Mafundisho na Maagano 2021
Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50: “Kile Kilicho cha Mungu Ni Nuru”


“Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50: ‘Kile Kilicho cha Mungu Ni Nuru,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
dimbwi wakati wa mapambazuko

Mei 10–16

Mafundisho na Maagano 49–50

“Kile Kilicho cha Mungu Ni Nuru”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 49–50, tafuta jumbe au kanuni ambazo unahisi zitakuwa zenye maana zaidi kwa watoto unaowafundisha. Chache zimependekezwa katika muhtasari huu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na wasaidie watoto kuelezea kuhusu jinsi Yesu Kristo anavyofanana na mchungaji mwema.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 49:12–14

Ninaweza kumfuata Yesu Kristo.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba wanaweza kumfuata Yesu Kristo kwa kumwamini Yeye, kutubu, kubatizwa, na kumpokea Roho Mtakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha karatasi nne za wayo na picha nne zinazowakilisha kumwamini Yesu Kristo, kutubu, kubatizwa, na kumpokea Roho Mtakatifu. Soma Mafundisho na Maagano 49: 12–14, na waombe watoto waonyeshe kwa kidole picha sahihi wakati kila moja inapotamkwa katika mistari. Waache watoto wakusaidie kuweka wayo kwenye sakafu na picha pembeni mwake, na waalike watoto kuchukuwa zamu kutembea juu ya wayo. Toa ushuhuda wako kwamba tunapofanya vitu katika picha hizi, tunamfuata Yesu Kristo.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kutengeneza vikaragosi vya vidole ambavyo vitawasaidia watoto kujifunza jinsi wanavyoweza kumfuata Yesu Kristo kwa kuwa na imani, kutubu, kubatizwa, na kupokea karama ya Roho Mtakatifu.

Mafundisho na Maagano 50:23–25

Nuru yangu ya kiroho inaweza kuzidi kung’aa zaidi na zaidi.

Dhana za kufikirika kama ukweli na roho zinaweza kuwa ngumu kwa watoto wadogo kuelewa, lakini kuzifananisha na nuru, kama Bwana anavyofanya katika Mafundisho na Maagano 50: 23–25, inaweza kusaidia.

Shughuli Yamkini

  • Tumia shughuli ambayo inaonyesha jinsi nuru yetu ya kiroho inavyoweza kuzidi kung’aa zaidi na zaidi. Unapaswa kuonyesha picha ya vitu ambavyo vinatoa nuru (kama vile mshumaa, balbu ya mwanga, na jua) na waache watoto wazipange katika utaratibu wa ung’aavu. Au waalike watoto wajifanye kuwa nuru inayokuwa ang’avu kwa kuinama na polepole kuinuka na kuinua juu mikono yao. Wasaidie kufikiri juu ya vitu vizuri wanavyoweza kufanya ili nuru yao ya kiroho ing’ae zaidi.

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu nuru yao ya kiroho, kama vile “Shine On” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,144). Shuhudia kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni alivyosaidia nuru yako kuzidi kuongezeka kung’aa zaidi. Waambie watoto kuhusu nuru unayoiona ndani yao.

Mafundisho na Maagano 50:41–44

Yesu Kristo ananipenda.

Yesu Kristo ni Mchungaji Mwema. Sisi ni kondoo Wake, na anampenda kila mmoja wetu. Ni kitu gani kitawasaidia watoto unaowafundisha kuhisi upendo Wake kwa ajili yao?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Yesu Kristo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.47, 84, au 116, na waulize watoto jinsi wanavyojua Yesu anawapenda watoto. Shiriki jinsi unavyojua Yesu anakupenda na kila mtoto katika darasa.

  • Tengeneza kondoo wa karatasi, andika juu yao majina ya watoto katika darasa, na wafiche kuzunguka chumba. Onyesha picha ya Mwokozi, na soma Mafundisho na Maagano 50:41–42. Wasaidie watoto kuelewa nini mistari hii inafundisha jinsi Yesu Kristo anavyohisi kuhusu wao. Waache watafute kondoo kuzunguka chumba na waweke juu ya ubao karibu na picha ya Yesu ili kwamba “na hakuna hata mmoja wao … atakayepotea” (mstari wa 42).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 49:12–14

Ninaweza kumfuata Yesu Kristo.

Bwana anahitaji sisi wote kufundisha wengine ili waweze kuja kwake kwa kuwa na imani, kutubu, kubatizwa, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wafananishe Mafundisho na Maagano 49:12–14 na kile Petro alichofundisha katika Matendo ya Mitume 2:38 pamoja na makala ya nne ya imani. Ni mifanano gani wanayopata? Kwa nini kweli hizi ni muhimu?

  • Waalike watoto kufanya kazi wawili wawili na wajifanye kwamba mmoja wao anataka kujua jinsi ya kumfuata Yesu Kristo. Mtoto mwingine kati ya hao wawili anaweza kumfundisha kwa kutumia Mafundisho na Maagano 49:12–14.

Mafundisho na Maagano 49:15–17

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwa mpango wa Mungu.

Watoto unaowafundisha wanaweza kukabiliana na jumbe zinazokanganya kuhusu ndoa. Mafundisho na Maagano 49: 15–17 inaweza kuwasaidia kuelewa jinsi Bwana anavyohisi kuhusu ndoa.

Shughuli Yamkini

  • Elezea kwamba Shakers walikuwa kundi ambalo liliamini watu hawapaswi kuoa au kuolewa (ona Kichwa cha habari kwenye Mafundisho na Maagano 49). Waombe watoto kutafuta vitu Bwana alivyofundisha kuhusu ndoa katika Mafundisho na Maagano 49:15–17.

  • Wasaidie watoto kuelewa nini msemo “ndoa imetakaswa na Mungu” unamaanisha. Waalike kufanya kazi wawili wawili kufananisha Mafundisho na Maagano 49:15–17 pamoja na ibara tatu za kwanza za “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu.” Kwa nini ndoa ni muhimu mno kwa Baba wa Mbinguni?

  • Imbeni pamoja mstari wa pili wa “Familia Zinaweza Kuwa Pamoja Milele” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,188) au wimbo wowote kuhusu familia. Wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kujiandaa kuoa au kuolewa katika hekalu siku moja na kuwa na familia ya milele.

    Picha
    wanandoa nje ya hekalu

    Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetakaswa na Mungu.

Mafundisho na Maagano 50:40–46

Yesu Kristo ni Mchungaji Mwema.

Mafundisho na Maagano 50: 40–46 ina picha ambayo inaweza kusaidia watoto unaowafundisha kuelewa jinsi Mwokozi anavyohisi kuhusu wao.

Shughuli Yamkini

  • Tengeneza mchezo unaolinganisha ukitumia misemo kutoka Mafundisho na Maagano 50:40–46. Kwa mfano, ungeweza kuandika “Msiogope, watoto wadogo” juu ya kadi ambayo italingana na kadi nyingine ambayo inasema “kwani ninyi ni wangu” (Mstari wa 41). Soma Mafundisho na Maagano 50:40–46 pamoja. Kisha changanya kadi sakafuni, mezani, au ubaoni, na waombe watoto kulinganisha misemo. Ni nini misemo hii inatufundisha kuhusu Yesu Kristo?

  • Kuwasaidia watoto kuelewa jinsi Mwokozi alivyo kama mchungaji mwema, waombe kusoma Mafundisho na Maagano 50:40–46 pamoja. Kisha onyesha video “Yesu Anatangaza Fumbo la Kondoo Aliyepotea” (ChurchofJesusChrist.org), na waombe watoto kutafuta kitu fulani katika video kinachowakumbusha juu ya kile walichosoma. Ni kwa jinsi gani Yesu anatuokoa? Jinsi gani tunaweza kuwa wachungaji wema kwa wengine?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Tayarisha muhtasari kwa ajili ya kila mtoto wa maneno haya: Niulize mimi kuhusu. Waache watoto wajaze sehemu tupu kwa kitu fulani walichojifunza katika darasa (wape msaada kama unahitajika) na bandika kwa pini muhtasari kwenye nguo zao kuchochea majadiliano nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Badilisha shughuli kwa ajili ya umri wa watoto unaowafundisha. Watoto wanapokua, wana mengi zaidi ya kuchangia darasani. Wana uzoefu zaidi na wanaweza kuwa bora zaidi kwenye kushiriki mawazo yao. Wakati unapowafundisha watoto wadogo, unaweza kuhitaji kuelezea zaidi kuliko na watoto wakubwa. Siku zote wape watoto fursa ya kushiriki wao wenyewe, na kisha wasaidie kama itahitajika.

Chapisha