Toba Chaguo la Furaha
Toba haiwezekani tu bali pia ni furaha kwa sababu ya Mwokozi wetu.
Nilipokuwa na umri wa miaka 12, familia yangu iliishi Goteborg, mji wa mwambao wa kusini mwa Sweden. Kwa kuwafahamisha, huu ni miji wa nyumbani wa mwenzetu mpendwa Mzee Per G. Malm,1 ambaye aliaga msimu huu wa kiangazi. Tunamkosa. Tunashukuru kwa ajili ya ungwana wake na huduma yake ya kingwana na kwa ajili ya mfano wa familia yake ya kupendeza. Na kwa hakika tunawaombe baraka bora zaidi ziwe zao.
Miaka hamsini iliyopita, tulihudhuria kanisa katika boma kubwa, lililokarabatiwa. Jumapili moja, rafiki yangu Steffan,2 shemasi mmoja pekee katika tawi, alinisalimia kanisani kwa msisimko kiasi. Tulikwenda kwenye eneo wazi la kanisa, na akatoa mfukoni mwake fataki kubwa na viberiti kadhaa. Kwa tendo la ujasiri wa kujitia la ujana, nilichukua fataki lile na kuwasha fyuzi ndefu ya rangi ya kijivu. Niliazimia kuzima ile fyuzi kabla haijalipuka. Lakini nilipochomeka vidole vyangu kwa kujaribu kufanya hivyo, niliangusha lile fataki. Steffan na mimi tulitazama kwa hofu fyuzi ilipoendelea kuchomeka.
Fataki ililipuka, na mvuke wa salfa ukajaza eneo wazi na kanisa. Kwa haraka tulikusanya mabaki ya fataki yaliyotawanyika na kufungua madirisha ili kujaribu kutoa harufu nje, kwa utoto tukitumaini kwamba hakuna mtu ambaye angejua. Kwa bahati nzuri, hakuna mtu aliyejeruhiwa na hakuna uharibifu uliofanyika.
Waumini walipokuja kwenye mkutano, waliweza kutambua harufu kali. Ilikuwa ni vigumu kuikosa. Harufu ilivuruga hali takatifu ya mkutano. Kwa sababu kulikuwa na mashemasi wawili tu, na katika kile kinachoweza tu kuelezwa kama wazo la kukaidi—nilipitisha sakramenti, ilihali sikuweza kuhisi kustahili kuipokea. Wakati trei ya sakramenti ilipowekwa kwangu, sikuchukua mkate wala maji. Nilihisi vibaya. Nilipatwa na aibu, na nilijua kuwa kile nilichokifanya kilimchukiza Mungu.
Baada ya kanisa, rais wa tawi, Frank Lindbergh, mtu mzee anayeheshimika, mwenye nywele ya kijivu, akaniuliza niende ofisini mwake. Baada ya kuketi chini, alinitazama kwa upole na kusema kuwa aliona kuwa sikuwa nimepokea sakramenti. Akauliza ni kwa nini. Nilishuku alijua ni kwa nini. Nilikuwa na hakika kila mtu alijua kile nilichofanya. Baada ya kumwambia, aliuliza jinsi nilivyohisi. Kupitia kwa machozi, nilimwambia kwa wasiwasi nikaomba msamaha na kwamba nilijua nilimkosea Mungu.
Rais Lindbergh alifungua nakala mzee ya Mafundisho na Maagano na akaniuliza nisome aya fulani zilizokuwa zimepigwa mistari. Nilisoma yafuatayo kwa sauti:
“Tazama, yule ambaye ametubu dhambi zake, huyu anasamehewa, na Mimi, Bwana, sizikumbuki tena.
“Kwa hili mnaweza kujua kama mtu ametubu dhambi zake—tazama, ataungama na kuziacha.”3
Kamwe sitasahau tabasamu lenye huruma la Rais Lindbergh nilipoangalia juu baada ya kumaliza kusoma. Kwa hisia kiasi, aliniambia kuwa alijisikia kuwa itakuwa vyema kwangu kuendelea kupokea sakramenti. Nilipotoka ofisini mwake, nilihisi furaha isiyoelezeka.
Furaha kama hiyo ni moja ya matokeo asili ya toba. Neno tubu linaonyesha “kujua baadaye” na linaonyesha “mabadiliko.”4 Kiuswidi, neno ni omvänd, ambayo inamaanisha “kugeuka kote.”5 Mwandishi Mkristo, C. S. Lewis, aliandika kuhusu haja na mbinu ya mabadiliko. Alisema kuwa toba inahusisha “kuwekwa tena katika njia sawa. Hesabu mbaya inaweza kuwekwa sawa: lakini tu kwa kurudi nyuma hadi upate kosa na kulirekebisha upya kutoka sehemu hiyo, kamwe si kwa kuendelea.”6 Kubadili tabia yetu na kurejea “njia sahihi” ni sehemu ya toba, bali ni sehemu tu. Toba halisi pia inajumuisha kugeuka kwa moyo wetu na mapenzi kwa Mungu na kutubu dhambi.7 Kama ilivyoelezwa katika Ezekieli kutubu ni “kugeuka kutoka … dhambi, … kutenda yaliyo halali na haki; … kurudisha rehani, … [na] kutembea katika sheria za uzima, asitende uovu wo wote.”8
Lakini hata haya ni maelezo pungufu. Hayaelezei vizuri nguvu inayowezesha toba, dhabihu ya upatanisho ya Mwokozi wetu. Toba halisi lazima ihusishe imani katika Bwana Yesu Kristo, imani kwamba Yeye anaweza kutubadilisha, imani kwamba Yeye anaweza kutusamehe, na imani kwamba Yeye atatusaidia kuepuka makosa zaidi. Aina hii ya imani hufanya Upatanisho Wake kuwa hai katika maisha yetu. “Tunapojua baadaye” na “kugeuka kutoka” kwa usaidizi wa Mwokozi, tunaweza kuhisi matumaini katika ahadi Zake na furaha ya msamaha. Bila mkombozi, matumaini haya ya asili na furaha ya toba ni mabadilisho tu tabia duni. Lakini kwa kudhihirisha imani Kwake, tunaongoka kwa uwezo Wake na utayari wa kusamehe dhambi.
Rais Boyd K. Packer alidhihirisha ahadi zenye matumaini za toba mnamo Aprili 2015 katika mkutano mkuu wake wa mwisho. Alielezea uwezo wa Upatanisho wa Mwokozi wa kupona katika kile ninachokitambua kama utakasaji wa hekima uliopatikana katika nusu karne ya huduma ya kitume. Rais Packer alisema: Upatanisho hauwachi alama, hakuna mabaki. Kinachoponya, hupona … Hupona tu, na kile huponya hubakia kimepona.”9
Aliendelea:
“Upatanisho, ambao unaweza kutudai sote, hauna makovu. Hiyo ina maana kwamba bila kujali kile tumefanya au mahali tumekuwa au jinsi kitu kilivyotokea, tukitubu kikweli, [Mwokozi] ameahidi kwamba Yeye atapatanisha. Na wakati Yeye alipopatanisha, hiyo ilimaliza hayo. …
“Upatanisho … unaweza kusafisha safi kila doa bila kujali jinsi lilivyo sugu au muda gani au ni mara ngapi limerudiwa.”10
Mfiko wa Upatanisho wa Mwokozi hauna mwisho kwa upana na kina, kwa ajili yako na yangu. Lakini kamwe hautalazimishwa juu yetu. Kama vile nabii Lehi alivyoeleza, baada ya sisi “kushauriwa kikamilifu” kwamba “tujue mema na maovu,”11 uko “huru kuchagua uhuru na uzima wa milele, kupitia kwa Mpatanishi mkuu wa watu wote, au kuchagua utumwa na kifo.”12 Kwa maneno mengine, toba ni chaguo.
Tunaweza—na wakati mwingine—kufanya maamuzi tofauti tofauti. Chaguzi kama hizo haziwezi kuonekana mbaya tokea mwanzo, lakini zinatuzuia sisi kujuta kweli na hivyo kuzuia utekelezaji wetu wa toba ya kweli. Kwa mfano, tunaweza kuchagua kuwalaumu watu wengine. Kama kijana wa miaka 12 katika Goteborg, ningeweza kumlaumu Steffan. Alikuwa ndiye aliyeleta ile fataki kubwa na viberiti kanisani kwanza. Lakini kuwalaumu wengine, hata kama ni haki, kunaturuhusu kutetea tabia zetu. Kwa kufanya hivyo, tunahamisha wajibu wa matendo yetu kwa wengine. Wakati wajibu umehamishwa, tunapunguza haja na uwezo wetu wa kutenda. Tunajigeuza wenyewe kuwa waathirika wa bahati mbaya, badala ya mawakala wenye uwezo wa kutenda huru.13
Uchaguzi mwingine ambao unazuia toba ni kupuuza makosa yetu. Katika tukio la fataki la Goteborg, hakuna mtu aliyejeruhiwa, hakuna uharibifu wa kudumu uliotokea, na mkutano ulifanyika hata hivyo. Ingekuwa rahisi kusema kwamba kulikuwa hakuna sababu ya kutubu. Lakini, kupuuza makosa yetu, hata kama hakuna madhara yaliyo dhahiri, huondosha hamasa ya mabadiliko. Wazo hili hutuzuia kuona kwamba makosa yetu na dhambi zina madhara ya milele.
Inavutia kufikiri kwamba dhambi zetu si kitu kwa sababu Mungu anatupenda bila kujali kile tumefanya. Kuna majaribu kuamini kile Nehori mlaghai aliwafundisha watu wa Zarahemla: “Kwamba wanadamu wote wataokolewa katika siku ya mwisho, na kwamba haistahili waogope au kubabaika … na, mwishowe, wanadamu wote watapokea uzima wa milele.”14 Lakini wazo hili potovu ni la uongo. Mungu anatupenda. Hata hivyo, kile tunachofanya kinajalisha Kwake. Ametoa maelekezo ya wazi kuhusu jinsi tunapaswa kuishi. Tunaita hizi amri Idhinisho lake na uzima wetu wa milele hutegemea tabia zetu, ikiwemo utayari wetu wa kutafuta toba ya kweli kwa unyenyekevu.15
Tunaacha toba halisi tunapochagua kumtenganisha Mungu na amri Zake. Hata hivyo, ikiwa sakramenti sio takatifu, haingejalisha kwamba harufu ya fataki ilikuwa sumbufu katika mkutano huo wa sakramenti wa Goteborg. Tunapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu kupuuza tabia ya dhambi kwa kudhoofisha au kupuuza uandishi wa Mungu wa amri Zake. Aidha, toba ya kweli inahitaji kutambua uungu wa Mwokozi na ukweli wa kazi Yake ya siku za mwisho.
Badala ya kufanya udhuru, hebu tuchague toba. Kupitia kwa toba, tunaweza kujirudia wenyewe, kama vile mwana mpotevu katika fumbo,16 na tutafakari juu ya umuhimu wa umilele wa matendo yetu. Tunapoelewa jinsi dhambi zetu zinaweza kuathiri furaha yetu ya milele, hatuwi tu wenye kujuta lakini pia kujitahidi kuwa bora zaidi. Tunapokabiliwa na majaribu, ni rahisi tujiulize, kwa maneno ya William Shakespeare:
Ninashinda nini kama nikipata kitu nitafutacho?
Ndoto, pumzi, povu ya furaha ya kidunia:
Ni nani hununua furaha ya dakika ili kuomboleza wiki yote?
Au anauza umilele ili kupata mwanasesere?17
Kama tumepoteza mwelekeo wa milele kwa ajili ya mwanasesere, tunaweza kuchagua kutubu. Kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, tuna nafasi nyingine. Kisitiari, tunaweza kubatilisha kidude cha kuchezea tulichokinunua kwa ushauri mbaya zaidi na kupokea tena matumaini ya milele. Kama Yeye alivyoeleza “Kwani, tazama, Bwana Mkombozi wako aliteseka hadi kifo katika mwili; kwa hiyo aliteseka maumivu ya watu wote, ili kwamba watu wote waweze kutubu na kuja kwake.”18
Yesu Kristo anaweza kusamehe kwa sababu alitoa thamana kwa ajili ya dhambi zetu.19
Mkombozi wetu huchagua kusamehe kwa sababu ya huruma, rehema, na upendo Wake usio na kifani.
Mwokozi wetu anataka kusamehe kwa sababu hii ni moja ya sifa zake za kiungu.
Na, kama Mchungaji Mwema aliye, anafurahi tunapotubu.20
Hata tunapohisi huzuni wa kiungu kwa matendo yetu,21 tunapochagua kutubu, mara moja tunamkaribisha Mwokozi katika maisha yetu. Kama Amuleki alivyofundisha, “Mje mbele na msishupaze mioyo yenu mara nyingine; kwani tazama, sasa ndio wakati na siku ya wokovu wenu; na kwa hivyo ikiwa mtatubu, na msishupaze mioyo yenu, mara moja mpango mkuu wa ukombozi utatimizwa kwenu.”22 Tunaweza kuhisi huzuni wa kiungu kwa matendo yetu na kwa wakati huo huo kuhisi furaha ya kuwa na usaidizi wa Mwokozi.
Ukweli kwamba tunaweza kutubu ni habari njema ya injili!23 Hatia inaweza kufagiliwa mbali.24 Tunaweza kujawa na shangwe, kupata ondoleo la dhambi zetu, na kuwa na amani ya dhamiri.”25 Tunaweza kuwa huru kutokana na hisia za kukata tamaa na utumwa wa dhambi Tunaweza kujazwa na mwanga wa ajabu wa Mungu na kutokuwa na “maumivu tena.”26 Toba haiwezekani tu bali pia ni furaha kwa sababu ya Mwokozi wetu. Bado nakumbuka hisia ambazo zilinitakasa katika ofisi ya rais wa tawi baada ya tukio la fataki. Nilijua nilikuwa nimesamehewa. Hisia za hatia zilitoweka kabisa, sononeko langu likaondolewa, na moyo wangu ukawa mwepesi.
Ndugu zangu, tunapohitimisha mkutano huu, nawakaribisheni mhisi furaha zaidi katika maisha yenu: furaha katika ufahamu kwamba Upatanisho wa Yesu Kristo ni halisi; furaha katika uwezo wa Mwokozi, utashi, na hamu ya kusamehe; na furaha katika kuchagua kutubu. Hebu tufuate maelekezo ya Mwokozi “kwa furaha … tuteke maji katika visima vya wokovu.”27 Hebu tuchague kutubu, tuziache dhambi zetu, ili kuigeuza mioyo yetu na mapenzi yetu ili kumfuata Mwokozi. Nashuhudia uhalisi wa uhai Wake. Mimi ni shahidi na mpokeaji wa fadhila Zake zisizo na kifani, rehema na upendo. Naomba kwamba baraka za ukombozi za Upatanisho Wake ziwe zenu sasa—na tena na tena na tena katika maisha yenu yote.28 kama vile imekuwa katika maisha yangu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.