2010–2019
Kuvutwa Karibu na Mungu
Oktoba 2013


10:22

Kuvutwa Karibu na Mungu

Mwokozi wetu anataka sisi tumpende Yeye kiukweli kiasi kwamba tutake kuweka sambamba mapenzi yetu na Yake.

Mjukuu wetu mwenye umri wa miaka sita, Oli,ambaye hupenda kuniita “Babu,” alikuwa achukuwe kitu fulani kutoka kwenye gari. Baba yake alikuwa amesimama ndani ya nyumba na, alifungua mlango wa gari kwa mbali, Oli bila kujuwa, na alipolikaribia, ndipo alilifunga tena wakati alipomaliza. Oli kisha alikimbilia ndani na tabasamu kubwa!

Familia yote ilimwuliza,”Uliwezaje kuufanya mlango wa gari ujifungue kwa ajili yako, kisha ujifunge tena?’ Yeye alitabasamu tuu.

Binti yetu, Mama yake, alisema, “Inawezekana ni kama Babu anavyofanya—inawezekana una nguvu za mazingaombwe kama yeye.

Wakati ilipotokea mara ya pili dakika chache baadaye, majibu yake kwa maswali yaliyofuata kuhusu uwezo wake mpya alioupata: “Inashangaza! Nafikiri ni kwa sababu Babu ananipenda na ni mmoja wa marafiki wangu wakubwa,na anani jali.

Nimebarikiwa kujua kikweli miujiza ya vitu ambayo vimetokea katika maisha ya Watakatifu waaminifu kote Afrika, Papua New Guinea, Australia, New Zealand, na visiwa vya bahari ya Pacific. Ninakubaliana na Oli—Nafikiri ni kwa sababu watu wale waaminifu wanajihisi sawa kuhusu Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi kama Oli anavyohisi kuhusu mimi. Wao wanampenda Mungu kama rafiki yao wa karibu, na Yeye huwatunza wao.

Wanashiriki wa Kanisa hili wanastahili, na wengi hupokea, ushuhuda wa kiroho na kufanya maagano matakatifu ya kumfuata Bwana. Na hata hivyo, baadhi humwendea bali wengine hawafanyi hivyo. Wewe uko katika kundi gani?

Mungu anafaa kuwa kitovu cha ulimwengu wetu---sehemu halisi ya makutano. Ndiye au Yeye wakati mwingine yuko mbali kutoka mawazo na nia ya mioyo yetu? (ona Mosia 5:13). Tahadhari ambayo sio tuu mawazo ya mioyo yetu ambayo ni muhimu lakini “nia.” Jinsi gani tabia na vitendo vyetu vinaonesha uadilifu wa nia zetu?

Kijana wetu Ben, alipokuwa na umri wa miaka 16 na akiongea katika mkutano wa kigingi, aliuliza swali: “utajisikiaje kama mtu fulani akikuahidi kitu fulani kila juma na asitimize ahadi?” aliendelea, “Tunachukua kwa umakini ahadi tunazofanya tunaposhiriki sakramenti na maagano ya kutii amri zake na siku zote kumkumbuka Yeye?”

Bwana anatupatia njia za kutusaidia kumkumbuka Yeye na nguvu Zake za kuidhinisha. Njia mojawapo ni kupitia ushirikiano wetu wa pamoja—dhiki Alma 32:6). ninapoangalia nyuma kwenye majaribu niliyokutana nayo, ni wazi kwamba yamesababisha kukua kwangu, uelewa, na huruma wangu.Vimenisogeza mimi karibu zaidi kwa Baba yangu wa Mbinguni na Mwanae, pamoja na ujuzi na kusafishwa vimeandikwa ndani ya moyo wangu.

Mwongozo na maelekezo yake ni muhimu. Alimsaidia kaka mwaminifu wa Yaredi kwa kutatua moja ya changamoto zake mbili wakati alipomwambia jinsi ya kupata hewa ndani ya mashua ambayo yalikuwa yamejengwa kwa imani (ona Etheri 2:20). Lakini, kiukweli, Bwana hakuacha kwa muda tu changamoto ambayo haikutatuliwa ya jinsi ya kutoa mwanga, lakini ndipo aliweka wazi kwamba Yeye, Bwana, ataruhusu majanga na majaribu ambayo yalihitaji utatuzi wake.Yeye, itakuwa ndiye angeupeleka upepe, mvua nyingi, na mafuriko (ona Etheri 2:23–24).

Kwa nini angefanya hivyo? Na kwa nini anaonya yeyote kati yetu kujiondoa kutoka chanzo cha hatari wakati angeweza kirahisi kuzuia hatari isitokee? Rais Wilford Woodruff alieleza hadithi ya kuonywa kiroho kuondoa behewa ambalo yeye, mke wake, na mtoto walikuwa wamelala, kumbe tu kugundua kwamba kimbunga muda mfupu baadaye kiling’oa mti mkubwa na kuuangusha mahali palepale ambapo behewa hapo mwanzo lilikuwa limesimama (ona Teachings of Presidents of the Church: Wilford Woodruff [2004], 47).

Katika mifano hii miwili, hali ya hewa ingeweza kurekebishwa kuziondoa hatari. Lakini sababu ni hii---badala ya kutatua tatizo mwenyewe, Bwana anatutaka sisi kujenga imani ambayo itatusaidia sisi kumtegemea Yeye katika kutatua matatizo yetu na kumwamini. Ndipo tutahisi upendo Wake zaidi muda wote, kwa nguvu zaidi, kwa uwazi zaidi, na kibinafsi zaidi. Tunakuwa tumeungana na Yeye na tunaweza kuwa kama Yeye. Sisi kuwa kama Yeye ni lengo Lake. Kiukweli ni utukufu Wake vilevile ni kazi Yake (ona Musa 1:39).

Mvulana alikuwa anajaribu kusawazisha sehemu yenye uchafu nyuma ya nyumba yake ili aweze kucheza pale pamoja na magari yake. Kulikuwa na jiwe kubwa lililokuwa linazuia kazi yake. Kijana alilisukuma na kulivuta kwa uwezo wake wote, lakini haikujalisha jinsi gani alivyojaribu kwa nguvu, jiwe halikuweza kusonga.

Baba yake aliangalia kwa muda kisha akaenda kwa kijana wake na kusema,”Unatakiwa utumie nguvu zako zote ili uondoe jiwe kubwa kama hili.”

Mvulana akajibu: “Nimetumia nguvu zangu zote!”

Baba yake akamsahihisha: “Hapana hujafanya hivyo. Hujaupata msaada wangu bado!”

Kisha waliinama chini pamoja na kuliondoa jiwe urahisi.

Baba wa rafiki yangu Vaiba Rome, rais wa kwanza wa kigingi cha Papua New Guinea, pia alifunzwa kwamba anaweza kumgeukia Baba yake wa Mbinguni wakati wa shida.Yeye na wanakijiji wenzake waliweza kuishi tuu kupitia mazao waliyolima. Siku moja, aliwasha moto ili kusafisha sehemu yake ya aridhi ya kilimo ya kijiji kwa ajili ya kupanda. Hata hivyo, muda mrefu wa joto ulikuwa umepita, na nyasi pamoja na miti ilikuwa imekauka sana. Kwa hiyo moto wake ukawa sawa kama ule wa Rais Thomas S. Monson, kama nabii wetu mwenyewe alivyoelezea katika mkutano mkuu uliopita (ona,” Utiifu huleta Baraka,” Ensign au Liahona, May 2013, 89–90). Ulianza kutapakaa kwenye aridhi yenye nyasi na vichaka, na katika maneno ya mwanawe, “moto mkubwa wa kutisha” ulitokea. Aliogopa kwamba wanakijiji wenzake na uwezekano wa kupotea mazao yao. Kama yangeharibiwa, atawajibika kwa sheria za kijiji. Akiwa hawezi kuuzima moto, ndipo akamkumbuka Bwana.

Na sasa nanukuu kutoka kwa mwanawe, rafiki yangu: “Alipiga magoti juu ya kilima katika vichaka na akaanza kuomba kwa Baba wa Mbiguni auzuwie ule moto. Ghafla kulitokea wingu kubwa jeusi juu ya pale alipokuwa anaomba, na ikanyesha kwa nguvu---lakini kule tu ambako moto ulikuwa unawaka. Alipoangalia kila upande kulikuwa na anga jeupe kila sehemu isipokuwa kule miale ya moto iliunguza. Hakuamini Bwana angemjibu mtu wa kawaida kama yeye, na akapiga magoti chini tena na akalia kama mtoto mdogo. Alisema ilikuwa ni hisia tamu sana” (ona Alma 36:3).

Mwokozi wetu anataka sisi kiukweli tumpende Yeye kiasi kwamba tutake kuweka sambamba mapenzi yetu na Yake. Ndipo tunaweza kuhisi upendo Wake na kujua utukufu Wake. Kisha ataweza kutubariki kama anavyotaka kufanya. Hii ilitokea kwa Nefi mwana wa Helamani, ambaye alifikia mahali Bwana alimwamini kikweli kweli na kwa sababu hiyo, aliweza kumbariki kwa vitu vyote alivyoomba (ona Helamani 10:4–5).

Katika Maisha ya Pi, kitabu cha kubuniwa cha Yann Martel, shujaa anazungumzia hisia zake kuhusu Kristo: “Sikuweza kumtoa kichwani mwangu. Na bado siwezi. Nilitumia siku tatu nzima kufikiri kuhusu Yeye. Na zaidi alivyonisumbua mimi, ni kidogo sana niliweza kumsahau. Na zaidi nilivyojifunza kuhusu Yeye, ni kidogo nilitaka kumwacha Yeye”([2001],57).

Hivi ndivyo hasa ninavyohisi kuhusu Mwokozi.Yuko karibu siku zote, hasa kwenye sehemu zilizowekwa wakfu na nyakati za shida; na wakati mwingine,wakati nisiotegemea, nahisi kama ananigongagonga kwenye bega kunijulisha ananipenda. Ninaweza kurudisha upendo huo kwa njia yangu isiyo kamilifu kwa kumpatia moyo wanguM&M 64:22, 34).

Takribani miezi michache iliyopita nilikaa na Mzee Jeffrey  R. Holland wakati anawapanga wamisionari kwenye Misheni zao. Wakati tunatoka alinisubiri, na tulipokuwa tunatembea aliweka mkono wake kwenye bega langu. Nilimwambia kuhusu yeye kufanya jambo kama hilihapo zamani huko Australia. Alisema, “Hii ni kwa sababu nakupenda!” Na nilijua kwamba ilikuwa kweli.

Ninaamini kwamba kama tungekuwa na upendeleo maalumu wa kutembea na miili yetu pamoja na Mwokozi kwamba tungeweza kuhisi mkono wake umewekwa juu ya mabega yetu kama vivyo. Kama wafuasi wakielekea Emau, mioyo yetu “ingewaka ndani yetu” (Luka 24:32). Huu ni ujumbe Wake: “Njoo na uone” (Yohana 1:39). Ni ya kibinafsi, ya kualika, na ya kukumbatia katika mwaliko wa kutembea pamoja na mkono wake ukizunguka mabega yetu.

Natuweze sote kuhisi na kujiamini kama Enoshi, kama inavyoonekana katika aya ya mwisho ya kitabu chake kifupi lakini chenye elimu kubwa: “Na ninafurahia siku ile ambayo huu mwili wenye kutokufa utajivika, na kusimama mbele yake, kisha nitaona uso wake kwa furaha, na ataniambia: Njoo kwangu, heri wewe, umetayarishiwa mahali katika nyumba za Baba yangu (Enoshi 1:27).

Kwa sababu ya wingi wa uzoefu na nguvu ambayo Roho ameshuhudia kwangu, Ninashuhudia bila shaka kwamba Mungu yu hai. Ninahisi upendo Wake. Ni hisia iliyo tamu sana. Natufanye kile kinachotakiwa kuweka sambamba mapenzi yetu pamoja na ya Kwake na kikweli kumpenda. Katika jina la Yesu Kristo, amina.