Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93: “Kupokea Utimilifu Wake”


“Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93: ‘Kupokea Utimilifu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Stefano anamwona Mungu na Yesu Kristo

Namwona Mwana wa Mtu Amesimama Mkono wa Kuume wa Mungu, na Walter Rane

Agosti 23–29

Mafundisho na Maagano 93

“Kupokea Utimilifu Wake”

Mafundisho na Maagano 93 inafundisha kwamba “ukweli ni maarifa ya mambo kama yalivyo, na kama yalivyokuwa, na kama yatakavyokuwa” (mstari wa 24). Unapojifunza sehemu hii, tafuta ukweli na andika kile unachojifunza. Upo tayari kufanya nini kuupokea ukweli? (Ona mistari ya 27–28).

Andika Misukumo Yako

“Unapopanda ngazi,” Joseph Smith alifundisha, “lazima uanze kutoka chini, na kupanda hatua kwa hatua, mpaka unafika juu; na ndivyo ilivyo kwa kanuni za injili—lazima uanze na ya kwanza, na kuendelea mpaka unajifunza kanuni zote za kuinuliwa” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith [2007], 268).

Wakati mwingine ngazi ile ya kuinuliwa inaonekana ni ya juu isivyowezekana, lakini tulizaliwa kuipanda mpaka juu. Mapungufu yoyote yale tunayoweza kuyaona ndani yetu, Baba wa Mbinguni na Mwanaye wanaona kitu fulani kitukufu ndani yetu, kitu fulani cha kiungu. Kama vile Yesu Kristo “alikuwa hapo mwanzo na Baba,” kwa hiyo “ninyi pia mlikuwepo” (Mafundisho na Maagano 93:21, 23). Kama vile Yeye “alivyoendelea kutoka neema hadi neema, mpaka alipopokea utimilifu,” kwa hiyo pia “mtapokea neema juu ya neema” (mistari ya 13, 20). Injili ya urejesho inatufundisha kuhusu asili ya kweli ya Mungu, na kwa hiyo pia inatufundisha kuhusu sisi wenyewe na kile tunachoweza kuwa. Licha ya juhudi za “yule mwovu” (mstari wa 39)—na licha ya kile unachohisi kwamba huna—wewe ni mtoto halisi wa Mungu mwenye kuweza kuwa “kwa wakati wake mpokee utimilifu wake” (mstari wa 19).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 93

Tunamwabudu Mungu Baba na Mwanaye, Yesu Kristo.

Kuzungumzia ufunuo katika Mafundisho na Maagano 93, Bwana alielezea, “Ninayatoa kwenu ninyi maneno haya ili muweze kufahamu na kujua namna ya kuabudu, na kujua nini mnachokiabudu, ili muweze kuja kwa Baba katika jina langu, na kwa wakati wake mpokee utimilifu wake” (mstari wa 19). Unapojifunza ufunuo huu, wekea alama kweli unazozipata kuhusu Viumbe tunavyoviabudu: Mungu Baba na Mwanaye, Yesu Kristo. Je, ni kitu gani unajifunza kuhusu “jinsi ya kuwaabudu” Wao? Kuhusu jinsi ya “kuja kwa Baba”?

Nabii Joseph Smith alifundisha, “Kama watu hawawezi kuelewa sifa ya Mungu, hawajielewi wao wenyewe”(Mafundisho: Joseph Smith, 40). Unapojifunza kuhusu Mwokozi kwa kujifunza Mafundisho na Maagano 93, pia tafuta kile unachojifunza kuhusu wewe mwenyewe. Kwa mfano, unajifunza nini kuhusu Yeye kutoka mistari ya 3, 12, 21, na 26? Ni kweli gani zinazofanana unazozipata kuhusu wewe mwenyewe katika mistari ya 20, 23, na 28–29? (Ona pia 1 Yohana 3:2; 3 Nefi 27:27; Dean M. Davis, “Baraka za Kuabudu,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 93–95.)

Mafundisho na Maagano 93:1–39

Utukufu wa Mungu ni nuru na kweli.

Unaweza kuona kwamba utukufu, nuru, na kweli vinakuja mara kwa mara katika ufunuo huu. Unapojifunza mistari ya 21–39 hasa, tengeneza orodha ya kweli unazojifunza kuhusu utukufu, nuru, na kweli. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinakutia moyo kutafuta nuru zaidi na kweli? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinaathiri jinsi unavyoishi maisha yako ya kila siku?

dirisha la vioo

Tunapokea nuru na kweli tunapotii amri za Mungu.

Mafundisho na Maagano 93:40–50

“Iweke sawa sawa nyumba yako mwenyewe.”

Karibia na mstari wa 40, Mafundisho na Maagano 93 inaonekana kubadilika kutoka mafundisho kuhusu utukufu wa Mungu na uwezekano wetu wa kiungu hadi kwenye maelekezo kuhusu malezi na kuweka nyumba zetu sawa sawa. Jinsi gani mafundisho ya Bwana kuhusu nuru, ukweli, na utukufu katika mistari ya 1–39 inakusaidia kuelewa na kufuata ushauri katika mistari ya 40–50?

Ona pia David A. Bednar, “More Diligent and Concerned at Home,,” Ensign au Liahona, Nov. 2009, 17–20.

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 93:2.Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo amekuwa “nuru ya kweli” katika maisha yetu? Ni kwa jinsi gani tumeona Nuru Yake kwa watu wengine wanaotuzunguka?

Mafundisho na Maagano 93:3–29.Ili kusaidia familia yako kujadili kile wanachojifunza katika sehemu ya 93 kuhusu Mwokozi na wao wenyewe, mngeweza kucheza mchezo wa kufananisha. Kwa mfano, mngeweza kuandaa seti moja ya karata na mistari kutoka sehemu ya 93 ambayo inafundisha kweli kuhusu Mwokozi (ona mistari ya 3, 12, 21, 26) na seti nyingine ambayo inafundisha kitu kinachofanana kuhusu sisi wenyewe (ona mistari ya 20, 23, 28–29). Wanafamilia wangeweza kuchukua karata kwa zamu kutoka kila seti, kusoma mistari, na kujaribu kutafuta kweli ambazo zinafanana. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinaathiri jinsi tunavyohisi kuhusu Mwokozi na kuhusu sisi wenyewe?

Mafundisho na Maagano 93:12–13, 20.Inamaanisha nini kupokea “neema juu ya neema” na kuendelea “kutoka neema hadi neema”? (mistari ya 12–13). Mistari hii inapendekeza nini kuhusu jinsi tunavyokua na kujifunza? Ni kwa jinsi gani kujua hivi kunaathiri jinsi tunayowatendea wengine—na sisi wenyewe?

Mafundisho na Maagano 93:24.Soma ufafanuzi wa ukweli unaopatikana katika mstari huu, na waalike wanafamilia kushiriki kitu fulani kutoka sehemu ya 93 ambacho wanafikiria kuwa ukweli wenye thamani kuu. Fafanuzi zipi zingine za ukweli tunazipata katika Yohana 14:6; Yakobo 4:13; au wimbo wa Kanisa kuhusu ukweli, kama vile “Oh Say, What Is Truth?” (Nyimbo za Kanisa, na. 272).

Mafundisho na Maagano 93:40.Pengine unaposoma mstari huu, familia yako ingeweza kuimba wimbo kuhusu kujifunza nyumbani, kama vile “Teach Me to Walk in the Light” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 177). Watoto wadogo wanaweza kufurahia kufanya vitendo vinavyoendana na maneno. Je, unahisi kuongozwa kufanya nini kualika “nuru na ukweli” zaidi katika nyumba yako?

Mafundisho na Maagano 93:41–50.Shaurianeni pamoja kama familia kuhusu nini kinaweza kisiwe “sahihi katika nyumba yenu.” Tunaweza kufanya nini “kuweka sawa sawa nyumba [yetu]”? (mistari ya 43–44).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Mie Mwana wa Mungu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3.

Kuboresha Kujifunza Kwetu

Soma zaidi ya mara moja. Unaweza kuchagua kusoma Mafundisho na Maagano 93 zaidi ya mara moja wakati wa wiki. Kila wakati unaposoma, unaweza kuona kwamba kweli tofauti zinajitokeza kwako au zinakutia moyo katika njia mpya. Kusoma mara nyingi pia kutatoa fursa kwako kutafakari kwa undani zaidi.

Yesu Kristo

Nuru na Ukweli, na Simon Dewey