2010–2019
Tazama Juu
Oktoba 2013


10:24

Tazama Juu

Leo ndiyo wakati wa Kutafuta ukweli na kuhakikisha kwamba ushuhuda wetu uwe strong.

Nilipokuwa na umri wa miaka minane, binamu wangu wawili nami tulitumwa kwa mji wa karibu kununua vyakula vya kutumia kwa muda wa siku 15 zijazo kwa watu 10 nyumbani kwetu. Nikitazama nyuma, ninashangazwa na kiasi cha imani bibi yangu shangazi na mjomba walikuwa nayo kwetu. Mbingu zilikuwa zimeng’aa asubuhi na jua lilikuwa limechomoza tuliondoka katika msafara wetu mdogo wa farasi tatu.

Katikati ya nyika, tulikuwa na wazo zuri kwamba tungeshuka na kucheza gololi. Kwa hivyo tulifanya hivyo---kwa muda mrefu. Tulikuwa tumefurahia sana mchezo wetu hivi kwamba hatukuona ‘ishara ya nyakati’ juu ya vichwa vyetu mawingu ya giza yaliyofunika anga. Kufikia wakati tulipogundua nini kilichokuwa kikitendeka, hatukuwa hata na wakati wa kupanda farasi wetu. Mvua kubwa na mvua ilitunyeshea kwa nguvu sana, na barafu ilikuwa inatupiga nyusoni zetu hata tusifikirie chochote ila kuvua farasi na kujificha chini ya blangeti za tandiko la farasi.

Tukiwa bila farasi, tumenyeshewa, na tunahisi baridi, tuliendelea na safari yetu, sasa tukijaribu kwenda kwa kasi tuwezavyo. Tulipokuwa tunakaribia kule tulipokuwa tunaenda, tuliona kuwa njia pana iliyokuwa ikiingia mjini ilikuwa imefurika na ilikuwa ni kama mto ikitujia. Sasa chaguo letu lililobaki lilikuwa kuangusha vikingo vyetu na kupanda ua la waya lililozingira mji. Ilikuwa usiku wakati ambapo, tukiwa tumechoka na kwa maumivu na kunyeshewa, tulitafuta pa kukaa katika nyumba ya kwanza tuliyoona tukiingia mjini. Familia nzuri changa hapo walitukausha, wakatulisha chakula kitamu cha maharagwe barito, na kisha wakatuweka kulala katika chumba chetu wenyewe. Punde tuligundua chumba kilikuwa na sakafu ya mchanga, basi tukawa na wazo lingine zuri. Tulichora duara sakafuni na kuendelea mchezo wetu wa gololi hadi tulipoanguka sakafuni kwa usingizi.

Kama watoto tulikuwa tu tunajifikiria. Kamwe hatukuwafikiria wapendwa wetu ambao walikuwa wakitutafuta mno kule nyumbani---ikiwa tulikuwa tumewafikiria, hatungechelewesha safari yetu kamwe katika jambo bure kama hilo. Na, kama tungekuwa na hekima zaidi, tungekuwa tumetazama angani, tukaona wingu la giza likikusanyika, na kuharakisha mwendo wetu kuwa mbele ya dhoruba. Sasa, hivi nilivyo na hekima kidogo zaidi, daima mimi hujikumbusha: “Usisahau kutazama juu.”

Kile nilichopitia na binamu zangu kilinifundisha kuwa makini kwa ishara za siku zetu. Tunaishi katika siku za dhoruba na dhiki Paulo ambazo alizielezea: “Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, …wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio na utakatifu; 3 …, wachonganishi, walafi, .., wapendao anasa badala ya kumpenda Mungu” (2 Timotheo 3:2–4).

Akizungumzia nyakati hizi, Mzee Dallin H. Oaks alisema: “Tunahitaji kufanya matayarisho ya kimwili na kiroho pamoja. … Na matayarisho ambayo huenda yakasahaulika kwa urahisi ni yale ambayo hayaonekani kwa urahisi na ni magumu zaidi---ya kiroho” ” (“Preparation for the Second Coming,” Ensign au Liahona, May 2004, 9). Kwa njia nyingine, usiache kutazama juu.

Kwa kuwa kuna mahitaji ya haraka ya matayarisho ya kiroho katika wakati wa dhiki kama hii, ninataka kutoa neno la onyo kuhusu ishara moja kuu ya siku za mwisho. Maisha yangu ya kazi yaliniweka mbele katika teknologia, hivyo basi ninatambua thamani iliyonayo, hasa katika mawasiliano. Habari nyingi ya binadamu hivi sasa zimo kwenye ncha za vidole vyetu. Lakini tovuti pia ina mengi ambayo ni machafu na ya kupotosha. Teknologia imewezesha zaidi uhuru wetu wa kusema, lakini pia inampa mwanablogu asiyekuwa na ujuzi heshima ya uongo. Hii ndiyo sababu, sasa, zaidi ya hapo awali, lazima tukumbuke kanuni hii ya milele: “Kwa matunda yao mtawatambua” (Mathayo 7:20).

Hasa, ninawatahadharisha msiangalie picha chafu au kuwasikiliza washtaki wa uongo wa Kristo na Nabii Joseph Smith. Vitendo vyote viwili huleta athari sawa: kupoteza Roho Mtakatifu, na nguvu yake ya kulinda, na kuhimili. Uovu na huzuni hufuata daima.

Akina ndugu na dada zangu wapendwa, mkiwahi kupata kitu kinacho tia shaka ushuhuda wako wa injili, ninawasihi mtazame juu. Tazamia chanzo cha hekima yote na ukweli. Kuza imani yenu na ushuhuda kwa neno la Mungu. Kuna wale duniani wanaotafuta kupuuza imani yenu kwa kuchanganya uongo na ukweli---nusu. Hii ndiyo maana kwa nini ni muhimu sana kubaki kila wakati ukiwa unastahili Roho. Kuwa na Roho Mtakatifu si tu jambo zuri la manufaa---ni muhimu katika kuishi kwako kiroho. Mkihifadhi maneno ya Kristo na kusikiliza kwa makini ushawishi wa Roho, hutadang’anyika Joseph Smith—Mathayo 1:37).Sisi lazima tufanye mambo haya.

Yesu Kristo, ambaye alikuwa mkamilifu, na Joseph Smith, ambaye alikiri mwenyewe kuwa hakuwa mkamilifu, wote wawili waliuliwa na washtaki wa uongo ambao hawangekubali ushuhuda wao. Tunawezaje kujua kwamba ushuhuda wao ni wa kweli---kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Joseph Smith ni nabii wa ukweli?

“Kwa matunda yao mtawajua.” Je, matunda mazuri yanaweza kutoka kwa mti mbaya? Najijulia mwenyewe kwamba Mkombozi wangu amenisamehe dhambi zangu na kuniweka huru kutokana na pingu zangu binafsi, akinileta kwa hali ya furaha ambayo hata sikujua ilikuwepo. Na najijulia mwenyewe kwamba Joseph Smith alikuwa nabii kwa sababu nimetumia ahadi rahisi katika Kitabu cha Mormoni: “Mwulize Mungu, Baba wa milele, katika jina la Kristo, ... na ikiwa mtauliza na moyo wa kweli, na kusudi halisi, mkiwa na imani katika Kristo, atawaonyesha ukweli wake kwenu, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu” (Moroni 10:4). Kwa kifupi: tazama juu.

Kuna wengine ambao huenda wakapendekeza kwamba ni lazima uwe na ushahidi wa kimwili ili kuamini katika Ufufuo wa Kristo au ukweli wa injili Yake ya urejesho. Kwao ninanukuu maneno ya Alma kwake Korihori, ambaye alikuwa anajaribu kuwashawishi wengine wasiamini: “Wewe umepata ishara za kutosha; utamjaribu Mungu wako? Unaweza kusema, nionyeshe ishara, wakati una ushuhuda wa hawa ndugu zako wote, na pia manabii watakatifu? Maandiko yamewekwa mbele yako” (Alma 30:44).

Wewe na mimi ni ushahidi ulio hai wa nguvu za ukombozi wa Mwokozi. Sisi ni ushahidi ulio hai wa utume wa Nabii Joseph na uaminifu wa Watakatifu wale wa awali ambao walibaki imara katika katika ushahidi wao. Kanisa la Yesu Kristo sasa limepanuka duniani kote na linakuwa kama isivyoshuhudiwa tena---likikubaliwa, kama katika nyakati za Kristo, na watu wanyenyekevu ambao hawahitaji kuona na kugusa ili kuamini.

Hakuna ajuaye wakati Bwana atakuja tena. Lakini nyakati hatari zimetufikia sasa. Leo ndiyo wakati wa kutazama juu kwa Chanzo cha ukweli na kuhakikisha kwamba ushuhuda wetu uko dhabiti, tayari kwa ajili ya majaribio ambayo hakika tutakumbana nayo.

Kwa kurejea kwa hadithi yangu, binamu zangu nami tuliamka asubuhi kwa jua kali na anga nzuri. Mtu akagonga mlangoni akiwatafuta wavulana watatu waliopotea. Alituweka juu ya farasi, na tukashika njia kurudi nyumbani kupitia nyika ile ile. Kamwe sitawahi kusahau kile tulichoona njiani kwenda nyumbani---umati wa watu ambao walikuwa wakitutafuta usiku mzima, matrekta na malori yao yakiwa yamekwama matopeni. Walikuwa wamepata saruji hapa na farasi kule, na walipotuona tukirudi nyumbani, ningehisi kutulia kwao na upendo wao. Katika njia ya kuingia mjini, watu wengi walingojea kutulaki, na mbele yao wote walikuwa bibi yangu mwenye upendo na mjomba wangu na shangazi. Walitukumbatia na kulia, wakiwa wamejawa na furaha kuwa waliwapata watoto wao waliopotea. Kilichokuwa cha ukumbusho mkubwa kwangu ni jinsi gani Baba etu wa Mbinguni mpendwa anatujali. Anasubiri kwa hamu kurudi kwetu nyumbani.

Kuna ishara za dhoruba zikikusanyika kote karibu nasi. Tutazame juu na kujitayarisha. Kuna usalama katika ushahidi wenye nguvu. Tuthamini na kuimarisha shuhuda zetu kila siku.

Najua tunaweza kuishi pamoja kama familia milele, kwamba Baba yetu wa Mbinguni anatusubiri, watoto Wake, na mikono yake ikiwa imenyoshwa. Najua kwamba Yesu Kristo, Mwokozi wetu, yu hai. Kama vile pamoja na Petro, mwili na damu havikukufunulia hivi, bali Baba yangu aliye Mbinguni (ona Mathayo 16:15–19). Katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.