2010–2019
Bwana Mponyaji
Oktoba 2016


13:0

Bwana Mponyaji

Huna haja ya kupata uzoefu wa huzuni unaosababishwa na dhambi, maumivu yaliyosababishwa na wengine, au uhalisi wa maumivu ya maisha ya duniani—peke yako.

Mojawapo ya nafasi zenye thawabu kwangu ni kusafiri----kujifunza kutoka kwa dada zangu ulimwenguni kote. Hakuna kitu cha ajabu kama kufanya kazi bega bega, ana kwa ana, moyo kwa moyo pamoja nanyi.

Wakati mmoja wa uzoefu kama huu, kiongozi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, aliuliza, “Kuna kitu mahususi ambacho Wanawake hawana budi kukizingatia?”

Nilimjibu, “ndiyo” hotuba ya Rais Russell M. Nelson ya “Ombi kwa Dada Zangu” ilipoingia akilini mwangu. Rais Nelson alifundisha, “Tunahitaji wanawake walio na uelewa imara wa mafundisho ya Kristo.”1

Nefi alielezea mafundisho ya Kristo kwa njia hii:

“Kwani lango ambalo mtaingilia ni toba na ubatizo kwa maji; na kisha unakuja msamaha wa dhambi zenu kwa moto kwa Roho Mtakatifu. …

Na sasa, … nauliza je, yote yamekamilishwa? “Tazama, nawaambia, Hapana; kwani hamjafika hapa ila tu kwa neno la Kristo na kwa imani isiyotingishika ndani yake, mkitegemea kabisa ustahili wa yule aliye mkuu kuokoa.

Kwa hivyo, lazima msonge mbele mkiwa na imani imara katika Kristo, mkiwa na mng’aro mkamilifu wa tumaini, na upendo kwa Mungu na wanadamu wote. Kwa hivyo, kama mtasonga mbele, mkila na kusherekea neno la Kristo, na mvumilie hadi mwisho, tazama, hivi ndivyo asema Baba: Mtapokea uzima wa milele.

“… Hii ndiyo njia; na hakuna njia nyingine wala jina lililotolewa chini ya mbingu ambalo mwanadamu anaweza kuokolewa katika ufalme wa Mungu. Na sasa, tazama, hili ndilo fundisho la Kristo.2

Kwa nini tunahitaji uelewa imara wa kanuni hizi?

Kila mara nakutana na wanawake Watakatifu wa Siku za mwisho wenye mahitaji makubwa ya msaada, bali hawamgeukii Yule anayeweza kutoa msaada wa milele. Kila mara wanakosa uelewa wa kina wa fundisho la Kristo na kutafuta uelewa kwa kutafuta “lile jengo kubwa na pana.”3

Tunapoongeza uelewa wetu wa fundisho la Kristo, sisi punde tuttagundua uelewa wa kina wa “mpango mkuu wa furaha.”4 Pia tunatambua kwamba Mwokozi wetu, Yesu Kristo, yupo katika kiini haswa cha mpango huu.

Tunapojifunza jinsi ya kutumia fundisho la Kristo kwenye hali zetu binafsi, upendo wetu kwa Kristo utakua. Na tutatambua kwamba “bila kujali tofauti zinazofahamika, sisi wote tunahitaji Upatanisho ule ule usio na mwisho.”55 Tunatambua kwamba Yeye ni msingi wetu— “mwamba wa Mkombozi wetu, … msingi imara, msingi  … ambao juu yake kama [sisi] tukijenga [sisi] hatuwezi kuanguka.”6

Jinsi gani fundisho hili linaweza kutubariki tunapotafuta amani na uelewa na kujitahidi kuvumilia kwa furaha katika safari zetu za duniani za kipekee?

Naomba nipendekeze kwamba tuanze, kama Nefi anavyosema, “na kwa imani isiyotingishika ndani yake [Kristo], mkitegemea kabisa ustahili wa yule aliye mkuu kuokoa.”7 Imani yetu katika Yesu Kristo inatuwezesha kupambana na changamoto yoyote.

Sisi, kwa kweli, mara nyingi tunakuta imani yetu imeongezeka na uhusiano wetu na Baba wa Mbinguni na Mwanae umetakaswa katika dhiki. Wacha nishirikishe mifano mitatu.

Kwanza, Mwokozi, Bwana Mponyaji, ana uwezo wa kubadili mioyo yetu na kutupa ahuweni ya kudumu kutoka huzuni iliyosababishwa na dhambi zetu wenyewe. Wakati Mwokozi alipomfundisha mwanamke Msamaria kisimani, alijua kuhusu dhambi zake kubwa. Hata hivyo, “Bwana hutazama katika moyo,”8 na pia Yeye alijua alikuwa na moyo wa kufundishika.

Wakati mwanamke alipokuja kisimani,Yesu—mfano halisi wa maji ya uhai—alisema kirahisi, “Nipe ninywe.” Mwokozi wetu vile vile atasema kwetu katika sauti tunayoitambua wakati tunapokuja Kwake—kwani anatujua. Hukutana nasi pale tulipo. Na kwa sababu ya vile alivyo na nini alichokifanya kwa ajili yetu, Yeye anaelewa. Kwa sababu amepata uzoefu wa maumivu yetu, Yeye anaweza kutupa maji ya uzima wakati tunapoyatafuta. Alifundisha haya kwa mwanamke Msamaria aliposema, “Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.” Hatimaye akielewa, mwanamke alijibu kwa imani na akaomba, “Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu.”

Baada ya mwanamke Msamaria kupata uzoefu huu na Mwokozi, “akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu,

Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?

Alikuwa amepokea ushahidi—ameanza kunywa maji ya uhai—alitamani kushuhudia utukufu wa uungu Wake kwa wengine.9

Tunapokuja Kwake kwa mioyo ya unyenyekevu na ya kufundishika—hata kama mioyo yetu ni mizito kwa makosa, dhambi, na kuvunja amri—Yeye anaweza kutubadili, “kwani ni mwenye uwezo mkubwa wa kuokoa.”10 Na kwa mioyo iliyobadilika, tunaweza kama mwanamke Msamaria—kwenda ndani ya miji yetu wenyewe—nyumba zetu, shule zetu,na sehemu zetu za kazi kushuhudia juu Yake.

Pili, Bwana Mponyaji anaweza kutufariji na kutuimarisha tunapohisi maumivu kwa sababu ya vitendo visivyo vya haki vya wengine. Nimekuwa na mazungumzo mengi na wanawake waliolemewa na mizigo mizito. Njia yao ya agano kutoka hekaluni imekuwa safari ngumu ya uponyaji. Wanateseka kutokana na maagano yaliyovunjika, mioyo iliyovunjika, na matumaini yaliyopotea. Wengi ni waathiriwa wa uasherati na matusi ya kijinsia yenye mhemuko, kila mara kama matokeo ya utawaliwa mbaya wa watu wengine.

Matukio haya, ingawa sio kosa lao wenyewe, yamewaacha wengi wakijisikia wenye makosa na kuaibika. Bila kujua jinsi ya kusimamia mihemuko yenye nguvu wanayoipata, wengi wanajaribu kuizika, wakiisukuma kina kirefu ndani yao wenyewe.

Tumaini na uponyaji haupatikani katika lindi kuu la giza la usiri lakini katika nuru na upendo wa Mwokozi wetu, Yesu Kristo,11 Mzee Richard G. Scott alishauri: “Kama wewe uko huru [umejizuia] dhambi kubwa wewe mwenyewe, usiteseke bure kwa ajili ya matokeo ya dhambi za wengine. … Unaweza kuhisi huruma. … Tena usijichukulie mwenyewe hisia za uwajibikaji kwa vitendo hivyo. … Utakapokuwa umefanya kile kilicho cha kutosha kumsaidia yule umpendae, weka mzigo miguuni pa Mwokozi. … Unapotenda hivyo, sio tu utapata amani bali itaonyesha imani yako katika uwezo wa Mwokozi kuchukua mzigo wa dhambi kutoka kwa mpendwa wako kupitia toba yake na utii.”

Aliendelea: “Uponyaji kamili utakuja kupitia imani yako katika Yesu Kristo na nguvu na uwezo Wake, kupitia Upatanisho Wake, kuponya makovu ya kile kisicho cha haki na kisicho stahili.”12

Kama unajikuta katika hali hii, uponyaji unaweza kuwa njia ndefu. Utahitaji kwamba utafute mwongozo na msaada ufaao, ikijumuisha kusahuriana na wenye ukuhani waliotawazwa  kikamilifu. Unapowasiliana kwa uwazi, weka mipaka ya kufaa, na pengine tafuta ushauri wa weledi. Kudumisha afya ya kiroho katika njia yote ni muhimu na ni lazima! Kumbuka utambulisho wako mtakatifu: wewe ni binti mpendwa wa Wazazi wa Mbinguni. Amini mpango wa milele wa Baba yako kwa ajili yako. Endelea kila siku kuongozea uelewa wako wa fundisho la Yesu Kristo. Tumia imani kila siku kunywa zaidi kutoka kisima cha Mwokozi cha maji ya uzima. Utegemee juu ya endaumenti ya nguvu iliyopatikana kwa kila mmoja wetu kupitia ibada na maagano. Na ruhusu nguvu ya uponyaji ya Mwokozi na Upatanisho Wake ndani ya maisha yako.

Tatu, Bwana Mponyaji anaweza kutufariji na kutuhimili tunapopitia maumivu “uhalisia wa maisha ya duniani,”13 kama vile majanga, ugonjwa wa akili, magonjwa, maumivu ya kudumu, na kifo. Hivi karibuni nimemfahamu msichana wa ajabu anaeitwa Josie ambaye anaeteseka na mfadhaiko kupita kiasi. Hapa ni kidogo tu ya safari yake kuelekea uponyaji wakati alipoishiriki nami:

“Ubaya wa giza huatokea kwa kile mimi na familia yangu na tunachukulia kuwa ‘siku za sakafuni.’ Inaanza na ujazo mkubwa wa fahamu na kiwango kikali cha hisia na upinzani kwa aina yoyote ya sauti, mguso, au mwanga. Ni kilele cha maumivu makali ya akili. Kuna siku moja hasa ya sakafuni ambayo sitaisahau kamwe.

“Ilikuwa mwanzo katika safari, ikifanya uzoefu hasa kuwa wa kutisha. Naweza kukumbuka kulia machozi yakitiririka usoni mwangu nilipokuwa natweta nikipania hewa. Lakini hata maumivu haya makali yaliyofifia akifananishwa na maumivu ambayo yalifuata nilipoona hofu kubwa ikimzidi mama yangu, akiwa anakata tamaa kunisaidia.

“Kwa akili zangu zilizovurugika ukaja moyo wake uliovunjika. Lakini tusichojua ni kwamba licha ya giza nene, tulikuwa muda mfupi tu kabla kupata muujiza mkubwa.

“Wakati saa moja ndefu ikiendelea, mama yangu alinong’ona tena na tena na tena, ‘Nitafanya chochote kuchukuwa hiki toka kwako.’

“Hata hivyo, giza lilizidi, na wakati niliposadiki siwezi kuendelea zaidi, wakati ule ule ndipo kitu cha ajabu kilitokea.

“Nguvu za miujiza na za ajabu ghafla ziliingia mwilini mwangu. Kisha, kwa ‘nguvu zaidi ya uwezo wangu,’14 nilitamka kwa mama yangu kwa uthibitisho mkubwa maneno saba ya kubadilisha maisha kama jibu la tamaa yake ya kubeba maumivu yangu. Nilisema, ‘Huna haja ya kufanya hivyo; mtu fulani tayari amefanya.’”

Kutoka lindi kuu la giza la kudhoofisha ugonjwa wa akili, Josie alijipatia nguvu zaidi kushuhudia juu ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Hakuponywa kabisa siku ile, lakini alipokea nuru ya tumaini katika muda wa giza kali. Leo, akitegemea uelewa imara wa fundisho la Kristo na kufanywa mpya kila siku na maji ya uzima ya Kristo, Josie anaendelea katika safari yake kuelekea kuponywa na kutumia imani isiyotikisika katika Bwana Mponyaji. Anawasaidia wengine njiani. Na anasema, “Wakati giza linaonekana kuendelea, nategemea kumbukumbu ya rehema Zake ororo. Inakuwa kama nuru ya kuongoza ninapotafuta njia kupitia muda mgumu,”15

Kina dada, nashuhudia kwamba—

Huna haja ya kuendelea kubeba mzigo wa huzuni iliosababishwa na dhambi—peke yako.

Huna haja ya kubeba maumivu yaliyosababishwa na matendo yasiyo ya haki ya wengine—peke yako.

Huna haja ya kupata uzoefu wa uhalisi wa maumivu ya maisha ya duniani—peke yako.

Mwokozi anasihi:

“Je mtarudi kwangu sasa, na kutubu dhambi zenu, na kugeuka ili niwaponye?

“… Nawaambia, ikiwa mtakuja kwangu, mtapata uzima wa milele. Tazama, mkono wangu wa rehema umenyoshwa kwenu, na yeyote atakayekuja … nitampokea.”16

“[Yeye] atafanya chochote kuchukua haya kutoka kwenu.” Kwa kweli, “[Yeye] tayari amefanya hivyo.” Katika jina la Yesu Kristo, Bwana Mponyaji amina.