Mafundisho na Maagano 2021
Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62: “Wenye Mwili Wako katika Mikono Yangu”


“Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60–62: ‘Wenye Mwili Wako katika Mikono Yangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Mei 31–Juni 6. Mafundisho na Maagano 60-62,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Mto Missouri

Moto wa Kambi huko Missouri, na Bryan Mark Taylor

Mei 31–Juni 6

Mafundisho na Maagano 60–62

“Wenye Mwili Wako katika Mikono Yangu”

Rais Ezra Taft Benson alifundisha kwamba wakati tunapojifunza maandiko, “shuhuda zitaongezeka. Kujitolea kutaimarishwa. Familia zitakingwa. Ufunuo binafsi utakuja” (“The Power of the Word,” Ensign, Mei 1986, 81).

Andika Misukumo Yako

Mnamo 1831, Joseph Smith alifanya mkutano na wazee wa Kanisa huko Kirtland. Huko, Bwana aliwapanga baadhi ya wazee wawili wawili na kuwatuma kwenda Wilaya ya Jackson, Missouri, kwa agizo hili: “Wafundishe njiani” (Mafundisho na Maagano 52:10). Wengi wa wazee walifanya hivyo kwa bidii, lakini wengine hawakufanya hivyo. Kwa hivyo muda ulipofika wa kurudi Kirtland, Bwana alisema, “Lakini kwa [wazee] wengine sipendezwi nao, kwani hawafungui vinywa vyao, bali wanaficha vipaji ambavyo nimewapa, kwa sababu ya kumwogopa mwanadamu” (Mafundisho na Maagano 60:2). Wengi wetu tunaweza kuhisi huruma kwa Wazee hawa—tunaweza pia kuhisi kusita kufungua vinywa vyetu na kushiriki injili. Pengine sisi pia tunakwamishwa na “kumwogopa mwanadamu.” Pengine tunatilia mashaka ustahiki au uwezo wetu. Bila kujali sababu zetu, Bwana “anajua udhaifu wa mwanadamu na namna ya [kutusaidia] (Mafundisho na Maagano 62). lililoenea kote katika ufunuo huu kwa wamisionari wa mwanzo ni hakikisho ambalo linaweza kutusaidia kushinda hofu zetu kuhusu kushiriki injili—au hofu zingine tunazoweza kuwa tunakabiliana nazo: “Mimi, Bwana, natawala katika mbingu juu.” “Ninaweza kuwatakasa.” “Wenye mwili wako katika mikono yangu.” Na “muwe na furaha, watoto wadogo; kwani mimi nipo katikati yenu.” (Mafundisho na Maagano 60:4, 7; 61:6, 36.)

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 60;62

Bwana anapendezwa pale ninapofungua kinywa changu kushiriki injili.

Sote tumekuwa na uzoefu ambapo tungeweza kushiriki injili na mtu, lakini kwa sababu fulani, hatukufanya hivyo. Unaposoma maneno ya Bwana kwa wamisionari wa mwanzo ambao walishindwa “kufungua vinywa vyao,” fikiria kuhusu fursa zako mwenyewe za kushiriki injili. Ni kwa jinsi gani ushuhuda wako wa injili ni kama “kipaji,” au hazina kutoka kwa Mungu? Ni katika njia zipi sisi wakati mwingine “huficha kipaji [chetu]”? (Mafundisho na Maagano 60:2; ona pia Mathayo 25:14–30).

Bwana aliwasahihisha wamisionari hawa wa mwanzo, lakini Yeye pia alijaribu kuwapa msukumo. Ni ujumbe upi wa kutia moyo kutoka Kwake unaupata katika sehemu ya 60 na 62? Ni kwa jinsi gani ujumbe huu unajenga ujasiri wako katika kushiriki injili? Katika siku zijazo, tafuta fursa za kufungua kinywa chako na kushiriki kile Mungu alichokuamini nacho.

Ona pia Mafundisho na Maagano 33:8–10; 103:9–10; Dieter F. Uchtdorf, “Kazi ya Umisonari: Shiriki Yaliyo Moyoni Mwako,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 15–18.

Picha
wamisionari ndani ya basi

Mungu ananitaka nishiriki injili na wengine.

Mafundisho na Maagano 61:5–6; 14–18

Je, maji yote yamelaaniwa na Bwana?

Onyo la Bwana katika Mafundisho na Maagano 61 lilikuwa, kwa sehemu, onyo kuhusu hatari ambazo watu Wake wangepitia wakati wakisafiri kwenda Sayuni kwenye Mto Missouri, ambao ulikuwa ukijulikana kipindi hicho kwa kuwa hatari. Onyo hili halipaswi kutafsiriwa kumaanisha kwamba tunapaswa kuepuka usafiri wa maji. Bwana anao “uwezo wote,” ikiwa ni pamoja na nguvu juu ya maji (mstari wa 1).

Mafundisho na Maagano 61–62

Bwana ana nguvu na anaweza kunilinda.

Njiani kurudi Kirtland, Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa walipata uzoefu wa kutishia maisha kwenye Mto Missouri (ona Watakatifu, 1:133–34). Bwana alitumia fursa hii kuwaonya na kuwaelekeza watumishi Wake. Unapata nini katika Mafundisho na Maagano 61 ambacho kinakuhimiza kumwamini Bwana wakati unapokabiliana na changamoto zako mwenyewe? Kwa mfano, kwa nini ni muhimu kujua kwamba Mungu ni “tangu milele hata milele”? (mstari wa 1).

Kuna utambuzi wa kufanana katika sehemu ya 62. Ni nini Bwana anakufundisha kuhusu Yeye na nguvu Yake katika ufunuo huu?

Tafakari uzoefu wa kujenga imani uliowahi kuwa nao wakati Bwana alipokusaidia kushinda jaribu la kiroho au kimwili.

Mafundisho na Maagano 62

Bwana ananitaka nifanye baadhi ya maamuzi “nionavyo [mimi] kuwa ni vyema.”

Wakati mwingine Bwana hutupatia maelekezo maalumu, na mambo mengine Yeye hutuachia sisi tuamue. Ni kwa jinsi gani unaona kanuni hii ikioneshwa katika Mafundisho na Maagano 62? (ona pia Mafundisho na Maagano 60:5; 61:22). Ni kwa jinsi gani umeona kanuni hii katika maisha yako? Kwa nini ni vizuri kwetu kufanya baadhi ya maamuzi bila maelekezo maalumu kutoka kwa Mungu?

Ona pia Etheri 2:18–25; Mafundisho na Maagano 58:27–28.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 60:2–3.Kwa nini baadhi ya wamisionari wa mwanzo walisita kushiriki injili? Kwa nini sisi wakati mwingine tunasita? Fikiria kuigiza jinsi ambavyo wanafamilia wangeweza kushiriki injili katika mazingira tofauti.

Mafundisho na Maagano 61:36–39.Ni sababu zipi tunaziona katika mistari hii za “kuwa na furaha”? (Ona pia Yohana 16:33). Pengine familia yako ingeweza kuandika au kuchora picha za vitu ambavyo vinawaletea furaha na kuvikusanya ndani ya chupa ya “kuwa na furaha”. (Hakikisha kujumuisha picha za Mwokozi na vikumbusho vya upendo Wake kwetu.) Kote katika wiki wakati wanafamilia wanahitaji ukumbusho wa sababu za kuwa na furaha, wangeweza kuchagua jambo kutoka kwenye chupa.

Mafundisho na Maagano 61:36.Ni kwa jinsi gani unaweza kuisaidia familia yako kukumbuka kwamba Mwokozi yuko “katikati [yetu]”? Mngeweza kuamua pamoja wapi ni mashuhuri kwa ajili ya kuweka picha Yake katika nyumba yenu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumwalika Mwokozi kwenye maisha yetu ya kila siku?

Mafundisho na Maagano 62:3.Pengine ungeweza kuwa na mkutano wa shuhuda wa familia baada ya kusoma mstari huu. Ili kufafanua ushuhuda ni nini, ungeweza kushiriki sehemu ya ujumbe wa Rais M. Russell Ballard “Ushuhuda Msafi” (Ensign au Liahona, Nov. 2004, 40–43). Kwa nini ni vizuri kuandika shuhuda zetu?

Mafundisho na Maagano 62:5, 8.Kwa nini Bwana anatoa amri kuhusu kila kipengele cha maisha yetu? Kulingana na mstari wa 8, ni kwa jinsi gani tunapaswa kufanya maamuzi?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Testimony,” Nyimbo za Kanisa, na. 137.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi

Mruhusu Roho aongoze kujifunza kwako. Mruhusu Roho Mtakatifu akuongoze. Kuwa mwepesi kuhisi minong’ono Yake wakati Anapokuongoza kwenye mambo unayohitaji kujifunza kila siku, hata kama minong’ono Yake inapendekeza kwamba usome au kujifunza mada tofauti na ile ambayo ungeipendelea au katika njia tofauti.

Picha
Yesu amembeba mwana kondoo

Mchungaji Mwema, na Del Parson

Chapisha