2010–2019
Mafundisho na Kanuni Zilizopo katika Makala ya Imani
Oktoba 2013


14:29

Mafundisho na Kanuni Zilizopo katika Makala ya Imani

Kila makala ya imani huongezea thamani ya kipekee kwenye uelewa wetu wa injili ya Yesu Kristo.

Nilipopewa kazi ya kunena katika kikao cha ukuhani cha mkutano mkuu, mara moja nilifikiria mwalimu wa Msingi wa ajabu. Hamu yake kuu ilikuwa ni kututayarisha kuwa wastahiki kupokea ukuhani. Alitufunza kwa makini sana juu ya mahitaji ya kufuzu kutoka kwa Msingi---kwa kukariri majina ya washiriki wa Jamii na Mitume Kumi na Wawili na Makala ya Imani. Pia alitufanya tuweke ahadi---kama sisi sote tungeweza kukariri Makala ya Imani kumi na tatu, tungechagua mahali na tungeenda kuvinjari kwa darasa letu la mwisho.

Tulichagua mahali maalum tulipopenda kutembea kwenye miteremko ya miamba juu ya bwawa katika lango la Logan Canyon katika Utah Kasikazini. Kulikuwa na mahali padogo tambarare katika kizingiti cha mwamba ambapo palikuwa na meko ya asili ambapo tungepika soseji katika mkate na kuchoma mashimelo. Wakati tulipochagua mahali hata hivyo, hatukufikiria mwalimu wetu, ambaye alikuwa ni mzee na kwa kweli hakuwa mwenye nguvu. Kama tungekuwa tumefikiria kwa makini sana, ingeweza kuonekana kwetu kwamba angekuwa na shida kutembea. Ahadi yake ilikuwa sharti lake, hata hivyo, naye alitufuata kwa uhodari.

Kwanza, tulipomaliza kukwea kilima kidogo. Siku zetu hakukuwa na nyaya za umeme za kuzuia njia ya kufika.  Kwa usaidizi fulani mwalimu wetu alifika juu kilimani. Mara tulipopita kilele tuliteremka kwenye mgongo wa safu wa mwamba hata mahali panapoitwa “Turtle Back.”

Baada ya kuwasili, ilimchukua mwalimu wetu muda kuhema vyema. Kufikia wakati tulipotayarisha mlo wetu na kuketi chini kula, yeye alikuwa ashapata nafuu ya kutosha kutufunza somo letu la mwisho. Alituambia jinsi alifurahia kutufunza katika Msingi miaka miwili iliyopita. Alitupongeza kuhusu jinsi tulikuwa na umahiri wa Makala ya Imani. Angetaja nambari katika mojawapo, na sisi tungemkariria. Kisha yeye angesema kukariri Makala ya Imani hakungekuwa na maana yoyote kushinda kujua maneno mengi pasipo kuelewa mada ya mafundisho na kanuni zilizopo ndani yake. Alitutia moyo tujifunze mafundisho ya injili katika kila Makala ya Imani. Alieleza kwamba mafundisho yanayopatikana katika Makala ya Imani yamegawanywa katika sehemu.

I.Uungu na Kanuni za Msingi za Kristo

Tunajifunza kutoka kwa makala ya imani ya kwanza kwamba katika Uungu kuna watu watatu: Mungu Baba, Yesu Kristo, na Roho Mtakatifu.

Makala ya pili hutufunza kwamba sisi tuna jukumu la matendo yetu wenyewe hapa duniani.

La tatu linapatiana ono la huduma ya Mwokozi kwa wokovu wa watoto wa Baba aliye Mbinguni.

La nne hufunza umuhimu wa kanuni na maagizo ya msingi.

Uwezo wa maneno ya mwalimu wetu umekuwa chanzo cha maongozi kwangu kwa sababu ya mkazo aliyoweka kwenye kujifunza injili. Maandiko yanatuongoza hata kwenye viwango vya ukweli ambavyo kwavyo tunaweza kupima elimu tunayopokea, hata kama iwe kweli au uongo. Mafundisho ya kweli huja kutoka kwa Mungu, chanzo cha msingi wa kweli zote. Mafundisho na dhana za fundisho la kweli yanapatikana katika injili ya Bwana na Mwokozi wetu. Mafundisho ya uongo kutoka kwa Shetani, baba wa uongo wote. Ana hamu ya kupotosha, kubadilisha, na kugeuza kweli zilizofunuliwa. Anataka kutulaghai ili baadhi yetu tupoteze njia yetu katika safari ya kurudi tena kwa nyumba yetu ya milele.

Maandiko yanatufunza jinsi ya kuepuka mafundisho ya uongo. Kwa mfano, katika barua ya Paulo kwa Timotheo, tunasoma:

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadhibu katika haki;

“Ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo njema” (2 Timotheo 3:16–17).

Haya mafundisho kwa Kanisa ni kama vile beteri ilivyo kwa rukono. Tunapoondoa beteri kutoka kwa rukono yako, inakuwa ya bure. Kanisa ambapo mafundisho ya ukweli hayafundishwi tena vivyo hivyo ni bure. Haliwezi kutuongoza kurudi tena kwa Baba yetu wa Mbinguni na nyumba yetu ya milele.

II. Mpangilio na Utaratibu wa Ukuhani

Baada ya kuelewa mafundisho ya msingi ya Kristo, makala ya imani ya tano na ya sita yanatufunza kuhusu mpangilio na utaratibu wa ukuhani. Chini ya maelekezo ya Bwana, Joseph Smith alianzisha Kanisa la Mwokozi akitumia mamlaka ya ukuhani---uwezo wa Mungu. Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni mpangilio ule ule ambao Kristo alianzisha na kuelekeza Yeye alipokuwa hapa ulimwenguni.

Ilikuwa siku tukufu jinsi gani kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery katika Mei 1829 wakati walienda katika kichaka kuomba kuhusu mafundisho ya ubatizo kwa ondoleo la dhambi ambayo walikuwa wamesoma kuhusu walipokuwa wanatafsiri Kitabu cha Mormoni. Kulikuwa na mafundisho mengi kuhusu ubatizo ambayo yalikuwa yanafunzwa na makanisa tofauti katika miaka ya mapema ya 1800, na Joseph na Oliver walijua hayo yote hayangekuwa kweli. Walitaka kujua kuhusu njia sahihi ya ubatizo na pia nani alikuwa na mamlaka ya kubatiza.

Katika jibu la maombi yao kwa Bwana, mjumbe kutoka mbinguni, Yohana Mbatizaji, aliwatokea. Yeye aliwawekelea mikono kwenye vichwa vyao na kutawaza juu yao mamlaka ya ubatizo kwa maneno haya: “Juu yenu ninyi watumishi wenzangu, katika jina la Masiya ninawatunukia Ukuhani wa Haruni, (M&M 13:1).

Ni siku ya ajabu jinsi gani katika historia ya dunia! Ukuhani ulikuwa umerejeshwa ulimwenguni.

Tunapopokea ukuhani, sisi hupokea mamlaka ya kutenda katika jina la Mungu na kuongoza katika njia za kweli na haki. Mamlaka haya ni chanzo muhimu kwa uwezo wa haki na ushawishi kwa manufaa ya watoto wa Mungu hapa ulimwenguni na yatadumu kupita pazia. Ilikuwa muhimu sana kwa ukuhani kurejeshwa kabla ya Kanisa la Yesu Kristo la kweli kupangwa. Hili somo la kimsingi sisi tunajifunza kutoka kwa makala ya imani ya tano na sita.

III. Nyenzo za Milele katika Safari ya Duniani

Makala ya Imani matatu yafuatayo ya —saba, nane, na tisa—yanaelezea nyenzo zinazopatikana kutufunza katika safari yetu duniani. Tunapatiwa karama za kiroho za kutuongoza sisi tunapofuata mafundisho ya Bwana na kutulinda sisi kutokana na uovu. Maandiko yana mwongozo mwengine---ikiwa tutasoma kwa makini neno la Mungu, Yeye atatufunua njia yetu ya kurudi kwa uzima wa milele.

Makala ya imani ya tisa hutufunza kwamba Mungu amefunua, anafunua, na atafunua katika siku za usoni kweli nyingi kuu na muhimu kwa manabii, waonaji na wafunuaji Wake. Sisi tunajifunza kwamba kama ziada ya kusikiliza sauti tuli, ndogo ya Roho na kusoma maandiko, kwamba chanzo kingine cha mwongozo ni viongozi wetu wa Kanisa, ambao uteuliwa, na kutengwa ili kubariki maisha yetu kupitia masomo wanayofunza.

IV. Washiriki Wamisionari

Makala ya imani ya kumi, kumi na moja, na kumi na mbili yanatuelekeza sisi jinsi ya kutekeleza kazi ya umisionari na kushiriki injili katika dunia ya mataifa mengi na sheria tofauti tofauti. Sisi tunajifunza kuhusu kukusanyika kwa Israeli katika matayarisho ya Ujio wa Pili wa Mwokozi. Tunafunzwa kwamba wanaume na wanawake ni mawakala juu yao wenyewe, na wanaweza kukubali au kukataa neno la Mungu kulingana na dhamira yao wenyewe. Mwisho, tunajifunza tunaposambaza injili ya Yesu Kristo katika pembe nne za ulimwengu kwamba lazima tuheshimu serikali za kila nchi tunayoingia. Kwa kweli, tunaamini katika kutii, kuheshimu, na kuhimili sheria ya kila nchi.

V. Sifa Tamanishi

Makala ya imani ya kumi na tatu inapatiana umaizi maalum katika jinsi tunavyofaa kuendesha maisha yetu na kuingiliana na watu. Inasema: “Tunaamini katika kuwa waaminifu, wakweli, wasafi, wakarimu, wema, na katika kufanya mema kwa watu wote; naam, twaweza kusema kwamba tumefuata maonyo ya Paulo—Tunaamini mambo yote, tunatumaini mambo yote, tumestahimili mambo mengi, na tunatumaini kuwa tutaweza kustahimili mambo yote. Kama kuna kitu chochote kilicho chema, chenye kupendeza, au chenye taarifa njema au chenye kustahili sifa, tunayatafuta mambo haya.”

Sisi sote tunapaswa kutamani kupata sifa hizi na kuishi maisha yanayozidhihirisha. Kweli zilizofunzwa katika Makala ya Imani hujenga moja juu ya ingine kama vile vijenzi vya rukono vinahimiliana kimoja na kingine. Kama vile msururu wa ugavi wa hali ya juu ambao unaongeza vijenzi kwa rukono, Makala ya Imani yanatoa ugavi kwetu kwa mafundisho muhimu ya Urejesho. Kila makala ya imani huongeza thamani kwa uelewa wetu wa injili ya Yesu Kristo.

Mwalimu wangu wa Msingi alinipa azimio la kujifunza mafundisho ya ufalme. Alinifunza mimi kutafuta maana ya kina inayopatikana katika haya makala ya imani rahisi. Aliniahidi mimi kwamba kama ninawekeza katika kujifunza hizi kweli takatifu kwamba elimu nitakayopata zitabadilisha maisha yangu kuwa bora, na mimi nashuhudia kwenu kwamba imekuwa hivyo.

Baada ya somo la ajabu la mwalimu wangu juu ya ule mlima katika Logan Canyon, tuligundua kwamba tumekaa sana kuliko vile tulivyokuwa tumepanga. Usiku ulikuwa unaingia na tukatambua kuwa tulikuwa na shida.

Mwalimu alikuwa anasumbuka kufika mahali petu maalum, lakini kurudi kulileta changamoto ingine kubwa. Hii ilileta matatizo katika chaguo letu la sehemu ya kujivinjari kwetu. Kushuka chini kulikuwa vigumu kwetu, lakini kulikuwa hata vigumu kwa mtu wa umri wake.

Tunapokuwa tunajaribu kumsaidia juu mlima, askari wa polisi wawili walitokea. Rais wa Msingi alikuwa amewatuma kututafuta, akihofia kuwa tulikuwa tumepotea. Sarakasi ya tukio na masomo yalifunzwa yalifanya uzoefu kutosahaulika katika maisha yangu.

Ninyi wavulana---nawahimiza mtumie akili zenu angavu kujifunza na kusoma Makala ya Imani na mafundisho yanayofunza. Ni miongoni mwa kauli muhimu sana na wazi sana za mafundisho katika Kanisa. Kama mtayatumia kama mwongozo wa kuelekeza mafunzo yenu ya injili ya Yesu Kristo, mtajipata mwenyewe mkiwa tayari kutangaza ushahidi wenu wa ukweli uliorejeshwa duniani. Mtaweza kutangaza kwa urahisi, wazi wazi, na kwa njia muhimu imani muhimu ninyi mnazozithamini sana kama mshiriki wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Mimi naongezea ushuhuda wangu juu ya ukweli wa Makala ya Imani kumi na tatu katika jina la Bwana na Mwokozi wetu, hata Yesu Kristo, amina.