2010–2019
Vitu Vidogo na Rahisi
Oktoba 2013


2:3

Vitu Vidogo na Rahisi

Acha sisi tufikie wengine kwa imani na kwa upendo.

Wapendwa wangu akina ndugu na akina dada, takribani majuma machache yaliyopita nilikuwa kwenye kituo cha mafunzo cha wamisionari kwenye jiji la Mexico kushiriki ujumbe pamoja na wamisionari. Mke wangu nami kwa makusudi tuliwasili masaa machache mapema.Na tulipokuwa tunatembelea bustani nzuri na mitaa iliyotunzwa vizuri ya KMM, hatungejizuia ila kuiona furaha iliyooneshwa kutoka sura za mamia ya wazee vijana na akina dada,kila mmoja akilenga kupata ujuzi wa lugha mpya na kujifunza kufurahia vyema kusudi lao kama wamisionari.

Nilipotulia ili nipate kwa ukamilifu kuona hali hii isiyo ya kawaida, nilifikiria juu ya maneno ya Alma alipomwamuru mwanawe Helamani kuweka historia ya watu wake kama sehemu ya kumbukumbu ambazo ameaminiwa nazo na kuweka vitu hivi wakfu ili kwamba viweze siku moja kwenda kwenye mataifa yote, ukoo, kabila, na watu.

Alma kisha akamwambia:

“Sasa labda unadhani kwamba huu ni upuuzi ndani yangu; lakini tazama nakwambia, kwamba kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka; na njia ndogo mara nyingi hufadhaisha wenye hekima.

Na Bwana Mungu hutumia njia zake ili kutimiza kusudi lake kuu na la milele; na kwa njia ndogo sana Bwana hufawadhaisha wale werevu na kutimiza wokovu wa roho nyingi(Alma 37:6–7).

Umasumu na ujana wa wamisionari wetu unadhihirisha njia ya Bwana,kwamba wale walio wanyenyekevu wanaweza “kuwaalika wengine kuja kwa Kristo kwa kuwasaidia kupokea injili kupitia imani katika Yesu Kristo na upatanisho wake,toba,ubatizo,kupokea karama za Roho Mtakatifu,na kuvumilia hadi mwisho”(Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Huduma ya Misionari [2004], 1).

Kama washiriki wa kanisa,tuna uwezo, kupitia kwa vitu vyetu vidogo na rahisi, “[kuwasadikisha] wengi kuhusu makosa ya njia zao,” na kusaidia kuwaleta “kwenye ufahamu wa Mungu wao hadi kwa wokovu wa nafsi zao”(Alma 37:8).

Katika tukio moja nilifuatana na Rais wa kigingi na askofu kutembelea mshiriki asiye shiriki kikamilifu.Tulimfundisha katika njia rahisi sana, kuhusu baraka za Sabato. Tulimwonyesha mapenzi yetu ya dhati. Alijibu, “kile ninachohitaji ilikuwa ni kupata mtu aje na kunipa abrazo,” au kumbatio.” Mimi mara moja nilisimama na kumkumbatia. Siku iliyofuata ilikuwa jumapili. Ndugu huyu huyu alikuja kwenye mkutano wa sakramenti pamoja na familia yake mzima.

Mwalimu mtembelezi alipomtembelea, Martha, mshiriki wa kata yetu, alimwambia mke wangu na mwenza wake kamwe wasirudi tena. Alikuwa ameamua kuacha kuja kanisani. Mmoja wa walimu watembelezi alimwomba Martha kama wangeimba wimbo pamoja mara moja kwa mara ya mwisho, na alikubali.Walipokuwa wanaimba, kitu cha ajabu kilitokea. Kidogo kidogo, Roho alianza kujaza chumba. Kila mmoja alimhisi. Moyo wa Martha ukaanza kulainika. Pamoja na macho yake kujaa machozi, aliwaeleza waalimu watembelezi wake hisia za moyo wake. Kwa wakati ule, alitambua kwamba injili ilikuwa kweli. Na sasa aliwashukuru waalimu wake watembelezi kwa kumtembelea na akaeleza ombi lake la wao kurudi. Kutoka siku ile na kuendelea, aliwapokea kwa furaha.

Martha alianza kuhudhuria kanisa pamoja na bintiye mdogo. Kwa miaka walihudhuria mara kwa mara, pamoja na Martha kutokata tamaa kwamba mumewe angeweza hatimaye kuchagua kuungana nao. Hatimaye siku ikaja Bwana alipogusa moyo wake, na alianza kuhudhuria pamoja nao, kama walivyofanya wasichana wao wengine mapema baada ya hapo familia hii ikaanza kuhisi furaha ya kweli ambayo inakuja kutokana na kuwa na baraka za injili ndani ya nyumba yao. Tangu hapo Martha amehudumia kwa uaminifu kwenye kata yetu kama Rais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, na mumewe alihudumia vizuri katika miito mbalimbali katika kata. Haya yote yalianza kwa kuimba wimbo, kitu kidogo na rahisi ambacho kilichogusa moyo wa Martha.

Naaman alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, mtu aliyeheshimika,mtu mwenye nguvu na shujaa; lakini alikuwa pia mwenye ukoma. (ona 2 Wafalme 5:1). Baada ya kushindwa kupata matibabu kwa ukoma wake kutoka kwa mfalme wa Israel, Naaman alikwenda kwenye nyumba ya Elisha, nabii. Elisha alimtuma mjumbe kwenda kwake, akisema:

“Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.

“Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. …

“ Watumishi wake wakamkaribia, wakamwambia, wakasema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi?

“Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi..” (2 Wafalme5:10–11, 13–14).

Nabii wetu, Rais Thomas  S. Monson, ametualika sote kwenda mbele na kuwaokoa ndugu na dada zetu. Alisema:”Ulimwengu unahitaji msaada wenu. Kuna miguu ya kuimarisha, mikono ya kushika kwa nguvu, mawazo ya kutia moyo, mioyo ya kutia hamasa na roho za kuokoa. Baraka za milele zinakungoja” (“To the Rescue,” Ensign, May 2001, 48; au Liahona, July 2001, 57).

Ninashuhudia kwamba wengi wa hao wanaohitaji msaada wetu wako pale wakitusubiri. Wako tayari kwa mashujaa ndugu na dada zao kuwafikia na kuwaokoa kupitia njia ndogo na rahisi. Mimi binafsi nimetumia masaa mengi kuwatembelea washiriki wasioshiriki kikamilifu wa kanisa ambao mioyo yao tayari imelainishwa na Bwana, ambao sasa wako tayari kupokea shuhuda zetu na mwonyesho wetu wa kweli wa upendo. Tunapowafikia na kuwaalika,watarudi kanisani bila kusita.

Tuwafikie wengine kwa imani na kwa upendo. Tukumbukeni ahadi ya Bwana:

“Na kama itakuwa kwamba utafanya kazi siku zako zote katika kutangaza toba kwa watu hawa, na kuleta, japo iwe nafsi moja kwangu, shangwe yako itakuwa kubwa jinsi gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu!

“Na sasa, kama shangwe yako itakuwa kubwa kwa hiyo nafsi moja ambayo umeileta kwangu katika ufalme wa Baba yangu, itakuwa shangwe kubwa namna gani kwako kama utazileta nafsi nyingi kwangu! (M&M 18:15–16).

Ninatoa ushuhuda wa upendo wa Bwana kwa watoto Wake wote. Ninajua Yeye yu hai na kwamba Yeye ni Mkombozi wetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.