Mafundisho na Maagano 2021
Juni 28–Julai 4. Mafundisho na Maagano 71–75: “Hakuna Silaha Iliyotengenezwa dhidi Yenu Itakayofanikiwa”


“Juni 28–Julai 4. Mafundisho na Maagano 71–75: ‘Hakuna Silaha Iliyotengenezwa dhidi Yenu Itakayofanikiwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Juni 28–Julai 4. Mafundisho na Maagano 71–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Yesu na kondoo

Dear to the Heart of the Shepherd, na Simon Dewey

Juni 28–Julai 4

Mafundisho na Maagano 71–75

“Hakuna Silaha Iliyotengenezwa dhidi Yenu Itakayofanikiwa”

Mzee Quentin L. Cook alifundisha, “Ushawishi wa Roho Mtakatifu mara nyingi unasindikiza kujifunza maandiko kibinafsi na sala nyumbani” (“Uongofu wa Kina na wa Kudumu kwa Baba wa Mbinguni na Bwana Yesu Kristo,” Ensign au Liahona, Nov. 2018, 10).

Andika Misukumo Yako

Tangu alipokuwa mvulana mdogo, Joseph Smith alipitia ukosoaji—hata maadui—wakati alipojaribu kuifanya kazi ya Mungu. Lakini yaweza kuwa ilikuwa hasa ya kuvunja moyo mwishoni mwa 1831 wakati Ezra Booth alipoanza kukemea Kanisa hadharani, kwa sababu kwenye hili mkosoaji alikuwa muumini wa zamani. Ezra alikuwa amemwona Joseph akitumia nguvu za Mungu kumponya mwanamke. Alikuwa amealikwa kumsindikiza Joseph kwenye utafiti wa kwanza wa nchi ya Sayuni huko Missouri. Lakini tangu hapo alikuwa amepoteza imani yake na, katika jaribio lake la kumkosoa Nabii, alichapisha mfululizo wa barua kwenye gazeti la Ohio. Na juhudi zake zilionekana kufaulu: “hisia zisizo za kirafiki … zilijitokeza dhidi ya Kanisa” (Mafundisho na Maagano 71, kichwa cha habari cha sehemu). Nini waumini wanapaswa kufanya katika hali sawa na hii? Wakati hakuna jibu moja sahihi kwa kila hali, inaonekana kwamba mara nyingi—ikijumuisha suala hili mnamo 1831—sehemu ya jibu la Bwana ni kutetea ukweli na kusahihisha uongo kwa “kutangaza injili” (mstari wa 1). Ndiyo, kazi ya Bwana daima itapata ukosoaji, lakini mwishoni, “hakuna silaha iliyotengenezwa dhidi [yake] itakayofanikiwa” (mstari wa 9).

Ona “Ezra Booth na Isaac Morley,” Ufunuo katika Muktadha,134.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 71

Bwana atafadhaisha ukosoaji wa kazi Yake katika wakati Wake mwenyewe.

Tunaweza kuwa na wasiwasi tunaposikia watu wakikosoa au kukejeli Kanisa au viongozi wake, hasa wakati tunapokuwa na woga kwamba watu tunaowafahamu na kuwapenda watashawishika na ukosoaji huo. Wakati jambo sawa na hilo lilipotokea Ohio mnamo 1831 (ona kichwa cha habari cha sehemu ya Mafundisho na Maagano 71), ujumbe wa Bwana kwa Joseph Smith na Sidney Rigdon ulikuwa wa imani, si wa woga. Unapojifunza Mafundisho na Maagano 71, nini unapata ambacho kinajenga imani yako katika Bwana na kazi Yake. Nini kinakuvutia kuhusu maelekezo Bwana aliyowapa watumishi Wake katika hali hii?

Ona pia Robert D. Hales, “Ujasiri wa Mkristo: Gharama ya Ufuasi,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 72–75; Jörg Klebingat, “Kutetea Imani,” Ensign, Sept. 2017, 49–53.

Mafundisho na Maagano 72

Maaskofu ni watumishi juu ya maswala ya kiroho na kimwili ya ufalme wa Bwana.

Wakati Newel K. Whitney alipoitwa kuhudumu kama askofu wa pili wa Kanisa, majukumu yake yalikuwa tofauti kidogo na yale ya maaskofu wa leo. Kwa mfano, Askofu Whitney alisimamia uwekaji wakfu wa mali na ruhusa ya kukaa Missouri, katika nchi ya Sayuni. Lakini unaposoma kuhusu wito na majukumu yake katika Mafundisho na Maagano 72, ungeweza kugundua baadhi ya muunganiko kwenye kile maaskofu wanachofanya leo—angalau katika roho, ikiwa si maelezo bayana ya majukumu yao. Kwa mfano, ni kwa njia zipi “unatoa hesabu ya usimamizi” kwa askofu wako? (mstari wa 5). Ni kwa mantiki ipi askofu wako “anaitunza ghala ya Bwana” na kusimamia uwekaji wakfu wa waumini wa kata? (ona mistari 10, 12). Ni kwa jinsi gani askofu amekusaidia?

Ona pia Mada za Injili, “Askofu,” topics.ChurchofJesusChrist.org.

Picha
mapipa na mifuko ya chakula

Newel K. Whitney alisimamia ghala la askofu.

Mafundisho na Maagano 73

Ninaweza kutafuta nafasi za kushiriki injili.

Baada ya Joseph Smith na Sidney Rigdon kurejea kutoka kwenye misheni zao fupi za kuhubiri ili kurekebisha baadhi ya uharibifu alioufanya Ezra Booth (ona Mafundisho na Maagano 71), Bwana aliwaambia warudi kwenye kazi ya kutafsiri Biblia (ona Kamusi ya Biblia, “Tafsiri ya Joseph Smith”). Lakini pia aliwataka kuendelea kuhubiri injili. Unaposoma Mafundisho na Maagano 73, fikiria jinsi unavyoweza kufanya kuhubiri injili kuwa endelevu, “ya kuweza kufanyika” (mstari wa 4)—au sehemu ya—uhalisia wa maisha yako kati ya majukumu yako mengine.

Mafundisho na Maagano 75:1–12

Bwana huwabariki wale wanaotangaza injili Yake kwa uaminifu.

Wakiitikia amri ya “Enendeni ulimwenguni mwote” mkaihubiri injili (Mafundisho na Maagano 68:8), wazee wengi waaminifu walitafuta taarifa za ziada kuhusu jinsi Bwana alivyowataka kutimiza amri hii. Ni maneno yapi na vishazi unavyopata katika Mafundisho na Maagano 75:1–12 ambayo yanakusaidia kuelewa jinsi ya kuhubiri injili kikamilifu? Ni baraka zipi Bwana anaahidi kwa wamisionari waaminifu? Fikiria jinsi maelekezo na baraka hizi zinavyohusika kwako wakati unaposhiriki injili.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 71.Ni nini Joseph Smith na Sidney Rigdon waliombwa kufanya wakati wengine walipokuwa wakikosoa Kanisa na viongozi wake? Ni kwa jinsi gani “tunatengeneza njia” kwa ajili ya watu kupokea ufunuo wa Mungu? (Mafundisho na Maagano 71:4).

Mafundisho na Maagano 72:2.Ni kwa jinsi gani maaskofu wamebariki familia yetu? Ni nini askofu wetu ametuomba kufanya, na ni kwa jinsi gani tunaweza kumuidhinisha? Pengine, familia yako ingeweza kutengeneza kadi ya kumshukuru askofu wenu kwa huduma yake.

Mafundisho na Maagano 73:3–4.Je, familia yako ingenufaika kutokana na kujifunza kuhusu Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia? (Ona Kamusi ya Biblia, “Tafsiri ya Joseph Smith”). Mngeweza kuchunguza vifungu kadhaa vya maneno ambavyo vilijerewa katika Tafsiri ya Joseph Smith na kujadili kweli za thamani Bwana alizofunua kupitia Joseph Smith. Kwa baadhi ya mifano, ona Tafsiri ya Joseph Smith ya Mwanzo 14:25–40 na Mwanzo 50:24–38 kwenye kiambatisho cha Biblia; marejeo kadhaa katika Mathayo 4:1–11; na Luka 2:46, rejeo c.

Mafundisho na Maagano 74:7.Mstari huu unatufunza nini kuhusu Yesu Kristo na watoto wadogo?

Mafundisho na Maagano 75:3–5, 13, 16.Unaweza kuisaidia familia yako kuelewa jinsi Bwana anavyotutaka tumtumikie Yeye kwa kuzungumza kuhusu tofauti kati ya “kukaa bure pasipo kazi” na “kufanya kazi kwa nguvu [zetu].” Pengine ungeweza kuchagua baadhi ya kazi za nyumbani na kuwaalika wanafamilia kuonesha kwa mifano kwa kufanya kazi hizo kivivu na kisha kwa nguvu zao zote. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumtumikia Bwana kwa nguvu zetu zote? Kulingana na Mafundisho na Maagano 75:3–5, 13, 16, ni nini Yeye anawaahidi watumishi Wake waaminifu.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Let Us All Press On,” Nyimbo za Kanisa, na. 243.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi.

Tafuta maneno na virai vyenye mwongozo. Unaposoma, Roho anaweza kuleta maneno fulani au virai kwenye umakini wako. Fikiria kuandika maneno au virai kutoka Mafundisho na Maagano 71–75 ambavyo vimekuvuvia.

Picha
mvulana pamoja na kiongozi wa ukuhani

Kielelezo cha mvulana pamoja na kiongozi wa ukuhani na D. Keith Larson

Chapisha