Kwa Ajili ya Maendeleo Yetu ya Kiroho na Kujifunza
Mafumbo ya Mungu hufunuliwa kwetu sisi kulingana tu na mapenzi Yake na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Nilipokuwa kijana mdogo, wazazi wangu walipokea zawadi ambayo ilikuja kutuvutia sana mimi na kaka yangu mdogo David. Zawadi hiyo ilikuwa ni mfano mdogo wa mabamba ya dhahabu ambayo Nabii Joseph Smith alipokea kutoka kwa malaika Moroni. Ninavyokumbuka, mfano huo wa mabamba ulikuwa na kurasa za bati zipatazo 10 au zaidi zilizokuwa na maneno juu yake. Hata hivyo, kurasa hizo sizo zilizotuvutia sisi.
Tulikuwa tumelewa tukisikia hadithi za Urejesho. Tulijua na tulikuwa tukiimba katika madarasa ya Msingi juu ya mabamba ya dhahabu yaliyofichwa chini katika upande wa mlimani na kutolewa na malaika Moroni kwa kumpa Joseph Smith.1 Kadiri udadisi wa akili zetu za ujana ulivyochochewa, kulikuwa na kitu kimoja ambacho hakika tulitamani kuona nini kilikuwa kimeandikwa juu ya sehemu ile ndogo ya mfano wa mabamba iliyo kuwa imefungwa kwa uthabiti kwa kamba ndogo mbili za bati?
Mabamba yale yalikaa kwenye pembe ya meza kwa siku kadhaa kabla ya udadisi wetu haujatushinda. Ingawa sisi kwa uwazi kabisa tulielewa kwamba haya hayakuwa mabamba halisi ambayo Moroni aliyatoa, sisi tulitaka kuiona ile sehemu iliyofungwa. Hivyo katika nyakati kadhaa, kaka yangu na mimi tulijaribu kwa kutumia visu vya kupakia siagi, vijiko vizee, na kitu kingine chochote tulichofikiri kingeweza kutenganisha sehemu ya mabamba iliyofungwa kiasi tu cha kutosha kuona kilichomo ndani—pasipo kuvunja zile kamba ndogo. Tulikuwa makini vya kutosha kutoacha alama ya udadisi utovu wa uvulana. Cha kukatisha tamaa na mkanganyiko, majaribio haya ya “kuchunguza mabamba yale” daima hayakuwa na mafanikio.
Bado mimi sijui nini—kama kilikuwepo chochote—kilichofichwa chini ya sehemu ile iliyofungwa. Lakini kitu cha kutia aibu katika hadithi yetu ni kwamba hadi siku ya leo, sina wazo lolote kuhusu ni nini kiliandikwa juu ya sehemu ile ya kurasa zile za bati ambazo zilikusudiwa zisomwe. Ninaweza tu kukisia kwamba kurasa zile zilikuwa na hadithi za Urejesho na shuhuda za Joseph Smith na za Mashahidi Watatu na wale Wanane, ambao waliona mabamba halisi ambayo Moroni aliyatoa.
Tangu kuumbwa kwa dunia, Baba wa Mbinguni mwenye upendo ametoa maelekezo, uongozi na mafundisho kwa watoto Wake kwa njia ya manabii. Maneno Yake yameridhiwa kupitia kwa manabii hawa na yamehifadhiwa kama maandiko kwa maendeleo yetu na kujifunza. Nefi anaelezea hilo kwa njia hii:
“Kwani nafsi yangu hufurahia katika maandiko, na moyo wangu huyatafakari, na nayaandika kwa ajili ya kujifunza na kwa faida ya watoto wangu.
“Tazama, nafsi yangu hufurahia katika mambo ya Bwana; na moyo wangu hutafakari daima juu ya mambo ambayo nimeyaona na kusikia.”2
Zaidi ya hayo, katika vipindi vya injili vilivyopita na katika kipindi hiki cha mwisho cha utimilifu wa nyakati, waumini wa Kanisa la Bwana wastahili wamebarikiwa kwa kuwa pamoja na Roho Mtakatifu daima, ambaye hutusaidia katika maendeleo yetu ya kiroho na katika kujifunza.
Nikijua bidii ya asili ya kaka mdogo wangu, ninataswiri kwamba alisoma maneno yale yote yaliyokuwa yameandikwa juu ya mfano ule wa mabamba nyumbani mwa wazazi wetu. Mimi , hata hivyo nilipuuza kweli zile za wazi na za thamani na badala yake nilitumia jitihada zangu katika kutafuta mambo yale ambayo hayakukusudiwa kufunuliwa.
Kwa huzuni, maendeleo na kujifunza kwetu yawezekana nyakati zingine yakacheleweshwa au hata kusimamishwa kwa tamaa mbaya ya “kuchunguza mabamba.” Vitendo hivi vinaweza kutupeleka sisi katika kutafuta vitu ambavyo si lazima tuvijue kwa wakati huu, wakati huo wote tukipuuza kweli zenye kupendeza ambazo zimekusudiwa kwa ajili yetu na kwa mazingira yetu—kweli ambazo Nefi anaelezea kama zimeandikwa kwa ajili ya kujifunza na kwa faida yetu.
Yakobo kaka ya Nefi alifundisha: “Tazama, kazi za Bwana ni kuu na za kushangaza. Namna gani ilivyo vigumu kuchunguza kina cha siri zake; na ni vigumu kwa mwanadamu aweze kugundua njia zake zote.”3
Maneno ya Yakobo yanatufundisha kwamba hatuwezi kwa mafanikio “kupekua mabamba” au kulazimisha siri za Mungu zifunuliwe kwetu. Badala yake, siri za Mungu hufunuliwa kwetu tu kulingana na mapenzi Yake na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.4
Yakobo anaendelea:
“Na hakuna mtu ajuaye njia zake isipokuwa zimefunuliwa kwake; kwa hiyo, ndugu zangu, msidharau mafunuo ya Mungu.
“Kwani tazama, kwa nguvu ya neno lake mwanadamu akaja juu ya uso wa dunia hii. … Ee kama ndiyo, kwa nini asiweze kuamuru dunia, au kazi za mikono yake juu ya uso wa dunia hii, kulingana na mapenzi na matakwa yake?
“Kwa hiyo, ndugu zangu, msitafute kumshauri Bwana, lakini kupata ushauri toka mkononi mwake.”5
Ili kuelewa siri za Mungu , au mambo yale ambayo yanaweza kueleweka tu kupitia ufunuo, ni lazima tufuate mfano wa Nefi, ambaye alisema, “Nikiwa bado mdogo sana, lakini hata hivyo nikiwa na umbo kubwa, na pia nikiwa na hamu kubwa ya kujua siri za Mungu, hivyo basi, nilimlilia Bwana; na tazama akanitembelea mimi, na aliulainisha moyo wangu kiasi kwamba niliamini maneno yote yaliyonenwa na baba yangu ”6 Bwana mwenyewe ameelezea zaidi kwamba Nefi ameonyesha imani, na kwa bidii amemtafuta kwa moyo mnyoofu, na ameshika amri Zake.7
Mfano wa Nefi wa kutafuta maarifa inajumuisha (1) hamu ya kweli, (2) unyenyekevu, (3) sala, (4) kumwamini nabii, na kufanyia kazi(5) imani, (6) bidii, na (7) utiifu. Mbinu hii ya kutafuta kwa kiasi kikubwa ni tofauti na “kuchunguza kwangu yale mabamba” au kujaribu kulazimisha kuelewa mambo yaliyokusudiwa kufunuliwa kulingana na wakati wa Bwana na kwa kupitia uwezo wa Roho Mtakatifu
Katika wakati huu wa kisasa, tumekuja kutegemea kuwa maarifa yanaweza na yanapaswa yapatikane mara moja, wakati ambapo taarifa haifahamiki kwa urahisi au kupatikana kwa urahisi, daima imekuwa ikitupiliwa mbali au haiaminiki. Kwa sababu ya wingi wa taarifa, baadhi bila kufahamu hukubali vyanzo vilivyopo pasipo kujua asili yake kuliko kutegemea utaratibu uliowekwa na Bwana kwa ajili ya kupokea ufunuo binafsi. Yakobo yawezekana alikuwa akielezea wakati wetu aliposema: “Lakini tazama, [wao] walikuwa watu wenye shingo ngumu; na walidharau maneno yaliyo wazi … na walitafuta mambo ambayo wao hawakuweza kuelewa. Kwa hiyo, kwa sababu ya upofu wao, upofu ambao ulikuja kwa kutazama ng’ambo ya alama, ilikuwa lazima wao waanguke; kwani Mungu aliondoa uwazi wake kutoka kwao, na kuleta kwao mambo mengi ambayo hawakuweza kuelewa, kwa sababu wao walitamani hilo.”8
Kwa namna nyingine Rais Dieter F. Uchtdorf anashauri. Yeye alizungumzia juu ya wamisionari, lakini maneno yake yanawafaa sawa wale wote watafutao ukweli “Wakati …Wamisionari wanapokuwa na imani katika Yesu Kristo” alisema, “watamwamini Bwana kiasi cha kutosha kufuata amri Zake—hata kama wao hawaelewi kabisa sababu ya amri hizo. Imani yao itajidhihirisha kwa njia ya bidii yao na kwa njia ya matendo yao.”9
Wakati wa mkutano mkuu wa Aprili iliyopita, Mzee Dallin H. Oaks alielezea: “Kanisa linafanya jitihada kubwa kuwa wazi kwa rekodi tulizonazo, lakini baada ya kuchapisha zote tulizonazo, waumini wetu wakati mwingine wameachwa na maswali ya msingi ambayo hayajibiki kwa kujifunza. … Mambo mengine yanawezekana kujifunza tu kwa njia ya imani.”10
Manabii wa kale walifundisha kanuni hiyo hiyo, wakionyesha kwamba kwa muda mrefu asili ya binadamu haijabadilika na kwamba utaratibu wa Bwana juu ya kujifunza hauna muda. Fikiria juu ya methali hii ya Agano la Kale: “Amini katika Bwana kwa moyo wako wote; usiegemee sana kwenye uelewa wako binafsi.”11
Isaya alieleza, akisema kwa ajili ya Bwana, “Kwani kama mbingu zilivyo juu zaidi kuliko dunia, na hivyo ndivyo njia zangu zilivyo juu zaidi kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko yenu.”12
Nefi aliongeza ushahidi mwingine wakati alipotangaza, “Ee Bwana, nimekutegemea wewe, na nitakutegemea wewe milele.”13
Imani na kutumaini katika Bwana tunahitajika sisi kukiri kwamba hekima Yake ni kuu kuliko yetu sisi. Lazima pia tutambue kwamba mpango Wake hutupa uwezekano mkubwa wa maendeleo yetu ya kiroho na kujifunza.
Hatukuwa kamwe tukitarajiwa “kuwa na [elimu] kamilifu ya mambo” wakati wa maisha ya hapa duniani. Badala yake, tumetarajiwa “kutumaini vitu visivyoonekana, ambavyo ni vya kweli.”14
Hata kwa imani kubwa ya Nefi, alikiri uelewa wake mdogo wakati alipomjibu yule malaika aliyemwuliza, “Je, wewe wajua ufadhili wa Mungu?” Nefi akajibu “ Mimi, najua kwamba anawapenda watoto wake; hata hivyo, Mimi sijui maana ya vitu vyote.”15
Vivyo hivyo, Alma alimweleza mwanawe Helamani, “Sasa siri hizi hazijajulishwa kwangu kwa ukamilifu; kwa hiyo nitavumilia.”16
Ninaelezea ushahidi wangu kwamba Baba yetu aliye Mbinguni anawapenda watoto Wake, lakini bado kama Nefi na Alma, Mimi sijui maana ya mambo yote. Wala sihitaji kujua mambo yote; mimi pia nitavumilia na na kumsubiri Bwana, nikijua “nina vitu vyote kama ushahidi kwamba hivi vitu ni kweli; na wewe pia una vitu vyote kama ushuhuda kwako kwamba ni vya kweli. …
“… Maandiko yamewekwa mbele yako, ndio, na vitu vyote vinaonyesha kwamba kuna Mungu; ndio, hata dunia, na vitu vyote vilivyo juu yake, ndio, na mwendo wake, ndio, na pia sayari zote ambazo huenda kwa utaratibu wao zinashuhudia kwamba kuna Muumba Mkuu.”17
Tunapotambua kwamba tumeundwa kwa ustadi wa Baba wa Mbinguni mwenye hekima na upendo, “ Ee, basi,” kwa nini tusimruhusu Yeye aongoze maendeleo yetu ya kiroho na kujifunza kwetu “kulingana na mapenzi na matakwa Yake” kuliko yetu wenyewe?18
Yeye yu Hai. Yesu Kristo ni Mwanaye wa Pekee na Mkombozi wa wanadamu. Kwa sababu ya Upatanisho Wake usio na mwisho, Yeye anayo hekima na ni mwenye uwezo wa kuona vyema ili atuongoze katika siku hizi za mwisho. Joseph Smith ni nabii Wake, aliyechaguliwa kurejesha ufalme Wake ulimwenguni kwa ukamilifu wake. Thomas S. Monson ni nabii Wake anayeishi na msemaji Wake leo. Juu ya haya natoa ushahidi wangu wa dhati katika jina la Yesu Kristo, amina