Mafundisho na Maagano 2021
Mei 17–23. Mafundisho na Maagano 51–57: “Mwaminifu, Mwenye Haki, na Mtumishi Mwenye Hekima”


“Mei 17–23. Mafundisho na Maagano 51–57: ‘Mwaminifu, Mwenye Haki, na Mtumishi Mwenye Hekima,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 17–23. Mafundisho na Maagano 51–57,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi

Picha
mkulima na maksai

Mkondo wa Kwanza, na James Taylor Harwood

Mei 17–23

Mafundisho na Maagano 51–57

“Mwaminifu, Mwenye Haki, na Mtumishi Mwenye Hekima”

Kwa kuongezea kwenye mawazo yaliyopendekezwa hapa, Roho anaweza kukushawishi kulenga kwenye kitu fulani kingine kutoka Mafundisho na Maagano 51–57 ambacho kinaweza kuwa muhimu kwa watoto unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waruhusu watoto wanaotaka kushiriki kitu fulani wanachojifunza kuvuta namba kutoka kwenye chombo ili kuamua utaratibu ambao watashiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 51:9

Naweza kuwa Mwaminifu.

Watoto wengi wadogo bado wanajifunza kile inachomaanisha kusema ukweli. Fikiria jinsi unavyoweza kuimarisha umuhimu wa kusema na kutenda kwa uaminifu.

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto kutoka Mafundisho na Maagano 51:9: “Ruhusu kila mtu atende kwa uaminifu” (ona pia Makala ya Imani 1:13). Waulize watoto kama wanajua kile inachomaanisha kuwa mwaminifu. Kuwasaidia waelewe vyema, wape mifano ya matendo ambayo ni ya uaminifu.

  • Shiriki hadithi chache za kawaida za watoto waliokabiliana na maamuzi kuhusu kuwa mwaminifu, kama vile uamuzi wa kukubali walipofanya kitu fulani kwa makosa. Tumia picha, vikaragosi vya soksi, au wanasesere wa karatasi kuzifanya hadithi kuwa za kuvutia zaidi. Waulize watoto kama watu hawa wanakuwa waaminifu au si waaminifu.

  • Imbeni wimbo kuhusu uaminifu, kama vile “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,159). Toa ushuhuda wako kuhusu kwa nini ni muhimu kuwa mwaminifu.

Mafundisho na Maagano 52:10; 53:3; 55:1

Kipawa cha Roho Mtakatifu kinapokelewa kwa kuwekewa mikono.

Kumpokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono kumetajwa mara kadhaa katika Mafundisho na Maagano 51–57. Hii inaweza kuwa fursa nzuri kufundisha watoto kuhusu ibada hii.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya mtoto akiwa anathibitishwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.104). Watake watoto kueleza nini kinatokea katika picha. Watake kupiga makofi wakati wanaposika “kuwekea mikono” au “kuweka mikono” unaposoma moja au zaidi ya mistari ifuatayo: Mafundisho na Maagano 52:10; 53:3; 55:1.

  • Wasimulie watoto kuhusu ulipopokea kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono baada ya kubatizwa. Wasaidie watoto kungojea kwa hamu kupokea kipawa hiki wao wenyewe. Jadiliana pamoja nao njia tunazoweza kumwalika Roho katika maisha yetu.

  • Imba “The Holy Ghost,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,105) au wimbo unaofanana. Onyesha maneno na vifungu vya maneno ambavyo vinafundisha kuhusu kipawa cha Roho Mtakatifu.

    Picha
    mvulana akithibitishwa

    Kielelezo cha mvulana akithibitishwa na Dan Burr

Mafundisho na Maagano 54:4–6

Tunapaswa daima kutimiza ahadi zetu.

Leman Copley aliweka agano kuwaruhusu Watakatifu kutoka Colesville, New York, waishi kwenye ardhi yake iliyoko Ohio. Lakini baada ya kuwasili, alivunja agano lake na kuwataka waondoke.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki pamoja na watoto nini kilitokea kwa Watakatifu waliokuja kuishi kwenye ardhi ya Leman Copley (ona sehemu ya kichwa cha habari cha Mafundisho na Maagano 54; ona pia “Sura ya 21: Ufunuo wa kuweka makazi katika Missouri,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 81–83). Wasaidie kufikiri jinsi Watakatifu walivyoweza kuhisi wakati Leman alipovunja ahadi yake.

  • Kata karatasi yenye mfano wa moyo katika vipande viwili vinavyolingana, na toa kila nusu kwa watoto wawili tofauti. Watake kuinua juu nusu zao pamoja kutengeneza moyo mzima. Waruhusu watoto wengine kuchukuwa zamu kuinua juu sehemu ya moyo. Wasaidie watoto kufananisha hii na ahadi au maagano tunayoyafanya pamoja na Mungu. Mungu daima atashikilia juu upande Wake wa maagano kama tunayashikilia juu ya kwetu.

  • Wakumbushe watoto kwamba wanapobatizwa, watafanya agano, na kuahidi, kutii amri za Mungu. Wasomee watoto kutoka Mafundisho na Maagano 54:6 jinsi Bwana anavyobariki watu wanaotimiza maagano yao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 51:19;55

Ninaweza kutumia baraka alizonipa Mungu kuwabariki wengine.

Bwana ametuamini kila mmoja wetu kwa zawadi na baraka tunazoweza kutumia kujenga ufalme wake.

Shughuli Yamkini

  • Ficha maneno “mwaminifu”, “mwenye haki”, na “mwenye busara” kuzunguka chumba. Watake watoto kutafuta maneno hayo, katika chumba na kisha kuyatafuta katika Mafundisho na Maagano 51:19. Someni mstari pamoja, na zungumzeni kuhusu kile inachomaanisha kuwa mtumishi. Kama ni muhimu, someni pamoja ibara ya kwanza ya “Mtumishi, Utumishi” katika Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org).

  • Wasimulie watoto kuhusu William W.Phelps, ambaye alikuwa mwandishi wa magazeti kabla ya kusikia injili na kuhamia Kirtland. Waombe watoto wasome Mafundisho na Maagano 55:1–4 na orodhesha kile Mungu alichotaka William kufanya. Kipi kati ya vitu hivi kinaweza kutumika kwetu sisi wote, na vipi ni maalumu kwa William kwa sababu ya ujuzi wake? Watake watoto kutambua ujuzi wanaouona kati ya wao kwa wao, na jadili jinsi wanavyoweza kutumia ujuzi huo kumhudumia Mungu na watoto Wake.

Mafundisho na Maagano 52:14–19

Mungu ana mpangilio kunisaidia nisidaganywe.

Katika mistari hii, Bwana alitoa mpangilio ili “kwamba [sisi] tusidanganywe” (Mafundisho na Maagano 52:14.) na walimu waongo na jumbe.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto mfano wa mpangilo (kama vile mpangilio kwa ajili ya kushona nguo au kutengeneza kitu fulani), na zungumza kuhusu kwa nini mipangilio ni yenye msaada. Kuwasaidia watoto kujifunza kuhusu mpangilio kutoka kwa Bwana, andika ubaoni vifungu vya maneno kama Yeye ambaye, ni sawa na,Yeye ambaye atakuwa, na Yeye ambaye sio. Watake watoto wasome Mafundisho na Maagano 52:15–18 na wajaze sehemu tupu. Kwa nini mpangilio huu ni wenye msaada kwetu? (ona mistari 14, 19).

  • Chora kitu fulani rahisi, na watake watoto kufuatisha mpangilio wako kufanya mchoro sawa na huo. Kisha peleleza pamoja nao mpangilio wa Bwana ulioandikwa katika Mafundisho na Maagano 52:14–19.

Mafundisho na Maagano 54

Ninapaswa daima kutimiza maagano yangu.

Hata kama maagano yetu ni ya kibinafsi, uaminifu wetu katika kuyatimiza unaweza kuathiri maisha ya wengine. Hadithi ya Leman Copley na Watakatifu kutoka Colesville, New York, ni kielelezo cha ukweli huu.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki pamoja na watoto nini kilitokea kwa Watakatifu waliokuja kutoka Colesville, New York kuishi kwenye ardhi ya Leman Copley (ona sehemu ya kichwa cha habari cha Mafundisho na Maagano 54; ona pia “Sura ya 21: Ufunuo wa Kuweka Makazi katika Missouri,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 81–82). Jinsi gani ungehisi kuwa mmoja wa hao Watakatifu na kufahamu ya kwamba Leman alivunja agano lake la kushiriki ardhi yake? Hii hadithi inatufundisha nini kuhusu kutimiza maagano yetu? Someni pamoja Mafundisho na Maagano 54:6 kujifunza kuhusu baraka Bwana anazotoa kwa wale wanaotimiza maagano yao.

  • Wakumbushe watoto juu ya maagano waliyoyafanya walipobatizwa (ona Mosia 18:8–10). Wasaidie wafikiri juu ya njia wanazotimiza maagano haya, na wasaidie kuona jinsi hii itakavyowaandaa kufanya maagano ya ziada hapo baadaye.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kama watoto wanaonekana kufurahia moja ya shughuli leo, pendekeza kwamba warudie shughuli hiyo nyumbani pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi kile unachofundisha. Ufundishaji wako utakuwa na nguvu zaidi kama unaweza kushuhudia kutoka kwenye uzoefu wako binafsi kuhusu baraka za kuishi injili. Unapochagua kanuni za kufundisha watoto, tafakari jinsi unavyoweza kuishi kanuni hizo kwa ukamilifu zaidi. (Ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13–14.)

Chapisha