Kama Chombo Kilichovunjika
Je! Unaweza kufanya nini vyema wakati changamoto za akili au kihisia zinapokukabili wewe au wale uanawapenda?
Mtume Petro aliandika kwamba wafuasi wa Yesu Kristo wanapaswa kuwa wawe “wenye kuhurumiana.”1 Katika dhana hiyo ningependa kuwazungumzia wale ambao wanateseka kutokana na aina ya ugonjwa wa akili ama ugonjwa wa kihisia, iwe magonjwa hayo ni mepesi ama ya kina, ama ya muda mfupi ama yanayodumu kwa maisha yote. Tunahisi utata wa maswala kama hayo tunapowasikia wafanisi wakizungumza juu ya matatizo ya fadhaa na kichaa, ya mvuto wa jenetiki na shurutisho la ugonjwa wa kiakili, wazimu na skizofrenia. Vyovyote kanganyishi inavyoweza kuwa, maradhi haya ni baadhi ya uhalisi wa maisha ya duniani, na haifai kuona aibu kamwe katika kuyakubali zaidi ya kukubali vita dhidi ya shinikizo la damu au kutokeza ghafula kwa uvimbe wa saratani.
Katika jitihada za kutafuta kiasi cha amani na ufahamu wa maswala haya magumu, ni muhimu kukumbuka kwamba tunaishi---na tulichagua kuishi---katika dunia iliyoanguka, ambapo kwa malengo matukufu kutafuta kwetu kwa uungu utatahiniwa na kujaribiwa mara kwa mara. Hakikisho kuu katika mpango kama huo ni kwamba Mwokozi aliahidiwa, Mkombozi ambaye kupitia kwa imani yetu Kwake angetuinua kwa ushindi juu ya majaribu na majaribio, hata ingawa gharama ya kufanya hivyo haingeeleweka kwa uzito wake kwake Baba ambaye alimtuma Yeye na Mwana ambaye alikuja. Ni tu ufahamu wa upendo huu mtukufu ambao utafanya mateso yetu madhaifu kwanza kuwa yanaweza kuhimilika, kisha kueleweka, na hatimaye kukomboleka.
Acheni mimi niachane na maradhi yasiyo ya kawaida niliyotaja na kuzingatia juu ya MMM---“maradhi ya mfadhaiko mkubwa”---au kwa kawaida zaidi, “mfadhaiko.” Ninapozungumzia haya, sizungumzii zile siku mbaya, makataa ya malipo ya kodi, au nyakati za kuvunja moyo ambazo sisi sote uwa nazo. Kila mtu atakuwa na wasiwasi ama kuvunjika moyo kwa wakati fulani. Kitabu cha Mormoni kinasema Amoni na nduguze walifadhaika na wakati mgumu2 na ndivyo inavyoweza kuwa hivyo kwetu sote. Lakini leo ninazungumzia jambo kubwa zaidi, ninazungumzia maradhi makali hadi kwamba kwa kiasi kikubwa huzuia uwezo wa mtu kufanya kazi kikamilifu, shimo katika akili lenye kina zaidi hata kwamba hakuna anayeweza kuwajibika kupendekeza kwamba hakika yatapotea ikiwa waathiriwa watavumilia na kuwa na dhamira mzuri ya maisha---ingawa mimi ni mtetezi mkubwa wa kuvumilia na kuwa na dhamira mzuri ya maisha!
La, huu usiku wa kiza wa akili na roho ni zaidi ya kuvunjika moyo tu. Nimeuona ukimjia mwanaume mwema wakati mkewe mpendwa wa miaka 50 alipoaga dunia. Nimeuona katika akina mama wapya na kile kinachoitwa kitasifida “huzuni baada ya mtoto.” Nimeuona ukiwapata wanafunzi walio na wasiwasi, wastaafu wa jeshi, akina bibi walio na wasiwasi kuhusu maisha mema ya watoto wao wazima.
Na mimi nimeshauona katika kina baba vijana wakijikakamua kukimu familia zao. Katika jambo hili wakati mmoja nimeuona ya kuogofya kwangu mwenyewe. Wakati mmoja katika maisha yetu ya ndoa wakati hofu za fedha zilikutana na uchovu mwingi, nilipatwa na pigo la kiakili ambalo lilikuwa haieleweki na halikutarajiwa kama ilivyokuwa kweli. Na kwa neema ya Mungu, na upendo wa familia yangu niliendelea kutenda na kufanya kazi, lakini hata baada ya miaka hii nimeendelea kuhisi huruma ya kina kwa wengi ambao wana maradhi sugu au wamearhitiwa sana na huzuni kunishinda mimi. Katika hali hiyo sote tumetiwa moyo na wale ambao, kwa maneno ya Nabii Joseph, “walitazama … na kufahamu giza la dhiki,” 3 na walihifadhiwa kuipitia, … ikiwa ni pamoja na Abraham Lincoln, Winston Churchill, na mmoja wa wanaume wale wakarimu na Wakikristo wa siku zetu, Mzee George Albert Smith kiumbe wa siku za mwisho mmojawapo wa wanaume wapole na wenye mfano kama Kristo wa kipindi chetu, ambaye alikumbana na mfadhaiko uliomrudia rudia kwa miaka fulani mapema na baadaye kuwa nabii wa nane mpendwa wa wote na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
Hivyo basi, unaichikulia vipi vizuri wakati changamoto za kiakili na kihisia zinakukabili wewe ama wale unaowapenda? Kwanza kabisa, kamwe usipoteze imani katika Baba yako aliye Mbinguni, ambaye anakupenda zaidi ya uwezavyo kuelewa. Rais Monson alisema kwa kina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kwa njia ya kuvuta hisia jioni ya Jumamosi iliyopita: “Kwamba upendo kamwe haubadiliki, … Upo hapo kwenu wakati muna huzuni au furaha, kuvunjika moyo au mkiwa na matumaini. Upendo wa Mungu upo hapo kwa ajili yako aidha mnaufaa au hamuufai. Upo hapo kawaida daima.”4 Kamwe msiwe na shaka, na kamwe msifanye mioyo yenu kuwa migumu. Kwa uaminifu tafuteni njia tukufu ambazo zimejaribu sana ambazo huleta Roho ya Bwana katika maisha yenu. Tafuteni ushauri ya wale wanaomiliki funguo za hali njema yako ya kiroho. Uliza na utunze nguvu ya baraka ya ukuhani. Pokea sakramenti kila wiki, na ushikilie kabisa ahadi za ukamilifu za Upatanisho wa Yesu Kristo. Kuwa na imani katika miujiza. Nimeshaona wengi sana sana wao wakija wakati kila ishara inaonyesha kwamba tumaini limepotea. Tumaini halipotei kamwe. Ikiwa halitakuja mara moja ama kikamilifu ama lisije hata kidogo, kumbuka mfano wa Mwokozi mwenyewe wa dhiki kikombe cha dhiki ambacho hakipiti kinywe na uwe mwenye nguvu, ukitegemea siku za furaha zilizopo mbele.5
Katika kuzuia maradhi inapowezekana kuwa mwangalifu kwa ishara za mfadhaiko kwako na kwa wengine ambao huenda ukaweza kuwasaidia. Kama ilivyo kwa, gari lako chunga ongezeko la joto, kasi kupindukia, ama tangi lililoisha mafuta. Unapokumbana na “mfadhaiko wa kutokomeza,” fanya marekebisho yanayohitajika. Uchovu ni adui wa kawaida wetu sote---kwa hivyo punguza mwendo, pumzika, jaza na jaza upya. Madaktari wanatuahidi kwamba tusipochukua muda wa kupona, bila shaka tutachukua wakati baadaye kuwa wagonjwa.
Vitu vikiendelea kutokomea, tafuta ushauri wa wataalam ambao wana mafunzo yaliyodhibitishwa, ufanisi, na maadili mema. Waambie ukweli kuhusu historia yako na mapambano. Kwa maombi na kwa kuwajibika zingatia ushauri wanaokupa na suluhisho wanaoagiza. Ikiwa una ugonjwa wa kibole, Mungu angekutarajia uulize baraka ya ukuhani na upate huduma bora ya matibabu inayopatikana. Hivyo pia na matatizo ya kihisia. Baba yetu wa Mbinguni anatarajia tutumie karama zote za ajabu Yeye amepatiana katika kipindi kitukufu.
Ikiwa wewe ndiye ulioathiriwa, au mlezi, ujaribu usilemewe kiasi cha kazi yako. Usidhani unaweza kutatua kila kitu. Tatua kile unaweza. Ikiwa hio itakuwa ushindi mdogo tu, kuwa na shukrani kwa ajili yake, na kuwa hivyo. Kuwa mvumilivu. Mara nyingi katika maandiko, Bwana anaamrisha mtu “asimame tuli” ama “atulie”---na kungoja6 Kustahimili kwa uvumilivu vitu vingine ni sehemu ya elimu yetu duniani.
Kwa walezi, katika juhudi zenu za kujitolea ili kusaidia kwa afya ya mtu mwingine, usiharibu yako mwenyewe. Katika mambo haya yote kuwa na hekima. “Haupaswi kukimbia zaidi kuliko nguvu zako.7 Chochote ulicho au usichoweza kupatiana, unaweza kutoa maombi yenu na kutoa “upendo usio unafiki.”8 “Na hisani huvumilia, na ni karimu; … huvumilia vitu vyote, huamini vitu vyote, … hutumaini vitu vyote, hustahamili vitu vyote. Hisani haikosi kufaulu kamwe .”9
Pia tukumbuke kwamba kupitia ugonjwa wowote ama changamoto ngumu, bado kuna mengi maishani ya kutumainia na kushukuru. Sisi ni zaidi ya upungufu wetu au maradhi yetu! Stephanie Clark Nielson na familia yake wamekuwa marafiki zetu kwa zaidi ya miaka 30. Agosti 16, 2008, Stephanie na mumewe Christian, walikuwa katika ajali ya ndege na moto uliotokea ulimteketeza vibaya sana hata kwamba vidole vya miguu vilivyochorwa ndiyo ambavyo vilikuwa vinaweza kutambulika wakati wanafamilia walikuwa wanatambua waathiriwa. Kulikuwa hamna uwezekano wa Stephanie kuishi. Baada ya miezi mitano akiwa kwenye usingizi mzito uliofanyizwa, yeye aliamka na kujiona mwenyewe. Kwa ajili ya kuteketea huku na mfadhaiko mkali sana hukaja. Akiwa na watoto wanne chini ya umri wa miaka saba, Stephanie hakutaka wao wamuone yeye tena kanwe. Alihisi haikuwa vyema yeye kuishi. “Nilifikiria ingekuwa rahisi,” Stephanie wakati mmoja aliniambia, “kama tu wangenisahau mimi na ningetoweka kutoka kwa maisha yao.”
Lakini kwa heshima yake ya milele, na kwa maombi ya mumewe, familia, marafiki, watoto watatu warembo, na mzaliwa wa tano kwa kina Nielson alizaliwa miezi 18 tu iliyopita, Stephanie alipigana kutoka kwa dhiki ya maangamizo kuwa mmoja wa “kina mama wenye kublogi” maarufu katika taifa, kwa uwazi akitangaza kwa watu milioni nne waliokuwa wakifuata blogi yake kwamba “madhumuni yake matakatifu” katika maisha ni kuwa mama na kuthamini kila siku ambayo yeye amepatiwa katika ulimwengu huu maridadi.
Hata kama masumbuko yako ni yapi, ndugu na kina dada---kiakili au kihisia au kimwili, au vinginevyo---usipige kura dhidi thamani ya maisha kwa kuyamaliza! Mtumainie Mungu. Shikilia upendo Wake. Jua kwamba siku moja machweo yatapambazuka kwa uangavu na vivuli vyote vya maisha ya duniani vitatoweka. Ingawa tunaweza kuhisi tuko kama “chombo kilichovunjika,” kama Mtunga Zaburi alivyosema, 10 ni sharti tukumbuke, kwamba chombo kiko katika mikono ya mfinyanzi mtukufu. Akili zilizovunjika zinaweza kuponywa kama vile mifupa iliyovujika na mioyo iliyovunjika huponywa. Wakati Mungu yuko kazini akifanya marekebisho hayo, wengine wetu tunaweza kusaidia kwa kuwa wenye neema, wasiohukumu, na wakarimu.
Nashuhudia juu ya Ufufuo mtakatifu, karama ya msingi usiosemeka katika Upatanisho wa Bwana Yesu Kristo! Pamoja na Mtume Paulo, Ninashuhudia kwamba kile ambacho kilipandwa katika uharibifu; siku moja kitafufuliwa katika kutoharibika, na kile kilichopandwa katika udhaifu hatimaye kitafufuliwa katika nguvu.11 Nashuhudia juu ya siku hiyo ambapo wapendwa ambao tuliwajua kuwa na ulemavu duniani watasimama mbele yetu wakiwa wametukuzwa na saada, wakamilifu wakupendeza mwilini na akilini. Itakuwa ni wakati mzuri kiasi gani! Sijui kama tutakuwa na furaha kwa ajili yetu wenyewe kwamba tumeshuhudia muujiza kama huo ama tukakuwa na furaha kwa ajili yao kwamba ni wakamilifu kabisa na hatimaye “wako huru.”12 Hadi saa hiyo ambapo huruma iliyotumiwa ya Kristo itakuwa dhahiri kwetu sote, na tuishi kwa imani, tushikilie tumaini kwa nguvu na tuonyesheni “kuhurumiana,”13 Mimi naomba katika jina la Yesu Kristo, amina.