelekea katika bahari ya wazi. Alianza kujivuta juu mwenyewe, mkono kwa mkono, akijua kwamba ikiwa atapoteza nguvu zake za kushikilia, bila shaka ataangamia. Baada ya kupanda theluthi moja tu ya mwendo, mikono yake yalichomeka kwa maumivu. Alikuwa mdhaifu sana kiasi kwamba alihisi kuwa hangeweza kushikilia tena.
Akiwa ameishiwa na nguvu, alipokuwa akiwaza kwa huzuni juu ya hatma yake, kwa kimya John alimlilia Mungu, akimwambia kwamba daima alikuwa anatii Neno la Hekima na alikuwa akiishi maisha safi—na yeye sasa alihitaji mno baraka zilizoahidiwa.
John baadaye alisema kwamba alipomaliza sala yake, alihisi wimbi kubwa la nguvu. Alianza kupanda kwa mara nyingine tena na kwa upesi sana alipanda. Alipofikia staha, kupumua kwake kulikuwa wa kawaida si kama ilivyokuwa mara ya mwisho. Baraka za afya zaidi na nguvu, zilizoahidiwa katika Neno la Hekima, zilikuwa zake. Alitoa shukrani kwa Baba yake wa Mbinguni wakati huo, na katika maisha yake yote, kwa majibu ya ombi lake la dhati la msaada.2
Ndugu zangu, natutunze miili yetu na akili zetu kwa kutazama kanuni zilizowekwa katika Neno la Hekima, mpango mtakatifu uliotolewa. Kwa moyo wangu wote na roho yangu yote, nashuhudia juu ya baraka tukufu ambazo zinatusubiri tunapotii. Kwamba hili liwe hivyo, naomba, katika jina la Bwana wetu na Mwokozi, Yesu Kristo, amina.