2010–2019
Mpaka Tutakapokutana Tena
Oktoba 2013


3:1

Mpaka Tutakapokutana Tena

Na tuonyeshe ongezeko la ukarimu kwa mmoja na mwingine; na daima tupatikane tukifanya kazi ya Bwana.

Ndugu na dada zangu, moyo wangu umejaa tele tunapofikia tamati ya mkutano mkuu huu wa Kanisa wa ajabu. Tumelishwa kiroho tilipokuwa tunasikiliza ushauri na shuhuda za wale ambao wameshiriki katika kila kikao.

Sisi tumebarikiwa kukutana hapa katika Kituo cha Mkutano hiki cha ajabu katika amani na usalama. Tumekuwa na usambazaji usio na kifani wa mkutano mkuu huu, ukifikia kuvuka mabara na bahari kwa watu kila mahali. Ingawa sisi kimwili tuko mbali na wengi wenu, sisi tunahisi roho yenu.

Kwa Ndugu zetu ambao wameachiliwa katika mkutano mkuu huu, acha nitoe shukrani za moyoni za Kanisa lote kwa miaka yenu ya huduma ya kujitolea. Wengi wasio na hesabu ambao walibarikiwa na mchango wenu katika kazi ya Bwana.

Mimi natoa shukrani kwa Kwaya ya Tabernacle na kwa zile kwanya zingine ambazo zilishiriki katika mkutano mkuu huu. Muziki ulikuwa mtamu sana na umeongezea pakubwa kwenye Roho ambayo sisi tumehisi katika kila kikao.

Nawashukuru kwa maombi yenu kwa niaba yangu na kwa niaba ya Viongozi wenye Mamlaka wote na maafisa wakuu wa Kanisa, Sisi tumeimarishwa nayo.

Na baraka za mbinguni ziwe pamoja nanyi. Na nyumba zenu zijazwe na upendo na staha na Roho wa Bwana. Na ninyi daima mlishe shuhuda zenu za injili, kwamba ziwalinde ninyi dhidi ya karamu ya adui.

Mkutano mkuu sasa umeisha. Tunaporudi nyumbani kwetu, na tufanye hivyo salama. Na Roho tuliyohisi hapa iwe na ikae pamoja nasi tunapoendesha yale mambo tunayotenda kila siku. Na sisi tuonyeshe ongezeko la ukarimu kwa mmoja na mwengine, na daima tupatikane tukifanya kazi ya Bwana.

Ndugu na dada zangu, na Mungu awabariki ninyi, Na amani ile Yeye amehahidi iwe pamoja nanyi sasa na daima. Kwaherini mpaka tutakapokutana tena katika kipindi cha miezi sita. Katika jina la Mwokozi wetu, hata Yesu Kristo Bwana, amina.