2010–2019
Kamwe Hatutatembea Peke Yetu
Oktoba 2013


2:3

Kamwe Hatutatembea Peke Yetu

Wewe siku moja utasimama kando na kutazama nyakati zako ngumu, na utagundua kwamba Yeye alikuwa daima kando yako.

Dada zangu wapendwa, roho tunayehisi jioni hii ni onyesho la nguvu zenu, uchaji wenu, na wema wenu. Kumnukuu Bwana: “Ninyi ni chumvi ya dunia. … Ninyi ni nuru ya ulimwengu.”1

Kama nilivyotafakari juu ya nafasi yangu ya kuwahutubia, nimekumbushwa juu ya upendo wa mke wangu mpendwa, Frances, aliokuwa nao juu ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Wakati wa maisha yake alihudumu katika nyadhifa nyingi katika Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Wakati yeye nami tulikuwa umri wa miaka 31, mimi niliitwa kama Rais wa Misheni ya Kanada. Katika miaka mitatu ya kazi hiyo, Frances alisimamia Miungano ya Usaidizi wa Kina Mama yote katika ili eneo kubwa, linalojumuisha mikoa ya Ontario na Quebec. Marafiki zake wengi wa karibu walikuja kwa sababu ya kazi hiyo, vile vile kutokana na wito mwingi ambayo yeye alikuja kuitwa katika Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama wa kata yetu wenyewe. Yeye alikuwa binti mwaminifu wa Baba yetu wa Mbinguni, mwenzi mpwendwa wangu, na rafiki yangu wa dhati. Ninamkosa sana kushinda vile maneno yanaweza kueleza.

Mimi pia naupenda Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Nashuhudia kwenu kwamba ulianzishwa kupitia maongozi na ni sehemu muhimu ya Kanisa la Bwana hapa juu ya ulimwengu. Haingewezekana kukisia wema wote ambao umekuja kutokana na shirika hili na nafsi zote ambazo zimebarikiwa kwa sababu yake.

Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama unajumuisha aina mbali mbali ya wanawake. Kuna wale kati yenu ambao ni waseja labda mko shuleni, labda mmeajiriwa---na hali mnajenga maisha kamili na bora. Wengine wenu mu kima mama wa watoto wanaokuwa mlio na shughuli nyingi. Hali wengine wenu mmepoteza waume wenu kwa sababu ya talaka au kifo na mnajishughulisha kulea watoto lakini mmegundua kwamba mahitaji yao kwa usaidizi wako bado yanahitajika. Kuna wengi wenu ambao mna wazazi wakongwe ambao wanahitaji utunzaji wenye upendo ambao ninyi tu ndiyo mtatoa.

Popote tulipo katika maisha, kuna nyakati ambapo sisi sote tuna changamoto na taabu. Ingawa ni tofauti kwa kila mmoja, ni kawaida kwa wote.

Nyingi za changamoto tunazokabiliana nazo zipo kwa sababu tunaishi katika hii dunia ya muda, iliyo na aina zote za watu. Nyakati zingine tunauliza kwa kukata tama, Je! Ninaweza vipi kukaza mtazamo wangu kwenye selestia kama mimi safari katika dunia hii ya telestia?”

Kutakuwa na nyakati ambapo ninyi mtatembea katika njia iliyozagaa miiba na iliyo na taabu. Kunaweza kuwa na nyakati ambapo utahisi kutengwa---hata kuzaiwa---kutoka kwa Mtoa wa kila kipawa kizuri. Una hofu kwamba unatembea peke yako. Badilisha hofu kwa imani.

Unapojipata katika hali kama hizi, nakusihi ukumbuke maombi. Nayapenda maneno ya Rais Ezra Taft Benson kuhusu maombi. Alisema:

“Kote katika maisha yangu ushauri huu wa kutegemea maombi umekuwa wa thamani zaidi kupita ushauri mwengine wowote mimi … nishapokea. Umekuwa sehemu yangu muhimu---nanga, chanzo thabiti cha nguvu, na msingi wa elimu yangu ya vitu vitukufu. …

“… Ingawa kinyume hutokea, katika maombi tunaweza kupata hakikisho, kwani Mungu ataongea imami kwenye nafsi. Imani ile, roho ya utulivu ile, ni baraka kuu ya maisha.”2

Mtume Paulo alishauri hivi:

“Acheni haja zenu na zijulikane na Mungu.

“Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”3

Ni ahadi tukufu jinsi gani! Imani ndiyo kile sisi tunatafuta, ndiyo kile sisi tunatamani.

Hatuwekwa hapa ulimwenguni kutembea peke yetu. Ni chanzo cha ajabu jinsi gani cha uwezo, cha nguvu na cha faraja kunachopatikana kwa kila mmoja wetu. Yeye ambaye anatujua sisi vyema kuliko sisi tunavyojijua wenyewe, Yeye ambaye huona taswira yote na ambaye anajua mwisho kutoka mwanzo, ametuhakikishia kwamba Yeye atakuwepo kwa ajili yetu ili kutoa usaidizi kama tutaomba tu. Sisi tuna ahadi: “Ombeni daima, na muwe wenye kuamini, na mambo yote yatafanyika kwa pamoja kwa faida yenu.”4

Maombi yetu yanapopaa mbinguni, acha sisi tusisahau maneno tuliyofunzwa na Mwokozi. Wakati alipokabiliana na uchungu mkali sana wa Gethasemane na kwenye msalaba, Yeye aliomba kwa Baba, “Si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.”5 Vigumu kama inavyoweza kuwa nyakati zingine, ni juu yetu, pia kuamini kwamba Baba yetu wa Mbinguni anajua kilicho bora jinsi na lini na katika njia gani ya kutoa usaidizi tunaotafuta.

Nayapenda maneno ya mshairi:

Sijui kwa mbinu gani adimu

Bali hili mimi najua: Mungu hujibu maomnbi.

Najua kwamba Yeye ametoa ahadi Yake

Ambalo huniambia maombi daima usikika

Na yatajibiwa, punde au badaye,

Basi mimi uomba na kungojea kwa utulivu.

Sijui ikiwa baraka zilizombwa

Zitakuja tu katika njia ninayofikiria,

Bali huancha maombi yangu na Yeye peke yake

Mapenzi yake ni ya hekimu kuliko yangu,

Nikiwa na hakikisho Yeye atapatia maombi yangu,

Au atatuma jibu fulani la baraka nyingi sana. .6

Bila shaka, maombi si tu kwa nyakati za shida. Tumeambiwa kila mara katika maandiko “tuombe daima”7 na tuweke maombi katika mioyo yetu.8 Maneno ya wimbo unaoenziwa na unaojulikana unauliza swali ambalo sisi tungejiuliza wenyewe kila siku: Je! Nilifikiria kuomba?”9

Mwenzi pamoja na maombi katika kutusaidia kujimudu katika dunia yetu ambayo kila mara huwa ni ngumu ni mafunzo ya maandiko. Maneno ya ukweli na maongozi yanayopatikana katika nguzo zetu nne ni mali ya thamani kwangu. Mimi kamwe sichoki kuyasoma. Mimi huinuliwa kiroho ninapoyapekua maandiko. Haya maneno matakatifu ya ukweli na upendo hutoa mwongozo kwa maisha yangu na kuelekeza njia hata ukamilisho wa milele.

Tunaposoma na kutafakari maandiko, tunapata uzoefu wa mnong’ono mtamu wa Roho hata kwa nafsi zetu. Tunaweza kupata majibu ya maswali yetu. Tutajifunza juu ya baraka ambazo huja kupitia kuweka amri za Mungu. Tutapata ushuhuda thabiti juu ya Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na juu ya upendo Wao kwetu. Mafunzo ya maandiko yanapotumika pamoja na maombi yetu, tunaweza kujua kwa uhakika kwamba injili ya Yesu Kristo ni ukweli.

Rais Gordon  B. Hinckley alisema, “Na Bwana hubariki kila mmoja wetu kusherekea maneno yake matakatifu na kupata kwao nguvu zile, amani ile, na elimu ile ‘ambayo inapita ufahamu wote’ (Wafilipi. 4:7).”10

Tunapokumbuka maombi na kuchukua muda wa kugeukia maandiko, maisha yetu yatabarikiwa bila kipimo na mizigo yetu itafanywa kuwa miepesi.

Acha mimi nishiriki nanyi tukio la jinsi Baba yetu wa Mbinguni alijibu maombi na kusihi kwa mwanamke mmoja na kumpatia amani na hakikisho ambalo yeye alikuwa ametafuta kwa moyo sana?

Shida za Tiffany zilianza mwaka jana wakati alipopata wageni nyumbani kwake kwenye sherehe ya Shukrani na kisha tena wakati Krismasi. Mumewe alikuwa amehitimu kutoka shule ya matibabu na sasa alikuwa katika mwaka wake wa pili kama daktari mkazi. Kwa sababu ya masaa mengi yanayohitajiwa kutoka kwake, yeye hakuweza kumsaidia kama vile wao wote wangependa, na basi mengi ya yale yalihitajika kufanywa wakati wa kipindi cha sikukuu, na juu ya utunzaji wa watoto wadogo wao wanne, ulimwangukia Tiffany. Akawa amelemewa sana, na akagundua kwamba mmoja ambaye anampenda sana aligunduliwa kuwa na saratani. Matatizo na hofu vikamzonga na hata akaingia katika kipindi cha kuvunjika moyo na mfadhaiko. Alitafuta msaada wa daktari, nab ado hakuna lolote lililobadilika. Hamu yake ya chakula ikapotea, na akaanza kupoteza uzito, ambavyo umbo lake dogo halingeweza kumudu. Akatfuta amani kupitia maandiko na kuomba ukombozi kutoka na huzuni huu ambao ulikuwa umemlemea. Wakati amani wala msaada hulionekana kutokuja, alianza kuhisi kutelekezwa na Mungu. Familia na marafiki zake walimwombea na walijaribu sana kwa moyo kusaidia. Walimletea chakula alichokuwa anakipenda sana katika kujaribu kumpatia afya ya mwili, lakini aliweza kumega kidogo tu na kisha alishindwa kumaliza.

Katika siku moja iliyokuwa ngumu hasa, rafiki alijaribu bila mafanikio kumvutia na chakula ambacho alikuwa anakipenda sana. Ilipoonekana kuwa jaribo halikuangua chochote, rafiki alisema, “Lazima kuna kitu fulani ambacho kinaonekana kizuri kwako.”

Tiffany alifikiria kwa muda mchache na kusema, “Kitu kile tu ninaweza kufikiria kinaonekana kwa kizuri ni mkate wa kuoka nyumbani.”

Lakini hakukuwa na wowote karibu.

Mchana uliofuata kengele ya mlango wa Tiffany ililia. Mumewe alikuwa nyumbani wakati huo na alienda kufungua. Wakati aliporudi, alikuwa amebeba boflo ya mkate wa kuoka nyumbani. Tiffany alishangaa sana wakati alimwambia kuwa imetoka kwa mwanamke anayeitwa Sherrie, ambaye hakuwa anamfahamu sana. Alikuwa rafiki ya Nicole, dadake Tiffany, ambaye aliishi Denver, Colorado. Sherrie alikuwa ametambulishwa kwa Tiffany na mumewe kwa kifupi sana miezi kadhaa mapema wakati Nicole na familia yake walikuwa wanakaa pamoja na Tiffany wakati wa sikukuu ya Shukrani. Sherrie, ambaye anaishi Omaha, alikuwa amekuja kutembelea nyumba ya Tiffany pamoja na Nicole.

Sasa, miezi baadaye, akiwa na mkate mtamu mkononi, Tiffany alimpigia simu Nicole dadake ili kushukuru kwa kumtuma Sherrie kwenye kazi ya rehema. Badala yake, aligundua Nicole hakuwa ametumana na hakujua chochote juu yake.

Hadithi yote inafumbuliwa Nicole anapomuuliza rafiki yake Sherrie kujua ni nini kilichomchochea yeye kupeleka ile boflo ya mkate. Kile alichogundua kilikuwa ni maongozi kwake, kwa Tiffany---na ni maongozi kwangu.

Asubuhi hiyo ya kupeleka mkate, Sherrie alikuwa amepata msukumo wa kuoka boflo mbili za mkate badala ya mmoja ambao alikuwa amepanga kuoka. Alisema kwamba alihisi msukumo wa kubeba boflo ya pili katika gari lake siku hiyo, ingawa hakujukua kwa nini. Baada ya chakula cha mchana katika nyumba ya rafiki yake, bintiye wa mwaka mmoja alianza kulia na alihitaji kurudishwa nyumbani ile alale. Sherrie alisita wakati hisia za wazi zilimjia kwamba anahitaji kupeleka boflo ya mkate ya ziada kwa dadake Nicole, Tiffany, ambaye aliishi safari ya dakika thelathini upande mwengine wa mji na ambaye hakuwa anamfahamu vyema. Alijaribu kurazini wazo hilo, akitaka kumpeleka bintiye aliyechoka sana nyumbani na kuhisi haya kuhusu kupeleka boflo ya mkate kwa watu ambao walikuwa wageni sana. Hata hivyo, msukumo wa kwenda kwa nyumba ya Tiffany ulikuwa mzito, basi akafuata msukumo huu.

Alipofika, mumewe Tiffany ndiye alifungua mlango. Sherrie alimkumbusha kwamba yeye alikuwa rafiki ya Nicole ambaye walikutana kwa muda mfupi katika sherehe za sikukuu ya Shukrani, na akampatia boflo ya mkate, na kuondoka.

Na kama ilivyotendeka kwamba Bwana alimtuma mgeni kabisa kuvuka mji ili kuleta na si tu mkate wa kuoka nyumbani uliotamaniwa lakini ujumbe wazi wa upendo kwa Tiffany. Kile kilichomtendekea hakiwezi kuelezewa kwa njia yoyote ingine. Alikuwa na haja ya dharura ya kuhisi kwamba yeye hakuwa peke yake---kwamba Mungu alikuwa anajua hali yake na hakuwa ametelekeza yeye. Ule mkate---kitu kile kile alichokuwa anataka---kililetwa kwake na mtu ambaye hakumfahamu vizuri, mtu ambaye hakuwa anajua mahitaji yake, lakini alisikiliza msukumo wa Roho na kufuata msukumo ule. Ikawa ishara ya wazi kwa Tiffany kwamba Baba yake wa Mbinguni anajua mahitaji yake na anampenda yeye ya kutosha hata kutumausaidizi. Yeye alijibu kilio chake cha kuomba msaada.

Dada zangu wapendwa, Baba yako wa Mbinguni anawapenda---kila mmoja wenu. Upendo huu haubadiliki. Hauvutiwi na sura zako, na mali yako, au na kiasi cha fedha ulichonacho katika akaunti yako ya benki. Haubadilishwi na talanta na uwezo wako. Kwa urahisi upo hapo tu. Upo hapo kwa ajili yako wakati unahuzunika au una furaha, umevunjika moyo au umekosa matumaini. Upendo wa Mungu upo hapo kwa ajili yako hata kama unahisi unafaa au haufai upendo . Kwa urahisi upo hapo daima.

Tunapomtafuta Baba yetu wa Mbinguni kupitia maombi ya dhati, uaminifu na madhumuni, kujifunza maandiko kwa hima, ushuhuda wetu utapata nguvu na kukita mizizi. Tutajua upendo wa Mungu kwetu. Tutaelewa kwamba hatutembei peke yetu. Nawaahidi ninyi kwamba siku mmoja mtasimama kando na mtazame nyakati zenu za shida, na mtatambua kwamba Yeye daima alikuwa hapo kando yako. Mimi najua hii ni kweli katika kumpoteza mwenzi wangu wa milele---Frances Beverly Johnson Monson.

Mimi nawaachieni upendo wangu. Mimi nawaachieni baraka zangu. Mimi nawaachieni shukrani zangu kwa mema yote mnayotenda na kwa maishi mnayoishi. Kwamba mbarikiwe na kila kipawa kizuri ndiyo maombi yangu katika jina la Mwokozi na Mkombozi wangu, hata Yesu Kristo aliye Bwana, amina.