Mafundisho na Maagano 2021
Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84: “Nguvu za Uchamungu”


“Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84: ‘Nguvu za Uchamungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Joseph Smith akipokea Ukuhani wa Melkizedeki

Urejesho, na Liz Lemon Swindle

Julai 26–Agosti 1

Mafundisho na Maagano 84

“Nguvu za Uchamungu”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 84, tafakari ushauri wa “kuishi kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu” (mstari wa 44). Ni kwa jinsi gani utaishi kwa maneno katika ufunuo huu?

Andika Misukumo Yako

Tangu ukuhani uliporejeshwa mnamo 1829, Watakatifu wa Siku za Mwisho wamekuwa wakibarikiwa kwa nguvu hiyo takatifu. Walibatizwa, kuthibitishwa, na kuitwa kutumikia kwa mamlaka ya ukuhani, kama vile ilivyo kwetu leo. Lakini kufikia nguvu ya ukuhani si sawa na kuielewa kikamilifu, na Mungu alikuwa na ziada Aliyotaka Watakatifu Wake kuelewa—hasa kwa urejesho uliokuwa ukija wa ibada za hekaluni. Ufunuo wa mwaka 1832 juu ya ukuhani, sasa Mafundisho na Maagano 84, uliongeza uoni wa Watakatifu wa kile ukuhani ulicho hasa. Na unaweza kufanya kitu sawa na hicho leo. Kwani kuna mengi ya kujifunza kuhusu nguvu takatifu ambayo inashikilia “ufunguo wa ufahamu wa Mungu,” ambayo hufanya “nguvu za Mungu,” zidhihirike na ambayo hututayarisha “kuuona uso wa Mungu, hata Baba, na kuishi” (mistari 19–22).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 84:1–5; 17–28

Ninaweza kufikia nguvu ya ukuhani na baraka za Mungu.

Unapofikiria neno ukuhani, nini huja akilini mwako? Ni mara ngapi unafikiria kuhusu ukuhani na ushawishi wake kwenye maisha yako ya kila siku? Baada ya kutafakari maswali haya, jifunze Mafundisho na Maagano 84:1–5, 17–28, na zingatia kile Bwana anachokutaka ujue kuhusu nguvu Yake ya ukuhani. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mistari hii kuelezea ukuhani kwa mtu na kufafanua malengo yake?

Ungeweza pia kutafakari kuhusu ibada za ukuhani ulizozishiriki. Ni kwa jinsi gani umeona “nguvu za uchamungu” (mstari wa 20) zikijidhihirisha ndani yake? Zingatia kile Bwana anachokutaka ufanye ili upokee nguvu zake kwa wingi kwenye maisha yako.

Ona pia M. Russell Ballard, “Wanaume na Wanawake na Nguvu ya Ukuhani,” Ensign, Sept. 2014, 28–33; Mada za Injili, “Ukuhani,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Mafundisho na Maagano 84:31–42

Ikiwa ninampokea Bwana na watumishi Wake, nitapokea vyote Baba alivyo navyo.

Mzee Paul B. Pieper alifundisha: “ni ya kupendeza kwamba katika kiapo na agano la ukuhani [Mafundisho na Maagano 84:31–42], Bwana anatumia vitenzi pata na pokea. Hatumii kitenzi tawaza. Ni hekaluni ambapo wanaume na wanawake—kwa pamoja—hupata na kupokea baraka na nguvu za Ukuhani wa Haruni na Melkizedeki” (“Uhalisia Uliofunuliwa wa Maisha ya Kufa,” Ensign, Jan. 2016, 21).

Unapojifunza Mafundisho na Maagano 84:31–42, tafuta maneno “pata” na “pokea.” Tafakari kile yanachoweza kumaanisha katika muktadha huu. Ni kwa jinsi gani “unampokea” Bwana na watumishi Wake?

Ungeweza pia kugundua ahadi katika mistari hii pamoja na kiapo na agano la ukuhani, ambalo Mungu “hawezi kulivunja” (mstari wa 40). Nini unapata ambacho kinakupa msukumo kuwa mwaminifu zaidi katika kumpokea Baba, watumishi Wake, na nguvu Yake ya ukuhani?

Ona pia Mwongozo kwenye Maandiko, “Agano,” “Kiapo,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org.

Mafundisho na Maagano 84:43–58

Ninakuja kwa Kristo wakati ninapofuata maneno Yake na kumsikiliza Roho Wake.

Kusoma maandiko mara kwa mara na maneno ya manabii ni zaidi ya kipengele cha kuweka alama ya kosa kwenye orodha ya mambo ya kufanya ya kiroho. Ni kweli zipi unapata katika Mafundisho na Maagano 84:43–58 ambazo zinakusaidia kuelewa kwa nini unahitaji kwa uendelevu kujifunza neno la Mungu? Ona tofauti kati ya iliyofifia na giza katika mistari hii; ni kwa jinsi gani “kufanya bidii ya usikivu kwa maneno ya uzima wa milele” kumeleta nuru, ukweli, na “Roho ya Yesu Kristo” kwenye maisha yako? (mistari 43, 45).

Ona Pia 2 Nefi 32:3; “Kitabu cha Mormoni—Jiwe Kuu la Tao la Dini Yetu,” Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Ezra Taft Benson (2014), 125–35.

Picha
mwanamke akijifunza maandiko

Kujifunza maandiko hunisaidia kuhisi ushawishi wa Roho.

Mafundisho na Maagano 84:6 2–91

Bwana atakuwa pamoja nami wakati ninapokuwa katika huduma Yake.

Unaposoma mistari hii, ungeweza kugundua njia Bwana alizosema Angewasaidia Mitume na wamisionari Wake. Ni kwa jinsi gani ahadi hizi zinahusika kwenye kazi Aliyotuomba kufanya? Kwa mfano, ni kwa jinsi gani ahadi katika mstari wa 88 zimetimizwa katika maisha yako?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 84:6–18.Baada ya kusoma jinsi Musa alivyopokea mamlaka ya ukuhani wake, mwenye ukuhani angeweza kushiriki uzoefu wake wa kutawazwa kwenye ofisi ya ukuhani. Ikiwezekana, angeweza kushiriki na kujadili mtitiriko wake wa mamlaka ya ukuhani. Kwa nini ni muhimu kwamba tuweze kufuatilia mamlaka ya ukuhani Kanisani kuanzia leo kurudi mpaka kwenye mamlaka ya Yesu Kristo? Ili kuomba mtiririko wa mamlaka, tuma barua pepe kwenda lineofauthority@ChurchofJesusChrist.org.

Mafundisho na Maagano 84:20–21.Ni lini familia yako ilipata uzoefu wa “nguvu za uchamungu” zikidhihirishwa kupitia ibada kama ubatizo au sakramenti? Pengine mngeweza kuzungumza kuhusu jinsi ibada hizi zinavyoleta nguvu ya Mungu kwenye maisha yetu. Ungeweza pia kuonesha picha ya hekalu na kujadili jinsi ibada za hekaluni zinavyotupatia nguvu ya ziada ili kuwa kama Mwokozi. Mnaweza kutaka kuimba wimbo kuhusu ukuhani, kama vile “The Priesthood Is Restored” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,89), na kujadili wimbo huu unafundisha nini kuhusu ukuhani.

Mafundisho na Maagano 84:43–44.Mngeweza kuandaa chakula au fadhila pamoja na kukipa jina kila kiungo kwa neno au kifungu cha neno kutoka mstari wa 44. Kwa nini ni muhimu kwamba tujumuishe viungo vyote? Kwa nini ni muhimu kuishi kwa kila neno la Mungu?

Mafundisho na Maagano 84:98–102.Tunajifunza nini kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye “wimbo mpya” (mstari wa 98) katika mistari hii? Nini tunaweza kufanya katika siku yetu ili kusaidia kuleta hali zilizofafanuliwa katika wimbo huu?

Mafundisho na Maagano 84:106–10.Ni kwa jinsi gani familia yetu “inajengwa kwa pamoja” kwa vipawa na juhudi za “kila mwanafamilia”? (mstari wa 110).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “The Priesthood Is Restored,” Kitabu cha nyimbo cha watoto,89; ona pia “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Maandiko Kwa Familia Yako.”

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa na fuatilia mialiko ya kutenda. Unapowaalika wanafamilia yako kutenda katika kile wanachojifunza, unawaonesha kwamba injili ni jambo la kuishi, si tu kuzungumziwa. Unaweza kuwaalika kufanya nini kutoka kwenye kujifunza kwako Mafundisho na Maagano 84?

Picha
Hekalu la Rome Italia

Hekalu la Rome Italia

Chapisha