Mafundisho na Maagano 2021
Juni 7–13. Mafundisho na Maagano 63: “Kile Ambacho Huja Kutoka Juu ni Kitakatifu”


“Juni 7–13. Mafundisho na Maagano 63: ‘Kile Ambacho Huja Kutoka Juu ni Kitakatifu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Juni 7–13. Mafundisho na Maagano 63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Shamba la Missouri

Springhill, Daviess County, Missouri, na Garth Robinson Oborn

Juni 7–13

Mafundisho na Maagano 63

“Kile Ambacho Huja Kutoka Juu ni Kitakatifu”

Kweli zilizofundishwa katika Mafundisho na Maagano 63 zinaweza kusaidia watoto unaowafundisha kujenga imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Kwa sababu una muda wenye kikomo pamoja nao, fikiria kweli zipi zitakuwa zenye maana zaidi kwao, Zenye msingi kwenye mahitaji yao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria juu ya njia rahisi, zenye ubunifu kuwapa watoto fursa za kushiriki kile wanachojifunza. Kwa mfano, tayarisha vipande vya karatasi vyenye ukubwa tofauti, na ruhusu kila mtoto achague kimoja kwa kubahatisha. Mtake mtoto mwenye karatasi ndefu sana kushiriki kwanza.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 63:23

Baba wa Mbinguni ananitaka kujifunza injili.

Watoto daima wanajifunza. Wasaidie waone kwamba Baba wa Mbinguni atawasaidia kujifunza kuhusu Yeye kama watatii amri zake.

Shughuli Yamkini

  • Soma Mafundisho na Maagano 63:23 kwa watoto, na watake kusikiliza kile ambacho Mungu atatupa kama tutatii amri. Wasaidie waelewe kwamba “mafumbo” ni mambo ambayo Mungu anaweza kutufundisha zaidi kuyahusu, kama jinsi ya kuwa zaidi kama Yesu Kristo.

  • Leta darasani picha ambazo zinawakilisha mada za injili watoto wanazoweza kujifunza zaidi kuzihusu, kama vile ubatizo, Mwokozi, mahekalu, na kadhalika. Zilaze picha zote kwa kuangalia chini katika sakafu, na waruhusu wafanye zamu kuzigeuza. Waombe kushiriki kile wanachokijua na maswali yoyote waliyonayo kuhusu kila mada.

Mafundisho na Maagano 63:49

Mimi nitafufuka.

Ama sasa au hapo baadaye, watoto unaowafundisha watafarijika kujua kwamba kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, wote ambao wamekufa watafufuliwa siku moja.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto picha ya mmoja wa wapendwa wako ambaye amekufa, na shiriki hadithi kuhusu mtu huyo. Soma Mafundisho na Maagano 63:49 kwa watoto, na shuhudia kwamba siku moja mtu huyo “atafufuka kutoka kwa wafu” na hatakufa tena. Waulize watoto kama wanamjua mtu fulani aliyekufa. Shuhudia kwamba, wote tutafufuliwa kwa sababu ya Yesu Kristo.

  • Onyesha picha za maziko, na Ufufuo wa Mwokozi (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 58,59). Watake kuzungumza kuhusu nini kinatokea katika picha hizo. Watake watoto walale chini unapowasimulia kuhusu mazishi ya Yesu na kusimama wima unapowasimulia kuhusu Kufufuka Kwake. Soma Mafundisho na Maagano 63:49, na toa ushuhuda wako kwamba siku moja wote tutafufuka kutoka kwa wafu kama vile Yesu alivyofanya.

    Picha
    Yesu akimtokea Mariamu

    Kaburi la Bustani, na Jon McNaughton

Mafundisho na Maagano 63:64

Ninapaswa kutendea vitu vitakatifu kwa unyenyekevu.

Tunaishi katika wakati ambao vitu vitakatifu mara kwa mara vinapuuzwa au hata kudhihakiwa. Unaweza kuwasaidia watoto kujenga hisia ya unyenyekevu kwa vitu vitakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto kutoka Mafundindisho na Maagano 63:63: “Kile ambacho huja kutoka juu ni kitakatifu.” Watake watoto kufikiria kitu ambacho ni muhimu kwao, kama vile mwanasesere wanayempenda au kitabu. Jinsi gani wanamtunza na kumlinda? Wasaidie kufikiria juu ya vitu ambavyo ni muhimu—au vitakatifu—kwa Baba wa Mbinguni. Jinsi gani tunapaswa kusema juu ya vitu hivi? Tunapaswa kuvitendea vipi?

  • Imbeni pamoja na watoto wimbo kuhusu unyenyekevu, kama vile “Reverently, Quietly” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,26). Wasaidie kufikiria juu ya jinsi wanavyoweza kuonyesha unyenyekevu kwa vitu vitakatifu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 63:9–10

Ishara zinakuja kwa imani na mapenzi ya Mungu.

Ezra Booth aliongoka Kanisani baada ya kuona Joseph Smith akiponya mkono wa Elsa Johnson. Lakini Ezra baadaye alipoteza imani yake, na akawa mkosoaji wa Nabii. Mafundisho na Maagano 63 ina maonyo dhidi ya kujaribu kujenga imani yetu kwenye ishara, kama vile uponyaji wa kimiujiza, badala ya kwenye udhibitisho wa kiroho wa ukweli.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na wasimulie watoto kwamba Joseph Smith alitumia ukuhani kuponya mkono wa Elsa Johnson, ambao hakuweza kuutumua kikamilifu kwa miaka miwili. Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 63:9–10, na watake kushiriki kitu fulani Bwana anachosema kuhusu imani na ishara (au miujiza).

  • Watake watoto kuchora nyumba iliyo juu ya mstatili na nyumba iliyo juu ya ncha ya pembetatu. Wasimulie watoto kwamba nyumba zinawakilisha imani zetu na shuhuda. Watake wasome Mafundisho na Maagano 63:9–10 na Helamani 5:12 Kisha watake waandike katika mstatili kile sisi tunapaswa kujenga imani yetu juu yake na katika pembetatu kile sisi hatupaswi kujenga imani yetu juu yake. Onyesha kwamba mstatili unatoa sehemu thabiti kujenga lakini pembetatu sio salama na thabiti. Kwa nini ni muhimu kujenga imani yetu juu ya Yesu Kristo kuliko juu ya vitu vingine?

Mafundisho na Maagano 63:23

Ninapotii amri, Mungu atanifundisha kweli Zake.

“Maajabu ya ufalme wa [Mungu]” yanapatikana tu kwa hao wanaotii amri za Mungu. Hii ndiyo sababu kuna maajabu kwa watu wengi. Kanuni hii itawasaidia watoto wanapotafuta ukweli.

Shughuli Yamkini

  • Andika ubaoni Kama nikitii amri, ndipo, na waombe watoto kuandika ubaoni njia tofauti ili kumalizia sentensi. Watake watoto wasome Mafundisho na Maagano 63:23 na tafuta kitu fulani wanachoweza kuongeza kwenye orodha yao. Waonyeshe watoto glasi ya maji, na waulize jinsi kweli za injili zilivyo kama maji kwetu sisi.

  • Waonyeshe watoto picha ya kisima, na watake kuchora picha ya kimojawapo. Baada ya kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 63:23, wasaidie kufikiria juu ya kweli wanazozijua kuhusu injili, na watake kuandika kweli hizi kuzunguka visima vyao. Jinsi gani kweli hizi ni kama “maji ya uzima”?

Mafundisho na Maagano 63:58–64

Sipaswi kulitaja jina la Bwana bure.

Watoto unaowafundisha wanaweza kuwasikia wengine wakilitaja jina la Mungu bila heshima na lugha chafu. Jinsi gani unaweza kuwasaidia kuelewa kwamba majina ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo “lazima yatamkwe kwa uangalifu”? (Mafundisho na Maagano 63:64).

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto kutoka Mafundisho na Maagano 63:58: “Hii ni siku ya kuonya.” Waombe wazungumze kuhusu maonyo wanayosikia kutoka kwa wazazi wao, waalimu, na viongozi wa Kanisa. Kisha wasaidie kutafuta maonyo kutoka kwa Bwana katika mistari 58–64. Zipi baadhi ya njia zinazofaa “kutumia jina la Bwana”? (mstari wa 62).

  • Rejeeni pamoja “Lugha” katika Kwa Nguvu ya Vijana, (kurasa 20–21). Waombe watoto kutengeneza mabango madogo kuwakumbusha juu ya kitu fulani walichojifunza kuhusu jinsi ya kutumia majina ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu unyenyekevu, kama vile “Reverence” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,31). Jinsi gani tunaweza kuwa na uhakika kwamba sisi ni wanyenyekevu tunapozungumza kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ikiwa huna muda kufanya ukurasa wa shughuli ya wiki hii katika darasa, fikiria kumpa kila mtoto nakala kwenda nayo nyumbani kuikamilisha pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jenga imani ya watoto. Baadhi ya watoto wanaweza wasihisi uwezo wa kujifunza injili wao wenyewe. Njia moja ya kuwasaidia kujenga kujiamini ni kuwasifia wanaposhiriki katika darasa. Waahidi watoto kwamba Roho Mtakatifu atawasaidia wanapojifunza.

Chapisha