Mafundisho na Maagano 2021
Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83: “Kwani yule Aliyepewa Vingi Kwake Huyo Vitatakiwa Vingi”


“Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83: ‘Kwani yule Aliyepewa Vingi Kwake Huyo Vitatakiwa Vingi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Kristo na kijana tajiri mtawala

Kristo na Kijana Tajiri Mtawala,, na Heinrich Hofmann

Julai 19–25

Mafundisho na Maagano 81–83

“Kwani yule Aliyepewa Vingi Kwake Huyo Vitatakiwa Vingi”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 81–83, andika kanuni ambayo inaweza kukusaidia kufanya mema kwa familia yako, rafiki zako, pamoja na wengine.

Andika Misukumo Yako

Mnamo March 1832, Bwana alimwita Jesse Gause kuwa mshauri wa Joseph Smith katika Urais wa Ukuhani Mkuu (sasa ukiitwa Urais wa Kwanza). Mafundisho na Maagano 81 ni ufunuo kwa Kaka Gause, ukimuelekeza katika wito wake mpya na kumwahidi baraka za kutumikia kwa uaminifu. Lakini Jesse Gause hakutumikia kwa uaminifu. Hivyo Frederick G. Williams aliitwa badala yake, na jina la kaka Williams lilichukua nafasi ya jina la Kaka Gause katika ufunuo.

Hilo linaweza kuonekana kama kipengele kidogo, lakini linadokeza ukweli muhimu: Wingi wa ufunuo katika Mafundisho na Maagano umeelekezwa kwa watu maalumu, lakini daima tunaweza kutafuta njia za kuutumia kwetu wenyewe (ona 1 Nefi 19:23). Ushauri wa Bwana kwa Frederick G. Williams wa “kuyaimarisha magoti yaliyo dhaifu” unaweza kugeuza akili zetu kwa watu ambao tungeweza kuwaimarisha (Mafundisho na Maagano 81:5). Ushauri wa Bwana kwa washiriki wa Taasisi ya Muungano wa “jifungeni wenyewe kwa agano hili” ili kukidhi mahitaji ya kimwili ya Kanisa unaweza kugeuza akili zetu kuelekea maagano yetu wenyewe. Na ahadi ya Bwana kwamba Yeye “angefungwa wakati ninyi mnapofanya ninayosema” inaweza kutukumbusha juu ya ahadi Zake kwetu wakati tunapotubu (Mafundisho na Maagano 82:10, 15). Hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa, kwani Bwana pia ametangaza, “lile nisemalo kwa mmoja ninalisema kwa wote” (mstari wa 5).

Ona “Newel K. Whitney and the United Firm,” “Jesse Gause: Counselor to the Prophet,” Ufunuo katika Muktadha, 142–47, 155–57.

ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 81

Naweza kuwa mwaminifu katika kufanya kile ambacho Bwana ananiomba kufanya.

Je, wakati mwingine unajiuliza jinsi unavyoweza kutimiza majukumu muhimu kwenye maisha yako? Kama mshauri wa nabii Joseph Smith, Frederick G. Williams hakika alikuwa na majukumu mengi muhimu. Katika sehemu ya 81, Bwana alimpa ushauri kuhusu jinsi ya kuyatimiza. Nini unapata katika sehemu hii ambacho kinaweza kukusaidia kutimiza majukumu yaliyotolewa kwako na Bwana?

Haya ni baadhi ya maswali ya kukusaidia kutafakari mstari wa 5:

  • Ni zipi baadhi ya njia mtu anaweza kuwa “dhaifu”? Inamaanisha nini “kuwasaidia” wale walio dhaifu?

  • Nini kingeweza kusababisha mikono ya mtu kuwa katika lugha ya picha “imelegea”? Ni kwa jinsi gani tunaweza “kuiinua” mikono hiyo?

  • Kifungu cha maneno “magoti dhaifu” kingeweza kumaanisha nini? Ni kwa jinsi gani tunaweza “kuimarisha” magoti hayo yaliyolegea?

Pengine kusoma mstari huu kumemleta akilini mtu fulani ambaye ungeweza “kumsaidia,” “kumwinua,” au “kumuimarisha.” Utafanya nini ili kumhudumia mtu huyo?

Sidney Rigdon, Joseph Smith, Frederick G. Williams

Urais wa Kwanza: Sidney Rigdon, Joseph Smith, Frederick G. Williams

Mafundisho na Maagano 82:1–7

Bwana ananialika kutubu na kuacha dhambi zangu.

Unaposoma Mafundisho na Maagano 82: 1–7, fikiria kutengeneza orodha mbili za mambo unayojifunza: maonyo kuhusu dhambi na kweli kuhusu msamaha. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinakusaidia kukinza majaribu ya adui?

Mafundisho na Maagano 82:8–10

Amri ni kwa ajili ya wokovu na ulinzi wangu.

Ikiwa wewe—au mtu unayemfahamu—amewahi kujiuliza kwa nini Bwana hutoa amri nyingi sana, Mafundisho na Maagano 82:8–10 ingeweza kusaidia. Ni utambuzi gani katika mistari hii ungeweza kukusaidia kumfafanulia mtu kwa nini unachagua kufuata amri za Bwana? Ungeweza pia kuzingatia jinsi amri Zake zilivyobadili maisha yako. Unajifunza nini kuhusu Bwana unaposoma mstari wa 10?

Ona pia Mafundisho na Maagano 130:20–21; Carole M. Stephens, “Mkinipenda, Mtazishika Amri Zangu,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 118–20.

Mafundisho na Maagano 83

“Wajane na yatima watahudumiwa.”

Mnamo April 1832, kama ilivyoelekezwa na Bwana, Joseph Smith alisafiri karibu maili 800 kuwatembelea Watakatifu ambao walikuwa wamekusanyika Missouri (ona Mafundisho na Maagano 78:9). Jamii moja aliyoitembelea ilijumuisha wajane ambao walikuwa wakilea watoto wao peke yao. Kati yao walikuwa Phebe Peck na Anna Rogers, ambao Nabii aliwafahamu kibinafsi. Huko Missouri mnamo miaka ya 1830, sheria za nchi ziliwapa wajane haki zenye ukomo kwenye mali za waume zao waliofariki. Tunajifunza nini kutoka sehemu ya 83 kuhusu jinsi Bwana anavyohisi kuhusu wajane na yatima? Je, unamfahamu yeyote katika hali hii ambaye angenufaika kutokana na upendo wako na kujali kwako?

Ona pia Isaya 1:17; Yakobo 1:27.

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 81:3.Ungeweza kutoa mioyo ya karatasi kwa wanafamilia na kuwaalika kuchora au kuandika jambo ambalo wangependa kuliombea. Zungumza kuhusu kile inachomaanisha “kusali daima kwa sauti na katika moyo.”

Mafundisho na Maagani 81:5Ili kujifunza kuhusu kanuni katika mstari huu, pengine wanafamilia wangeweza kushiriki mifano ya wakati walipohisi “wadhaifu” au “waliolegea” na mtu fulani akawasaidia au kuwaimarisha. Mngeweza pia kutazama video kuhusu kuwatumikia wengine, kama vile “Works of God” or “The Miracle of the Roof” (ChurchofJesusChrist.org). Jadilini kuhusu jinsi familia yenu inavyoweza kutumikiana mara kwa mara katika njia rahisi.

Mafundisho na Maagano 82:8–10.Pengine mchezo rahisi ungeweza kusaidia familia yako kuhisi wenye shukrani kwa amri za Mungu. Mwanafamilia mmoja angeweza kutoa maelekezo ili kumsaidia mwanafamilia aliyefungwa macho kutengeneza sandwichi au kupita njia yenye vizuizi. Fikiria jambo la kufurahisha na la ubunifu! Kisha jadilini jinsi amri za Mungu zilivyo kama maelekezo katika mchezo huu.

Mafundisho na Maagano 82:18–19.Nini kila mwanafamilia anaweza kufanya ili “aweze kuongeza talanta [yake]” na “kuongeza talanta zingine”? Ingeweza kuwa ya kufurahisha kuwa na maonesho ya familia ya talanta. Fikiria njia za kujumuisha talanta ambazo hazionekani kwa urahisi (kama vile vipawa vya roho; ona Mafundisho na Maagano 46:11–26). Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia na kushiriki vitu tulivyonavyo ili kubariki familia zetu na majirani? Inamaanisha nini kutumia talanta zetu “jicho likiwa kwenye utukufu wa Mungu”?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Have I Done Any Good?Nyimbo za Kanisa, na. 223; ona pia “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Maandiko kwa Familia Yako.”

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali yanayoongoza kwenye kutenda. Zingatia maswali ambayo yanawachochea wanafamilia wako kutafakari kuhusu jinsi wanavyoweza kuishi injili kikamilifu zaidi. “Haya kwa kawaida si maswali ya majadiliano; ni kwa ajili ya tafakari binafsi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,31).

Yesu anamponya mtu

Kielelezo cha Yesu akimponya mtu na Dan Burr