Mafundisho na Maagano 2021
Julai 5–11. Mafundisho na Maagano 76: “Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele”


“Julai 5–11. Mafundisho na Maagano 76: ‘Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021) (2020)

“Julai 5–11. Mafundisho na Maagano 76,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Kundi la nyota katika anga

Kimbilio, na Shaelynn Abel

Julai 5–11

Mafundisho na Maagano 76

“Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele”

Katika sehemu ya 76, Bwana alielezea jinsi Anavyotaka kufunua ukweli kwetu (ona mistari 7–10). Soma maandiko ukiwa na imani kwamba Yeye anaweza na atafunua kwako “mambo ya Mungu” (mstari wa 12) ambayo unahitaji kujua. Kisha andika umaizi unaopokea “wakati [ukiwa] bado katika Roho” (mistari 28, 80, 113).

Andika Misukumo Yako

“Nini kitatokea kwangu baada ya kufa?” Karibu kila dini ulimwenguni inazungumzia swali hili katika baadhi ya utaratibu mmoja au mwingine. Kwa karne, tamaduni nyingi za Kikristo, zikitegemea mafundisho ya Biblia, zimefundisha juu ya mbingu na dunia, juu ya paradiso kwa ajili ya wenye haki na mateso kwa ajili ya waovu. Lakini je, familia yote ya mwanadamu inaweza kweli kugawanyika kwa kuzingatia hasa wema na uovu? Na neno mbingu linamaanisha nini hasa? Mnamo Februari 1832, Joseph Smith na Sidney Rigdon walijiuliza ikiwa hakukuwa na ya ziada ya kujua juu ya mada hiyo (ona Mafundisho na Maagano 76, kichwa cha habari cha sehemu).

Hakika kilikuwepo. Wakati wakitafakari mambo haya, Bwana “aligusa macho ya ufahamu [wao] nayo yakafunguka” (mstari wa 19). Joseph na Sidney walipokea ufunuo wa kupendeza sana, mpana sana, wa kuangaza sana, ambao Watakatifu kwa urahisi waliuita “Ono.” Lilifungua madirisha ya mbinguni na kuwapa watoto wa Mungu mtazamo wa kupanua mtazamo wa umilele. Ono lilifunua kwamba mbingu ni tukufu na pana na yenye mjumuisho zaidi kuliko watu wengi walivyowahi kufikiria kabla. Mungu ana rehema nyingi na ni mwenye haki kuliko tunavyoweza kufikiri. Na watoto wa Mungu wana takdiri ya milele yenye utukufu kuliko tunavyoweza kudhani.

Ona Watakatifu, 1:147–50; “Ono,” Ufunuo katika Muktadha, 148–54.

ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 76

Wokovu huja kupitia Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.

Wakati Wilford Woodruff anasoma ono lililoelezewa katika sehemu ya 76, alisema, “nilihisi kumpenda Bwana zaidi kuliko hapo kabla katika maisha yangu” (ona, “Sauti za Urejesho” mwishoni mwa muhtasari huu). Pengine umekuwa na hisia sawa na hizo wakati uliposoma ufunuo huu. Hata hivyo, hakuna baraka tukufu iliyoelezewa katika sehemu ya 76 ingewezekana bila Mwokozi. Pengine ungeweza kutambulisha kila mstari katika sehemu ya 76 ambao unamtaja Bwana Yesu Kristo. Ni nini mistari hii inakufundisha kuhusu Yeye na jukumu Lake katika mpango wa Mungu? Ni kwa jinsi gani inashawishi jinsi unavyohisi kuhusu Yeye? Unaposoma na kutafakari, unaweza kupokea misukumo kuhusu jinsi unavyoweza “[kupokea] ushuhuda wa Yesu” na kuwa zaidi “jasiri” katika hilo (mstari wa 51, 79).

Mafundisho na Maagano 76:39–44; 50–112

Mungu anakusudia kuokoa “kazi zote za mikono yake.”

Baadhi ya watu, ikiwa ni pamoja na waumini wa mwanzo wa Kanisa, walipinga ono katika sehemu ya 76 kwa sababu lilifundisha kwamba karibu kila mmoja angeokolewa na kupokea baadhi ya falme za utukufu. Kupinga kwao kunaweza kuwa kulikuja, kwa sehemu, kutokana na kutokuelewa kuhusu Mungu na uhusiano Wake kwetu. Unaposoma ufunuo huu, nini unajifunza kuhusu sifa ya Mungu na mpango Wake kwa watoto Wake.

Fikiria tofauti kati ya kuokolewa (kutokana na kifo cha kimwili na kifo cha kiroho; ona mistari 39, 43–44) na kuinuliwa (kuishi na Mungu na kuwa kama Yeye; ona mistari 50–70)

Ona pia Yohana 3:16–17; Mafundisho na Maagano 132:20–25.

Mafundisho na Maagano 76:50–70; 92–95

Baba yangu wa Mbinguni anataka nipokee uzima wa milele katika ufalme wa selestia.

Je, umewahi kujiuliza—au kupata hofu—kuhusu ikiwa utastahili au la kwa ufalme wa selestia? Unaposoma maelezo ya wale wanaopokea utukufu huu (ona mistari 50–70, 92–95), kuliko kutazama tu orodha ya mambo unayolazimika kufanya, tazama kile ambacho Mungu amefanya—na anachofanya—kukusaidia kuwa kama Yeye. Je, kusoma ono katika njia hii kunaathiri jinsi unavyohisi kuhusu juhudi zako binafsi?

Ungeweza pia kufikiria kuhusu jinsi ilivyo baraka kuu kujua maelezo haya kuhusu ufalme wa selestia. Ni kwa jinsi gani ono hili la utukufu wa selestia linaathiri jinsi unavyofikiria na kutaka kuishi maisha yako ya kila siku?

Ona pia Musa 1:39; Joy D. Jones, “Thamani ipitayo Kipimo,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 13–15; J. Devn Cornish, “Je Mimi ni Mzuri vya Kutosha? Nitaweza Kweli?Ensign au Liahona, Nov. 2016, 32–34.

chumba katika nyumba ya karne ya kumi na tisa

Joseph Smith aliona ono la falme za utukufu katika chumba hiki.

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 76:22–24, 50–52, 78–79, 81–82. Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu umuhimu wa shuhuda zetu? Ni jukumu gani shuhuda zetu zinalo katika takdiri yetu ya milele? Ingeweza kusaidia kutazama maana za jasiri ili kujadili jinsi ya kuwa “majasiri katika ushuhuda wa Yesu” (mstari wa 79). Mngeweza pia kuimba “I Will Be Valiant” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,162).

Mafundisho na Maagano 76:24.Familia yako ingeweza kugundua muunganiko kati ya kweli katika sehemu ya 76 na zile zilizofundishwa katika “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3); moja ya kweli hizi unapatikana katika Mafundisho na Maagano 76:24. Ni kwa jinsi gani ulimwengu ungekuwa tofauti kama kila mmoja angeelewa kwamba sisi sote ni watoto wa Mungu? Ni kwa jinsi gani ukweli huu unaathiri jinsi tunavyowatendea wengine? Pengine kutazama picha za wana na mabinti tofauti wa Mungu kwenye dunia hii kungeweza kuisaidia familia yako kutafakari swali hili. (Ona pia “Wasilisho la Video: I Am a Child of God,” ChurchofJesusChrist.org.)

Fikirieni kuimba “I Am a Child of God” pamoja na kutafuta miunganiko mingine kwenye kanuni katika sehemu ya 76 (ona, kwa mfano, mistari 12, 62, 96).

Mafundisho na Maagano 76:40–41.Ikiwa tungepaswa kufanyia ufupisho “habari njema” (mstari wa 40), katika mistari hii kwenye kichwa cha habari cha gazeti au tweet, ungesema nini? Ni habari zipi njema zingine tunapata katika sehemu ya 76?

Mafundisho na Maagano 76:50–70.Ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia familia yako kutazamia na kujiandaa kwa uzima wa milele katika ufalme wa selestia? Mngeweza kushirikiana kwa pamoja kutafuta picha, maandiko, na mafundisho ya kinabii yanayoendana na vifungu katika Mafundisho na Maagano 76:50–70. Mngeweza kupata mambo haya katika magazeti ya Kanisa, kwenye ChurchofJesusChrist.org, au kwenye rejeo ya maandiko. Kisha mngeweza kukusanya picha hizi, maandiko, na mafundisho kwenye bango ambalo lingeweza kuikumbusha familia yenu juu ya malengo ya milele.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Know That My Redeemer Lives,” Nyimbo za Kanisa, na. 136.

 ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho: Shuhuda za “Ono”

Wilford Woodruff

Wilford Woodruff alijiunga na Kanisa mnamo Desemba 1833, takribani miaka miwili baada ya Joseph Smith na Sidney Rigdon kupokea ono lililoandikwa katika Mafundisho na Maagano 76. Alikuwa akiishi New York wakati huo na alijifunza kuhusu “Ono” kutoka kwa wamisionari waliokuwa wakitumikia kwenye eneo. Miaka kadhaa baadaye alizungumzia misukumo yake ya ufunuo huu:

“Nilifunzwa tangu utoto wangu kwamba kulikuwa na Mbingu moja na Jahanamu moja, na kuambiwa kwamba waovu wote walikuwa na adhabu moja na wenye haki utukufu mmoja. …

“… Niliposoma ono … , liliangaza akili yangu na kunipa shangwe kubwa, ilionekana kwangu kwamba Mungu ambaye alifunua kanuni hiyo kwa mwanadamu alikuwa mwenye busara, mwenye haki na mkweli, aliye na zote sifa bora na hisia nzuri na ufahamu, nilihisi Yeye alikuwa na msimamo kwenye vyote upendo, rehema, haki na hukumu, na nilihisi kumpenda Bwana zaidi kuliko hapo kabla katika maisha yangu.”1

“Ono [ni] ufunuo ambao unatoa mwanga zaidi, ukweli zaidi, na kanuni zaidi kuliko ufunuo wowote katika kitabu kingine chochote tulichowahi kusoma. Unaweka wazi ufahamu wetu wa hali ya sasa, wapi tulitoka, kwa nini tuko hapa, na wapi tunakwenda. Mtu yeyote anaweza kujua kupitia ufunuo huo kile sehemu yake na hali yake itakavyokuwa.”2

“Kabla sijamwona Joseph nilisema sikujali alikuwa na umri gani, au udogo wake; sikujali jinsi alivyoonekana—iwe nywele zake zilikuwa ndefu au fupi; mwanaume aliyeleta ufunuo huo alikuwa nabii wa Mungu. Nililijua hilo mimi mwenyewe.”3

Phebe Crosby Peck

Wakati Phebe Peck aliposikia Joseph na Sidney wakifundisha juu ya “Ono,” alikuwa akiishi Missouri na kulea watoto watano kama mzazi mmoja. Ono lilimvutia na kumvuvia kiasi kwamba aliandika yafuatayo kushiriki kile alichojifunza pamoja na ndugu zake:

“Bwana anafichua siri za Ufalme wa mbinguni kwa Watoto wake. … Joseph Smith na Sidney Rigdon walitutembelea majira ya kuchipua yaliyopita, na tulikuwa na mikutano mingi ya shangwe wakati walipokuwa hapa, na tulikuwa na siri nyingi zilizofunuliwa kwenye mtazamo wetu, ambazo zilinipa faraja. Tungeweza kuona wema wa Mungu katika kuandaa makao ya amani kwa ajili ya watoto wake. Na yule ambaye hatapokea utimilifu wa injili na kusimama kama askari jasiri katika kusudi la Kristo hawezi kuishi katika uwepo wa Baba na Mwana. Lakini kuna mahali palipoandaliwa kwa ajili ya wale wote ambao hawapokei, lakini ni mahali pa utukufu wa chini kuliko kuishi katika ufalme wa selestia. Sitajaribu kusema zaidi kuhusiana na mambo haya jinsi yalivyo sasa katika chapisho na yanavyosonga mbele ulimwenguni. Na pengine utakuwa na fursa ya kusoma wewe mwenyewe, na ukifanya hivyo, natumaini utasoma kwa moyo wa umakini na wa sala, kwani mambo haya yana thamani kukumbukwa. Na ninatamani kwamba mtafute ndani yake, kwani ni kile kinachopelekea furaha yetu katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao.”4

Muhtasari

  1. Remarks,” Deseret News, Mei 27, 1857, 91.

  2. Deseret News, Aug. 3, 1881, 481; ona pia Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Wilford Woodruff (2004), 120–21.

  3. “Remarks,” Deseret Weekly, Sept. 5, 1891, 322.

  4. Barua ya Phebe Crosby Peck kwa Anna Jones Pratt, Aug. 10, 1832, Maktaba ya Historia ya Kanisa, Jiji la Salt Lake; matamshi na tahajia vimebadilishwa.

Wasilisho la falme tatu za utukufu

Falme kwa Utukufu, na Annie Henrie Nader