“Juni 21–27. Mafundisho na Maagano 67–70: ‘Wenye Thamani … Utajiri wa Dunia Yote”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Juni 21–27. Mafundisho na Maagano 67–70,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi
Juni 21–27
Mafundisho na Maagano 67–70
“Wenye Thamani … Utajiri wa Dunia Yote”
Kabla hujasoma mapendekezo katika muhtasari huu, jifunze Mafundisho na Maagano 67–70, na andika misukumo ya kiroho unayopokea. Misukumo hii itakusaidia wewe kutengeneza mpango wa kufundishia wenye kuvutia. Kisha badilisha mpango huo na mawazo kutoka kwenye muhtasari huu, kutoka Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia, au kutoka kwenye magazeti ya Kanisa.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Watake watoto kuchora picha ya kitu fulani walichojifunza kutoka kwenye mafunzo yao ya maandiko nyumbani au katika Msingi. Kama wanapata shida kufikiria nini cha kuchora, ungeweza kuwakumbusha juu ya baadhi ya mada katika Mafundisho na Maagano 67–70, kama vile ubatizo, kupata ushuhuda wa maandiko, au wazazi wakiwafundisha watoto injili.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Mafundisho na Maagano ina funuo kutoka kwa Mungu.
Mnamo Novemba 1831, viongozi wa Kanisa waliamua kuweka funuo za Joseph Smith katika kitabu kwa ajili ya kila mtu kuzisoma. Leo funuo hizo zimechapishwa katika Mafundisho na Maagano.
Shughuli Yamkini
-
Waambie watoto kuhusu jinsi funuo za Joseph Smith zilivyochapishwa katika kitabu (ona “Sura ya 23: Mafundisho na Maagano,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 90–92, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Shiriki ushuhuda wako kwamba Mafundisho na Maagano ina funuo ambazo zinaweza kutusaidia leo. Shiriki moja ya mistari unayoipenda kutoka Mafundisho na Maagano.
-
Waonyeshe watoto kila moja ya vitabu vitakatifu kimoja kimoja, na wakati unapokishika kila kimoja juu shiriki kidogo kuhusu jinsi tulivyokipata (ona ruhusa ya haki ya ingizo la kila kitabu katika Mwongozo kwenye Maandiko). Wakati unapoinua juu Mafundisho na Maagano, shiriki pamoja na watoto kile kinachofanya kitabu hiki cha maandiko kuwa cha kipekee (kwa mfano, kina funuo zilizotolewa katika wakati wetu).
Mafundisho na Maagano 68:25–28
Ninaweza kubatizwa wakati nitakapokuwa na umri wa miaka minane.
Katika Mafundisho na Maagano 68:25–28, Bwana alimwambia Joseph Smith kwamba watoto wanapaswa kujifunza kuwa na imani katika Yesu Kristo, kutubu, na kubatizwa wakati wanapofika umri wa miaka minane. Alisema pia kwamba wanapaswa kujifunza kusali na kutii amri za Mungu.
Shughuli Yamkini
-
Watake watoto kuhesabu mpaka nane kwa kutumia vidole vyao. Ni kitu gani cha muhimu kuhusu kuwa na umri wa miaka nane? Wasaidie watoto kutambua kwamba wakati wanapokuwa na umri wa miaka minane, wanaweza kubatizwa. Kwa kutumia maneno na mafungu ya maneno yanayopatikana katika Mafundisho na Maagano 68:25–28, Shiriki pamoja nao baadhi ya mambo Bwana anayotaka wajifunze kabla hawajafikisha umri wa miaka nane (ona pia Makala ya Imani 1:4). Wasaidie kuelewa mawazo ambayo yanaweza kuwa hayafahamiki kwao.
-
Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “Baptism” au“When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 100–10. 103). Watake watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu kubatizwa na nini wanaweza kufanya kujiandaa.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Mafundisho na Maagano 67: 4, 9
Funuo zilizotolewa kupitia Joseph Smith ni za kweli.
Mengi ya maelekezo katika Mafundisho na Maagano 67–70 yanahusu juhudi za Watakatifu kuchapisha funuo za Joseph Smith. Hii ingeweza kuwa fursa ya kuwasaidia watoto kutambua kwamba katika funuo hizi, zilizochapishwa sasa katika Mafundisho na Maagano, tunaweza kupata sauti ya Bwana.
Unapojitayarisha kufundisha, ungeweza kurejelea Watakatifu, 1:140–43 au “Sura ya 23: Mafundisho na Maagano” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 90–92).
Shughuli Yamkini
-
Waonyeshe watoto Biblia, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu. Wasaidie watoto kutengeneza orodha ubaoni ya kile kinachofanya kila kitabu cha maandiko kuwa tofauti na kile kinachovifanya vifanane. Kama walihitaji msaada, shiriki pamoja nao maelezo ya vitabu hivi katika Mwongozo kwenye Maandiko. Waulize watoto jinsi wanavyoweza kujua kwamba maandiko ni ya kweli. Tunajifunza nini kutoka Mafundisho na Maagano 67:4, 9 kuhusu funuo Bwana alizotoa kwa Joseph Smith?
-
Shiriki mstari kutoka Mafundisho na Maagano ambao unaimarisha “ushuhuda wako wa kweli wa amri hizi” (mstari wa 4). Wape watoto fursa za kushiriki mstari wanaoupenda wenyewe. Waelezee watoto kwamba viongozi wa Kanisa wakati huu waliamua kuchapisha shuhuda zao za funuo alizozipokea Joseph Smith. Walipofanya hivyo, mmoja wa viongozi, Levi Hancock, aliandika sambamba na jina lake, “Kamwe lisifutwe” (Ushuhuda, mnamo Novemba 2 1831,”Kitabu cha Ufunuo 1, 121 josephsmithpapers.org). Kwa nini Levi Hancock aliweza kutaka jina lake “kamwe lilifutwe” kutoka kwenye ushuhuda uliochapishwa? Wape watoto fursa ya kuandika shuhuda zao za kile walichojifunza mpaka sasa katika Mafundisho na Maagano.
Wakati viongozi wa Kanisa letu wanazungumza kwa msukumo, wanazungumza “neno la Bwana.”
Wakati watumishi wa Bwana wanapozungumza kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, maneno yao ni mapenzi, akili, neno, na sauti ya Bwana (ona mstari wa 4). Kujua ukweli huu kunaweza kusaidia watoto kutaka kusikiliza na kufuata mafundisho yao.
Shughuli Yamkini
-
Watake watoto kusoma Mafundisho na Maagano 68:3–4 katika vikundi vidogo na shiriki pamoja na kila mmoja kile wanachojifunza kutoka kwenye mistari hii. Watake watoto kuandika kitu fulani walichojifunza ubaoni. Kwa nini huu ni ukweli muhimu kujua?
-
Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 68:3–4 pamoja, wape watoto nakala za jumbe kadhaa za hivi karibuni kutoka mkutano mkuu. Watake kutafuta katika jumbe kweli ambazo Bwana alitufundisha kupitia watumishi Wake.
Ninaweza kuwa “mkweli na mwaminifu.”
Wakati Oliver Cowdery alipohitaji kusafiri kwenda Missouri, Bwana alimwita John Whitmer, mtu fulani aliyekuwa “mkweli na mwaminifu” (Mstari wa 1), Kwenda pamoja naye. Jinsi gani watoto wanaweza kuwa wakweli na waaminifu kama John Whitmer?
Shughuli Yamkini
-
Waambie watoto kwamba wakati Bwana alipomtuma Oliver Cowdery kwenda Missouri, Alisema kwamba mtu fulani “mkweli na mwaminifu” (mstari wa 1) anapaswa kwenda pamoja naye, kwa hiyo alimtuma John Whitmer. Inamaanisha nini kuwa mkweli na waaminifu? Jinsi gani tunaweza kuhakikisha sisi ni wakweli na waaminifu ili kwamba Bwana aweze kututumia kubariki wengine?
-
Watake watoto wachache kueleza kuhusu mtu fulani wanayemjua ambaye wanafikiri ni “mkweli na mwaminifu.” Wanajua vipi kwamba mtu yule ni mkweli na mwaminifu? Wasaidie waone kwamba Bwana alimwamini John Whitmer kwa sababu alikuwa, wakati huu, mkweli na mwaminifu (ona Mafundisho na Maagano 69:1–2)). Imbeni pamoja wimbo ambao unawatia moyo watoto kuwa wakweli na waaminifu kama Mwokozi, kama vile “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Watake watoto kuelezea kwa mtu fulani nyumbani Mafundisho na Maagano ni nini, yanatoka wapi, na kwa nini ni muhimu kwao.