Mafundisho na Maagano 2021
Julai 5–11. Mafundisho na Maagano 76: “Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele”


“Julai 5–11. Mafundisho na Maagano 76: “Tuzo Lao Litakuwa kuu na Utukufu wao Utakuwa wa Milele,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 5–11. Mafundisho na Maagano 76,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
kundi la nyota angani

Kimbilio, na Shaelynn Abel

Julai 5–11

Mafundisho na Maagano 76

“Tuzo Lao Litakuwa Kuu na Utukufu Wao Utakuwa wa Milele”

Unapojifunza Mafundisho na Maagano 76, tafakari kile Baba wa Mbinguni anawataka watoto katika darasa lako kujua kuhusu Yeye, Mwokozi, wao wenyewe , na majaliwa yao ya milele.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waonyeshe watoto picha au kurasa za shughuli kutoka muhtasari wa wiki hii au mihutasari iiliyopita. Waache watoto wakuambie kile wanachoona katika picha hizi na kile wanachokumbuka kujifunza kutokana na picha hizo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 76:24

Sisi sote tu watoto wa Mungu.

Rais Dallin H. Oaks alisema kwamba kama tunamfundisha “kijana wazo lenye nguvu kwamba yeye ni mtoto wa Mungu,” tunaweza kumpa “heshima yake na motisha kwenda kinyume na matatizo ya maisha” (“Mawazo Yenye Nguvu,” Ensign, Nov. 1995, 25).

Shughuli Yamkini

  • Kuwasaidia watoto kuelewa uwezo wao wa kuwa kama Mungu, tafuta njia za kuwaonyesha kwamba watoto wa wanyama wanakua na kuwa kama wazazi wao—pengine watoto wangeweza kufananisha picha za wanyama na picha za watoto wa wanyama. Fungua maandiko kwenye Mafundisho na Maagano 76:24, na waeleze watoto kwamba sisi wote ni “wana na mabinti wa Mungu.” Toa ushuhuda wako kwamba Mungu ni Baba yetu na kwamba tunaweza kukua kuwa kama Wazazi wetu wa Mbinguni.

  • Imbeni pamoja “I am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3), na watake watoto kujionyesha wenyewe wanapoimba “Mimi.” Watake kuimba huo wimbo tena, wakibadilisha “Mimi ni” na “wewe ni” na kumwonyesha mtu mwingine katika darasa.

Mafundisho na Maagano 76:40–42

Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu.

Neno injili linamaanisha habari njema. Habari njema ambayo injili inaleta ni kwamba Yesu Kristo “alikuja ulimwenguni … kuusafisha kutokana na uovu wote” (mstari wa 41).

Shughuli Yamkini

  • Wasimulie watoto kuhusu baadhi ya habari nzuri ulizozisikia hivi karibuni. Watake kushiriki habari nzuri walizozisikia. Kisha shiriki pamoja nao habari nzuri za injili kwa kusoma Mafundisho na Maagano 78:41–42. Waulize watoto jinsi habari hii nzuri inavyowafanya wahisi. Shiriki pamoja nao furaha ambayo habari hii nzuri inakuletea.

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo. Waulize watoto kama wanajua kile Yesu Kristo alichofanya kwa ajili yetu. Waonyeshe watoto kitu fulani ambacho ni kichafu na kitu fulani kisafi (kama kitambaa au karatasi), na eleza kwamba dhambi ni kama uchafu kwenye nafsi zetu, lakini Yesu Kristo alikuja kutusaidia tuwe wasafi tena.

    Picha
    Yesu na watoto

    Waruhusu Watoto Wadogo, na J. Kirk Richards

Mafundisho na Maagano 76:62

Baba wa Mbinguni ananitaka mimi nirudi kuishi na Yeye milele.

Ono la Joseph Smith na Sidney Rigdon la ufalme wa selestia lilionyesha baraka kuu ambazo Mungu ameziandaa kwa ajili ya watoto Wake, pamoja na vitu ambavyo lazima tuvifanye ili kupokea baraka hizo.

Shughuli Yamkini

  • Waeleze watoto kuhusu falme tatu za utukufu ambazo Joseph na Sidney waliziona katika ono lao. (Unaweza kuwasomea watoto sehemu ndogo au yote ya “Sura ya 26: Falme Tatu za Mbinguni” [Hadithi za Mafundisho na Maagano, 97–103] au onyesha video zinazohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org.) Waulize watoto nini wanachokipenda kuhusu ono. Fokasi mahsusi kwenye kuelezea ufalme wa selestia, na shuhudia kwamba hapa ni pale Baba wa Mbinguni anataka kila mmoja wetu awepo.

  • Soma kwa watoto Mafundisho na Maagano 76:62, na waalike watoto kuchora picha zao wenyewe pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika ufalme wa selestia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 76:41–42, 69

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba baraka za utukufu Mungu anazoziahidi kwa waaminifu katika maisha yajayo zinawezekana tu kwa sababu ya Mwokozi Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni Nini Yesu Kristo amefanya kwa ajili yangu? Mtake kila mtoto kusoma kimoyo moyo mstari wa 5, mistari 41–42, au mstari wa 69 katika Sehemu ya 76, wakitafuta uwezekano wa majibu kwa maswali ubaoni. Waruhusu kushiriki majibu yao (ona pia “Alimtuma Mwana Wake, Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35). Jinsi gani tunaweza kuonyesha shukrani zetu kwa kile Mwokozi alichofanya kwa ajili yetu?

  • Andika makala ya tatu ya imani ubaoni, ukiacha sehemu tupu katika sehemu za maneno muhimu. Wape watoto maneno haya yaliyokosekana kwenye vipande vya karatasi, na watake kuweka maneno yao katika sehemu sahihi ubaoni. Nini makala hii ya imani inatufundisha kuhusu kwa nini tunamhitaji Yesu Kristo? (Ona pia video “Why We Need a Savior,” ChurchofJesusChrist.org).

Mafundisho na Maagano 76:12, 15–19, 114–16

Kujifunza maandiko kunaweza kunisaidia “kuelewa mambo ya Mungu.”

Joseph Smith na Sidney Rigdon walipokea Mafundisho na Maagano 76 walipokuwa wanatafakari maandiko. Wasaidie watoto waone jinsi kujifunza maandiko kunavyoweza kualika ufunuo kupitia Roho Mtakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto kama wanajua nini Joseph Smith na Sidney Rigdon walikuwa wanafanya walipoona ono katika Mafundisho na Maagano 76. Watake wasome Mistari 15–19 kugundua. Shiriki muda wakati ulipopokea msukumo wakati unasoma maandiko, na watake watoto kuzungumza kuhusu hisia za kiroho walizokuwa nazo walipokuwa wanasoma maandiko.

  • Watake watoto kufumba macho yao na wajaribu kufanya kazi, kama kupaka rangi picha au kufungua maandiko kwenye mstari maalumu. Ni vitu gani ambavyo ni vigumu kufanya wakati macho yetu yamefumbwa kiroho? Someni pamoja Mafundisho na Maagano 76:12, 15–19, 114–16 kugundua kile tunachohitaji kufanya kuwa na macho yetu yaliyofunguliwa kiroho.

Mafundisho na Maagano 76:50–70

Baba wa Mbinguni ameandaa ufalme wa utukufu wa selestia kwa ajili yangu.

Kujua kuhusu utukufu wa selestia Mungu aliouandaa kunaweza kuwavutia watoto “kushinda kwa imani” (mstari wa 53) majaribu na vishawishi wanavyokabiliana navyo.

Shughuli Yamkini

  • Kama mtu fulani angetuuliza, “Kwa nini nimfuate Yesu Kristo na kutii amri Zake?” tutasema nini? Watake watoto kutafuta majibu katika Mafundisho na Maagano 76:50–70, ambayo yalielezea hao wanaopokea uzima wa milele katika ufalme wa selestia. Waruhusu watoto waigize kujibu swali. Toa ushuhuda wako wa baraka kuu ambazo Baba wa Mbinguni ameandaa kwa ajili yetu kama tutamfuata Yesu Kristo.

  • Chora picha kubwa ya jua kwenye kipande cha karatasi, na ikate kwenye vipande kadhaa vya fumbo. Mpe kila mtoto kipande, pamoja na moja ya vifungu vya maandiko yafuatayo kusoma: Mafundisho na Maagano 76:51; 76:52; 76:53; 131:1–2. Watake watoto kutafuta katika mistari yao kitu fulani ambacho lazima tukifanye kuupokea uzima wa milele katika ufalme wa selestia (baadhi ya mistari ina jibu zaidi ya moja), na waliandike kwenye kipande chao cha jua. Wanapofanya kazi pamoja kuunganisha fumbo, onyesha kujiamini kwako kwao ili pamoja na msaada wa Mwokozi, waweze kustahili kwa ufalme wa selestia.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watake watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kufundisha familia zao kile walichojifunza kuhusu ono waliloliona Joseph Smith na Sidney Rigdon.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Someni maandiko. Hata kama watoto unaowafundisha hawawezi bado kusoma, tumia maandiko mara kwa mara unapowafundisha. Waruhusu waone kwamba kweli mnazoshirikiana zinakuja kutoka kwenye maandiko.

Chapisha