Mafundisho na Maagano 2021
Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48: “Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”


“Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48: ‘Takeni Sana Karama Zilizo Kuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 3–9. Mafundisho na Maagano 46–48,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
watu wakikutana kando ya dimbwi

Mkutano wa Kambi, na Worthington Whittredge

Mei 3–9

Mafundisho na Maagano 46–48

“Takeni Sana Karama Zilizo Kuu”

Unaposoma Mafundusho na Maagano 46–48, andika misukumo unayopokea. Kisha ungeweza kuuliza, kama Mzee Richard G. Scott alivyopendekeza, “Kuna chochote zaidi ninapaswa kujua?” (“Kupata Mwongozo wa Kiroho,”,” Ensign au Liahona, Nov.2009, 8).

Andika Misukumo Yako

Wakati Parley P. Pratt, Oliver Cowdery, Ziba Peterson, na Peter Whitmer Jr. Walipoondoka Kirtland na kuhamia kwenye mashamba mengine ya kazi, waliacha zaidi ya waongofu mia moja ambao walikuwa na ari kubwa lakini uzoefu au maelekezo kidogo. Hakukuwa na vitabu vya maelekezo, hakuna mikutano ya mafunzo ya uongozi, hakuna matangazo ya mkutano mkuu—kwa kweli, hakukuwepo hata nakala nyingi za Kitabu cha Mormoni kwa ajili ya kupitia. Wengi wa hawa waaminio wapya walikuwa wamevutwa kwenye injili ya urejesho kwa ahadi ya madhihirisho ya kustaajabisha ya Roho, hasa yale waliyoyafahamu kutokana na kujifunza Agano Jipya, 1 Wakorintho 12:1–11). Punde, baadhi ya madhihirisho yasiyo ya kawaida ya ibada—ikiwa ni pamoja na kuanguka ardhini au kuteleza kama nyoka—yalitambulishwa kwenye mikutano ya Kanisa. Wengi walipata wakati mgumu kutambua madhihirisho yapi yalikuwa ya Roho na yapi hayakuwa ya Roho. Alipoona mkanganyiko, Joseph Smith aliomba kwa ajili ya usaidizi. Jibu la Bwana lina thamani ile ile leo, wakati watu wanapokataa na kupuuzia mambo ya Roho. Bwana alifunua kwamba madhihirisho ya kiroho ni halisi na kufafanua kile yanachomaanisha—karama kutoka kwa Baba mpendwa wa Mbinguni, “zilizotolewa kwa manufaa ya wale ambao wanampenda [Yeye] na kushika amri [Zake] zote” (Mafundisho na Maagano 46:9).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 46:1–6

Wote wanaotafuta kwa bidii wanakaribishwa kuabudu katika Kanisa la Bwana.

Mikutano ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho inapaswa kuwa kati ya mikusanyiko yenye kukaribisha na kuvuvia katika ulimwengu. Ni kwa jinsi gani Bwana anatupatia ushauri katika Mafundisho na Maagano 46:1–6 ili kuwapokea wale wanaohudhuria mikutano yetu? Je, rafiki zako na watu katika ujirani wako wanahisi kukaribishwa kwenye shughuli za ibada za kata yako? Je, nini unafanya kufanya mikutano ya Kanisa lako kuwa mahali ambapo watu wanataka kurejea tena? Tafakari jinsi juhudi zako za kumfuata Roho Mtakatifu katika mikutano ya Kanisa zinaweza kuathiri uzoefu wako.

Ona pia 3 Nefi 18:22–23; Moroni 6:5–9; “Welcome,” video, ComeUntoChrist.org; “Msisimko wa Kidini kati ya Waongofu wa Mwanzo wa Ohio,” Ufunuo katika Muktadha, 105–11.

Mafundisho na Maagano 46:7–33

Mungu ametoa karama za kiroho ili kuwabariki watoto wake.

Watakatifu wa mwanzo waliamini katika karama za kiroho lakini walihitaji mwongozo kuhusu lengo lao. Unapojifunza kuhusu karama za Kiroho kwa kutumia Mafundisho na Maagano 46:7–33, tafakari kwa nini ni muhimu kwamba “daima [ukumbuke] ni kwa nini zinatolewa” (mstari wa 8). Fikiria jinsi mistari hii inavyohusika kwenye kauli hii kutoka kwa Mzee Robert D. Hales: “Karama hizi zimetolewa kwa wale ambao ni waaminifu kwa Kristo. Zitatusaidia kujua na kufundisha kweli za injili. Zitatusaidia kuwabariki wengine. Zitatuongoza kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni” (“Vipawa vya Kiroho,” Ensign, Feb. 2002, 16). Nini kingine unajifunza kutokana na mistari hii kuhusu madhihirisho ya kiroho? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinakusaidia “usije kudanganywa”? (mstari wa 8).

Tafakari karama zako za kiroho ni zipi—na jinsi unavyoweza kuzitumia “kwa manufaa ya watoto wa Mungu” (mstari wa 26). Kama una baraka ya baba mkuu, pengine inaonesha karama ulizopewa.

Ona pia Mada za Injili, “Karama za Kiroho,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Mafundisho na Maagano 47

Bwana anataka Kanisa Lake litunze historia.

Wito wa John Whitmer wa kutunza historia ya Kanisa uliendeleza utamaduni wa muda mrefu wa watunza historia miongoni mwa watu wa Mungu (ona 2 Nefi 29:11–12; Musa 6:5; Ibrahamu 1:28, 31). Kwa kweli, cheo cha Mwana historia wa Kanisa na Mtunza Kumbukumbu bado kinaendelea mpaka leo. Kwa nini unadhani kutunza historia ni muhimu sana kwa Bwana? Tafakari hili wakati unaposoma maelekezo Yake kwa John Whitmer kuhusu jukumu lake katika Mafundisho na Maagano 47. Pia fikiria uzoefu binafsi unaohitaji kuwekea kumbukumbu. Kwa mfano, ni nini Bwana amekufundisha ambacho unataka kuhifadhi?

Unapotafakari maswali haya, fikiria umaizi huu kutoka kwa Mzee Marlin K. Jensen wa sabini, ambaye alihudumu kama Mwanahistoria wa Kanisa na Mtunza Kumbukumbu kuanzia 2005 mpaka 2012:

“Tunatunza kumbukumbu ili zitusaidie kukumbuka. … Tunatamani kuwasaidia waumini wa Kanisa kukumbuka mambo makuu ambayo Mungu amefanya kwa watoto Wake. … Masomo yaliyopita yanatusaidia kuendana na wakati wetu uliopo na yanatupatia tumaini kwa ajili ya wakati wetu ujao” (“Kutakuwako Kumbukumbu Iliyotunzwa kati Yenu,” Ensign, Dec. , 28, 33).

Ili kujifunza zaidi kuhusu kazi ambayo kwa sasa inafanywa chini ya uelekezi wa Mwanahistoria wa Kanisa, tembelea history.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
John Whitmer

John Whitmer aliitwa kutunza historia ya Kanisa.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 46:2–6.Tunaweza kufanya nini kama familia kuhakikisha kwamba wengine wanahisi kukaribishwa kwenye mikutano yetu ya Kanisa? (Ona pia 3 Nefi 18:22–23). Picha inayoambatana na muhtasari huu ingeweza kuongezea kwenye mjadala huu.

Mafundisho na Maagano 46:7–26.Ni karama zipi za kiroho tunaziona kwa kila mmoja wetu? Ni kwa jinsi gani karama hizo zinaweza kubariki familia yetu?

Mafundisho na Maagano 47.Ni kwa jinsi gani unaweza kuwahimiza familia yako kuweka kumbukumbu ya historia zao binafsi kwa wiki nzima? Ungeweza kushiriki baadhi ya yale uliyoandika kutoka kwenye shajara yako binafsi au shiriki hadithi kuhusu babu aliyekwisha fariki (ona FamilySearch.org). Baadhi ya familia huweka kando dakika chache kila wiki kwa ajili ya kila mmoja kuandika katika shajara zao. Ungeweza kutoa baadhi ya vidokezo vya shajara, kama vile “Nini kilitokea wiki hii ambacho ungependa wajukuu zako wajue kukihusu?” au “Ni kwa jinsi gani uliona mkono wa Bwana katika maisha yako wiki hii?” Watoto wadogo wangeweza kuchora picha za uzoefu wao, au ungeweza kuwarekodi wakisimulia hadithi zao. Ni baraka zipi huja kutokana na kutunza “historia ya kila siku”? (mstari wa 1).

Mafundisho na Maagano 48.Watakatifu katika Ohio waliamriwa kushiriki ardhi yao na wale waliokuwa wakihamia Ohio kutoka mashariki ya Marekani. Je, nini tunaweza kushiriki ili kukidhi mahitaji ya wengine?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Have I Done Any Good?” (Nyimbo za Kanisa, na. 223).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia hadithi na mifano. Mwokozi mara nyingi alitumia hadithi na mifano kufundisha kanuni za injili. Fikiria mifano na hadithi kutoka kwenye maisha yako mwenyewe ambazo zinaweza kufanya kanuni za injili kuwa hai kwa familia yako (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,22).

Picha
watu kanisani

Baba wa Mbinguni huwapa watoto Wake karama za kiroho ili kubariki maisha ya wengine.

Chapisha