Kwa Wajukuu Wangu
Kuna amri moja muhimu ambayo itasaidia kukabiliana na changamoto na kupelekea hata kwenye kiini cha maisha ya familia yenye furaha
Mwaka huu wajukuu wetu wawili wa kwanza wataoa. Katika miaka michache wengi kama 10 hivi wa binamu zao huenda wakafikia hatua maishani mwao ambapo watafuata katika dunia ya ajabu ya uumbaji wa familia.
Matarajio hayo ya furaha yamenisababisha kutafakari kwa undani walivyoniomba ushauri. Kimsingi wameuliza, “Ni chaguo gani ninaweza kufanya ambayo yatanielekeza kwa furaha?” Na kwa upande mwingine, “Chaguo gani huenda zikanielekeza kwenye kukosa furaha?
Baba wa Mbinguni ametuumba kila mmoja wetu kipekee. Hakuna wawili wetu wapitao matukio sawa. Hakuna familia mbili ambazo ni sawa. Basi si ajabu kwamba ushauri kuhusu jinsi ya kuchagua furaha katika maisha ya familia ni mgumu kutoa. Bado Baba mpwendwa wa Mbinguni ameweka njia sawa ya furaha kwa watoto Wake wote. Chochote sifa zetu za kibinafsi au chochote kitakachokuwa matukio yetu, kuna mpango mmoja tu wa furaha. Mpango huo ni kufuata amri zote za Mungu.
Kwetu sisi sote, ikijumuisha wajukuu wangu wanaofikiria juu ya ndoa, kuna amri moja kuu ambayo itasaidia kukabiliana na changamoto na kuelekeza kwenye msingi wa maisha ya familia ya furaha. Inatumika kwa mahusiano yote bila ya kujali hali. Imerudiwa katika maandiko na katika mafunzo ya manabii katika siku zetu. Hapa kuna msemo wa Biblia juu ya ushauri wa Bwana kwa wote ambao wanataka kuishi pamoja milele katika upendo wa furaha:
“Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu, na kusema,
“Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?
“Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
“Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
“Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
“Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.”1
Kutoka kwa kauli hiyo rahisi si vigumu kufupisha yote ambayo nimejifunza kuhusu ni chaguo gani zinazoelekeza kwa furaha katika familia. Ninaanza na swali, “ Ni chaguo gani zimenielekeza kumpenda Bwana na moyo wangu wote na roho na akili zangu zote?” Kwangu mimi imekuwa kuchagua kujiweka mahali ambapo nilihisi furaha ya kusamehewa kupitia Upatanisho wa Bwana.
Miaka iliyopita, nilimbatiza kijana kule Albuquerque, New Mexico, ambaye mmisionari mwenza nami tulikuwa tumemfundisha. Nilimtia huyu mvulana majini na kumleta juu tena. Lazima iwe alikuwa karibu mrefu kama mimi kwa sababu alizungumza maskioni mwangu. Akiwa na maji kutoka kwenye kidimbwi na machozi yakitiririka usoni mwake na furaha katika sauti yake, alisema, “Mimi ni msafi, mimi ni msafi.“
Nimeona machozi hayo hayo ya furaha katika macho ya mtu ambaye alielezea maneno ya Mtume wa Mungu: Yeye alikuwa amemwambia, baada ya mahojiano ya kina na ya upendo, “Nakusamehe kwa jina la Bwana. Yeye atakupatia hakikisho la msamaha Wake katika wakati Wake mwenyewe na kwa njia Yake mwenyewe.” Na Yeye alifanya hivyo.
Nimeona ni kwa nini Bwana anaweza kusema kwamba wakati dhambi zimesamehewa. Yeye hawezi kuzikumbuka tena. Kwa uwezo wa Upatanisho, watu niliowajua vyema na kuwapenda walifanywa wawe wapya, na madhara ya dhambi yalifutiliwa mbali. Moyo wangu umejazwa na upendo kwa Mwokozi na Baba mpendwa aliyemtuma Yeye.
Baraka hiyo kuu imekuja kwa kuwahimiza watu ambao ninawajali kwenda kwa Mwokozi kwa faraja kutoka kwa uchungu ambao Yeye tu anawezakuutoa. Ndiposa ninawahimiza wale ninaowapenda wakubali na kutimiza kila wito wanaopewa Kanisani. Chaguo hilo ni ni mojawapo wa funguo kuu za furaha ya familia.
Shinikizo katika kila hatua ya maisha zinaweza kutujaribu kukataa au kupuuza wito wa kumtumikia Mwokozi. Hiyo inaweza kutuweka katika hatari ya kiroho kwetu wenyewe, wenzi wetu, na familia zetu. Baadhi ya wito unaweza kuonekana kuwa si muhimu, lakini maisha yangu, na familia yangu, ilibadilishwa kuwa bora kwa kukubali kwangu wito wa kufundisha jamii ya mashemasi. Nilihisi upendo wa mashemasi hao kwa Mwokozi na upendo Wake kwa ajili yao.
Nimeona hiyo ikifanyika katika maisha ya rais mstaafu wa kigingi na misheni katika wito Wake wa yeye kushauri jamii ya walimu. Najua kuhusu mwingine ambaye amekuwa Askofu na kisha Sabini wa Eneo ambaye alitumiwa na Bwana kumsaidia mvulana katika jamii ya walimu ambaye alijeruhiwa katika ajali. Miujiza kutoka huduma hiyo iligusa maisha ya watu wengi, ikijumuisha yangu, na kuongeza upendo wao kwake Mwokozi.
Tunapowahudumia wengine, tuna uwezekano mkubwa wa kuomba uenzi wa Roho Mtakatifu. Mafanikio katika huduma ya Bwana daima hutoa miujiza zaidi ya nguvu zetu wenyewe. Mzazi anayekabiliana na mtoto katika uasi mkubwa anajua hii ni kweli, kama alivyo mwalimu mtembelezi akijiwa na mwanamke anayetafuta faraja wakati mume wake alimwambia atamwacha. Watumishi wote wana shukrani waliomba asubuhi hio kwa Bwana atume Roho Mtakatifu kama mwenzi.
Ni tu kwa ushiriki wa Roho Mtakatifu kwamba tunaweza kutumaini kutiwa nira sawa katika ndoa huru kutokana na ugomvi. Nimeona jinsi ushirikiano huo ni muhimu kwa ajili ya furaha kuu katika ndoa. Miujiza ya kuwa kitu kimoja inahitaji msaada wa mbinguni, na inachukua muda. Lengo letu ni kuishi pamoja milele katika uwepo wa Baba wa Mbinguni na Mwokozi wetu.
Babangu na mamangu walikuwa tofauti sana. Mamangu alikuwa mwimbaji na msanii. Babangu alipenda kemia. Mara moja katika tamasha ya simfoni, mamangu alishangaa wakati babangu alisimama na kuanza kuondoka kabla makofi kuanza. Mamangu alimuuliza alipokuwa akienda. Jibu lake lilisemwa katika umaasumu wote: “Naam, imeisha, sivyo?” Ni tu ushawishi mpole wa Roho Mtakatifu ulimfikisha hapo pamoja naye katika nafasi ya kwanza na kumrudisha tena kwenye tamasha muda baada ya muda.
Mamangu aliishi kule New Jersey kwa miaka 16 ili babangu angeweza kusaidia familia kwa kufanya utafiti na kufundisha kemia. Kwake ilikuwa ni kujitolea kutengwa kutoka kwa mama yake mjane na dada yake, ambaye alikuwa hajaolewa ambaye alikuwa amemtunza katika nyumba nzee ya shamba ya familia. Wote wawili walikufa wakati mama alikuwa mbali katika New Jersey. Hizo ndizo zilikuwa nyakati pekee nilimuona mamangu akilia.
Miaka mingi baadaye babangu alipewa kazi kule Utah. Alimuuliza mamangu, tena katika umaasumu wote, “Mildred, unafikiri napaswa nifanye nini?”
Alisema, “Henry, fanya chochote unachofikiria ni bora.”
Alikataa kazi hiyo. Asubuhi ifuatayo alimwandikia barua ambayo nigependa ningalikuwa nayo bado. Mimi nakumbuka akimwambia, “Usiifungulie hapa. Nenda ofisini na uifungulie huko.” Ilianza na mkemeo. Alikuwa amemwahidi miaka iliyopita kwamba kama angewahiweza, angempeleka kuwa karibu na familia yake. Alishangazwa na kujieleza kwake kwa kuudhika. Hakuwa amekumbuka hamu ya moyo wake. Alituma ujumbe mara moja akikubali kazi.
Alisema, “Mildred, mbona haukuniambia?”
Alisema, “Ulistahili kukumbuka.”
Daima alizungumzia chaguo la kuhama na kwenda Utah kama lake mwenyewe, kamwe si kama dhabihu ya kazi yake ya kikazi. Walikuwa wamepokea muujiza wa kuwa kitu kimoja. Ingekuwa bora kama Baba angekuwa amekumbushwa na Roho Mtakatifu juu ya ahadi aliyokuwa ametoa miaka mingi awali. Lakini alimruhusu Roho Mtakatifu kufanya moyo wake kuwa mwepesi ili kwamba chaguo lake [Mildred] likawa lake.
Baba wa Mbinguni ana mtizamo kamili, anajua kila mmoja wetu, na anajua maisha yetu ya baadaye. Anajua matatizo tutakayopitia. Alimtuma Mwanawe ateseke ili kwamba angejua jinsi ya kutusaidia katika majaribio yetu yote.
Tunajua kwamba Baba wa Mbinguni ana watoto wa kiroho katika dunia hii ambao wakati mwingine huchagua dhambi na huzuni kubwa. Ndiposa alimtuma Mzaliwa Wake wa Kwanza kuwa Mkombozi wetu, kitendo kikuu cha upendo katika viumbe vyote. Ndiposa lazima tutarajie kwamba itachukua msaada wa Mungu na muda kutukwatua, kututayarisha kwa ajili ya maisha ya milele, kuishi na Baba yetu.
Maisha katika familia yatatujaribu. Hiyo ni mojawapo wa makusudi ya Mungu katika kutupatia zawadi ya maisha ya duniani---kutuimarisha kwa kupitia majaribio. Hiyo itakuwa kweli hasa katika maisha ya familia, ambapo tutapata furaha kubwa na huzuni kubwa na changamoto ambazo wakati mwingine huenda zikaonekana kuwa zaidi ya uwezo wetu kuzivumilia.
Rais George Q. Cannon alisema haya kuhusu jinsi Mungu amekutayarisha wewe na mimi na watoto wetu kwa ajili ya majaribio tutakayokabiliana nayo: “Hakuna mmoja wetu bali ule upendo wa Mungu umetolewa juu yake. Hakuna mmoja wetu ambaye Yeye hajamtunza na kumpapasa. Hakuna mmoja wetu ambaye Yeye hajataka kumuokoa, na ambaye Yeye hajaunda njia ya kumuokoa. Hakuna mmoja wetu ambaye Yeye hajamtolea malaika Wake kwa ulinzi juu yake. Tunaweza kuwa duni na kudharaulika katika mitazamo yetu wenyewe, na katika mitazamo ya watu wengine, lakini ukweli unabakia kwamba sisi ni watoto wa Mungu, na Yeye ametoa kwa kweli malaika Wake---viumbe visivyoonekana vya uwezo na nguvu---ulinzi juu yetu, na wanatulinda na wako nasi katika utunzaji wao.”2
Kile Rais Cannon alifundisha ni kweli. Utahitaji hakikisho hilo, kama vile nimelihitaji na kulitegemea.
Nimeomba kwa imani kwamba mtu niliyempenda angetafuta na kuhisi nguvu ya Upatanisho. Nimeomba na imani kwamba malaika wanadamu wangekuja katika msaada wao, na walikuja.
Mungu amebuni njia ya kuokoa kila mmoja wa watoto Wake. Kwa wengi, hiyo inajumuisha kuwekwa na ndugu ama dada ama wazazi wakuu ambao wanawapenda licha ya kile wanachofanya.
Miaka iliyopita rafiki yangu alimzungumza juu ya bibi yake. Alikuwa ameishi maisha kamili, akiwa daima mwaminifu kwa Bwana na kwa Kanisa Lake. Hata hivyo, mmoja wa wajukuu wake alichagua maisha ya uhalifu. Mwishowe alihukumiwa kifungo gerezani. Rafiki yangu alieleza kwamba bibi yake, alipoendesha gari njiani kwenye barabara kuu kumtembelea mjukuu wake katika gereza, alikuwa na machozi machoni mwake alipoomba kwa uchungu, “Nimejaribu kuishi maisha mema. Kwa nini nina hili janga la mjukuu ambaye anaonekana kuwa ameharibu maisha yake?”
Jibu lilimjia akilini kwa maneno haya: “Nilimpatiana kwako kwa sababu nilijua unaweza na ungeweza kumpenda licha ya kile alichofanya.”
Kuna somo la ajabu kwetu sote. Njia ya wazazi na wazazi wakuu na watumishi wote wa Mungu wenye upendo haitakuwa rahisi katika dunia inayooza. Hatuwezi kuwalazimisha watoto wa Mungu kuchagua njia ya furaha. Mungu hawezi kufanya hivyo kwa sababu ya walaka aliyotupa.
Baba wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa wanawapenda watoto wote wa Mungu bila kujali kile wanachochagua kufanya na kuwa. Mwokozi alilipa bei ya dhambi zote, haijalishi zinatisha vipi. Hata ingawa lazima kuwe na haki, fursa ya huruma imetolewa ambayo haitaibia haki.
Alma alionyesha tumaini hilo kwa mwanawe Koriantoni kwa maneno haya: “Kwa hivyo, kulingana na haki, mpango wa ukombozi haungeletwa, tu kwa tabia ya toba ya wanadamu katika hali hii ya majaribio, ndio, hali hii ya kujitayarisha; kwani isingekuwa masharti haya, rehema haingefaa isipokuwa iangamize kazi ya haki. Sasa kazi ya haki haingeangamizwa; ikiwa hivyo, Mungu angekoma kuwa Mungu.”3
Ujumbe wangu basi kwa wajukuu wangu, na kwetu sote tunaojaribu kufua familia za milele, Ni kwamba kuna furaha iliohakikishiwa kwa waaminifu. Kutoka kabla ya ulimwengu kuweko, Baba wa Mbinguni mwenye upendo na Mwanawe Mpendwa waliwapenda na kufanya kazi na wale ambao Wao walijua wangetanga. Mungu atawapenda milele.
Mnayo faida ya kujua kwamba walijifunza mpango wa wokovu kutoka kwa mafundisho waliyopata katika ulimwengu wa roho. Wao pamoja nanyi walikuwa waaminifu kutosha kuruhusiwa kuja katika dunia wakati wengine wengi hawakuruhusiwa.
Kwa usaidizi wa Roho Mtakatifu, kweli zote zitaletwa kwa ukumbusho wetu. Hatuwezi kumlazimisha hiyo juu ya wengine, lakini tunaweza kuwaacha waione maishani mwetu. Tunaweza daima kuchukua ujasiri kutokana na uhakika kwamba sote wakati mmoja tulihisi furaha ya kuwa pamoja kama mwana wa familia ya Baba yetu wa Mbinguni. Kwa usaidizi wa Mungu tunaweza kuhisi tumaini hilo na shangwe hio tena. Naomba hiyo iweze kuwa hivyo kwa sisi sote katika jina la Bwana Yesu Kristo, amina.