Mafundisho na Maagano 2021
Mei 24–30. Mafundisho na Maagano 58–59: “Kujishughulisha kwa Shauku katika Kazi Njema”


“Mei 24–30. Mafundisho na Maagano 58–59: ‘Kujishughulisha kwa Shauku katika Kazi Njema,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 24–30. Mafundisho na Maagano 58–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi

Picha
Mtaa wa Independence Missouri

Independence, Missouri, na Al Rounds

Mei 24–30

Mafundisho na Maagano 58–59

“Kujishughulisha kwa Shauku katika Kazi Njema”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 58–59, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Misukumo hii inaweza kukusaidia kupanga kufundisha mafundisho uliyojifunza kwa watoto. Unaweza pia kupata mawazo katika muhtasari wa somo hili, katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia au katika magazeti ya Kanisa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Watake watoto wachache kushiriki kitu fulani walichofanya kwa kipindi cha wiki hii kujifunza kutoka kwenye maandiko.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 58:27–28

Baba wa Mbinguni amenipa uwezo wa kuchagua.

Wasaidie watoto kujua kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka kufanya chaguzi nzuri ambazo zinaleta furaha kwenye maisha yetu na kwa wengine.

Shughuli Yamkini

  • Soma vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 58:27–28 kuwasaidia watoto waelewe kwamba wanaweza kuchagua kufanya mazuri. Weka sura ya furaha kwenye upande mmoja wa chumba na uso wenye huzuni upande mwingine. Unajihisi nini unapochagua kufanya mazuri? Elezea hali kadhaa pamoja na uchaguzi mzuri au mbaya kwa kila moja. Baada ya kuelezea kila hali na uchaguzi, waombe watoto kusimama karibu na sura yenye furaha kama uchaguzi ni mzuri na karibu na sura yenye huzuni kama ni mbaya.

  • Waonyeshe watoto chombo chenye rangi nyingi tofauti za penseli za rangi. Waonyeshe chombo cha pili chenye penseli ya rangi moja tu. Waulize watoto chombo gani kati ya hivi wangependa kukitumia. Kwa nini? Eleza kwamba kuwa na uwezo wa kuchagua ni baraka kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatupenda na wanatutaka kufanya chaguzi nzuri.

  • Waambie watoto kuhusu wakati ambao ulifanya uchaguzi mzuri, na eleza jinsi ulivyojihisi baadaye. Watake watoto wachore picha ya hadithi yako au hadithi yao wenyewe. Kisha waache washiriki picha zao pamoja na darasa na kueleza kile walichojifunza kutoka kwenye hadithi.

Mafundisho na Maagano 59:7

Baba wa Mbinguni ananitaka niwe mwenye shukrani.

Jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto waelewe umuhimu wa kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka zao?

Shughuli Yamkini

  • Waeleze watoto kitu fulani ambacho una shukrani nacho, na watake kushiriki vitu walivyo na shukrani navyo. Soma Mafundisho na Maagano 59:7, na wasaidie watoto kufikiri juu ya njia ambazo wanaweza kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka zao. Wangeweza kutengeneza nini cha kupeleka nyumbani kuwakumbusha kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka zao?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu shukrani, kama vile “For Health and Strength” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,21). Watake watoto wabadili maneno katika wimbo kwa vitu vingine walivyo na shukrani navyo.

  • Waache watoto wachore picha za vitu walivyo na shukrani navyo.

Mafundisho na Maagano 59:9–12

Sabato ni siku ya Bwana.

Unaposhiriki furaha uliyoipata kwa kuiweka siku ya Sabato kuwa takatifu, unaweza kuwasaidia watoto waione Sabato kama siku tunayomwabudu Mungu.

Shughuli Yamkini

  • Lete picha au vitu ambavyo vinaonyesha vitu vizuri tunavyoweza kuvifanya siku ya Jumapili kumwabudu Bwana na kupata furaha. Baadhi ya mawazo yanapatikana katika Mafundisho na Maagano 59:9–12) na “Kuishika Siku ya Sabato” (Kwa Nguvu ya Vijana, 30–31. Kwa mfano, kuwakilisha sakramenti, ungeweza kuonyesha Picha ya 108 katika Kitabu cha sanaa ya injili au kikombe cha sakramenti na kipande cha mkate. Jinsi gani kila moja ya vitu hivi vinatusaidia kumkaribia zaidi Baba na Yesu Kristo siku ya Sabato?

  • Kamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii pamoja na watoto ili kuwapa mawazo kuifanya Sabato siku takatifu.

    Picha
    mkate na vikombe vya sakramenti

    Kushiriki sakramenti kunatusaidia kuheshimu siku ya Sabato.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 58:27–28

Uhuru wa kuchagua ni uwezo wa kuchagua.

Mungu ametupa uwezo wa kuchagua, na kwa uwezo huo tunaweza “kufanya mambo mengi kwa hiari yetu wenyewe, na kutekeleza haki nyingi” (mstari wa 27). Jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha waone kwamba hata kama kuna uovu ulimwenguni, “uwezo upo ndani yao” “kufanya mazuri? (mstari wa 28).

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto kipande cha karatasi ambacho kina neno uchaguzi limeandikwa kwenye upande mmoja matokeo limeandikwa kwenye upande mwingine. Eleza kwamba chaguzi zina matokeo, au athari ambazo kiasilia zinafuata matendo. Mtake mtoto achague karatasi kuonyesha kwamba unapochagua karatasi, unapata vyote uchaguzi na matokeo ya uchaguzi ule. Mwombe mtoto asome Mafundisho na Maagano 58:27–28 Ni chaguzi gani tunaweza kufanya ambazo “zitatekeleza haki nyingi” au matokeo mazuri? (mstari wa 27). Lini tumefanya chaguzi nzuri ambazo zilikuwa na matokeo ambayo yaliwabariki wengine?

  • Andika vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 58:27 kwenye vipande vya karatasi, na toa kimoja kwa kila mtoto. Watake kusoma mistari kimoyo moyo na kutafakari vifungu vya maneno yake. Watake watoto kukaa katika mpangilio ambao vifungu vya maneno yao vinatokea katika mistari 27–28 na washirikiane kile walichojifunza. Ni upi ujumbe wa Bwana kwetu katika mistari hii?

  • Imbeni wimbo kuhusu chaguzi, kama vile “Choose the Right“ (Nyimbo, na. 239). Uliza maswali kusaidia watoto kutafakari maneno ya wimbo—kwa mfano, Nani anasaidia kukuongoza kufanya chaguzi sahihi? Nani anajaribu kukufanya wewe ufanye chaguzi zisizo sahihi? Jinsi gani kuchagua yaliyo sahihi kunakufanya uhisi?

Mafundisho na Maagano 59:9–16

Sabato ni siku ya Bwana.

Bwana amesema kwamba kuadhimisha Sabato kunatusaidia “[wenyewe] tusiwe na mawaa kutoka ulimwenguni” (Mafundisho na Maagano 59:9). Je, unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kuiheshimu Sabato na kuifanya kuwa ishara ya upendo wao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Watake watoto kusoma Mafundisho na Maagano 59:9–16 wawili wawili, na watake kuandika kitu fulani wanachojifunza kuhusu siku ya Sabato kutoka kila mstari. Baada ya dakika chache, kitake kila kikundi kushiriki pamoja na darasa kile walichoandika. Tutafanya nini kitofauti siku ya Sabato kwa sababu ya kile tulichojifunza?

  • Tayarisha mchezo rahisi wa kulinganisha ambao watoto wanalinganisha vifungu vya maneno kutoka Mafundisho na Maagano 59:9–16) kwa mstari sahihi. Chagua vifungu vya maneno ambavyo vinafundisha nini Bwana anatutaka tufanye siku ya Sabato. Jadili kile vifungu hivi vya maneno vinatufundisha kuhusu siku ya Bwana na jinsi tunavyoweza kuja karibu zaidi Kwake.

  • Siku ya Sabato ni “siku ya Bwana” (Mafundisho na Maagano 59:12.)—Siku ya kuonyesha kwamba tunakumbuka kazi nyingi za Bwana tunapomwabudu Yeye (ona Kamusi ya Biblia, “Sabato”). Wasaidie watoto kutafakari kazi hizi kwa kuwataka wasome vifungu hivi vifuatavyo vya maandiko na kuwaonyesha picha zinazolingana: Mwanzo 2:1–3 (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 3); Yohana 20:1–19 (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 59). Ni kazi gani zingine zenye nguvu za Bwana tunazoweza kukumbuka siku ya Sabato? Nini kingine tunachojifunza kuhusu Sabato kutoka Mafundisho na Maagano 59:9–16?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watake watoto kushiriki pamoja na familia zao kitu fulani wanachoweza kufanya ili kuiweka Sabato siku takatifu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jenga kujiamini kwa watoto. Baadhi ya watoto wanaweza wasihisi uwezo wa kujifunza injili wao wenyewe. Waahidi watoto kwamba Roho Mtakatifu atawasaidia kujifunza.

Chapisha