Je, Tunajua Kile Tulichonacho?
Maagizo na maagano ya ukuhani hutukubalisha kupokea ukamilifu wa baraka zilizoahidiwa kwetu na Mungu, zinazowezeshwa na Upatanisho wa Mwokozi.
Katika “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Urais wa Kwanza na Jamii ya Mitume Kumi na Wawili wanasema: “Binadamu wote---wa kiume na wa kike---wameumbwa katika mfano wa Mungu. Kila moja ni mwana na binti mpendwa wa wazazi wa mbinguni, na hivyo basi, kila moja ana asili ya kiungu na kudura.”1 Ili kupata kudura hii ya kiungu, kila mwana na binti wa Mungu anahitaji maagizo na maagano ya ukuhani.
Tunahitaji ubatizo. Tunapoingizwa katika maji ya ubatizo, tunaagana kuchukua jina la Kristo juu yetu, kila wakati tukimkumbuka, kutii amri Zake, na kumtumikia hadi mwisho, ili tuweze kila mara kuwa na Roho Wake kuwa nasi.2
Tunamhitaji karama za Roho Mtakatifu. Kupitia agizo hilo, sisi tunayekubaliwa uenzi wa Rohowa kila wakati. Rais Wilford Woodruff alifunza: Kila mwanaume au mwanamke ambaye huingia katika Kanisa la Mungu na kubatizwa kwa ondoleo la dhambi ana haki ya ufunuo, haki ya Roho ya Mungu, ya kuwasaidia wao katika kazi zao, katika usimamizi wa watoto wao, katika kushauri watoto wao na wale ambao wao wameitwa kusimamia. Roho Mtakatifu sio tu kwa wanaume, wala kwa mitume au manabii; ni wa kila mwanamume na mwanamke mwaminifu, na kwa kila mtoto aliyekomaa kutosha kupokea injili ya Kristo.”3
Tunahitaji kupokea endaumenti ya hekalu. Mzee M. Russell Ballard alisema: “Wanaume na wanawake wanapoenda hekaluni, wao hupewa nguvu sawa, ambayo kwa maelezo ni nguvu ya ukuhani. … Endaumenti kwa kweli ni karama ya nguvu.”4
Tunahitaji agano la kuunganisha, linaloelekeza kwa uzima wa milele, “karama kuu ya zote za Mungu.”5 Agano hili la ukuhani hupokelewa tu na mwanaume na mwanamke pamoja. Mzee Russell M. Nelson alifundisha, “Mamlaka ya Ukuhani yamerejeshwa ili kwamba familia ziweze kuunganishwa milele.”6
Tunahitaji fursa ya kufanya upya maagano yetu kila wiki tunapopokea sakramenti. “Manabii na mitume wa siku za Mwisho wamefundisha kwamba tunapopokea sakramenti kwa kustahili, tunafanya upya si tu agano letu la ubatizo mbali “maagano yote yaliyofanywa na Bwana.”7
Maagizo na maagano haya ya ukuhani hutukubalisha kupokea ukamilifu wa baraka zilizoahidiwa kwetu na Mungu, zinazowezeshwa na Upatanisho wa Mwokozi. Yanawaami wana na binti wa Mungu na nguvu, nguvu ya Mungu,8 na hutupatia fursa ya kupokea uzima wa milele---ili kurudi kwa uwepo wa Mungu na kuishi Naye katika familia Yake ya milele.
Hivi majuzi nilienda na viongozi wa ukuhani kutembelea nyumba za wanawake wanne kule Honduras. Akina dada hawa na familia zao walihitaji funguo na mamlaka ya ukuhani, maagizo na maagano ya ukuhani, na nguvu na baraka za ukuhani.
Tulimtembelea dada mpendwa ambaye ameolewa na ana watoto wawili warembo. Yeye ni mwaminifu na mhudhuriaji kamini Kanisani, na anafundisha watoto wake kuchagua mema. Mumewe anaunga mkono ushiriki wake Kanisani, lakini yeye si mshiriki. Familia yao ni imara, lakini ili kufurahia nguvu zaidi, wanahitaji Baraka zaidi za ukuhani. Wanahitaji baba kupokea maagano ya ubatizo na karama ya Roho Mtakatifu na apate kutawazwa katika ukuhani. Wanahitaji nguvu ya ukuhani ambayo inaweza kuja kupitia endaumenti na kuunganishwa.
Tembezi letu la pili lilikuwa kwa nyumba ya akina dada wawili ambao hawajaolewa, wanawake wa imani kuu. Mmoja ana mwana anayejitayarisha kuenda misheni. Dada yule mwingine anapokea matibabu ya saratani. Katika wakati wa kuvunjika moyo na kukata tamaa, wao hukumbuka Upatanisho wa Mwokozi na hujazwa na imani na tumaini. Wote wawili wanahitaji baraka za ziada na nguvu zinazopatikana kupitia maagano ya hekalu. Tuliwahimiza wajiunge na wamisionari wa siku za baadaye katika nyumba yao katika kujitayarisha kupokea baraka hizo.
Tembezi letu la mwisho lilikuwa kwa nyumba ya dada ambaye mumewe aliaga dunia hivi majuzi katika ajali mbaya. Mwongofu mpya wa Kanisa, hakuwa ameelewa kwamba angeweza kupokea endaumenti yake mwenyewe na kuunganishwa na mumewe. Tulipomfundisha kwamba baraka hizi zingeweza kupatikana kwa ajili yake na mumewe aliyefariki, alijawa na tumaini. Akiwa anajua kwamba kupitia maagizo ya hekalu na maagano familia yake inaweza kuunganishwa pamoja, ana imani na amedhamiri kukumbana na majaribio yaliyo mbele.
Mwana huyu wa mjane anajitayarisha kupokea Ukuhani wa Haruni. Kutawazwa kwake katika ukuhani kutakuwa baraka kuu kwake na kwa familia yake. Watakuwa na mwenye ukuhani katika nyumba yao.
Nilipokutana na wanawake hawa kule Honduras, niliona kwamba walikuwa wanajitahidi kuweka familia zao kuwa hai katika injili. Watoa shukrani kwa washiriki wa kata wanaoweka maagano ambao wanawalinda kwa upole na kusaidia kukidhi mahitaji yao ya kimwili na kiroho. Hata hivyo, kila mmoja wa akina dada hawa alikuwa na mahitaji ambayo hayakuwa yametekeleza kikamilifu.
Katika kila moja ya nyumba tulizotembelea, kiongozi wa ukuhani mwenye hekima alimwuliza kila dada ikiwa alikuwa amepokea baraka ya ukuhani. Kila wakati jibu lilikuwa hapana. Kila dada aliuliza na kupokea baraka ya ukuhani siku hiyo. Kila moja alilia alipokuwa akitoa shukrani kwa faraja, uongozo, himizo, na ushawishi uliokuja kutoka kwa Baba wa Mbinguni kupitia mwenye ukuhani wa kustahiki.
Akina dada hawa walinivutia. Walionyesha heshima kwa Mungu na nguvu na mamlaka Yake. Nilikuwa na shukrani pia kwa viongozi wa ukuhani waliotembelea nyumba hizi pamoja nami. Tulipoondoka kwa kila nyumba, tulishauriana pamoja kuhusu jinsi ya kusaidia familia hizi kupokea maagizo ambayo walihitaji ili kuendelea kwenye njia ya maagano na kuimarisha nyumba zao.
Kunayo siku hizi haja kuu ya wanaume na wanawake kukuza heshima kwa ajili ya kila mmoja na mwingine kama wana na binti wa Mungu na heshima kwa Baba wetu wa Mbinguni na ukuhani Wake---nguvu na mamlaka Yake.
Yeya anao mpango kwetu, na tunapotumia imani yetu na kuwa na tumaini katika mpango Wake, heshima yetu Kwake na kwa nguvu na mamlaka ya ukuhani Wake itaimarishwa.
Katika mafunzo ya duniani kote ya viongozi juu ya Strengthening the Family and the Church through the Priesthood,, tulifunza: “kwamba kina dada ambao hawatakuwa na mwenye ukuhani nyumbani kwao ... hawafai kuhisi kamwe kuwa peke yao. Wanabarikiwa na kuimarishwa kupitia maagizo waliyopokea na maagano wanayoweka. Hawafai kusita kujitolea wakati msaada unahitajika. Mzee M. Russell Ballard alifunza kwamba kila mwanamke Kanisani anahitaji kujua kwamba ana askofu, rais wa jamii ya wazee, mwalimu wa nyumbani, ama mwenye uhuhani mwingine mwenye kustahiki ambaye anaweza kumtegemea ambaye anaweza kuja nyumbani na kuwasaidia yeye na, kama Dada Rosemary M. Wixom aliongezea “kuwapa baraka.”9
Mzee Ballard pia amefunza: “Baba yetu wa Mbinguni ni mkarimu kwa nguvu Yake. Wanaume wote na wanawake wote wana kibali cha nguvu hii kwa ajili ya usaidizi katika maisha yetu wenyewe. Wote ambao wamefanya maagano matakatifu na Bwana, na wanaoheshimu maagano yao, wanastahili kupokea ufunuo wa kibinafsi, kubarikiwa na utumishi wa malaika, na kuzungumza na Mungu.”10
Sote tunahitajiana. Wana wa Mungu wanahitaji mabinti wa Mungu, na mabinti wa Mungu wanahitaji wana wa Mungu.
Tuna karama tofauti na uwezo tofauti. Wakorintho wa Kwanza mlango wa 12 inahimiza haja ya wana na mabinti wa Mungu, kila mmoja wetu, kutimiza wajibu wetu wa kibinafsi na majukumu kulingana na mpango wa Bwana kwamba wote waweze kufaidika.11
Wana wa Mungu, je, mnajua ninyi ni akina nani? Je, mnajua kile mlichonacho? Je, ninyi ni wastahiki kutumia ukuhani na kupokea nguvu na baraka za ukuhani? Je, mnakubali wajibu na majukumu yenu kuimarisha nyumba kama baba, babu, wana, ndugu, na wajomba? Je, ninyi mnaonyesha heshima kwa wanawake, uwanawake, na umama?
Mabinti wa Mungu, je, sisi tunajua sisi ni akina nani? Je, sisi tunajua kile tulichonacho? Je, sisi ni wastahiki kupokea nguvu na baraka za ukuhani? Je, sisi tunapokea karama ambazo sisi hupewa kwa shukrani, neema, na hadhi? Je, sisi tunakubali wajibu na majukumu yenu kuimarisha nyumba kama akina mama, bibi, binti, dada, na mashangazi? Je, sisi tunaonyesha heshima kwa wanaume, uume na ubaba?
Kama wana na mabinti wa agano, je, tunayo imani katika Baba yetu wa Mbinguni na mpango Wake wa milele kwa ajili yetu? Je, tunayo imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake? Je, tunaamini kwamba tunayo asili na kudura ya kiungu? Na katika jitihada zetu kutimiza hatima hii na kupokea vitu vyote ambavyo Baba anavyo,,12 je, tunaelewa umuhimu wa kupokea maagizo ya ukuhani na kufanya, kuweka na kufanya upya maagano na Bwana?
Sisi ni wana na mabinti wapendwa wa wazazi wa mbinguni, wenye asili na kudra takatifu. Mwokozi wetu, Yesu Kristo, alitupenda kutosha kutoa maisha Yake kwa ajili yetu. Upatanisho Wake unapatiana njia kwetu kuendelea kwenye mapito ya kwelekea mbinguni kupitia maagizo na maagano tukufu ya ukuhani.
Maagizo haya ya ukuhani na maagano yalirejeshwa duniani kupitia kwa Nabii Joseph Smith, na leo Rais Thomas S. Monson anashikilia funguo zote za ukuhani duniani.
Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kunapatikana mamlaka ya ukuhani ya kusimamia maagizo ambayo kwayo tunaweza kuingia katika maagano ya kudumu na Baba yetu wa Mbinguni katika jina la Mwanawe Mtakatifu. … Mungu atatii ahadi Zake kwako unapoheshimu maagano yako na Yeye.”13
Kwa haya nashuhudia katika jina la Yesu Kristo, amina.