2010–2019
Maombolezo ya Yeremia: Tahadhari Utumwa
Oktoba 2013


14:35

Maombolezo ya Yeremiah: Tahadhari Utumwa

Changamoto yetu ni kuepuka utumwa wa aina yoyote, kumsaidia Bwana kuwakusanya wateule Wake, na kujitolea kwa ajili ya kizazi chipukizi.

Mapema katika ndoa yetu, mke wangu, Mary, nami tuliamua kwamba kwa kiwango kiwezekanacho tungechagua shughuli ambazo tungehudhuria pamoja. Pia tulitaka tuwe wenye hekima kwa bajeti yetu. Mary anapenda muziki na hakika alikuwa na wasiwasi kwamba huenda ningesisitiza zaidi hafla za michezo, basi aliafiki kwamba kwa matukio yote ya kulipwa, kungekuwa na michezo miwili ya nyimbo, muziki ya opera, ama michezo ya kitamaduni kwa kila mchezo wa mpira wa kulipiwa.

Mwanzoni, nilikuwa na ukinzani kwa kipengele cha opera, lakini muda ulivyopita nilibadilisha mtazamo wangu. Nikaja kufurahia hasa opera za Giuseppe Verdi.1 Wiki hii itakuwa maadhimisho ya 200 ya kuzaliwa kwake.

Katika ujana wake Verdi alifurahishwa na nabii Yeremia, na katika 1842 akiwa na umri wa miaka 28, alipata umaarufu na opera Nabucco, aina ya Kiitaliano iliyofupishwa ya jina Nebukadireza, mfalme wa Babeli. Opera hii ina dhana zilizochukuliwa kutoka kwa vitabu vya Yeremia, Maombolezo, na Zaburi katika Agano ya Kale. Opera hii inajumuisha kutekwa kwa Yerusalemu na kufungwa na utumwa wa Wayahudi. Zaburi 137 ndicho kiini cha Verdi cha “Kibwagizo cha Watumwa wa Kiebrania” inayogusa moyo na kuvutia. Kichwa cha Zaburi hii katika maandiko yetu ni ya matukio ya kuvutia: “Wakiwa utumwani, Wayahudi waliomboleza kando ya mito ya Babeli---Kwa sababu ya huzuni, hawangeweza kuimba nyimbo za Sayuni.

Lengo langu ni kurejelea aina nyingi za utumwa na ukandamizaji. Nitalinganisha baadhi ya hali za siku zetu na zile za siku za Yeremia kabla ya kuangamizwa kwa Yerusalemu. Katika kutoa sauti hii ya onyo, nina shukurani kwamba wengi wa washiriki wa Kanisa wanaepuka kwa wema tabia ambayo ilimchukiza Bwana sana katika wakati wa Yeremia.

Unabii na maombolezo ya Yeremia ni muhimu kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Yeremia na Yerusalemu ya siku zake ndiyo usuli wa sura za kwanza katika Kitabu cha Mormoni. Yeremia alikuwa nabii wa siku za nabii Lehi.2 Bwana alimfahamisha Yeremia kuwa tukio kubwa juu ya kuchaguliwa kwake kabla ya dunia: “Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua, na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”3

Lehi alikuwa na wito wa kipekee, utume, na kazi kutoka kwa Bwana. Hakuitwa katika ujana wake lakini katika utu uzima wake. Mwanzoni, yake ilikuwa ni sauti ya onyo, lakini baada ya kutangaza kwa uaminifu ujumbe kama ule wa Yeremia, Bwana aliamuru kwamba alipaswa kuchukua familia yake na kutoka kwenda jangwani.4 Katika kufanya hivyo, Lehi hakubariki familia yake tu bali pia watu wote.

Wakati wa miaka kabla ya kuangamizwa kwa Yerusalemu,5 jumbe ambazo Bwana alimpa Yeremia zinatisha. Yeye alisema:

“Watu wangu wamebadili utukufu wao kwa ajili ya kitu kisichofaidi.

“… Wameniacha mimi, niliye chemichemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.”6

Akizungumzia majanga ambayo yangewajia wenyeji wa Yerusalemu, Bwana aliomboleza, “ [Kwao] mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, na [wao] hawajaokoka.”7

Mungu alikusudia kwamba waume kwa wake wangekuwa huru kufanya chaguo kati ya mema na maovu. Wakati chaguzi za uovu zinakuwa hali halisi ya tamaduni ama nchi, kuna matokeo mabaya katika maisha haya na maisha yanakuja. Watu wanaweza kuwa watumwa ama kujiweka utumwani siyo tu kwa madawa hatari, ya kulevya lakini pia kwa falsafa hatari zenye uraibu, ya ambazo huchepua kutoka kwa maisha ya haki.

Kugeuka kutoka kwa kumwabudu Mungu wa kweli na aliye hai na kuabudu miungu ya uongo kama vile utajiri na umaarufu na kushiriki katika tabia isiyoadilifu na ya haki huelekeza katika utumwa katika maonyesho yake yote ya kudhuru kisiri. Haya hujumuisha utumwa wa kiroho, kimwili na kiakili na wakati mwingine huleta uangamizo. Yeremia na Lehi pia walifundisha pia kwamba wale ambao ni mwenye haki lazima wamsaidie Bwana kujenga Kanisa na ufalme Wake na kukusanya Israeli iliyotawanyika.8

Jumbe hizi zimepata mwangwi na kuimarishwa kupitia karne nyingi katika maongozi yote ya Mungu. Zimo kwenye kiini cha Urejesho wa injili ya Yesu Kristo katika haya, maongozi ya Mungu ya mwisho.

Ufungwa wa Wayahudi na kutawanywa kwa makabila ya Israeli, ikijumuisha makabila kumi, ni vipengele muhimu vya mafundisho katika Urejesho wa injili. Makabila kumi ya Israeli yaliyopotea yalijumuisha Ufalme wa Kaskazini wa Israeli na walichukuliwa mateka mpaka Ashuru katika miaka 721 kabla ya Kristo.. Walikwenda katika nchi za kaskazini.9 Makala ya imani ya kumi yetu inasema, “Tunaamini katika kukusanyika kiuhalisi kwa Israeli, na katika urejesho wa Makabila Kumi.”10 Pia tunaamini kwamba sehemu ya agano ambalo Bwana alifanya na Ibrahimu, si tu ukoo wa Ibrahimu ambao ungebarikiwa lakini pia kwamba watu wote duniani wangebarikiwa. Kama vile Mzee Russell M. Nelson amesema, mkusanyiko “si suala la kieneo. ‘Ni suala la kujitolea kwa mtu binafsi. Watu wanaweza kuletwa kwa ufahamu wa maarifa ya Bwana’ [3 Nephi 20:13] bila ya kuondoka nyumbani kwao.”11

Mafundisho yetu ni wazi: “Bwana alitawanya na kuwatesa makabila kumi na mawili ya Israeli kwa sababu ya uovu wao na uasi. Hata hivyo, Bwana pia [alitumia] huu mtawanyiko kwa watu wake waliochaguliwa miongoni mwa mataifa ya ulimwengu kubariki mataifa hayo.”12

Tunajifunza masomo yenye thamani kutoka kwa kipindi hiki cha janga. Tunapaswa tufanye kila kitu kadri ya uwezo wetu ili kuepuka dhambi na uasi uliosababisha utumwa.13 Tunatambua pia kwamba kuishi maisha ya haki ni sharti la kumsaidia Bwana katika kukusanya wateule Wake na katika mkusanyiko halisi ya Israeli.

Utumwa, ukandamizaji, ulevi, na ubarakala huja kwa aina nyingi. Zinaweza kuwa na utumwa halisi wa kimwili, lakini pia zinaweza kupoteza ama kuharibiu wakala wa kimaadili ambao unaweza kuzorotesha maendeleo yetu. Yeremia yu wazi kwamba uovu na uasi vilikuwa sababu kuu ya kuangamizwa kwa Yerusalemu, na utumwa katika Babeli.14

Aina zingine za utumwa zina madhara sawa kwa roho ya binadamu. Wakala wa kimaadili unaweza kutumiwa vibaya kwa njia nyingi.15 Nitataja nne ambazo hasa ni haribifu katika utamaduni wa sasa.

Kwanza, uraibu unaoathiri wakala, hukinza imani ya kimaadili, na kuharibu afya njema, husababisha utumwa. Athari za madawa ya kulevya na pombe, uasherati, picha za ngono, kamari, ufungwa wa kifedha, na mateso mengine hulazimisha juu ya wale walio katika utumwa na kwenye jamii mzigo wa mkuu vile kwamba ni vigumu kupima.

Pili, uraibu fulani ama mapendeleo ambayo kwa asili si maovu yanaweza kutumia mgawo wa thamani wa muda wetu ambao ungeweza kutumika kwa njia nyingine kukamilisha malengo ya heri. Hii inaweza kujumuisha matumizi kupita kiasi ya mitandao ya kijamii, video na michezo ya elektroniki, michezo, burudani, na mengine mengi.16

Jinsi tunavyohifadhi wakati kwa ajili ya familia ni moja ya masuala muhimu zaidi tunayokumbana nayo katika tamaduni nyingi. Wakati fulani ambapo nilikuwa mshiriki pekee wa Kanisa katika kampuni yetu ya mawakili, wakili mmoja mwanamke alinielezea jinsi yeye daima alihisi kama mfanya kiinimacho akijaribu kuweka mipira mitatu hewani kwa wakati mmoja. Mpira moja ulikuwa kazi yake kama wakili, mmoja ulikuwa ndoa yake, na mmoja ulikuwa watoto wake. Alikuwa karibu amekata tamaa juu ya wakati wake mwenyewe. Alikuwa na wasiwasi sana kuwa mpira moja mara yote ulikuwa ardhini. Nilipendekeza tukutane kama kikundi na kujadili vipaumbele vyetu. Tuliamua kwamba sababu ya msingi ya sisi kufanya kazi ilikuwa kusaidia familia zetu. Tulikubaliana kwamba kutengeneza fedha zaidi haikuwa muhimu hata karibu kama familia zetu, lakini tulitambua kwamba kuwahudumia wateja wetu kwa kadri ya uwezo wetu ilikuwa muhimu. Majadiliano kisha yakahamia kwa kile ambacho tulikuwa tukifanya kazini ambacho hakikuwa muhimu na kilikuwa kinyume na kuacha muda kwa ajili ya familia. Je, kulikuwa na shinikizo ya kubaki kazini ambalo halikuwa muhimu?17 Tuliamua kwamba lengo letu lingekuwa mazingira mema kwa ajili ya familia kwa wanawake na wanaume. Hebu tuwe katika mstari wa mbele katika kulinda muda kwa ajili ya familia.

Tatu, ufungwa ulioenea kote katika siku zetu, kama ilivyokuwa katika historia, ni itikadi ama imani za kisiasa ambazo ni kinyume na Injili ya Yesu Kristo. Kugeuza falsafa za wanadamu kwa ajili ya ukweli wa injili inaweza kutuelekeza mbali na urahisi wa ujumbe wa Mwokozi. Wakati Mtume Paulo alitembelea Athene, alijaribu kufundisha juu ya Ufufuo wa Yesu Kristo. Juu ya juhudi hii tunasoma katika Matendo ya Mitume, “Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana nafasi kwa neno lo lote, ila kutoa habari na kusikiliza habari za jambo jipya.18 Umati ulipogundua asili rahisi ya kidini ya ujumbe wa Paulo, ambayo haikuwa mpya, waliikataa.

Hii ni nembo ya siku zetu ambapo kweli wa injili mara nyingi hukataliwa ama kutoholiwa ili kuzifanya kupendeza zaidi kielimu ama kuwa sambamba na hali ya sasa ya utamaduni na falsafa za kiakili. Kama sisi hatutakuwa makini, tunaweza kutekwa na mienendo hii na kujiweka katika utumwa wa kiakili. Kuna sauti nyingi sasa zinazowaambia wanawake jinsi ya kuishi.19 Zinakinzana kila mara. Ya wasiwasi hasa ni falsafa ambazo hukosoa ama hukashifu wanawake ambao huchagua kujitolea inavyohitajika ili kuwa mama, walimu, walezi, ama marafiki kwa watoto.

Miezi michache iliyopita, wajukuu wetu wawili wadogo walitutembelea---mmoja kila wiki. Nilikuwa nyumbani na niliwafungulia mlango. Mke wangu, Mary, alikuwa katika chumba kingine. Katika kila tukio, baada ya kunikumbatia, walisema karibu jambo sawa. Waliangalia angalia na kisha kusema, “Napenda kuwa nyumbani kwa Bibi. Yu wapi Bibi?” Sikuwaambia, lakini nilikuwa nafikiri, “Je, si hii ni nyumba ya Babu pia?” Lakini nikagundua kwamba wakati nilikuwa kijana, familia yetu ilikuwa ikienda nyumbani kwa Bibi. Maneno ya wimbo maarufu yakanijia mawazoni, “Mtoni na kupitia msituni hadi nyumbani kwa Bibi sisi twaenda.”

Sasa, acheni niseme bila shaka kwamba ninafurahishwa sana na fursa za elimu na nafasi nyinginezo ambazo zinapatikana kwa wanawake. Ninafurahia jambo la kwamba kazi ngumu na kazi ya nyumbani ya kuchosha inayohitajika kwa wanawake imepungua katika sehemu nyingi za dunia kwa sababu ya matumizi ya kisasa na kwamba wanawake wanatoa michango mikuu katika kila uwanja wa jitihada. Lakini tukiruhusu utamaduni wetu upunguze uhusiano maalum ambao watoto wanao na akina mama na akina bibi na wengine ambao wanawalea, tutakuja kujuta.

Nne, vikosi vinavyokiuka kanuni za kidini zilizoshikiliwa kwa dhati vinaweza kusababisha utumwa. Mojawapo wa aina ya uchochezi zaidi ni wakati watu wema ambao wanahisi kuwajibika kwa Mungu kwa ajili ya tabia zao wanalazimishwa katika shughuli ambazo zinakiuka dhamiri zao, kwa mfano, wahudumu wa kiafaya wanaolazimishwa kuchagua kati ya kusaidia na utoaji wa mimba dhidi ya dhamiri zao au kupoteza ajira zao.

Kanisa ni kikundi kidogo kiasi hata wakati linapohusishwa na watu ambao wana dhana sawa. Itakuwa vigumu kubadilisha jamii kwa ujumla, lakini ni lazima tufanye kazi ili kuboresha utamaduni wa kimaadili unaotuzingira. Watakatifu wa Siku za Mwisho katika kila nchi wanapaswa wawe raia wema, washiriki katika mambo kisiasa, wajielimisha juu ya masuala, na wapige kura.

Msisitizo wetu wa kimsingi, hata hivyo, lazima daima uwe kufanya dhabihu yoyote muhimu kulinda familia yetu wenyewe na kizazi chipukizi.20 Wengi wao bado hawako utumwani kwa uraibu mkubwa ama falsafa za uongo. Lazima tusaidie kuwachanja kutokana na dunia inayoonekana kuwa kama Yerusalemu ambayo Lehi na Yeremia walipitia. Aidha, tunahitaji kuwatayarisha kufanya na kuweka maagano matakatifu na kuwa wajumbe wakuu wa kumsaidia Bwana kujenga kanisa Lake na kukusanya Israeli iliyotawanyika na wateule wa Bwana kila mahali.21 Kama vile Mafundisho na Maagano yanavyosema vyema, “Wenye haki watakusanywa kutoka miongoni mwa mataifa yote, na watakuja Sayuni, wakiimba nyimbo za shangwe zisizo na mwisho.”22

Changamoto yetu ni kuepuka utumwa wa aina yoyote, kumsaidia Bwana kuwakusanya wateule Wake, na kujitolea kwa ajili ya kizazi chipukizi. Lazima daima tukumbuke kwamba hatujiokoi wenyewe. Tunawekwa huru kwa upendo, neema, na dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi. Wakati familia ya Lehi ilipokimbia, waliongozwa na nuru ya Bwana. Tukiwa wa wakweli kwa nuru Yake, tufuate amri Zake, na kutegemea uhalali Wake, tutaepuka utumwa wa kiroho, kimwili na kiakili pamoja na maombolezo ya kutangatanga katika nyika yetu wenyewe, kwani Yeye ni mwenye nguvu kuokoa.

Acha tuepuke dhiki na huzuni ya wale ambao huanguka ufungwani na hawawezi tena kuvumilia kuimba nyimbo za Sayuni. Katika jina la Yesu Kristo, Amina.

Muhktasari

  1. Opera nyingi za Verdi, kama vile Aida, La traviata, na Il trovatore, ni miongoni mwa opera maarufu zinazofanywa kote duniani siku hizi.

  2. Ona 1 Nefi 5:13; 7:14.

  3. Yeremia 1:5.

  4. Ona 1 Nefi 2:2–3.

  5. Maangamizo ya Hekalu la Sulemani, kuanguka kwa Yerusalemu, na utumwa wa kabila la Yuda ilitokea karibu na miaka The destruction of Solomon’s temple, the downfall of Jerusalem, and the captivity of the tribe of Judah occurred in about 586 kabla Kristo.

  6. Yeremia 2:11, 13.

  7. Yeremia 8:20. Yeremia hapo mapema alikuwa ameandika maombolezo ya Bwana ya toba, “Naumwa katika moyo wangu wa ndani” (Yeremia 4:19) na akisihi, “kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja … atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo. (Yeremia 5:1).

  8. Ona Yeremia 31; 1 Nefi 10:14.

  9. Ona 2 Wafalme 17:6;Mafundisho na Maagano 110:11.

  10. Makala ya Imani 1:10; ona pia 2 Nefi 10:22.

  11. Russell M. Nelson, “The Book of Mormon and the Gathering of Israel” (hotuba iliyotolewa katika warsha ya marais wa misheni wapya, Juni 26, 2013).

  12. Guide to the Scriptures, “Israel,” scriptures.lds.org.

  13. Bwana akiongea katika siku zetu, alisema, “Na dunia yote hukaa katika dhambi, na kuugulia gizani na chini ya utumwa wa dhambi … kwa sababu hawaji kwangu” (Mafundisho na Maagano 84:49–50).

  14. Watu wasio na hatia, kwa kaweli, pia wao huwekwa utumwani.

  15. Kanuni za kimaandiko hazibadiliki, bali mbinu za utumwa, vifungoni, na maangamizo yamepiga kasi kwa njia ambayo haijapata kuonekana.

  16. Hii ilielezwa ifaavyo na kiasi kwa ucheshi fulani kwenye kurasa ya juu ya New York Times Magazine mwaka jana (Apr. 8, 2012) ikirejelea asili ya kutawala ya michezo ya elektroniki. Inasoma, “The Hyperaddictive, Time-Sucking, Relationship-Busting, Mind-Crushing Power and Allure of Silly Digital Games.” Na kisha katika uandishi mdogo: “(Ambayo si kusema sisi hatuzipendi pia.)” Hii, kwa njia la kuchekesha, inasisitiza umuhimu wa utumiaji hekima katika matumizi yetu ya uvumbuzi wa teknolojia ya ajabu ya umri wetu.

  17. Semo la kawaida katika mazingira mengi ya kazi ni “Sisi hufanya kazi kwa bidii, na hucheza kwa bidii.” Wakati mshikamano wa wafanyikazi ni muhimu, wakati “kazi na kucheza” unachukua wakati wote wa familia, inajishinda yenyewe.

  18. Acts 17:21; emphasis added.

  19. Ona Keli Goff, “Female Ivy League Graduates Have a Duty to Stay in the Workforce,” Guardian, Apr. 21, 2013, www.theguardian.com/commentisfree/2013/apr/21/female-ivy-league-graduates-stay-home-moms; Sheryl Sandberg, Lean In: Women, Work, and the Will to Lead (2013); Anne-Marie Slaughter, “Why Women Still Can’t Have It All,” The Atlantic, June 13, 2012, www.theatlantic.com/magazine/print/2012/07/why-women-still-cant-have-it-all/309020; Lois M. Collins, “Can Women ‘Have It All’ When It Comes to Work and Family Life?” Deseret News, June 28, 2012, A3; Judith Warner, “The Midcareer Timeout (Is Over),” New York Times Magazine, Aug. 11, 2013, 24–29, 38; Scott Schieman, Markus Schafer, and Mitchell McIvor, “When Leaning In Doesn’t Pay Off,” New York Times, Aug. 11, 2013, 12.

  20. Kanisa limehimiza maaskofu wasaidie familia kwa kutumia muda zaidi na vijana, wasichana, na vijana watu wazima. Maaskofu wamehimizwa kugawa majukumu zaidi katika baraza la kata katika jamii za Ukuhani wa Melkizedeki, kwa vitengo, na kwa washiriki ambao wana uwezo maalum ili kusaidia wengine ipasavyo.

  21. Ona Mafundisho na Maagano 29:7.

  22. Mafundisho na Maagano45:71.