Funga Majeraha Yao
Ninaomba kuwa tuweze kujitayarisha kutoa huduma yoyote ya kikuhani ambayo Bwana ataweka kwetu katika safari yetu ya hapa duniani.
Sisi sote tumebarikiwa na jukumu kwa wengine. Kushikilia ukuhani wa Mungu ni kumwajibikia Mungu kwa uzima wa milele wa watoto Wake. Hiyo ni halisi, hiyo ni ajabu, na nyakati zingine hiyo inaweza kuhisika ya kushinda.
Kuna marais wa jamii ya wazee wanaosikiliza usiku wa leo ambao wanajua kile ninachomaanisha. Hapa kuna kile kilichotendeka kwa mmoja wenu. Kuna uwezekano kimewatendekea wengi wenu ---na zaidi ya mara moja. Utondoti unaweza kutofautiana, lakini hali ni sawa sawa.
Mzee usiyemjua vyema amekuuliza usaidizi. Umejua kwamba anafaa kuhamisha mke wake na mtoto mchanga mvulana kutoka kwa fleti pale wanapoishi hadi ingine karibu na hapo.
Yeye na mke wake walikuwa tayari wamemuomba rafiki kama anaweza kuwaazima lori kwa siku moja ili ahamishe nyumba yake na vitu vya kibinafsi. Rafiki aliwapa lori. Huyu baba kijana alianza kupakia vyombo vyote walivyomiliki kwenye lori, lakini baada ya dakika chache, yeye aliumia mgongo. Rafiki yake ambaye alikuwa amempa lori alikuwa na shughuli nyingi kuweza kumsaidia. Baba kijana alihisi kukata tama. Alikufikiria wewe, rais wa jamii ya ukuhani wake.
Wakati aliomba usaidizi, ilikuwa mapema mchana. Ilikuwa siku ambapo Kanisa ukutana jioni. Ulikuwa tayari umemuahidi kumsaidia mke wako na mradi ya nyumbani siku hiyo. Watoto walikuwa wamekuomba hufanye kitu pamoja na wao, lakini bado ulikuwa haujafanya hivyo.
Pia ulijua kwamba washiriki wa jamii yako, hasa wale waliokuwa waaminifu sana, wale kwa kawaida wewe huwaita kusaidia, walikuwa katika wakati mgumu sawa na ule wewe ulikuwa nao.
Bwana alijua kwamba mngekuwa na siku kama hizo wakati Yeye alikuita katika wadhifa huu, kwa hivyo Yeye alikupa hadithi ya kukutia moyo. Ni methali ya wenye ukuhani walio na mzigo mzito. Sisi wakati mwingine huiita hadithi ya Msamaria mwema. Lakini hasa ni hadithi ya mwenye ukuhani jasiri, katika hizi siku zenye shughuli nyingi za siku za mwisho.
Hadithi hii inalingana vyema na mtumishi wa ukuhani aliye na mzigo mzito. Kumbuka tu kwamba wewe ni Msamaria na si kuhani au Mlawi ambaye alimpita mtu aliyejeruhiwa.
Wewe unaweza kuwa haujafikiria kuhusu hii hadithi wakati unapokabiliana na changamoto kama hizo. Lakini naomba kuwa mtafanya hivyo wakati siku kama hizo zitakuja tena, kama vile hakika zitafanya hivyo.
Hatuambiwi katika maandiko kwa nini Msamaria alikuwa anasafiri katika barabara kutoka Yerusalemu hadi Yeriko. Hamna uwezekano kwamba alikuwa anajivinjari peke yake kwa vile alikuwa anajua kwamba wezi walikuwa wanavizia wale wasiofahamu. Alikuwa kwenye safari ya shughuli, na kama ilivyokuwa desturi, yeye alikuwa na punda pia mafuta na divai.
Katika maneno ya Msamaria, wakati alipomuona mtu aliyejeruhiwa alisimama, kwa sababu “yeye alikuwa na huruma.”
Zaidi hata ya kuhisi huruma tu, alifanya kitendo. Daima kumbuka vitu mahususi vya tukio hili:
“Akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
“Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.”1
Wewe na wenye kushikilia ukuhani ambao mmeitwa kuwaongoza mna angalau mahakikisho matatu. Kwanza, Bwana atakupa, ikiwa wewe utaomba, hisia za huruma ambazo Yeye huhisi kwa wale walio na mahitaji. Pili, Yeye atawapa na wengine, kama vile mwenye mkahawa, kuungana nanyi katika huduma yenu. Tatu, Bwana, kama vile msamaria Mwema, atawazawadia bila kipimo wale wote wanaojiunga katika kutoa msaada kwa wale walio na mahitaji.
Ninyi marais wa jamii kuna uwezekano mshatenda juu ya haya mahakikisho zaidi ya mara moja. Mmeshawauliza wengine wa ukuhani wa Bwana ili kusaidia, kwa imani kwamba watajibu kwa huruma. Hamtakuwa na hofu ya kuwauliza wale ambao walijibu mara nyingi katika siku zilizopita kwa sababu mnajua kwamba wao huhisi huruma mara moja. Mmewauliza wao mkijua kwamba katika siku zilizopita wao walihisi ukarimu wa Bwana wakati wao walichagua kusaidia. Mmeshawauliza baadhi ya wale tayari wana mzigo mzito sana, mkijua kwamba jinsi dhabihu ilivyo kubwa ndivyo zawadi ilivyo kubwa watakayopokea kutoka kwa Bwana. Wale ambao wameshasaidia hapo awali wameshahisi shukrani zisizo na kifani za Mwokozi.
Mnaweza kuwa pia mmepata maongozi kutomuomba mtu fulani kupakia na kupakua lile lori. Kama viongozi mnawajua washiriki wenu wa jamii na familia zao vyema. Bwana anawajua wao yyema kabisa.
Yeye anajua ni mke wa nani aliyekuwa karibu kizio cha kuvunjika kwa sababu mume wake amekuwa hapati muda wa kufanya kile yeye anahitaji kufanya ili kutunza mahitaji yake. Yeye anajua ni watoto gani ambao watabarikiwa kwa kumwona baba yao akienda mara ingine tena kusaidia wengine au ikiwa watoto walihitaji kuhisi kwamba wao wanafaa kupewa kipaumbele na baba zao hata yeye kutumia wakati na wao siku hiyo. Lakini Yeye pia anajua ni nani anayehitaji mwaliko wa kuhudumu lakini anaonekana kama siye anayeweza au anayependelea.
Huwezi kuwajua washiriki wote wa jamii yako vyema kabisa, lakini Mungu anawajua. Kwa hivyo, mnavyofanya hivyo mara nyingi sana, mmeomba kujua ni nani wa kumuuliza kuwasaidia wengine. Bwana anajua ni nani atakayebarikiwa kwa kuulizwa kusaidia na ni familia ya nani itakayobarikiwa kwa kutoulizwa. Huu ndiyo ufunuo unaoweza kutarajia kuja kwako mnavyoongoza katika ukuhani.
Niliona kile kilichotendeka nilipokuwa kijana. Mimi nilikuwa msaidizi wa kwanza katika jamii ya ukuhani. Askofu aliniita siku nyumbani kwetu. Alisema kwa alikuwa anataka mimi niandamane naye kumtembelea mjane aliyekuwa katika shida kuu. Yeye alisema ananiitaji mimi.
Nilipokuwa ninamgonja anichukue hapo nyumbani kwetu, nilifadhaika. Nilijua kwamba askofu alikuwa na washauri wenye nguvu na hekima. Mmoja wao alikuwa hakimu mashuhuri. Yule mwengine alimiliki kampuni kubwa na baadaye alipata kuwa Kiongozi mwenye Mamlaka. Askofu huyu wakati fulani angekuja kuhudumu kama Kiongozi mwenye Mamlaka. Kwa nini askofu huyu alikuwa anamwambia kuhani asiye na uzoefu, “Mimi nahitaji msaada wako”?
Vyema, sasa najua vyema kabisa kile ambacho angelisema kwangu: “Bwana ana haja ya kukubariki wewe.” Hapo nyumbani kwa mjane, nilimwona akimwambia yule mwanamke kwamba hatapata msaada wowote kutoka kwa Kanisa mpaka atakapojaza fomu ya bajeti yeye alimuacha nayo mapema. Njiani kwenda nyumbani alicheka juu ya kushangaa kwangu na kusema, “Hal, atakapothibiti matumizi yake ataweza kuwasaidia wengine.
Wakati mwingine, askofu alinichukua mimi pamoja naye hadi nyumba ya wazazi walevi ambao waliwatuma washichana wawili wadogo kukutana nasi mlangoni. Baada ya yeye kuongea na wale wasichana wawili, tuligeuka na kusema nami, “Hatuwezi kubadilisha janga hili katika maisha bali, lakini wanaweza kuhisi Bwana anawapenda.”
Jioni moja nyingine yeye alinichukua hadi nyumbani kwa mtu ambaye hakuwa amekuja kanisani kwa miaka mingi. Askofu alimwambia jinsi alimpenda yeye na jinsi kata ilikuwa inamhitaji yeye. Haikuonekana kuwa athari yoyote kwa mtu huyu. Lakini wakati huo, na kila wakati askofu alinichukua pamoja naye, ilikuwa athari kuu kwangu.
Hapana njia yoyote ninayoweza kujua askofu alikuwa ameomba ili kujua ni kuhani gani angebarikiwa na matembezi haya. Kuna uwezekano aliwachukua makuhani wengine pamoja naye mara nyingi. Lakini Bwana alijua siku moja nitakuwa askofu anayewaalika wale imani yao imeingia baridi kuja kwa joto la injili. Bwana alijua siku moja nitapewa jukumu la ukuhani kwa mamia na hata maelfu ya watoto wa Baba wa Mbinguni ambao wako katika dhiki ya mahitaji ya muda.
Ninyi wavulana hamwezi kujua vile vitendo ya huduma ya ukuhani ambavyo Bwana anawatayarishia ninyi kupeana. Lakini jukumu kuu la kila mwenye kushikilia ukuhani ni kutoa msaada wa kiroho. Sisi sote tuna jukumu hili. Linakuja na kuwa mshiriki wa jamii. Linakuja na kuwa mshiriki wa familia. Kama imani ya yeyote katika katika jamii yenu au familia yenu inashambuliwa na Shetani, mtahisi huruma. Sawa sawa na huduma na rehema zilizotolewa na Msamaria, ninyi pia mtawahudumia wao kwa zeri kwenye majeraha yao katika wakati wao wa mahitaji.
Katika huduma yenu kama wamisionari wa muda, mtaenda kwa maefu ya watu walio na haja kubwa ya kiroho. Wengi, mpaka mtakapowafunza wao, hamtajua hata kwamba walikuwa na majeraha ya kiroho ambayo, yakiwacha bila tiba, yatalete dhiki isiyo na mwisho. Ninyi mtaenda katika kazi ya Bwana kuwakomboa wao. Ni Bwana tu awezaye kufunga majeraha yao ya kiroho wanapokubali maagizo yanayoelekeza katika uzima wa milele.
Kama mshiriki wa jamii, kama mwalimu wa nyumbani, na kama mmisionari, hauwezi kuwasaidia watu kurekebisha uharibifu wa kiroho usipokuwa imani yako mwenyewe imechangamka. Hii humaanisha zaidi ya kusoma maandiko kila mara na kuomba juu yake. Maombi kwa dakika chache na kutupa macho katika maandiko si matayarisho ya kutosha. Hakikisho la kile unahitaji huja na ushauri huu kutoka kwa sehemu ya 84 ya Mafundisho na Maagano: “Wala msiwaze kabla nini cha kusema; bali yahifadhini katika akili zenu daima maneno ya uzima, nanyi mtapewa saa ile ile mtakayosema sehemu ile ambayo itakayokusudiwa kwa kila mtu.”2
Ahadi hiyo inaweza tu kudaiwa ikiwa sisi “tunathamini” maneno ya uzima na kufanya hivyo bila kusita. Sehemu ya kuthamini ya haya maandiko imemaanisha kwangu kuwa jambo la kuhisi kitu kuhusu maneno. Kwa mfano, ninapokwenda kujaribu kumsaidia mtu anayeyumbayumba katika imani yake kuhusu wito mtukufu wa Nabii Joseph Smith, hisia unirudia mimi.
Si tu maneno kutoka kwa Kitabu cha Mormoni. Ni hisia za hakikisho la ukweli ambao huja wakati ninaposoma hata mistari michache kutoka kwa Kitabu cha Mormoni. Siwezi kuahidi kwamba itakuja kwa kila mtu aliyeambukizwa na shaka kuhusu Nabii Joseph au Kitabu cha Mormoni. Mimi najua ya kwamba Joseph Smith ni Nabii wa Urejesho. Ninajua kwamba Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu kwa sababu nimekithamini.
Mimi najua kutokana uzoefu kwamba unaweza kupata hakikisho la ukweli kutoka kwa Roho kwa sababu umeshakuja kwangu. Wewe nami sharti tuwe na hakikisho kabla Bwana hajatuweka katika njia ya msafiri tunayempenda ambaye amejeruhiwa na maadui wa ukweli.
Kuna matayarisho mengine ambayo sharti tufanye. Ni silka ya uanadamu kuwa wagumu juu ya maumivu ya wengine. Hiyo ndiyo sababu moja ya kwa nini Mwokozi hufanya mengi ili kusimulia juu ya Upatanisho Wake na Yeye Mwenyewe kujichukulia maumivu na huzuni wa watoto wote wa Baba yetu wa Mbinguni ili kwamba Yeye aweze kujua jinsi ya kuwasaidia wao.
Hata wale walio bora kati watu walio na ukuhani wa Baba wa Mbinguni hakuwakufikia kiwango cha fadhila kwa urahisi. Mwenendo wetu wanadamu ni kukosa subira na yule mtu ambaye haoni ukweli ambao ni wazi kabisa kwetu. Ni lazima tuwe makini sana kwamba kukosa subira kwetu kusikaonekane kama kuhukumu au kukataa.
Tunapojitayarisha kutoa usaidizi kwa Bwana kama watumishi wa ukuhani Wake, kuna maandiko ya kutuelekeza. Yana kipawa tutakachohitaji kwa safari yetu, popote pale Bwana atatuma. Msamaria mwema alikuwa na hicho kipawa. Sisi tutakihitaji, na Bwana ametuambia jinsi ya kukipata:
“Lakini hisani ni upendo msafi wa Kristo, na inavumilia milele; na yeyote atakayepatikana nayo katika siku ya mwisho, itakuwa vyema kwake.
“Kwa hivyo, ndugu zangu wapendwa, ombeni kwa Baba kwa nguvu zote za moyo, kwamba mjazwe na upendo huu, ambao ametoa kwa wote ambao ni wafuasi wa kweli wa Mwana wake, Yesu Kristo; ili muwe wana wa Mungu; kwamba wakati atakapoonekana tutakuwa kama yeye, kwani tutamwona vile alivyo; ili tuwe na tumaini hili; ili tutakaswe hata vile alivyo mtakatifu.”3
Ninaomba kwamba tuweze kujitayarisha wenyewe ili kutoa huduma yoyote ya ukuhani ambayo Bwana anaweza kuiweka mbele yetu katika safari yetu duniani. Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.