Nguvu ya Usafi wa Wanawake
Welewa wako ni kufanya mema na kuwa mwema na unapofuata Roho Mtakatifu, mamlaka yako ya kimaadili na ushawishi yatakua.
Tangu kale, jamii zimetegemea nguvu ya usafi ya wanawake. Ingawa kwa hakika hayo siyo ushawishi chanya wa pekee unaotumika katika jamii, usafi wa kimsingi unaotolewa na wanawake umedhihirisha faida ya kipekee kwa wema wa jamii. Labda, kwa sababu imeenea sana, mchango huu wa wanawake mara ningi umuhimu wake hauzingatiwa. Ningependa kuonyesha shukrani kuhusu ushawishi wa wanawake wema, kutambua baadhi ya falsafa na mienendo inayoitishia, na kutoa ombi kwa wanawake kukuza nguvu ya usafi wa kiasili ulio ndani yao.
Wanawake wamezaliwa na uzuri fulani, karama ya kiungu ambayo huwafanya wajuzi katika kuinua sifa kama vile imani, ujasiri, uvumilivu, na ukuaji katika mahusiano na katika tamaduni. Wakati tunapowatukuza “imani isiyo na unafiki” inayopatikana katika Timotheo, Paulo alielezea kwamba imani “ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike.”1
Miaka Mingi iliyopita nilipoishi nchini Mexico, nilijionea mwenyewe kile ambacho Paul alimaanisha. Nakumbuka mama mmoja mdogo, mmoja kati ya wengi wa wanawake wa Kanisa katika Mexico ambao imani yao katika Mungu hutofautisha maisha yao ya kiasili kiasi kwamba wanaonekana kutoyatambua. Mwanamke huyu mpendwa alionyesha mamlaka ya usafi unaotoka kwenye uzuri ambao uliwashawishi wote wanaomzunguka kwa uzuri. Pamoja na mumewe, walijikana vitu vya anasa na mali kwa ajili ya vipaumbele vya hali ya juu, vinavyoonekana bila wazo la pili. Uwezo wake wa kuonyesha ulifanikisha kuanza kwake, kupinda na kuwianisha na watoto wake ulikuwa ni wa kipekee. Alikuwa na majukumu mengi na kazi zake mara zote ni zile za kujirudia na za ulazima, na kwa mara zote chini yake kulikuwa na ujasiri mzuri, fikra ya kuifanya kazi ya Mungu. Kama ilivyo kwa Mwokozi, yeye aliinuliwa kwa kuwabariki wengine kupitia huduma na kujitolea. Alionyesha mfano wa upendo.
Nimebarikiwa isivyo kawaida kwa ushawishi wa usafi wa wanawake, hasa mama yangu na mke wangu. Kati ya wanawake wengine ninaowatazamia kwa shukrani ni Anna Daines. Anna na mme wake, Henry, na watoto wao wanne walikuwa ni kati ya waanzilishi wa kwanza wa Kanisa katika New Jersey Marekani. Kuanzia mwaka 1930, wakati Henry alipokuwa mwanafunzi wa Udaktari katika Chuo Kikuu cha Rutgers, Yeye na Anna walifanya kazi bila kuchoka wakienda shule na wakijishughulisha na shughuli za kijumuia katika mji wa Metuchen, ambako waliishi, ili kuushinda ujinga uliokubalika kiundani wa unyanyasaji dhidi ya Wamormoni na kuifanya jamii sehemu bora kwa waazi wote kulea watoto wao.
“Anna kwa mfano alijitolea katika kituo cha Metuchen cha YMCA na kuwa muhimu sana. Kwa muda wa mwaka mmoja aliteuliwa Rais wa tawi saidizi la Kina Mama na kisha akaulizwa kugombea moja kati ya nafasi tatu wanawake katika bodi ya wakurugenzi wa YMCA. Alishinda bila kupingwa, na hivyo akaungana na baraza lile lile ambalo miaka michache tu iliyopita liliwakataa watakatifu kukusanyika katika jengo lao!” 2
Familia yangu ilihamia katika Kata ya New Brunswick nilipokuwa kijana. Dada Daines alinitambua na kudhihirisha imani kwa uwezo wangu ambayo ilinipa msikumo wa kufukia kilele---juu ya vile ningeweza bila kutiwa moyo naye. Wakati mmoja, kwa sababu ya onyo muafaka kutoka kwake, niliepukana na hali ambao kwa kweli ingeniongoza kwa majuto. Ingawa sasa hayuko tena, ushawishi wa Anna Daines unaendelea kuhisiwa na kudhihirishwa katika maisha ya watoto wake na uzao wake na wengine wasiohesabika, mimi nikiwa mmoja wao.
Bibi yangu Adena Warnick Swenson alinifundisha kuwa makini katika huduma ya ukuhani, Alinitia moyo kukariri baraka ya sakramenti kwa mkate na maji, akielezea kwamba kwa njia hii ninaweza kuzielezea katika welewa mkubwa na hisia. Kwa kuona jinsi alivyomwidhinisha babu yangu, Baba Mkuu wa Kigingi, ilijenga ndani yangu utulivu katika mambo haya matakatifu. Bibi Swenson hakujifunza jinsi ya kuendesha gari, lakini angewafundisha wavulana jinsi ya kuwa waume wenye ukuhani.
Ushawishi wa usafi wa Mwanamke hauhisiwi kwa nguvu zaidi au wenye kutumiwa kwa manufaa zaidi sehemu nyingine yoyote isipokuwa nyumbani. Hakuna njia nyingine bora ya kuwalea kizazi kinachoinuka kuliko katika nyumbani ya kiasili, ambako baba na mama wanafanya kazi katika uwiano kutosheleza mahitaji, kufundisha, na kuwalea watoto wao.
Kwa matukio yote yale, mama anaweza kuweka ushawishi usiolinganishwa na mtu mwingine yeyote katika uhusiano wowote. Kwa nguvu ya mfano wake na mafunzo, wanawe hujifunza kuheshimu uanawake na kujumuisha nidhamu na maadili ya hali ya juu katika maisha yao. Mabinti zake wanajifunza kufurahia na kukuza uadilifu wao wenyewe na kusimama kwa ajili ya kilicho sahihi tena na tena, ijapokuwa haina sifa. Upendo na mategemeo makubwa ya mama huwaongoza watoto wake kuishi na kutenda bila visababu kuwa makini kuhusu elimu na maendeleo binafsi, na kutoa michango endelevu kwa wema wa wote walio karibu nao. Mzee Neil A. Maxwell aliuliza: “Wakati historia kamili ya binadamu inafunuliwa je itakuja na mirindimo ya risasi au sauti za kuvutia nyimbo? Mapatano ya kusimamisha vita yaliyofanywa na wanajeshi au wanawake wanaoweka amani katika nyumba na katika ujirani? Je kile kilichotokea katika utoto na jiko kitakuwa cha kushawishi zaidi ya kile kilichotokea katika serikali?”3
Kilichotukuka zaidi ni jukumu la mwanamke katika uumbaji wa kutengeneza maisha. Tunajua kwamba miili yetu ina mwanzo wa kiungu4 na kwamba lazima tupate kuzaliwa kimwili na kuzaliwa kiroho ili kuufikia ulimwengu wa juu wa Ufalme wa Mungu wa Selestia. 5 Hivyo, wanawake wana jukumu la ya kipekee, (wakati mwingine wakijitolea mhanga maisha yao wenyewe), katika kazi ya Mungu na utukufu wake, “kuleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu”6 Kama bibi, mama na vioo vya jamii, wanawake wamekuwa ni walezi wa kiini cha maisha, wakifundisha kila kizazi umuhimu wa usafi wa kimwili---tendo la ndoa kabla ya ndoa na uaminifu katika ndoa. Kwa njia hii, wamekwa vishawishi vilivyoelimika katika jamii; wametuletea wanaume bora; wameendeleza uzuri wa mazingira ambamo tunakuza watoto wenye afya na usalama.
Akina dada, sitaki niwasifie zaidi kama tunavyofanya wakati mwingine katika siku ya akina mama mazungumzo ambayo huwafanya muwe na wasiwasi. Hamuhitajiki kuwa wakamilifu;7 Sidai kwamba ninyi ni (miongoni mwenu niliyempendelea ambaye yumo karibu yenu wakati huu) Ninachomaanisha ni kwamba haijalishi kama haujaolewa ama umeolewa, kama umepata watoto au la, kama ni mzee au mdogo au uko wa makamo, mamlaka ya usafi ni ya muhimu na kwamba labda tumeshindwa kugundua thamani ya ushawishi wetu. Kwa hakika kuna tabia na nguvu inayofanya kazi ambayo itamaliza na hata kuondoa ushawishi wako, kwa kudhuru mtu, familia na jamii kwa ujumla. Ngoja niwatajie nguvu tatu kama tahadhari au onyo.
Falsafa ya hatari ambayo inakandamiza ushawishi wa usafi wa wanawake ni udhoofishaji wa ndoa na umama na kazi za nyumbani kama kazi. Baadhi huchukulia kazi za nyumbani kwa kuikataa moja kwa moja, kwa kuteta kwamba inabeza wanawake na kwamba dai endelevu la kukuza watoto ni mfumo wa unyanyasaji.8 Wanawadhihaki kile wanachokiita “njia ya wamama” kama kazi. Hii siyo haki au sawa. Hatuangamizi dhamani ya kile wanawake au wanaume wanakipata katika njia zozote zile au kazi---sisi sote tunafaidi kutokana na mafanikio haya---lakini bado tunatambua kwamba hakuna uzuri mkuu kama umama na ubaba katika ndoa. Hakuna kazi ya juu, na hakuna kiasi cha pesa, mamlaka, au sifa na jumuiya inayoweza kushinda zawadi kuu ya kifamilia. Kitu chochote kile ambacho mwanamke anaweza kutikimiza, ushawishi wake wa kimaadili unatumika zaidi ya kawaida kuliko hapa.
Mitazamo juu ya jinsia ya binadamu inatishia ushawishi wa nguvu ya usafi ya wanawake ni kupunguzwa kwa hadhi ya umama na utunzaji wa nyumbani kama kazi. Utoaji mimba kwa ajili ya mtu au urahisi wa kijamii unapiga katika moyo wa mwanamke nguvu nyingi takatifu na kuharibu mamlaka yake ya usafi. Hiyo hiyo ni kweli katika uasherati na nguo za kubana ambazo hayashushi tu hadhi ya wanawake bali pia huimarisha uongo kuwa hali ya jinsia ya mwanamke huamua thamani yake.
Kwa muda mrefu kumekuwa na desturi “viwango mara mbili” ambayo inawategemea wanawake kuongozwa kingono wakati tunasahau utovu wa maadili wa wanaume. Mapungufu hayo ya haki “viwango mara mbili” ni dhahiri, na imekatazwa na kukataliwa. Katika kukataliwa huko, mtu anaweza kutegemea kwamba mwanaume atainuka juu, katika kiwango cha usafi kimoja, lakini mara nyingi kinyume chake kimetokea—wanawake na wasichana wametiwa moyo kuwa wa kipenzi zaidi kama vile “viwango mara mbili” inavyowategema kuwa. Mwanzoni viwango vya juu vya wanawake vilidai ahadi na jukumu kutoka kwa wanaume, na sasa tuna mahusiano ya mapenzi bila fikra, familia zisizo na baba, na umaskini unaoongezeka. Fursa sawa katika uchafu kirahisi inawaibia wanawake ushawishi wao wa usafi na inashusha hadhi ya jamii yote. 9 Katika mpangilio huu bila dhamani, ni wanaume ambao “wamefunguka” na wanawake na watoto wanapata shida zaidi ya wote.
Sehemu ya tatu ya wasiwasi inatoka kwa wale, katika jina la usawa, wanaotaka kufuta tofauti zote kati ya wa kiume na wa kike. Mara nyingi hii huchukua mfumo wa kuwalazimisha wanawake kuwa na tabia za kiume—kuwa na fujo zaidi, wagumu na wagomvi. Ni dhahiri sasa katika sinema na michezo ya video kuona wanawake wakiwa katika sehemu za fujo za ajabu, wakiacha miili iliyokufa na maangamizo kama matokeo ya matendo yao. Inaharibu roho kuona kuona wanaume katika nafasi hizo na hivyo hivyo si pungufu wakati wanaume wanakuwa wanachochea na kupata shida katika fujo.
Rais Mkuu mstaafu wa Wasichana Rais Margaret D Nadauld alifundisha: “Dunia ina wanawake wa kutosha ambao ni sugu; tunahitaji wanawake ambao ni wapole. Kuna wanawake wa kutosha ambao hulazimisha mambo; tunahitaji wanawake ambao ni wakarimu. Kuna wanawake wa kutosha ambao ni wajeuri; tunahitaji wanawake wanyenyekevu. Tuna wanawake wa kutosha ambao wanafahamika na ni matajiri; tunahitaji wanawake zaidi wenye imani. Tunao wenye tamaa wengi; tunahitaji wenye wema. Tunao wengi wenye madhambi; tunahitaji wengi wenye usafi. Tunao wengi wanaojulikana, tunahitaji wasafi.”10 Katika ukungu wa jinsia ya kike na kiume, tunapoteza tofauti, inayolinganisha zawadi ya wanaume na wanawake ambayo kwa pamoja inazalisha lengo zima.
Ombi Langu kwa wanawake na wasichana leo ni kulinda na kukuza nguvu ya usafi ambayo imo ndani yenu. Tunza uzuri asilia na wema na vipaji unaokuja nao hapa duniani. Fikra zako ni kufanya wema na kuwa mwema, na unapofuata Roho Mtakatifu, mamlaka yako ya usafi na ushawishi yatakua. Kwa wasichana nawaambia, usipoteze nguvu ya usafi hata kabla ya kuukuza. Chukua taadhali kwamba lugha yako ni safi, siyo ya kulazimisha; kwamba mavazi yako yanaashiria heshima, na siyo ubatili; kwamba matendo yako yanaashilia usafi, siyo ya wapenzi. Huwezi kuwainua wengine kwenye usafi kwa mkono mmoja kama unafurahia maovu kwa mkono mwingine.
Akina dada, katika mahusiano yenu yote, ni uhusiano na Mungu, Baba yenu wa Mbinguni, ambaye ni kiini cha nguvu ya usafi, ambayo lazima daima uweke kuwa kwanza katika maisha yenu. Kumbuka kwamba nguvu ya Yesu ilikuja kupitia ibada yake moja kwa mapenzi ya Baba Yake. Hakutetereka katika kile ambacho kilimpendeza Baba Yake.11 Jitahidi kuwa aina hiyo ya mfuasi wa Baba na Mwana na ushawishi wako hautafifia.
Na Msiwe na wasiwasi kufanya ushawishi huo bila woga au msamaha. “kuwa tayari kutoa na kujibu kwa kila [mtu mwanamke, na mtoto] ambaye anakuuliza sababu kwa tumaini ulilokuwa nalo.”12 “Tangaza neno; kuwa wa haraka kwa sababu, kutopitwa na wakati; onya, kanya, inua kwa uvumilivu na mafundisho.”13 “Waleeni watoto wenu katika mwanga na kweli.”14 Wafundishe [wao] kusali, na kutembea wima mbele za Mungu.”15
Katika maombi haya kwa wanawake, na isitokee mtu yeyote kupotosha maana kiutashi. Kwa kuwasifia na kutia moyo nguvu ya usafi katika wanawake, sisemi kwamba wanaume na wavulana kwa namna fulani wamepata ahueni kutoka katika kazi zao za kusimamia ukweli na haki, kwamba wajibu wao kutumikia, kujitolea, na kuongoza kwa namna moja ni wa chini kuliko wa wanawake au unaweza kuachiwa wanawake. Wanaume, na tusimame na wanawake, tusaidiane mizigo na kukuza ushiriki wetu wa nguvu ya usafi.
Wapendwa akina dada, tunategemea nguvu ya usafi mnayoileta duniani, katika ndoa, katika familia, katika Kanisa. Tunategemea katika baraka mnayoileta kutoka mbinguni kutokana na maombi na imani zenu. Tunaomba kwa ajili ya ulinzi wenu na furaha na ushawishi wenu uidhinishwe. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.