Mkutano Mkuu: Kuimarisha Imani na Ushuhuda
Ee, tunahitaji mkutano mkuu jinsi gani! Kupitia mkutano mkuu imani yetu huimarisha na shuhuda zetu kupata kina.
Asante, Rais Monson, kwa mafunzo yako na mfano wako wa huduma kama Kristo na kutupatia jukumu sisi sote kuwa wamisionari. Sisi daima tunakuombea.
Katika kipindi chetu, Mwokozi Yesu Kristo alitaja mkusanyiko wa Watakatifu kama “mkutano mkuu wangu.”1 “mkutano mkuu wangu”1
Popote tulipo katika ulimwengu huu, vyovyote tunavyopokea haya matangazo, nashuhudia kwamba tunakusanyika katika mkutano mkuu Wake. Pia mimi nashuhudia kwamba tutasikia neno Lake, kwa Yeye anasema, “iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa.”2
Mikutano mikuu daima imekuwa sehemu ya Kanisa la Yesu Kristo la kweli. Adamu aliwakusanya uzao wake na kutoa unabii wa mambo yatakayokuja. Musa alikusanya wana Israeli na kuwafunza amri alizokuwa amepokea. Mwokozi alifunza umati uliokuwa umekusanyika kote katika Nchi Takatifu na kwenye bara la Amerika. Petro aliwakusanya waumini katika Yerusalemu. Mkutano mkuu wa kwanza katika hizi siku za mwisho ulifanywa miezi miwili tu baada ya Kanisa kuanzishwa na mikutano imeendelea hivyo hadi siku ya leo.
Mikutano mikuu hii daima iko chini ya maelekezo ya Bwana, ikiongozwa na Roho Yake.3 Sisi hatupatiwi mada mahususi. Katika wiki na miezi, kila mara kupitia kukosa usingizi usiku, tunamgojea Bwana. Kupitia mfungo, kuomba, kujifunza, na kutafakari, tunajifunza ujumbe ambao Yeye anataka sisi tutoe.
Wengine wanaweza kuuliza, “Kwa nini maongozi hayaji kwa urahisi na upesi zaidi?” Bwana alimfunza Oliver Cowdery, “Unalazimika kulichunguza katika akili yako; ndipo uniulize kama ni sahihi.”4 Jumbe za mkutano mkuu huja kwetu baada ya matayarisho ya maombi, kupitia Roho Mtakatifu.
Kanuni hii ni kweli kwa washiriki wote wa Kanisa tunapojitayarisha ili kushiriki katika mikutano ya kata, vigingi, na mkutano mkuu. Tunajifunza katika akili zetu kile tunahitaji na tunatamani kutoka kwa Baba wa Mbinguni, na sisi huomba ili kuelewa na kutumia kile ambacho sisi tumefunzwa. Wakati wa mkutano mkuu unapofika, tunajitolea “tukiweka kando mambo ya ulimwengu, [ili] kutafuta mambo bora.”5 Kisha tunakusanya familia zetu kusikia neno la Bwana, kama watu wa Mfalme Binyamini walivyofanya.6
Watoto na vijana wanapenda kujumuishwa. Tunafanya makosa makubwa ikiwa tunadhamia kwamba mkutano mkuu uko juu ya akili na usikivu wa kiroho wao. Kwa washiriki vijana wa Kanisa, nawaahidi kwamba ikiwa ninyi mtasikiliza, mtahisi Roho kabisa ndani yao. Bwana atatuambia ninyi kile Yeye anataka ninyi mfanye na maisha yenu.
Katika mikutano tunapokea neno la Bwana lililodhamiriwa kwetu. Mshiriki mmoja alishuhudia: “Nilipokuwa nikisikiliza hotuba yako, nilishangaa. … Hotuba yako ilikuwa ujumbe wa kibinafsi moja kwa moja kutoka kwa Bwana hadi kwa familia yangu. Mimi sijapata uzoefu kama huo wa onyesho la Roho katika maisha yangu wakati ambapo Roho Mtakatifu aliongea moja kwa moja nami.”
Mwengine alisema, “Mimi kamwe sijahisi kwa undani kwamba hotuba ilikuwa inatolewa kwangu.”
Hii inawezaka kwa sababu Roho Mtakatifu hubeba neno la Bwana hata kwenye mioyo yetu kwa njia tunazoweza kuelewa.7 Ninapoandika habari katika mkutano mkuu, mimi daima siandiki hasa kile msemaji anasema; mimi huandika maelekezo ya kibinafsi ya kiroho yanayotolewa kwangu.
Kile kinachosemwa si muhimu kama kile tunachosikia na kile tunachohisi.8 Hio kwa nini tunafanya juhudi za kupata uzoefu wa mkutano mkuu katika mazingira ambapo sauti tuli, ndogo ya Roho inaweza kusikia, kuhisiwa, na kueleweka.
Eh, ni jinsi gani tunahitaji mkutano mkuu! Kupitia mikutano mikuu imani yetu huimarishwa na shuhuda zetu kukita mzizi. Na tunapoongoka, tunaimarisha mmoja na mwengine ili tusimame imara mbele ya mishale ya moto katika hizi siku za mwisho.9
Katika miongo ya majuzi, Kanisa limekingwa pa kubwa kutoka na kuoeleweka na mateso yaliyowapata Watakatifu wa awali. Haitakuwa hivyo daima. Ulimwengu unasonga mbali kutoka kwa Bwana kwa upesi na mbali sana kuliko kitambo. Adui amewachiliwa huru ulimwenguni. Sisi tunatazama, tunasikia, tunasoma, tunajifunza, na kushiriki maneno ya manabii ili tupata maonyo na ulinzi. Kwa mfano “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” lilitolewa kitambo sana kabla hatujapata changamoto zinazokabili familia. “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Manabii” ilitayarisha mapema zaidi ya wakati tungeihitaji sana.
Inawezekana tusijue sababu zote za kwa nini manabii na wasemaji wa mkutano mkuu hutuhutubia sisi mada fulani katika mkutano mkuu, lakini Bwana anajua. Rais Harold B. Lee alifunza: “Usalama tulionao kama washiriki wa kanisa hili ni … kutii maneno na amri ambazo Bwana atatoa kupitia nabii Wake. Kutakuwa na kitu ambacho kitahitaji subira na imani. Unaweza kuwa haupendelei kile kinachokuja kutoka kwa viongozi wenye mamlaka wa Kanisa. Kinaweza kuwa kinakinzana na maoni yako ya [kibinafsi]. Kinaweza kuwa kinakinzana na maoni yako ya kijamii. Kinaweza kuwa kinahitilafiana na baadhi ya maisha yako ya kijamii. Lakini ikiwa utasikia vitu hivi, kama vile vinatoka kwenye mdomo wa Bwana Mwenyewe, kwa subira na imani, ahadi kwamba ‘milango ya jahanamu haitawashinda; … na Bwana Mungu atazitawanya nguvu za giza kutoka mbele zako, naye atasababisha mbingu zitetemeke kwa ajili yenu, na kwa utukufu wa jina lake’ (M&M 21:6).”10
Rais Lee alijuaje kile tutakabiliana nacho katika siku zetu? Alijua kwa sababu yeye alikuwa nabii, mwonaji, na mfunuaji. Na ikiwa tunasikia na kuwatii manabii sasa, ikijumuisha wale ambao wataongea katika mkutano huu hasa, tutaimarishwa na kulindwa.
Baraka kuu kabisa za mkutano mkuu huja kwetu baada ya mkutano kuisha. Kumbuka mapangilio uliondikwa kila mara katika maandiko: tunakusanyika kusikia maneno ya Bwana, na tunarudi nyumbani kwetu kuyaishi.
Baada ya Mfalme Binyamini kuwafunza watu wake, “akalikiza ule umati, na wakarejea, kila mmoja, kulingana na jamii zao, manyumbani kwao.”11 Katika siku zake, Mfalme Limhi alifanya vivyo hivyo.12 Baada ya kuwafunza na kuwahudumia watu katika hekalu huko Utele, Mwokozi aliwasihi watu, “Kwa hivyo, nendeni nyumbani kwenu, na mfikirie vitu ambavyo nimesema, na mwulize kutoka kwa Baba, katika jina langu, ili muweze kufahamu, na kutayarisha akili zenu kwa kesho, na nitakuja kwenu tena.”13
Tunapokubali mwaliko wa Mwokozi tunapotafakari na kuomba ili kuelewa kile tumefunzwa na kisha kusonga mbele na kutenda mapenzi Yake. Kumbuka maneno ya Rais Spencer W. Kimball: “Mimi nimeamua kwamba nikienda nyumbani kutoka kwa huu mkutano [mkuu] … kuna sehemu nyingi, nyingi sana katika maisha ambazo ninaweza kukamilisha. Nimefanya orodha ya sehemu hizi akilini, na natarajia kuzifanyia kazi punde tunapomaliza.”14 Rais Monson majuzi alisema: Mimi nawahimiza msome hotuba hizi … na mtafakri jumbe zilizomo ndani yake. Nimepata katika maisha yangu mwenyewe kwamba ninanufahika zaidi kutoka kwa haya mahuburi yenye maongozi wakati ninapojifunza juu yake kwa kina kikuu.”15
Kama ziada ya kutualika sisi kuwa na mafunzo ya maandiko kibinafsi na ya familia, Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tujifunze kila mara na kutumia kile tumejifunza kutoka kwa mkutano mkuu huu. Nashuhudia kwamba wale ambao wanaweza imani yao katika Bwana na kushika ushauri huu kwa imani watapata nguvu nyingi za kujibariki wenyewe na familia zao kwa vizazi vijavyo.
Baba wa Mbinguni amepatiana njia. Katika mkutano mkuu huu, asilimia 97 ya Kanisa inaweza kusikia jumbe hizi katika lugha zao wenyewe. Mamilioni ya washiriki katika nchi 197 watatazama mkutano mkuu huu katika lugha 95. Katika siku mbili au tatu tu jumbe hizi zitaonekana katika LDS.org kwa Kiengereza, katika Kingereza na katika kipindi cha wiki moja zitaanza kupatikana katika lugha 52. Sasa tunapokea magazeti ya Kanisa yaliyochapishwa katika kipindi cha wiki tatu za mkutano mkuu. Hatuhitaji kuongejea miezi ili hotuba zifike kwa njia posta. Kwenye kompyta, simu, vyombo vingine vya eletroniki, tunaweza kusoma, kusikiliza, kutazama, na kushiriki mafundisho ya manbii. Wakati wowote, mahali popote, tunaweza kupanua elimu yetu, kuimarisha imani yetu na ushuhuda, kulinda familia zetu, na kuwaelekeza nyumbani salama.
Jumbe za mkutano mkuu pia zitajumuishwa katika mtalaa wa vijana katika mtandao. Wazazi, mnaweza kupata masomo ya vijana kwa ajili yenu wenyewe katika LDS.org. Tafuta kujua kile watoto wako wanajifunza, na hukifanye kuwa mada ya mafunzo yako mwenyewe, mazungumzo ya familia, jioni za familia nyumbani, mabaraza ya familia, na mahojiano ya kibinafsi na kila mmoja wa watoto wako kuhusu kile wanahitaji ili kufunzwa kibinafsi..
Mimi ninawahimiza washiriki wote watumie nyenzo katika tovuti za Kanisa na apuleti za rukono. Zinaendelea kuboreshwa kila mara ili kwamba ziwe rahisi kutumia na kuwiana na maisha yetu. Katika LDS.org hutap nyenzo za kukusaidia kujifunza injili, na kuimarisha nyumba zenu, na familia zenu, na kuhudumu katika wito wako. Pia unaweza kutafuta wahenga ambao wanahitaji maagizo ya hekalu na nyenzo za kukuhimili katika kazi ya wokovu, ikijumuisha kushiriki injili. Wazazi wanaweza kuchukua uongozi katika kuwatayarisha watoto wao kwa ubatizo, ukuhani, wamisionari wa muda na katika hekalu. Zinaweza kutusaidia kutembea katika njia iliyosonga na nyembamba ya maagizo na maagano ya hekalu na kuhitimu kwa baraka za uzima wa milele.
Katika mkutano mkuu wa Aprili iliyopita, katika mkutano mkuu wa ukuhani, niliongea kuhusu picha baba yangu aliyochora ya shujaa akiwa na dereya ili kunifunza kuhusu kuvalia dereya yote ya Mungu na ulinzi wa kiroho inayouleta.
Baada ya kikao hicho kuisha, baba mmoja alielezea familia kile yeye alikuwa amejifunza. Alimpatia maongozi, Jason, mwana wao kijana kupekua LDS.org ili kusikia ujumbe wangu mwenyewe. Siku chache baadaye alitokea katika jioni ya familia nyumbani ili kushiriki somo na kaka na dada zake. Huyu hapa.
Ujumbe rahisi wa mkutano mkuu, unaongozwa na Bwana, unapokelewa na mtoto, ulifunzwa kwa familia katika njia ya kibinafsi, ya nguvu. Mimi naipenda dereya ya wema yake. Naipenda ngao yake ya imani kukinga mishale ya moto ya adui. Hizi ndizo baraka za mkutano mkuu.
Ndugu na kina dada, mimi natoa ushahidi wangu maalum kwamba Bwana Yesu Kristo yu hai na anasimama katika kichwa cha Kanisa hili. Huu ni mkutano mkuu Wake. Mimi ninawaahidi katika jina Lake kwamba kama mtaomba kwa hamu ya dhati ili kusikia sauti ya Baba yenu wa Mbinguni katika hizi jumbe za mkutano mkuu huu, mtagundua kwamba Yeye amesema nanyi ili kuwasaidia, kuwaimarisha, na kuwaongoza nyumbani katika uwepo Wake. Katika jina la Yesu Kristo, amina.