Mafundisho na Maagano 2021
Juni 28–Julai 4. Mafundisho na Maagano 71–75: “Hakuna Silaha Iliyotengenezwa Dhidi Yenu Itakayofanikiwa”


Juni 28–Julai 4. Mafundisho na Maagano 71–75: ‘Hakuna Silaha Iliyotengenezwa Dhidi Yenu Itakayofanikiwa””,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

Juni 28–Julai 4. Mafundisho na Maagano 71–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Yesu na kondoo

Dear to the Heart of the Shepherd, na Simon Dewey

Juni 28–Julai 4

Mafundisho na Maagano 71–75

“Hakuna Silaha Iliyotengenezwa Dhidi Yenu Itakayofanikiwa”

Watoto unaowafundisha wanaweza kujifunza mengi katika darasa lako, lakini watajifunza mengi zaidi kama watajenga tabia ya kujifunza maandiko nyumbani. Fikiria ni kwa jinsi gani unaweza kuhimiza na kusaidia kujifunza injili nyumbani.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kukaa sakafuni katika duara, na zungusha mpira kwa mmoja wao. Muombe mtoto yule kushiriki jambo alilojifunza hivi karibuni kuhusu injili nyumbani au katika darasa la msingi. Kisha mwalike mtoto kuzungusha mpira kwa mwingine. Rudia hivi mpaka kila mtoto amepata nafasi ya kushiriki jambo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 72: 2, 10

Bwana amemwita askofu kunisaidia.

Watoto wadogo wanaweza wasijue mengi kuhusu nini askofu anafanya kuwahudumia wao na waumini wengine wa kata. Unaweza kuwasaidia kushukuru huduma ya askofu wao.

Shughuli Yamkini

  • Lete vitu darasani ambavyo vinawakilisha majukumu ya askofu, kama vile karatasi nyembamba ya zaka, maandiko, au picha ya askofu akitoa ushauri (ona picha mwishoni mwa muhtasari wa wiki hii katika Njoo—Unifuate Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Soma Mafundisho na Maagano 72:2, na ueleze kwamba Bwana amemwita askofu kutusaidia. Tumia vitu ulivyoleta kuwasaidia watoto kuelewa baadhi ya vitu ambavyo askofu anafanya kuhudumia kata.

  • Wachukuwe watoto kwa matembezi kwenye ofisi ya askofu (unaweza kutaka kuratibu na walimu wengine). Waelezee baadhi ya hali wakati watakapokutana na askofu katika ofisi yake (kama vile usaili wa ubatizo au maafikiano ya zaka). Wasimulie watoto jinsi ulivyobarikiwa kwa huduma ya askofu.

  • Wasaidie watoto kutengeneza kadi kumpa askofu, kumshukuru kwa kile anachofanya kusaidia kazi ya Bwana.

Mafundisho na Maagano 75:3

Ninaweza kutoa juhudi yangu kubwa kwa Bwana.

Hata katika umri mdogo, watoto wanaweza kupata furaha katika kufanya kadiri ya uwezo wao mkubwa kutii amri za Bwana,

Shughuli Yamkini

  • Mtake kila mtoto kufanya zamu kuigiza jinsi ambavyo wangefanya tendo la huduma, kama vile kufagia chumba katika kanisa au kuosha vyombo nyumbani. Soma Mafundisho na Maagano 75:3, na watake watoto kuonyesha jinsi watakavyoifanya kiuvivu utakaposema “wala msiwe wavivu” na onyesha jinsi ya kufanya kazi kwa bidii unaposema “lakini fanya kazi kwa nguvu zako zote.” Kwa nini ni muhimu kwamba tunafanya kwa uwezo wetu wote tunapomhudumia Bwana?

  • Shirikiana na watoto hadithi za Rais Dieter F. Uchtdorf kuhusu kazi kutoka “Kanuni Mbili kwa ajili ya Uchumi wowote” (Ensign au Liahona, Nov. 2009, 55–58. Tunajihisi vipi tunapojua tumefanya kwa nguvu zetu zote?

  • Imbeni wimbo kuhusu kufanya kazi pamoja, kama vile “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,198). Wasaidie watoto kufanya vitendo vinavyoendana na maneno.

    Picha
    Mapipa na magunia ya chakula

    Waumini wa Kanisa wa Mwanzo wakati mwingine walitoa chakula kwa Kanisa kusaidia wengine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 71

Ninaweza kutetea ukweli kwa kushiriki ushuhuda wangu.

Bwana hategemei watoto kujibu wakosoaji wa Kanisa kama alivyomwita Joseph Smith na Sidney Rigdon kufanya. Lakini unaweza kuwasaidia kuelewa kwamba ushuhuda wao wa kawaida wa ukweli unaweza kuwa na athari kubwa kwa wengine.

Shughuli Yamkini

Mafundisho na Maagano 72:8

Bwana anawaita maaskofu kumsaidia kufanya kazi Yake.

Askofu anaweza kuwa na ushawishi chanya wenye nguvu katika maisha ya kijana. Unaweza kufanya nini kusaidia watoto wamwone askofu kama mwakilishi wa Bwana Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwamba mnamo mwaka 1831 Bwana alimwita askofu wa Kanisa, Edward Partrige, kuondoka kutoka Kirtland, Ohio, kuwa askofu katika Independence, Missouri (ona “Sura ya 17: Maaskofu wa kwanza wa Kanisa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 64–66). Soma Mafundisho na Maagano 72:8 pamoja na watoto, na watake kusikiliza ni nani Bwana alimwita kuhudumu kama askofu mpya katika Kirtland. Kwa nini Bwana anawaita maaskofu? Shiriki na watoto uzoefu wakati ulipobarikiwa kwa huduma ya askofu.

  • Watake watoto kutengeneza orodha ya baadhi ya vitu walivyoviona askofu anafanya kusaidia watu katika kata. Watake watoto wachore picha za askofu akifanya kitu fulani walichokitaja. Toa ushuhuda wako kwamba askofu wako aliitwa na Bwana kuwa mtumishi Wake. Kwa nini tuna shukrani kwamba Bwana amemwita askofu katika kata yetu?

Mafundisho na Maagano 73:3

Bwana alimwamuru Joseph Smith kurejesha kweli zenye thamani ambazo zilipotea kutoka kwenye Biblia.

Kama sehemu ya wito wake kama nabii, Joseph Smith aliamriwa na Bwana kufanya marejeo yenye msukumo ya Biblia. Marejeo haya, ambayo Bwana aliyaita “tafsiri” (Mafundisho na Maagano 90:13.), yalirejesha kweli muhimu ambazo zilikuwa zimepotea au kuondolewa kutoka kwenye Biblia zaidi ya karne nyingi.

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwamba wakati Joseph Smith na Sidney Rigdon waliporudi kutoka Misheni fupi karibu na Kirtland, Ohio, Bwana aliwataka kuendelea na kazi kwenye mradi muhimu. Watake watoto wasome Mafundisho na Maagano 73:3 kutafuta mradi huo ulikuwa upi. Kuwasaidia watoto kuelewa kile Bwana alitaka Joseph na Sidney kutafsiri, soma pamoja nao sehemu za kuingia kwenye Kamusi ya Biblia “Tafsiri ya Joseph Smith (JST).”

  • Zungusha nakala ya Biblia, na ruhusu watoto kuifungua na kuona jinsi kurasa nyingi zilivyo ndani yake. Watake watoto kujifanya walikuwa wameombwa kutafsiri Biblia kwenye lugha nyingine. Ni uwezekano gani wanao kuweza kufanya makosa kadhaa? Eleza kwamba wakati watu walipotafsiri au kunakili Biblia kabla ya wakati wa Joseph Smith, walifanya makosa kadhaa, na wakati mwingine waliondoa kweli muhimu. Bwana alimwamuru Nabii Joseph Smith kufanya masahihisho yenye msukumo. Kwa nini kazi ya Joseph Smith ni ya thamani kwetu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watake watoto kuchagua kitu fulani watakachofanya kwa sababu ya kile walichojifunza leo, kama vile kumshukuru askofu kwa huduma zake au kujiandaa kulinda imani zao kwa kujifunza Makala za Imani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Husisha milango ya fahamu. “Watoto wengi (na watu wazima) wanajifunza vyema zaidi wakati milango mingi ya fahamu inapohusishwa. Tafuta mbinu za kuwasaidia watoto kutumia milango yao ya fahamu ya kuona, kusikia, na kugusa wanapojifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha