Mafundisho na Maagano 2021
Juni 21–27. Mafundisho na Maagano 67–70: “Thamani … Utajiri wa Dunia Yote”


“Juni 21–27. Mafundisho na Maagano 67–70: ‘Thamani … Utajiri wa Dunia Yote,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Juni 21–27. Mafundisho na Maagano 67–70,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
revelation manuscript book in display case

Juni 21–27

Mafundisho na Maagano 67–70:

“Thamani … Utajiri wa Dunia Yote”

Japokuwa nyingi za funuo katika Mafundisho na Maagano zilikua zimekusudiwa kwa watu maalumu katika mazingira maalumu, zilikuwa “zenye faida kwa wote” (“Ushuhuda wa Mitume Kumi na Wawili kwenye Ukweli wa Kitabu cha Mafundisho na Maagano,” utangulizi wa Mafundisho na Maagano). Unapojifunza, tafuta kweli na kanuni ambazo zina faida kwako.

Andika Misukumo Yako

Kutoka 1828 mpaka 1831, Nabii Joseph Smith alipokea funuo nyingi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni pamoja na ushauri wa kiungu kwa ajili ya watu binafsi, maelekezo juu ya kuongoza Kanisa, na maono yenye uvuvio ya siku za mwisho. Lakini Watakatifu wengi hawakuzisoma. Ufunuo ulikuwa bado haujachapishwa, na nakala chache zilizokuwepo zilikuwa zimeandikwa kwa mkono kwenye karatasi ambazo hazikufungwa pamoja ambazo zilisambazwa kwa waumini na kuchukuliwa kote na wamisionari.

Kisha, mnamo Novemba 1832, Joseph aliitisha baraza la viongozi wa Kanisa ili kujadili kuhusu uchapishaji wa ufunuo. Baada ya kutafuta mapenzi ya Bwana, viongozi hawa walifanya mipango ya kuchapisha Kitabu cha Amri—utangulizi wa Mafundisho na Maagano ya leo. Punde kila mtu angeweza kusoma wao wenyewe neno la Mungu lililofunuliwa kupitia nabii aliye hai, ushahidi hai kwamba “funguo za siri za ufalme wa Mwokozi wetu zimekabidhiwa tena kwa mwanadamu.” Kwa hizi na sababu zingine nyingi, Watakatifu wakati huo na sasa wanachukulia ufunuo huu kuwa “ni wa manufaa … kwa Ulimwengu wote” (Mafundisho na Maagano 70, kichwa cha habari cha sehemu).

Ona Watakatifu, 1:140–43.

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 67:1–9; 68:3–6

Mungu anawalinda watumishi Wake na maneno wanayozungumza katika jina Lake.

Uamuzi wa kuchapisha ufunuo uliopokelewa na Joseph Smith ulionekana kama rahisi, lakini baadhi ya viongozi wa mwanzo wa Kanisa hawakuwa na uhakika kama lilikuwa wazo zuri. Wasiwasi mmoja ulikuwa ni juu ya mapungufu kwenye lugha aliyotumia Joseph Smith kuandika ufunuo. Ufunuo katika sehemu ya 67 ulikuja kama jibu la wasiwasi huo. Nini unajifunza kuhusu manabii na ufunuo kutoka mistari 1–9? Je ni umaizi gani wa ziada unapata kutoka 68:3–6?

Kabla ya Kitabu cha Amri kuchapishwa, viongozi kadhaa wa Kanisa walitia saini ushuhuda ulioandikwa kwamba ufunuo katika kitabu ni wa kweli. Ili kuona nakala ya ushuhuda wao, ona “Testimony, circa 2 November 1831,” Revelation Book 1, 121, josephsmithpapers.org.

Mafundisho na Maagano 68:1–8

Uvuvio kutoka kwa Roho Mtakatifu unaakisi mapenzi ya Bwana.

Maneno katika mistari hii yalizungumzwa wakati Orson Hyde na wengine walipoitwa “kuitangaza injili isiyo na mwisho kwa Roho wa Mungu aliye hai, kutoka taifa hadi taifa, na kutoka nchi hadi nchi” (mstari wa 1). Ni kwa jinsi gani tangazo katika mstari wa 4 lingeweza kumsaidia mtu ambaye ametumwa kuhubiri injili? Ni kwa jinsi gani maneno haya yanahusika kwako? Fikiria wakati ambapo “uliongozwa na Roho Mtakatifu” (mstari wa 3) kusema au kufanya jambo. Ni kipi unapata katika mistari hii ambacho kinaweza kukupa ujasiri wa kufuata uvuvio wa kiroho?

Mafundisho na Maagano 68:25–28

Wazazi wanawajibika kuwafundisha watoto wao?

Dada Joy D. Jones, Rais Mkuu wa Msingi, alifundisha, “Muhimu kwenye kuwasaidia watoto kuwa kizazi kinzani kwa dhambi ni kuanza katika umri mdogo kwa upendo kuwafundisha kanuni za msingi za injili na mafundisho—kutoka kwenye maandiko, Makala ya Imani, kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana, nyimbo za darasa la msingi, nyimbo za Kanisa, na ushuhuda wetu wenyewe—ambao utawaongoza watoto kwa Mwokozi” (“Kizazi Kinzani kwa Dhambi,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 88).

Kulingana na Mafundisho na Maagano 68:25–28, ni “kanuni zipi za msingi za mafundisho” ambazo Dada Jones alizitaja ambazo wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao? Kwa nini hili ni jukumu muhimu walilopewa wazazi? Ni nini ungemwambia mzazi ambaye hahisi kuwa na sifa za kufundisha mambo haya kwa watoto wake?

Ona pia Tad R. Callister, “Wazazi: Waalimu Wakuu wa Injili wa Watoto Wao,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 32–34.

Picha
Familia ikijifunza

Nyumbani ni sehemu bora kwa watoto kujifunza injili.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 67:10–14.Ni kwa jinsi gani wivu, hofu, na kiburi vinatuzuia kusogea karibu na Bwana? Kwa nini “mwanadamu wa tabia ya asili” hawezi kuwa kwenye uwepo wa Mungu? (mstari wa 12; ona pia Mosia 3:19). Ni nini tunapata katika mistari hii ambacho kinatuvuvia “kuendelea katika uvumilivu hadi [tutakapokuwa] tumekamilika”? (mstari wa13).

Kama familia, mngeweza pia kurejea ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Hatimaye—Muwe Wakamilifu” (Ensign au Liahona, Nov. 2017, 40–42).

Mafundisho na Maagano 68:3–4.Wanafamilia wangeweza kushiriki uzoefu ambao umeimarisha imani yao kwamba maneno ya watumishi wa Mungu ni “mapenzi ya Bwana,” “nia ya Bwana,” na “uweza wa Mungu kwa wokovu” (mstari wa 4). Au wangeweza kutafuta ujumbe wa mkutano mkuu wa karibuni ambao unahusika kwenye changamoto ambayo familia yako inaweza kuwa inapitia.

Mafundisho na Maagano 68:25–35.Mistari hii ina ushauri muhimu kwa “sheria kwa wakazi wa Sayuni” (mstari wa 26). Ni nini tunavuviwa kuboresha baada ya kusoma mistari hii? Ingeweza kuwa ya kufurahisha kutengeneza picha zinazoonesha baadhi ya kanuni katika mistari hii na kuzificha kuzunguka nyumba yenu. Kisha, katika siku zijazo wakati mtu anapoipata picha, ungeweza kutumia hiyo kama fursa ya kufundisha kuhusu kanuni hiyo. Kwa nini nyumbani ni mahala pazuri zaidi kwa watoto kujifunza mambo haya?

Mafundisho na Maagano 69:1–2.Oliver Cowdery alitumwa kwenda Missouri akiwa na nakala zilizoandikwa za ufunuo wa nabii kwa ajili ya kuchapishwa, pamoja na pesa za kusaidia kujenga Kanisa huko. Ni ushauri gani Bwana aliutoa katika mstari wa 1 kuhusu safari ya Oliver? Kwa nini ni muhimu kuwa pamoja na watu “ambao watakuwa wakweli na waaminifu”? (mstari wa 1). Ni lini marafiki walitushawishi kufanya maamuzi mazuri au mabaya? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kuwa ushawishi mzuri kwa wengine?

Mafundisho na Maagano 70:1–4.Bwana aliwapa baadhi ya wazee jukumu la kusimamia uchapishaji wa ufunuo. Hata kama hatuna jukumu hilo maalumu, ni katika mtazamo upi tungeweza kufikiriwa kuwa “wasimamizi wa mafunuo na amri”? (mstari wa 3).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa “Home Can Be a Heaven on Earth,” Nyimbo za Kanisa, na. 298.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kutumia maandiko katika maisha yetu. Baada ya kusoma kifungu cha maandiko, waalike wanafamilia kukitumia katika maisha yao. Kwa mfano, ungeweza kuwaalika kufikiria juu ya hali zinazofanana ambazo wangeweza kukabiliana nazo zinazohusisha kanuni zinazofanana za injili.

Picha
Mtambo wa uchapishaji wa Grandin

Kitabu cha Amri, utangulizi wa Mafundisho na Maagano, kilichapishwa kwenye mtambo kama huu.

Chapisha