Mafundisho na Maagano 2021
Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46:–48: “Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”


“Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48: ‘Takeni Sana Karama zilizo Kuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 3-9. Mafundisho na Maagano 46–48,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

watu wakikutana Bwawani

Mkutano wa Kambi, na Worthington Whittredge

Mei 3–9

Mafundisho na Maagano 46–48

“Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”

Unaposoma fikiria juu ya watoto unaowafundisha Mafundisho na Maagano 46–48. Rejelea “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” mwanzoni mwa nyenzo hii kwa ajili ya nyongeza ya mawazo ya kuzingatia.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kuchora picha za kitu walichojifunza katika somo la wiki iliyopita au walichojifunza nyumbani wiki iliyopita. Wape dondoo za kuwakumbusha kama itahitajika. Halafu acha wazungumzie juu ya hizo picha zao.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 46:2–6

Ninaweza kuwasaidia wengine wajisikie wanakaribishwa kanisani.

Sote, pamoja na watoto, tunataka kujisikia kukaribishwa na kukubalika. Unawezaje kutumia mistari hii ili kuwasaidia watoto kuwafanya wengine wajisikie wanakaribishwa kanisani?

Shughuli Yamkini

  • Soma Mafundisho na Maagano 46:5 kwa sauti, na uwaambie watoto kwa maneno yako mwenyewe mstari huu unamaanisha nini. Onyesha picha za watu kutoka ulimwenguni kote. Waulize watoto ni yupi kati ya watu hawa Baba wa Mbingu angetaka tuwaalike kwenye mikutano yetu ya Kanisa. Wasaidie watoto kufanya mazoezi ya kukualika wewe au kualikana wao kwa wao kuja kwenye mkutano au shughuli ya Kanisa.

  • Waombe watoto kufikiria kuwa rafiki yao anakuja kanisani kwa mara ya kwanza. Wasaidie kufikiria njia wanazoweza kumsaidia rafiki yao kujisikia anakaribishwa. Waache wafanyie mazoezi ni kipi wangekisema au kukifanya ikiwa wangemuona rafiki yao akiingia kanisani au darasani kwa mara ya kwanza.

Mafundisho na Maagano 46:13–26

Baba wa Mbinguni hunibariki kwa karama Zake.

Kila mmoja wa watoto unaowafundisha ni mwana au binti wa Baba wa Mbinguni, na Yeye amewabariki kwa karama za Kiroho.

Shughuli Yamkini

  • Tumia Mafundisho na Maagano 46:13–26 au “Mlango wa 20: Karama za Roho” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 77–80) kuelezea kwa watoto karama zingine ambazo Baba wa Mbinguni hutupatia kupitia Roho wake na kwa nini Yeye huzitoa. Ikiwezekana, onyesha vitu au picha ambazo zinawakilisha kila karama. Sitisha mara kwa mara ili kuwauliza watoto ni kwa jinsi gani karama hizi zinavyoweza kumbariki mtu.

  • Mpe mtoto kitu ambacho kinaweza kugawanywa, kama kipande cha mkate au wanasesere wawili wa kuchezea. Muombe mtoto amgawie kile ulichompa mshiriki mwingine wa darasa. Fafanua kwamba Baba wa Mbinguni hutupatia karama, na anataka tuzitumie katika kusaidia wengine. Waambie watoto kuhusu wakati ambapo ulibarikiwa kwa sababu mtu alishirikiana nawe karama zake za kiroho.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 46:8–26

Baba wa Mbinguni hunipa karama za kiroho ili kuwabariki wengine.

Karama zilizoelezewa katika Mafundisho na Maagano 46—na karama zingine nyingi za kiroho—zimetoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu. Unaweza kuwasaidia watoto kutambua karama walizopewa—na zingine wanazoweza kutafuta—wakati mnapojifunza Mafundisho na Maagano 46 kwa pamoja.

Shughuli Yamkini

  • Andika kwenye vipande vya karatasi baadhi ya karama za kiroho zinazopatikana kwenye Mafundisho na Maagano 46:13-26 na Makala ya Imani 1:7, na uzifiche chumbani humo. Alika kila mtoto kutafuta moja ya karatasi hizo na apekue mistari ili kuona ni wapi zawadi hiyo imetajwa katika maandiko. Kisha someni kwa pamoja Mafundisho na Maagano 46:8–9,12. Je, kwa nini Baba wa Mbinguni hutupatia karama za kiroho?

  • Wasaidie watoto kuorodhesha kwenye ubao karama za Roho zilizotajwa kwenye Mafundisho na Maagano 46. Wakati kila karama ikiorodheshwa, zungumza juu ya jinsi gani karama hiyo inavyoweza kutumika kuwabariki wengine. Maelezo kwenye “Mlango wa 20: Karama za Roho” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 77–80) yanaweza kusaidia. Waambie watoto kwamba kila mmoja ana karama za kiroho. Watie moyo ili wamwombe Baba wa Mbingu awasaidie kutambua karama zao na jinsi wanavyoweza kuzitumia katika kuwasaidia wengine.

Mafundisho na Maagano 47: 1, 3

Naweza kuandika historia yangu.

Bwana alimuita John Whitmer kutunza historia ya Kanisa. Leo tumebarikiwa sana kwa sababu ya historia za Kanisa ambazo zimetunzwa kwa miaka mingi.

Shughuli Yamkini

  • Someni kwa pamoja Mafundisho na Maagano 47:1,3, na uwaombe watoto kugundua kile ambacho Bwana alimtaka John Whitmer akifanye. Je, neno “daima” linamaanisha nini katika mstari wa 3? Je, ni kwa namna gani sisi tumebarikiwa kwa kujua juu ya historia ya Kanisa?

  • Ikiwa watoto unaowafundisha huandika shajara, waombe wazungumzie juu ya aina ya vitu wanavyoandika kwenye shajara zao. Watoto wangeweza kufurahia kusikia hadithi kutoka kwenye shajara yako ya utotoni au toka kwenye shajara ya babu.

  • Waonyesha watoto mifano ya njia ambazo wangeweza kutunza historia ya kawaida ya maisha yao. Kwa mfano, wanaweza kuandika kwenye kitabu, kukusanya picha toka kitabu chakavu, kuchapa kwenye talakilishi, au kurekodi sauti au video. Wasaidie watoto kuorodhesha vitu ambavyo ingekuwa vizuri kuvijumuisha katika historia zao binafsi, kama vile ushuhuda wao juu ya Yesu Kristo. Waalike watoto kutengeneza tangazo au bango la kwenda nalo nyumbani likiwa na baadhi ya mawazo haya ili kuwakumbusha kuandika historia zao binafsi.

    msichana akijifunza

    Shajara ni njia mojawapo tunayoweza kutunza historia.

Mafundisho na Maagano 48:1–4

Ninaweza kuwasaidia wengine kwa kushiriki kile ambacho nimepewa.

Bwana aliwahimiza Watakatifu huko Ohio kuwasaidia Watakatifu wengine kwa kugawana nao ardhi yao na pesa zao. Je, unawezaje kutumia mistari hii ili kuwasaidia watoto kupata njia za kushiriki na wengine kile ambacho Mungu amewapa?

Shughuli Yamkini

  • Waoneshe watoto Ramani ya New York na Ohio (ona muhtasari wa Aprili 12–18 katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Fafanua kwamba Bwana aliwaamuru Watakatifu huko New York na maeneo mengine wakusanyike Ohio, lakini wengi wao walipofika hawakuwa na pesa za kutosha kujenga nyumba. Wasaidie watoto kutafuta katika Mafundisho na Maagano 48:1–4 kile ambacho Bwana aliwaamuru Watakatifu huko Ohio kukifanya ili kusaidia. Waulize watoto kile ambacho wangetaka kukifanya ili kusaidia kama wangekuwa wanaishi huko Ohio wakati huo. Je, ni kipi tumepewa leo ambacho tungeweza kukitumia ili kuwasaidia wengine? Kwa mfano, ona “The Coat” (video, ChurchofJesusChrist.org).

  • Someni Mafundisho na Maagano 48:4 kwa pamoja, na waalike watoto kutafuta kitu ambacho Bwana aliwaamuru Watakatifu wakifanye ili kuisaidia kazi Yake. Fafanua kuwa kujiwekea akiba ya fedha kungewaruhusu wao kununua ardhi na siku moja kujenga hekalu. Je, tunaweza kujiwekea akiba ya fedha ili kwamba tuweze kusaidia kuifanya kazi ya Bwana? Onyesha video “First Things First” (ChurchofJesusChrist.org), na jadili jinsi watoto kwenye video hii walivyotimiza agizo la Bwana la kujiwekea akiba ya fedha.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kuwauliza wanafamilia nyumbani kuhusu karama ya kiroho ambayo wanahisi kuwa wao wamepewa. Pia wahimize watoto kusali na kutafuta karama ya Roho ambayo wao wangependa kukuza.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kujifunza kutoka kwenye maandiko. Watoto wadogo yawezekana wasiweze kusoma sana, lakini bado unaweza kuwasaidia kujifunza kutoka kwenye maandiko. Kwa mfano, ungeweza kusoma kifungu cha maneno na kuwaalika kusimama au kuinua mkono wakati wanaposikia neno au kirai husika.