Unataka Kuponywa?
Tunapotubu na kuongolewa kwa Bwana, tunaponywa na kutakaswa, na hatia yetu hufangiliwa mbali.
Wakati wa karamu ya furaha ya Yerusalemu, Mwokozi aliuacha umati ili kuwatafuta wale wenye shida nyingi. Aliwapata huko Bethesda, kwenye bwawa karibu na soko la kondoo ambalo lilijulikana kwa kuwavutia wenye shida.
Injili ya Yohana inatuambia kwamba karibu bwawa “hapo palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani vipofu, viwete, waliopooza, wakingojea maji yatibuliwe.
“Kwani malaika alikuwa wakati fulani, akayatibua maji na yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao” (Yohana 5:3–4).
Ujio wa Mwokozi unaelezewa katika taswira nzuri ya uchoraji wa Carl Bloch wenye kichwa cha habari Kristo Anawaponya Wagonjwa katika Bethsaida. Bloch alimwonyesha Yesu kwa upole akimnyayua “mtu aliyekosa nguvu” (Yohana 5:7) aliyekuwa amelala kando ya bwawa, akisubiri. Hapa, neno : dhaifu linamaanisha mtu ambaye hana nguvu na linatilia mkazo rehema na neema na uororo wa Mwokozi, aliyekuja kimyakimya kuwatumikia wale walioshindwa kujihudumia wenyewe.
Katika mchoro, mtu mwenye mateso alijikunyata sakafuni kwenye vivuli, akiwa amechoka na kukata tamaa baada ya mateso ya udhaifu wake kwa miaka 38.
Wakati Mwokozi akiinua upande wa nguo kwa mkono mmoja, Aliuangalia mwingine na akauliza swali lililopenya: “Je, unataka kuponywa?”
Yule mtu akajibu, “Bwana, mimi sina mtu, wa kuniingiza bwawani wakati maji yanapotibuliwa: lakini ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu” (Yohana 5:6–7).
Kuona changamoto zisizowezekana za mtu yule, Yesu anatoa jibu kubwa na lisilotarajiwa akasema:
“Simama, chukua mkeka wako na uende.
“Na mara moja yule mtu akaponywa, na akachukua mkeka wake, na akaanza kutembea” (Yohana5:8–9).
Katika mfano mwingine wa upendo, Luka anatuambia kwamba Mwokozi, akiwa anasafiri kwenda Yerusalemu, aliwakuta watu 10 wenye ukoma. Kwa sababu ya ugonjwa wao, “wakasimama mbali” (Luka 17:12).. Walikuwa wametengwa---wachafu na wasiotakikana.
“Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu,” wakapaza sauti (Luka 17:13)—kwa maneno mengine, “Kuna chochote Wewe unachoweza kutufanyia?”
Mganga Mkuu, akiwa amejawa na huruma, huku akijua kwamba imani lazima ilete miujiza na hivyo akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani” (Luka 17:14).
Walipokuwa wanakwenda kwa imani, miujiza ikatokea. Unaweza kuhisi furaha waliyokuwanayo waliposhuhudia miili yao ikitakaswa, ikiponywa na kurejeshwa mbele ya macho yao?
“Mmoja wao, alipoona kwamba ameponywa, akarudi, na kwa sauti kubwa alimtukuza Mungu,
“Na akaanguka kifudifudi miguu pake [Bwana], akimshukuru yeye. …
“Naye [Yesu] akamwambia, Inuka, enenda zako: imani yako imekuokoa” (Luka 17:15–16, 19).
Kama daktari na mpasuaji wa awali, kiini cha utendaji wangu kilikuwa kurekebisha na kusahihisha maumbile. Yesu Kristo anaponya yote maumbile na roho, na uponyaji huanza na imani.
Je, unakumbuka wakati imani na furaha yako ilikuwa imejaa tele? Kumbuka wakati ushuhuda wako mwenyewe au wakati Mungu alipokuthibitishia kwamba wewe ni mwana au binti Yake na kwamba anakupenda sana kabisa. Kama wakati huo unaonekana kupotea, unaweza kupatikana.
Mwokozi hutushauri jinsi ya kuponywa, kufanywa kuwa wazima au kuwa kamili:
“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
“Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi. ” (Mathayo 11:28–30).
“Njooni mnifuate” (Luka 18:22) anatualika tuyaache maisha yetu ya kale na shauku za kilimwengu, na kuwa viumbe vipya ambapo “vitu vya kale havina nafasi [na] vitu vyote viwe vipya” 2 Wakorintho 5:17), hata kuwa na moyo mpya, mwaminifu. Na sisi tunaponywa tena.
“Njoo karibu yangu nami nitakuja karibu yako; nitafuteni kwa bidii nanyi mtaniona; ombeni nanyi mtapata, bisheni, nanyi mtafunguliwa” (M&M 88:63).
Tunapomkaribia Yeye, tunagundua kwamba maisha yamewekwa kuwa magumu na kwamba upinzani upo katika kila kitu” (2 Nefi 2:11) si mkamilifu katika mpango wa wokovu. Upinzani, badala yake, ni sehemu muhimu ya maisha na unaimarisha matamanio yetu na huzisafisha chaguo zetu. Mabadiliko ya maisha yenyewe hutusaidia kutengeneza uhusiano wetu wa milele na Mungu----na huchora mfano wake kwenye nyuso zetu pale tunapoitoa mioyo yetu Kwake (ona Alma 5:19).
“Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Luka 22:19) ndio Mwokozi wetu aliuliza wakati ilianzisha kile tunachokiita Sakramenti. Ibada hii ya mkate na maji hufanya upya maagano matakatifu tuliyofanya na Mungu na hualika uwezo wa Upatanisho katika maisha yetu. Sisi tunaponywa kwa kuziacha zile tabia na maisha ambayo yanakomaza mioyo yetu na kufanya shingo zetu kwa ngumu.Tunapoweka chini silaha zetu za uasi” (Alma 23:7), tunakuwa kama ajenti wa kweli kwetu sisi wenyewe” (M&M 58:28), bila kupofushwa na kudanganywa na Shetani au kusikiliza sauti mbaya za walimwengu.
“Tunapotubu na kuongolewa kwa Bwana, tunaponywa na hatia zetu zitafagiliwa mbali. Tunaweza kujiuliza, kama alivyofanya Enoshi, “Imefanywaje?” Bwana anajibu: :Kwa sababu ya imani yako kwa Kristo. … Kwa hiyo, enenda, imani yako imekuponya” (Enoshi 1:7, 8).
Corrie ten Boo, mwanamke Mkristo Mdachi, alipata kuponywa bila kujali alikuwa kifungoni kipindi cha Vita Kuu vya Pili vya Dunia. Alitaabika sana, lakini tofauti na dada yake mpendwa Betsie, ambaye alifariki kwenye moja ya kambi, Corrie alipona.
Baada ya vita, mara nyingi aliongea waziwazi kuhusu tukio na kuponywa na kusamehe. Katika tukio moja mlinzi mmoja wa Kinazi ambaye alikuwa miongoni mwa waliomletea Corrie machungu huko Ravensbruk, Ujerumani, alimjia, akifurahia ujumbe wa Kristo wa toba na upendo.
‘“Ninafuraha iliyoje kwa ujumbe wako, Fraulein, alisema. ‘Kufikiria hivyo, ukiwa ukisema, Amenisafisha dhambi zangu!’
“Mkono wake ulinyooshwa kunisalimia,” Corrie anakumbuka.“Na mimi, ambaye nilihubiri mara nyingi … umuhimu wa kusamehe, sikutoa mkono wangu.
“Pamoja na kuwa na hasira, mawazo ya kulipa kisasi yaliongezeka, nikaona dhambi zake. … Bwana Yesu, niliomba, nisamehe na nisaidie nimsamehe yeye.
“Niijaribu kutabasamu, [na] nilisumbuka kuunyosha mkono wangu. Nilishindwa, Sikujisikia, hata chembe moja ya ukarimu na hisani. Na tena nikaomba kimya kimya.Yesu, siwezi kumsamehe yeye.Nipe msamaha Wako.
“Nilipoushika mkono wake kitu cha ajabu kikatokea. Toka mabegani mwangu hadi mikononi kuelekea viganjani, mkondo ulikuwa unatoka kwangu kuelekea kwake, wakati huo moyo wangu ukajawa na furaha kwaajili ya ndugu huyu.
“Na hivyo nikagundua kwamba haikuwa tena katika toba yetu zaidi ya mazuri yetu ambayo huuponya ulimwengu, bali kwa njia Yake. Anapotuambia tuwapende adui zetu, Anatupa, pamoja na amri, upendo wenyewe.”1
Corrie ten Boom alitakaswa.
Raisi Thomas S. Monson amesema, “Kuna maisha ya aina moja yanayowasaidia wale wenye matatizo au waliolemewa na huzuni na uchungu---hata Bwana Yesu Kristo.”2
Kama unajiona si msafi, hupendwi, hauna furaha, si mstahiki au si kamili, kumbuka. “Hayo yote yasiyo mazuri yanaweza kuwa mazuri kwa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.”3 Muweni na imani na subira katika wakati na madhumuni ya Mwokozi kwako. “Usiogope, amini tu” (Marko 5:36).
Mnahakikishiwa Mwokozi bado anatafuta kurekebisha nafsi zetu na mioyo yetu. Anawasubiri mlangoni na anabisha mlango, Acha tuanze tena kwa kuomba, kutubu na kusamehe na kusahau. Na tumpende Mungu and tuwatumikie majirani wetu, tusimame katika sehemu takatifu kwa maisha yaliyosafishwa. Mtu mdhaifu katika bwawa la Bethseda, mkoma katika njia ya kwenda Yerusalemu, na Corrie ten Boom aliponywa. “Unataka utakaswe?” Simama, na tembea. “Neema Yake inatosha” (2 Wakorintho 12:9), na hautatembea peke yako.
Nimekuja kujua kwamba Mungu yu hai. Ninajua kwamba sisi sote ni watoto Wake na kwamba Anatupenda kama tulivyo na jinsi tutakavyokuwa. Ninajua kwamba Alimtuma Mwanawe kuja ulimwenguni kujitoa dhabihu kwa ajili ya wanadamu wote na kwamba wale waipokeao injili Yake na kuifuata watatakaswa na kukamilishwa---“katika wakati wake mwenyewe, na katika njia yake mwenyewe, na kulingana na mapenzi yake mwenyewe (M&M 88:68), Kwa neema Zake ororo. Huu ni ushahidi wangu kwenu katika jina la Yesu Kristo, amina.