Mafundisho na Maagano 2021
Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83: Kwani “Yule Aliyepewa Vingi kwake Huyo Vitatakiwa Vingi”


“Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83: Kwani ‘Yule Aliyepewa Vingi kwake Huyo Vitatakiwa Vingi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 19–25. Mafundisho na Maagano 81–83,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Kristo na kijana tajiri mtawala

Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofmann

Julai 19–25

Mafundisho na Maagano 81–83

Kwani “Yule Aliyepewa Vingi kwake Huyo Vitatakiwa Vingi”

Jinsi gani funuo katika Mafundisho na Maagano 81–83 zinasaidia watoto unaowafundisha kufanya mema miongoni mwa familia zao na marafiki?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Watake watoto kushiriki kitu fulani walichofanya kumsaidia mtu fulani wiki hii. Jinsi gani kuhudumia wengine kunaweza kutusaidia kuwa kama Mwokozi wetu?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 81:3

Ninapaswa kusali daima.

Bwana alipomwita Frederick G. Williams kuwa mshauri wa Nabii Joseph Smith, Alimshauri Frederick kuwa “mwaminifu … katika sala daima.”

Shughuli Yamkini

  • Soma kwa watoto ushauri wa Bwana wa kuwa “mwaminifu … katika sala daima, kwa sauti na katika moyo wako, hadharani na faraghani” (Mafundisho na Maagano 81:3). Elezea inamaanisha nini kusali katika mioyo yetu, na shiriki mfano binafsi. Wasaidie watoto wafikiri nyakati wanapoweza kusali “hadharani na faraghani.”

  • Wafundishe watoto jinsi ya kusali. Sisitiza kwamba wanaweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa baraka zao na wamwombe kwa kile wanachohitaji. Wimbo kuhusu sala, kama vile “I Thank Thee, Dear Father”(Kitabu cha Nyimbo za Watoto,7), unaweza kuwasaidia watoto kujua nini cha kusema katika sala zao. Mpe kila mtoto zamu ya kusema sala fupi.

  • Watake watoto kufikiria juu ya vitu ambavyo wangeweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwavyo au wamwombe kwavyo. Waruhusu kuchora picha za vitu hivi na kuzishiriki na darasa.

Mafundisho na Maagano 81:5; 82:19.

Ninaweza kuwahudumia hao wanaonizunguka.

Baba wa Mbinguni anajua mahitaji ya kila mmoja wa watoto wake, na mara kwa mara hutumia watu wengine—kama watoto unaowafundisha—kusaidia kukidhi mahitaji hayo. Jinsi gani utaweza kuwasaidia watoto watambue mahitaji ya wengine na kuwahudumia?

Shughuli Yamkini

  • Soma Mafundisho na Maagano 81:5 kwa watoto, na kuwasaidia kuelewa vifungu vya maneno kama “Wasaidie wadhaifu” na “inyooshe mikono iliyolegea.” Waruhusu waigize njia tunazoweza kufanya kile Bwana anachokitaka katika mstari huu. Tumia picha au video kusimulia hadithi za kawaida za Yesu Kristo akihudumia wengine (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 41, 42, 46, 4755; biblevideos.ChurchofJesusChrist.org). Jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Mwokozi wa kusaidia wengine?

  • Imba mstari wa nne wa “I feel My Savior’s Love” (Kitabu cha nyimbo za watoto, 74–75) au wimbo mwingine kuhusu huduma. Eleza kuhusu wakati ambapo mtu fulani alikusaidia kuhisi upendo wa Mwokozi kwa kukuhudumia.

  • Soma Mafundisho na Maagano 82:19 kwa watoto, ukisisitiza fungu la maneno “kutafuta ustawi wa jirani yake.” Eleza kwamba hii inamaanisha kufanya vitu ambavyo vinawasaidia majirani zetu—pamoja na familia yetu. Wasaidie watoto kufikiri juu ya njia wanazoweza kumtumikia mtu fulani wiki hii.

    wavulana wakichimba

    Mungu anatutaka kuwahudumia wengine ili kuonyesha upendo wetu Kwake.

Mafundisho na Maagano 82:10

Mungu anaahidi baraka ninapomtii Yeye.

Wanapokua, watoto wanaweza kustaajabu kwa nini Mungu anatupatia amri nyingi mno. Unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Anatupatia amri ili kutubariki.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya amri ambazo Mungu ametupatia (ona, kwa mfano, Kutoka 20:4–17; Mathayo 22:37–39; Mafundisho na Maagano 89:5–17). Chora picha ubaoni kuwasaidia watoto kuelewa na kukumbuka amri hizi. Toa mifano ya jinsi amri za Mungu zinavyoweza kutubariki na kutulinda.

  • Soma kwa watoto, Mimi, Bwana, ninafungwa wakati ninyi mnapofanya ninayosema” (Mafundisho na Maagano 82:10). Watake watoto kurudia kifungu hiki cha maneno mara kadhaa pamoja nawe, na fikiria juu ya njia za kuwasaidia kukikumbuka, kama vile kuwataka kupiga makofi kwa mapigo ya kifungu cha maneno. Shuhudia kwamba tunapotii amri za Mungu, Yeye hutimiza ahadi zake kwetu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 81:3

Ninaweza kusali “kwa sauti na [ndani] ya moyo wangu.”

Jinsi gani unaweza kuwatia moyo watoto kumgeukia Bwana “daima katika sala” wakati wanapokuwa na mahitaji?

Shughuli Yamkini

  • Mwalike mtu fulani kusoma Mafundisho na Maagano 81:3, na waulize watoto inamaanisha nini kusali “katika moyo [wako].” Shiriki uzoefu uliposali kwa sauti au katika moyo wako na Bwana akakusaidia. Pia watake watoto kushiriki uzoefu wao wenyewe. Jinsi gani sala inaweza kutuleta karibu zaidi kwa Baba wa Mbinguni?

  • Soma au imba pamoja na watoto wimbo kuhusu sala, kama vile “Did You Think to Pray?” au “Secret Prayer” (Nyimbo za Kanisa, na. 140, 144). Watake watoto kushiriki kifungu cha maneno kutoka kwenye wimbo kinachowasaidia kuelewa kitu fulani kuhusu sala. Wape muda kutafakari nini wanaweza kufanya kuboresha sala zao na kisha andika mawazo yao.

Mafundisho na Maagano 81:5

Mungu ananitaka kuhudumia na kuwaimarisha hao wenye mahitaji.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba kuna njia nyingi wanazoweza kuhudumia familia zao, marafiki, na majirani kila siku.

Shughuli Yamkini

  • Chora picha za mikono na magoti ubaoni. Watake watoto wasome Mafundisho na Maagano 81:5 kujifunza kile Bwana anachosema kuhusu sehemu hizi za mwili. Angalia video “Pass It On” (ChurchofJesusChrist.org), au shiriki jinsi wewe na watoto mlivyowaona watu wakihudumiana. Jinsi gani tunaweza kuwafahamu zaidi watu wenye mahitaji wanaotuzunguka? Watake watoto kuhudumia angalau mtu mmoja wiki hii. Kwa mawazo kuhusu njia za kuwahudumia wengine, imba wimbo kuhusu huduma, kama vile “Have I Done Any Good?” (Nyimbo za Kanisa, na. 223).

  • Watake watoto kufanya zamu kupanga dhumna (au vitu vinavyofanana) wakati ukitaja njia wanazoweza kuwahudumia wengine. Mtake mtoto kuangusha domino moja na tilia maanani jinsi inavyoathiri zingine. Jinsi gani huduma zetu zina matokeo kwa watu wanaotuzunguka? (Ona pia video “Dominoes,” ChurchofJesusChrist.org.) Elezea kuhusu jinsi huduma ya upendo ya mtu fulani ilivyokutia moyo kumhudumia mtu mwingine.

Mafundisho na Maagano 82:8–10

Mungu anaahidi baraka ninapomtii Yeye.

Watoto wanapojenga imani katika ahadi za Mungu, utayari wao kutii amri zake utakua.

Shughuli Yamkini

  • Watake watoto kufikiria wana rafiki anayefikiri kwamba Mungu ametoa amri nyingi mno. Waombe watafute Mafundisho na Maagano 82:8–10 kwa ajili ya kitu fulani, ambacho kingemsaidia rafiki yao kuelewa kwa nini Mungu anatoa amri. Shiriki jinsi amri za Mungu zilivyokubariki, na watake watoto kushiriki mawazo yao pia.

  • Kuwasaidia watoto kuelewa ahadi za Baba wa Mbinguni kwetu ligawe darasa katika makundi matatu, na lipe kila kundi moja ya maandiko yafuatayo kusoma: Mafundisho na Maagano 1:37–38; 82:10; 130:20–21. Watake kushiriki nini wanajifunza kuhusu ahadi za Baba wa Mbinguni. Jinsi gani utii wetu unaathiri baraka tunazoweza kupokea? Wasaidie watoto kufikiria juu ya mifano kutoka kwenye maisha yao au kutoka kwenye maandiko wakati utii ulipoleta baraka kutoka kwa Mungu.

  • Shiriki uzoefu binafsi ambao unashuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa katika Mafundisho na Maagano 82:8–10. Jinsi gani umekuja kuamini katika Bwana na ahadi Zake?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watake watoto kufikiria juu ya jinsi ambavyo wangependa kumhudumia mtu fulani katika familia yao wiki hii. Wakati wa somo la wiki ijayo, waombe waelezee kile walichofanya.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kuwa wanafunzi wazuri. Kufundisha kunamaanisha zaidi ya kushiriki ukweli. Kunamaanisha kusaidia wengine kujenga kujitegemea kiroho. Badala ya kirahisi kuwasimulia watoto jinsi wanavyoweza kuwahudumia wengine, kwa mfano, watie moyo kufikiria juu ya mawazo yao.