Mafundisho na Maagano 2021
Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 62– 60: “Wenye Mwili Wako katika Mikono Yangu”


“Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62: ‘Wenye Mwili Wako katika Mikono Yangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Mto Missouri

Kambi ya usiku Missouri, na Bryan Mark Taylor

Mei 31–Juni 6.

Mafundisho na Maagano 60–62

“Wenye Mwili Wako katika Mikono Yangu”

Kumbuka kwamba matayarisho yako bora ya kufundisha Mafundisho na Maagano 60–62 yatakuja kupitia kujifunza kwako kibinafsi na kifamilia kwa sehemu hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Mpe kila mtoto nafasi ya kushiriki kitu fulani alichojifunza kutoka kwenye maandiko kwa kipindi cha wiki iliyopita au kutoka darasa la Msingi la Jumapili iliyopita. Baada ya kila mtoto kushiriki, muombe mtoto mwingine katika darasa kufanya muhtasari wa kile alichosema.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 60:4; 61:1–2, 36; 62:1

Maandiko yananifundisha kuhusu Yesu Kristo.

Mafundisho na Maagano 60–62 yana maelezo mengi ambayo yanaweza kusaidia watoto unaowafundisha kuelewa Yesu Kristo ni nani na kuongeza upendo wao kwa ajili Yake.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo, na waombe watoto kushiriki kwa nini wanampenda Yesu. Chagua vifungu vichache vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 60–62 ambavyo vinakufundisha kuhusu Mwokozi, na vishiriki na watoto (ona, kwa mfano, Mafundisho na Maagano 60:4; 61:1–2, 36; 62:1). Wasaidie watoto kurudia vifungu vichache vya maneno pamoja na wewe. Shiriki jinsi unavyohisi kuhusu Yesu Kristo.

  • Onyesha picha chache za Yesu kutoka utumishi wake wa kidunia (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 34–61). Acha watoto wakusaidie kusimulia kile Yesu anachofanya katika picha. Jinsi gani anaonyesha upendo wake kwa ajili ya watoto wa Baba wa Mbinguni? Waeleze watoto kuhusu moja ya maandiko unayoyapenda ambayo yanafundisha kuhusu Yesu.

  • Imba pamoja na watoto “I’m Trying to Be Like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79; ona pia video ya kuimba pamoja kwenye ChurchofJesusChrist.org). Mnapoimba kuhusu njia za kuwa kama Yesu, simama mara chache na waombe watoto kumalizia sentensi “I can be like Jesus by …”

    Picha
    Mwokozi aliyefufuka

    Kwa Sababu Hii Nimekuja, na Yongsung Kim

Mafundisho na Maagano 62:3

Yesu Kristo ananitaka kushiriki injili Yake.

Watoto wanapenda kushiriki kile wanachojua pamoja na wengine. Wasaidie waelewe kwamba wakati wanaposhiriki kile wanachojua kuhusu injili, Baba wa Mbinguni anawafurahia.

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwamba Bwana aliwataka Nabii Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa kusafiri kutoka Kirtland, Ohio, kwenda Jackson County, Missouri. Aliwataka kuhubiri injili njiani na walipokuwa wanarudi nyumbani. Soma Mafundisho na Maagano 62:3, na waombe watoto kusikiliza kile wamisionari walichofanya ambacho kilimpendeza Bwana. Shuhudia kwamba Bwana anapendezwa na sisi wakati tunaposhiriki injili pamoja na wengine.

  • Wasaidie watoto kutengeneza beji ambazo zinaonyesha wanataka kuwa wamisionari wa Kanisa. Waache wavae beji zao na wafanye mazoezi ya kushiriki shuhuda zao wao kwa wao.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168). Wasaidie watoto kufikiria juu ya kile ambacho wangesema kama mtu fulani angewauliza nini wanakipenda kuhusu Yesu Kristo na Kanisa Lake. Waalike kuchora picha za vitu wanavyopenda kuhusu injili ya Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 60:7, 13; 62:3, 9

Ninaweza kufungua mdomo wangu kushiriki injili ya Yesu Kristo.

Ushuhuda wa mtoto unaweza kuwa wenye nguvu kubwa kama wa mtu mzima, kwa sababu nguvu ya ushuhuda inakuja sio kutokana na umri wa mtu au uzoefu lakini kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wasaidie watoto kuweza kujiamini kwamba wanaweza kufungua vinywa vyao na kushiriki pamoja na wengine kile wanachojua ni kweli.

Shughuli Yamkini

  • Ni baraka gani Bwana alizoahidi katika Mafundisho na Maagano 60:7; 62:3, 9 kwa wale wanaoshiriki injili Yake? Jinsi gani kushiriki injili kunabariki wengine? Fikiria kushiriki uzoefu kutoka kwenye maisha yako wakati uliposhiriki injili—Ni baraka gani zilikuja kutokana na juhudi zako? Waalike watoto kushiriki uzoefu wowote waliokuwa nao. Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “Go Forth with Faith” (Nyimbo, na. 263), na zungumza kuhusu baraka zilizotamkwa katika wimbo.

  • Wasaidie watoto waigize hali ambazo wanaweza kushiriki injili pamoja na rafiki zao. Kwa mfano, nini watakachosema kama mtu fulani angewauliza kwa nini wanakwenda Kanisani? Au vipi kama rafiki aliwaona wamevaa pete ya CTR au wakisoma Kitabu cha Mormoni na kuulizwa maswali? Wangesema nini?

Mafundisho na Maagano 60:7; 61: 1–2, 36; 62: 1, 14–17

Bwana yupo tayari kunisamehe kama nitatubu.

Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa hawakuwa wakamilifu. Wakati mwingine walibishana na hawakuwa na subira (ona “Ezra Booth na Issac Morley,” Ufunuo katika Muktadha, 133). Lakini Bwana alikuwa mwenye huruma kwao na siku zote alitoa msamaha kama walitubu.

Shughuli Yamkini

  • Soma pamoja na watoto Mafundisho na Maagano 60:7; 61:2, na watake kutafuta maneno ambayo mistari hii inayo kwa pamoja. Wakumbushe watoto kwamba ufunuo huu ulitolewa kwa Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa. Ni nini Bwana aliwataka wajue? Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu jinsi Bwana anavyohisi kuhusu sisi tunapofanya makosa?

  • Andika Yesu Kristo yuko vipi? Ubaoni. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 61:1–2, 36; 62:1, na tengeneza orodha ya majibu kwa swali hili ambayo watoto wanapata katika mistari. Jinsi gani sifa ubaoni zinatusaidia kuelewa kwa nini Mwokozi yupo tayari kutusamehe sisi? Ni njia gani tunaweza kufuata mfano Wake?

Mafundisho na Maagano 60:5; 61:22; 62:5–8

Bwana ananitaka kutumia uhuru wangu wa kuchagua na Roho Wake kufanya chaguzi nzuri.

Jinsi gani unaweza kutumia mistari hii kufundisha watoto jinsi Bwana anavyowasaidia kufanya chaguzi nzuri?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kuzungumza kuhusu muda walipohitaji kufanya uamuzi. Jinsi gani waliamua nini cha kufanya? Someni pamoja Mafundisho na Maagano 62:5, 7–8 kujifunza kuhusu kile Bwana alichosema kwa wazee waliokuwa karibu kusafiri kutoka Missouri kwenda Kirtland, Ohio. Chaguzi gani walihitaji kufanya kuhusu safari yao? Ni nini Bwana ametupatia kutusaidia kufanya chaguzi? Waambie watoto kuhusu jinsi ulivyotumia mwongozo wa Roho na uamuzi wako bora kufanya maamuzi.

  • Ligawe darasa katika makundi matatu, na liombe kila kundi kusoma moja ya mistari ifuatayo, ambayo Bwana aliwaelekeza baadhi ya wamisionari kuhusu jinsi ya kukamilisha misheni zao: Mafundisho na Maagano 60:5; 61:22; 62:5. Tunaona nini kuhusu maelekezo ya Bwana katika mistari hii? Kwa nini wakati mwingine ni vizuri kwa ajili yetu kutumia uamuzi wetu wenyewe badala ya kusubiri maelekezo maalumu kutoka kwa Mungu kwa kila jambo?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kufanya mazoezi ya kushiriki injili na mwanafamilia. Kwa mfano, wangeweza kushiriki kitu fulani walichojifunza katika darasa la msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda darasani kwako. Kutoa ushuhuda wako mara kwa mara kutawasaidia watoto unaowafundisha kupata shuhuda zao wenyewe. Ushuhuda unaweza kuwa rahisi kama “Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wenu” au “Ninahisi vizuri ndani ninapojifunza kuhusu Yesu Kristo.”

Chapisha