Mafundisho na Maagano 2021
Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50: “Kile Kilicho cha Mungu Ni Nuru”


“Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50: Mafundisho na Maagano 49–50: ‘Kile Kilicho cha Mungu Ni Nuru,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 10–16. Mafundisho na Maagano 49–50,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
dimbwi kwenye machweo ya jua

Mei 10–16

Mafundisho na Maagano 49–50

“Kile kilicho cha Mungu ni nuru”

“Yule ambae huipokea nuru na kukaa ndani ya Mungu, hupokea nuru zaidi, na nuru hiyo huzidi kung’ara hata mchana mkamilifu” (Mafundisho na Maagano 50:24). Tafakari jinsi unavyopokea nuru kwa kukaa ndani ya Mungu.

Andika Misukumo Yako

Mwokozi ni “mchungaji wetu mwema” (Mafundisho na Maagano 50:44). Yeye anajua kwamba wakati mwingine kondoo wanatangatanga na kwamba nyika ina hatari nyingi. Hivyo Yeye kwa upendo anatuongoza kwenye usalama wa injili Yake, mbali na hatari kama vile “roho nyingi ambazo ni roho za uongo, ambazo zimeenea katika nchi, zikiudanganya ulimwengu”(Mafundisho na Maagano 50:2). Kumfuata Yeye mara kwa mara humaanisha kutupilia mbali mawazo au tamaduni zisizo sahihi. Hili lilikuwa kweli kwa Leman Copley na wengine huko Ohio ambao waliikubali injili iliyorejeshwa lakini bado walishikilia baadhi ya imani ambazo hazikuwa sahihi. Katika Mafundisho na Maagano 49, Bwana alitangaza kweli ambazo zilisahihisha imani za kipindi cha nyuma za Leman kuhusu mada kama vile ndoa na Ujio wa Pili wa Mwokozi. Na wakati waongofu wa Ohio “walipopokea … roho ambazo [hawakuweza] kuzielewa,” Bwana aliwafundisha jinsi ya kutambua madhihirisho ya kweli ya Roho (Mafundisho na Maagano 50:15). Mchungaji Mwema alikuwa mvumilivu; Yeye alijua kwamba Watakatifu hao wa mwanzo walikuwa—kama vile sisi sote—“watoto wadogo” ambao “lazima wakue katika neema na katika ujuzi wa ukweli” (Mafundisho na Maagano 50:40).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 49:5–23

Kweli za injili zinaweza kunisaidia kutambua mafundisho ya uongo.

Kabla ya kujiunga na Kanisa, Leman Copley alikuwa sehemu ya kundi la kidini lililojulikana kama Muungano wa Jumuiya ya Waumini wa Kuonekana kwa Kristo Mara ya Pili, pia likijulikana kama Shakers (ona “Leman Copley and the Shakers,” Ufunuo katika Muktadha, 117–21). Baada ya mazungumzo na Leman, Joseph Smith alitafuta ufafanuzi kutoka kwa Bwana kuhusu baadhi ya mafundisho ya Shakers, na Bwana alijibu kwa ufunuo katika sehemu ya 49.

Unaweza kupata baadhi ya imani za Shaker zilizotajwa katika kichwa cha habari cha sehemu ya 49. Fikiria kuwekea alama au kuandika kweli katika mistari 5–23 ambazo zinasahihisha imani hizo. Fikiria kuhusu mafundisho mengine ya uongo au tamaduni ulimwenguni leo. Ni kweli zipi za injili zinaweza kukusaidia kujilinda dhidi ya uongo au tamaduni hizo?

Mafundisho na Maagano 49:15–17

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwa mpango wa Mungu wa milele.

Ni kweli zipi kuhusu ndoa unajifunza kutoka Mafundisho na Maagano 49:15–17? Kwa nini unahisi ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwenye mpango wa Baba wa Mbinguni? Mzee David A. Bednar alitoa sababu mbili: “Sababu ya 1: Asili ya roho za mwanamume na mwanamke zinakuja pamoja na kukamilishana kila moja, na kwa hiyo wanaume na wanawake wamekusudiwa kukua pamoja kuelekea kuinuliwa. … Sababu ya 2: Kwa mpango mtakatifu, wote mwanamume na mwanamke wanatakiwa kuwaleta watoto kwenye maisha ya duniani na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya makuzi na malezi ya watoto” (“Ndoa ni Muhimu kwa Mpango Wake wa Milele,” Ensign, Juni 2006, 83–84).

Ona pia Mwanzo 2:20–24; 1 Wakorintho 11:11; “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 145.

Picha
wanandoa nje ya hekalu

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetakaswa na Mungu.

Mafundisho na Maagano 50

Mafundisho ya Bwana yanaweza kunilinda kutokana na uongo wa shetani.

Waongofu wapya huko Ohio walikuwa na shauku ya kupokea madhihirisho ya kiroho yaliyoahidiwa kwenye maandiko, lakini Shetani alikuwa pia na shauku ya kuwalaghai. Walijiuliza, Wakati mtu anapopiga kelele au kuzimia, je, huo ni ushawishi wa Roho?

Fikiria kwamba uliombwa kuwasaidia waongofu hawa wapya kuelewa jinsi ya kutambua madhihirisho ya kweli ya Roho Mtakatifu na kuepuka kudanganywa na uigaji wa Shetani. Ni kanuni zipi unapata katika Mafundisho na Maagano 50 ambazo ungeweza kushiriki? (Ona hasa mistari 22–25, 29–34, 40–46).

Ona pia 2 Timotheo 3:13–17.

Mafundisho na Maagano 50:13–24

Walimu na wanafunzi wanainuliwa pamoja kwa Roho.

Njia moja unayoweza kujifunza Mafundisho na Maagano 50:13–24 ni kuchora picha ya mwalimu na mwanafunzi na, pembeni ya kila mmoja, tengeneza orodha ya maneno na vifungu kutoka kwenye mistari hii ambayo inakufundisha kitu kuhusu kujifunza na kufundisha injili. Ni lini umekuwa na uzoefu ambao ulikufundisha umuhimu wa Roho katika kufundisha na kujifunza? Fikiria kile unachoweza kufanya ili kuboresha juhudi zako kama anayejifunza na kufundisha injili.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 49:2.Inamaanisha nini “kutamani kujua ukweli kwa kiasi fulani, lakini siyo wote”? Pengine ungeweza kuonesha picha iliyofunikwa sehemu ndogo na waruhusu wanafamilia kubashiri picha hiyo ni nini. Nini hutokea wakati tunapokubali sehemu tu ya ukweli? (ona 2 Nefi 28:29). Ni kwa jinsi gani utimilifu wa injili ni baraka kwetu?

Mafundisho na Maagano 49:26–28.Ni kwa jinsi gani tumebarikiwa kwa ahadi ya Bwana “nitakwenda mbele yenu na nitawafuata nyuma; na nitakuwa kati yenu”? Wanafamilia wangeweza kushiriki uzoefu wakati walipohisi Bwana “akienda mbele [yao] au kuhisi kwamba Yeye alikuwa “katikati [yao].”

Mafundisho na Maagano 50:23–25.Mngeweza kukusanyika katika chumba chenye giza ili kusoma Mafundisho na Maagano 50:23–25 na kidogo kidogo ongeza nuru zaidi kwa kuwasha mishumaa au kuwasha balbu moja baada ya nyingine. Mngeweza pia kusoma mistari hii wakati mkitazama mawio ya jua asubuhi. Tunaweza kufanya nini ili kufanya nuru yetu ya injili iendelee kukua? Wakati wanafamilia wanapojifunza kitu kipya kuhusu injili katika kipindi cha wiki, wahimize wakishiriki pamoja na familia kwa kuandika ujumbe na kuupachika kwenye chemli au nuru zingine ndani ya nyumba.

Mafundisho na Maagano 50:40–46.Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 50:40–46, ungeweza kuonesha picha ya Mwokozi ambayo inaambatana na muhtasari huu na uliza maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani unaweza kugundua Mwokozi anawapenda kondoo? Ni kwa jinsi gani Mwokozi ni kama mchungaji kwetu? Ni vifungu gani vya maneno kutoka kwenye maandiko vinaakisi wazo kwamba Mwokozi ni mchungaji na sisi ni kondoo Wake?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Shine On,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,144.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa mwenye kubadilika kulingana na hali. Nyakati nzuri zaidi za kufundisha, hasa nyumbani, mara nyingi ni za wazi na zisizotarajiwa: mlo wa familia unaweza kuchochea mjadala kuhusu kusherehekea neno la Mungu, na dhoruba ya mvua ingeweza kuwa nafasi ya kushuhudia juu ya maji yaliyo hai. Ikiwa mmejiandaa kiroho, Bwana anaweza kuwapatia “katika wakati ule ule, kile mtakachosema” (Mafundisho na Maagano 100:6).

Picha
Yesu akiwa na mwana kondoo

Mchungaji Mpole, na Kim Yongsung

Chapisha