Kushiriki na Wengine Injili ya Urejesho
Kile tunachoita “kazi ya umisionari kwa waumini” si mpango lakini ni mtazamo wa upendo na fursa ya kuwafikia wale waliotuzunguka.
I.
Akifikia mwishoni mwa huduma Yake duniani Mwokozi wetu, Yesu Kristo, aliwaamuru wanafunzi Wake: “Enendeni duniani kote, na mkawafundishe mataifa yote” (Mathayo 28:19) na “Nendeni ulimwenguni kote, na fundisheni injili kwa kila kiumbe” (Marko 16:15). Wakristo wote wako chini ya amri hizi za kushiriki injili hii na kila mtu. Wengi huita hii kama “maagizo makuu.”
Kama vile Mzee Neil L. Andersen alivyoelezea katika kikao cha asubuhi, Watakatifu wa siku za mwisho kwa hakika ni miongoni mwa wale waliojitoa kwa dhati kwenye wajibu huu mkubwa. Yatupasa kuwa, kwa sababu tunajua kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote na kwamba katika siku hizi za mwisho Yeye amerejesha maarifa muhimu ya nyongeza na uweza wa kubariki watoto Wake wote hao. Mwokozi ametufundisha kuwa tuwapende kaka zetu na dada zetu wote, na tunaheshimu mafundisho haya kwa kushiriki na wengine ushahidi na ujumbe wa injili ya urejesho “miongoni mwa mataifa, koo, tamaduni, na watu wote” (M&M 112:1). Hii ni sehemu muhimu ya kile kinachomaanisha kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho. Tunaitazamia hiyo kama fursa ya kufurahia. Nini kingeweza kuwa cha furaha zaidi kuliko kushiriki kweli za milele pamoja na watoto wa Mungu?
Leo tunazo nyenzo nyingi za kufundishia injili ambazo hazikuwepo katika vizazi vile vya awali. Tunazo Televisheni, Intaneti, na chaneli za habari za kijamii. Tunao ujumbe mwingi wa kuitambulisha injili ya urejesho. Tunao umaarufu wa Kanisa katika mataifa mengi tu. Tunayo idadi kubwa ya wamisionari. Lakini tunatumia nyenzo hizi zote kwa juhudi zote? Ninaamini wengi wetu tungesema hapana. Tunatamani tungekuwa na juhudi zaidi katika kutimiza wajibu huu wa kiuungu tuliopewa wa kutangaza injili ya urejesho ulimwenguni kote.
Kuna mawazo mengi mazuri juu ya kushiriki injili na wengine ambayo yatafanya kazi katika vigingi kimoja kimoja au nchi. Hata hivyo, kwa sababu sisi ni kanisa la ulimwengu wote, nataka kuongelea juu ya dhana ambayo itafanya kazi popote, kuanzia tawi jipya kabisa hadi tawi kongwe, toka tamaduni ambazo sasa zinaipokea injili ya Yesu Kristo hadi tamaduni na mataifa ambayo yazapingana vikali na dini. Nataka kuongea juu ya mawazo ambayo unaweza kutumia kwa watu ambao ni waumini wa kweli wa Yesu Kristo pia watu ambao hawajapata kulisikia jina Lake, kwa watu ambao wameridhika na maisha yao ya sasa pia watu ambao wanajaribu kujiboresha wenyewe kwa uwezo wao wote.
Naweza kusema nini ambacho kitasaidia katika kushiriki kwako injili, bila kujali mazingira yako yo yote? Tunahitaji msaada wa kila muumini na kila muumini anaweza kusaidia, kwani kuna kazi nyingi sana za kufanya tunaposhiriki injili ya urejesho na kila taifa, jamii, kabila, na kila mtu.
Wote tunajua kwamba kushiriki kwa muumini katika kazi ya umisionari ni muhimu sana ili kupata vyote wongofu na watu kubaki Kanisani. Rais Thomas S. Monson alisema: “Sasa ni wakati wa waumini na wamisionari kuja pamoja … [na] kufanya kazi katika shamba la Bwana ili kuzileta roho Kwake. Yeye ameandaa njia ili sisi tufundishe injili kwa njia nyingi, na Yeye atatusaidia katika kazi zetu kama tutatenda kwa imani ili kutimiza kazi Yake.”1
Kushiriki injili iliorejeshwa ni kazi yetu ya Kikristo ya heshima na ya maisha yote. Mzee Quentin L. Cook anatukumbusha, “Kazi ya umisionari siyo moja ya vibao 88 vya piano ambavyo mara chache hupigwa; ni kordi kuu katika melodi ya lazima ambayo inahitajika kupigwa daima katika maisha yetu yote kama tunataka kubaki katika maafikiano na kujitolea kwetu kwa dhati katika Ukristo na katika injili ya Yesu Kristo.”2
II.
Kuna vitu vitatu kila muumini anaweza kufanya ili kushiriki na wengine injili, bila kujali mazingira wanayoishi na kufanya kazi. Sisi wote tunapaswa kufanya haya yote.
Kwanza, wote tunaweza kusali ili kuwa na hamu ya kusaidia katika sehemu hii muhimu ya kazi ya wokovu. Jitihada zote zinaanza na hamu.
Pili, tunaweza kushika amri sisi wenyewe. Waumini waaminifu, watiifu ni mashahidi wenye ushawishi zaidi wa ukweli na thamani ya injili ya urejesho. Hata cha muhimu zaidi, ni kwamba kwa waumini waaminifu daima watakuwa na Roho Mwokozi pamoja nao, ili kuwaongoza watafutapo kushiriki katika kazi hii kuu ya kufundisha injili ya urejesho ya Yesu Kristo.
Tatu, tunaweza kusali ili kupata maongozi juu ya kile sisi tunaweza kufanya katika hali zetu binafsi ili kushiriki injili na wengine. Hii ni tofauti na kuwaombea wamisionari au kusali juu ya kile ambacho wengine wanaweza kufanya. Tunapaswa kusali juu ya kile sisi tunachoweza kufanya, kibinafsi. Tusalipo, yatupasa kukumbuka kwamba sala kwa ajili ya maongozi ya jinsi hii zitajibiwa kama zitaambatana na dhamira ya kutenda—kitu ambacho maandiko hukiita nia ya dhati au kusudi kamili la moyo. Sali ukiwa na dhamira ya kutendea kazi maongozi utakayopokea, ukimwahidi Bwana kwamba kama Yeye atakupa maongozi ya kuongea na mtu fulani juu ya injili, wewe utafanya hivyo.
Tunahitaji mwongozo wa Mwokozi kwa sababu kwa wakati wo wote baadhi wako—tayari na wengine hawako—tayari kwa ajili ya kweli za ziada za injili ya urejesho. Tusijiweke wenyewe kuwa waamuzi juu ya nani yu tayari na nani hayuko tayari. Bwana anajua mioyo ya watoto Wake wote, na kama tutaomba kwa ajili ya maongozi, Yeye atatusaidia kumpata mtu ambaye Yeye anamjua yuko “katika maandalizi ya kulisikia hilo neno” (Alma 32:6).
Kama Mtume wa Bwana, ninamsihi kila muumini na familia katika Kanisa kusali kwa Bwana ili awasaidie kuwapata watu wa walioandaliwa kupokea ujumbe wa injili ya urejesho ya Yesu Kristo. Mzee M. Russell Ballard ametoa ushauri huu muhimu, ambao mimi nauunga mkono: “Mwamini Bwana. Yeye ni Mchungaji Mwema. Anawajua kondoo Wake. … Kama hatutajishughulisha, wengi ambao wangesikia ujumbe wa Urejesho watakuwa wamepitwa. … Kanuni ni rahisi sana—sali, binafsi, na katika familia yako, kwa ajili na fiursa za umisionari.”3 Tuonyeshapo imani yetu fursa hizi zitakuja bila “nguvu yoyote au… majibu ya kukataa Zitatiririka kama matokeo halisi ya upendo wetu kwa kaka na dada zetu.”4
Mimi najua hili ni kweli. Nami naongeza ahadi yangu kwamba kwa imani katika msaada wa Bwana, tutaelekezwa, tutaongozwa, na kupata furaha kubwa katika kazi hii yenye umuhimu wa milele ya upendo. Tutakuja kuelewa kwamba ufanisi katika kishiriki injili ni kuwaalika watu kwa upendo na nia safi ili kuwasaidia wao, bila kujali mjibizo wao.
III.
Hapa ni baadhi ya mambo mengine tunayoweza kufanya ili kufundisha injili kwa mafanikio.
-
Tunahitaji kukumbuka kwamba “watu hujifunza pale wawapokuwa tayari kujifunza, siyo tunapokuwa tayari kuwafundisha.”5 Kile tukipendacho sisi, kama vile mafundisho muhimu ya ziada katika Kanisa la urejesho, kwa kawaida siyo kile ambacho wengine wapendacho. Wengine ni dhahiri kabisa wanapenda matokeo ya mafundisho, na siyo mafundisho yenyewe. Kadiri wanavyoangalia au wanavyoguswa na athari za injili ya urejesho ya Yesu Kristo katika maisha yetu, wanaguswa na Roho na kuanza kuvutiwa na mafundisho. Wanaweza pia kuvutiwa wanapokuwa wanatafuta furaha zaidi, ukaribu na Mungu, au uelewa bora juu ya madhumuni ya maisha.6 Kwa hiyo ni lazima kwa uangalifu na kwa sala tutafute utambuzi juu ya namna ya kuomba juu ya mtu mwingine avutiwe kujifunza zaidi. Hii itategemea mambo kadhaa, kama vile hali ya mazingira ya sasa ya mtu huyo na uhusiano wetu na yeye. Hili ni mada zuri kulijadili katika mabaraza, akidi, na katika Miungano ya Usaidizi ya Kina Mama.
-
Tuongeapo na wengine, tunahitaji kukumbuka kwamba mwaliko wa kujifunza zaidi juu ya Yesu Kristo na injili Yake ni mwaliko wa kujifunza juu ya Kanisa letu.7 Tunataka watu waongolewa katika injili. Hii ndiyo nafasi kuu ya Kitabu cha Mormoni. Hisia juu ya Kanisa hufuata wongofu kwa Yesu Kristo; haziitangulii hili. Wengi wenye wasi wasi na makanisa hata hivyo wana upendo kwa Mwokozi. Weka vitu vya kwanza, kwanza.
-
Tutafutapo kuwatambulisha watu katika injili ya urejesho tunapaswa kufanya hili katika njia hali na kumjali kwa upendo mtu huyo. Hii hutokea pale tunapojaribu kuwasaidia wengine wenye matatizo wameyatambua au wakati tunapofanya kazi nao katika kuhudumia jamii, kama vile kupunguza dhiki, kuwajali maskini na wenye shida, au tunapoboresha maisha ya wengine.
-
Jitihada zetu za kufundisha injili hazipaswi kuishia kwenye mzunguko wa marafiki zetu na washirika tu. Wakati wa Olimpiki tulijifunza kwamba dereva wa teksi MSM huko Rio De Janeiro ambaye alikuwa akibeba vitabu vya Mormoni katika lugha saba tofauti na alitoa kimoja kwa yeyote ambaye angekipokea. Yeye alijiita “teksi dereva mmisionari” Alisema, “Mitaa ya Rio De Janeiro ndiyo … eneo [langu] la misheni”8
Clayton M. Christensen, ambaye ana uzoefu wa kuvutia kama muumini mmisionari, anaelezea kwamba “kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita, tumechunguza kwamba hakuna uwiano kati ya kina cha uhusiano na uwezekano kwamba mtu atavutiwa katika kujifunza juu ya injili.”9
-
Uaskofu wa kata unaweza kupanga kuwa na mkutano rasmi wa sakramenti ambao katika mkutano huo waumini wanaweza kuombwa kuwaleta watu wanaovutiwa. Waumini wa kata hawatasita kuwaleta marafiki zao kwenye mkutano wa namna hiyo kwa sababu watakuwa na uhakika zaidi kwamba yaliyomo katika mkutano yatapangiliwa vizuri kuleta mvutio na kuwasilisha Kanisa vyema.
-
Kuna fursa nyingine nyingi za kufundisha injili. Kwa mfano, kiangazi hiki tu nilipokea barua ya furaha kutoka kwa muumini mpya ambaye aliijua injili ya urejesho pale mwanafunzi mwenzake wa zamani alipompigia simu ili kumwulizia juu ya maradhi yaliyokuwa yamempata. Aliandika: “Nilielielimishwa kwa jinsi alivyojitambulisha kwangu kwanza. Baada ya miezi michache ya kujifunza kutoka kwa wamisionari, nikabatizwa. Misha yangu yameboreka tanga hapo.”10 “Sote tunawajua wengi ambao maisha yao yangeboreshwa na injili ya urejesho. Je, tunawafikia hao?
-
Uvutiwaji na ustadi wa waumini wetu vijana katika vyombo vya habari vya kijamii huwapa wao fursa za kipekee za kuwagusa na kuwavutia wengine katika injili. Akielezea kuonekana kwa Mwokozi kwa Wanefi, Mormoni anaandika, “Aliwafundisha na kuwahudumia watoto …, na akalegeza ndimi zao … kwamba wakaweza kunena”(3 Nefi 26:14). Leo nadhani tungesema “legeza vidole vyao ili waweze kunena.” Endeleeni, vijana!
Kushiriki injili si mzigo bali ni furaha. Kile tunachoita “kazi ya umisionari kwa waumini” si mpango lakini ni mtazamo wa upendo na fursa ya kuwafikia wale waliotuzunguka. Pia ni fursa ya kushuhudia jinsi tunavyojisikia juu ya injili ya urejesho ya Mwokozi wetu. Kama Mzee Ballard alivyofundisha, “Ushahidi wa wongofu wetu unaoonekana wazi zaidi na juu ya namna tunavyojisikia juu ya injili katika maisha yetu ni utayari wetu wa kushiriki injili na wengine.”11
Ninashuhudia juu ya Yesu Kristo, ambaye ndiye Nuru na Uzima wa Ulimwengu (ona 3 Nefi 11:11 Injili Yake ya urejesho huangaza njia yetu hapa ulimwenguni. Upatanisho Wake hutupa sisi uhakika wa maisha baada ya kifo na nguvu ya kun’gan’gania kuelekea maisha ya milele. Na Upatanisho Wake hutupa sisi fursa ya kusamehewa dhambi zetu na, chini ya mpango mtukufu wa wokovu, kufuzu kupata uzima wa milele, “zawadi kuu katika zawadi zote za Mungu”(M&M 14:7). Katika jina la Yesu Kristo, amina.