Mafundisho na Maagano 2021
Julai 12–18. Mafundisho na Maagano 77–80: “Nitawaongoza”


“Julai 12–18. Mafundisho na Maagano 77–80: ‘Nitawaongoza,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 12–18. Mafundisho na Maagano 77–80,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
kondoo wakimfuata Yesu

Kwenda Nyumbani, na Yongsung Kim

Julai 12–18

Mafundisho na Maagano 77–80

“Nitawaongoza”

Bwana alimwambia Joseph Smith kwamba “angeongea katika masikio [yake] maneno ya hekima (Mafundisho na Maagano 78:2). Ni maneno yapi ya hekima unapokea wakati unapojifunza Mafundisho na Maagano 77–80?

Andika Misukumo Yako

Chini ya miaka miwili baada ya Kanisa la Yesu Kristo kurejeshwa, lilikuwa limekua kwa zaidi ya waumini 2,000 na lilikuwa likisambaa kwa kasi. Mnamo March 1832 Joseph Smith alikutana na viongozi wa Kanisa “kujadili utaratibu wa Kanisa”: hitaji la kuchapisha ufunuo, kununua ardhi ya kukusanyikia, na kuwatunza masikini (ona Mafundisho na Maagano 78, kichwa cha habari cha sehemu). Ili kukidhi mahitaji haya, Bwana aliita idadi ndogo ya viongozi wa Kanisa kuunda Taasisi ya Muungano, kundi ambalo lingeunganisha nguvu zao kwenye “kuendeleza kazi” ya Bwana (mstari wa 4) katika maeneo haya. Lakini hata katika maswala kama hayo ya utawala, Bwana alifokasi kwenye mambo ya milele. Hatimaye, lengo la kiwanda cha uchapishaji au ghala—sawa na kila kitu kingine katika ufalme wa Mungu—ni kuwaandaa watoto Wake kupokea “mahali katika ulimwengu wa selestia” na “utajiri wa milele” (mistari 7, 18). Na ikiwa baraka hizo ni ngumu kustahimili kwa sasa, katikati ya maisha yaliyojaa shughuli za kila siku za maisha, Yeye anatuhakikishia, “changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza” (mstari wa 18).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 77

Mungu anafunua siri Zake kwa wale wanaotafuta kuzijua.

Miaka kumi na miwili baada ya Ono la Kwanza, mwaliko katika Yakobo 1:5 wa “kumwomba Mungu” uliendelea kumwongoza Joseph Smith wakati alipopungukiwa hekima. Wakati yeye na Sidney Rigdon walipokuwa na maswali kuhusu kitabu cha Ufunuo wakati walipofanyia kazi tafsiri yenye uvuvio ya Biblia, Joseph kiuhalisia alitafuta hekima kutoka kwa Mungu. Unaposoma Mafundisho na Maagano 77, fikiria kuandika umaizi wako kwenye sura zinazohusika katika kitabu cha Ufunuo.

Kwa kuongezea, tafakari jinsi unavyoweza kufuata mfano wa Nabii Joseph wakati unaposoma maandiko. Ungeweza kumwuliza Baba wa Mbinguni, “Ni nini ninapaswa kuelewa?”

Picha
Joseph Smith na Sidney Rigdon wakisoma

Tafsiri ya Biblia, na Liz Lemon Swindle

Mafundisho na Maagano 78

Taasisi ya Muungano ilikuwa nini?

Taasisi ya Muungano ilianzishwa ili kusimamia uchapishaji na maswala ya biashara ya Kanisa huko Ohio na Missouri. Iliundwa na Joseph Smith, Newel K. Whitney, na viongozi wengine wa Kanisa ambao waliunganisha rasilimali zao ili kukidhi mahitaji ya kimwili ya Kanisa linalokua. Kwa bahati mbaya, Taasisi ya Muungano iliangukia kwenye madeni na ilisambaratika mnamo 1834 wakati madeni yalipokuwa makubwa.

Ona pia “Newel K. Whitney na Taasisi ya Muungano,” Ufunuo katika Muktadha, 142–47; “Taasisi ya Muungano,” Church History Topics, ChurchofJesusChrist.org/study/church-history.

Mafundisho na Maagano 78:1–7

Ninaweza kusaidia “kuendeleza kazi” ya Kanisa.

Bwana alimwambia Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa kwamba kutunza ghala na kiwanda cha uchapishaji kungesaidia “kuendeleza kazi, ambayo mmejioza” (Mafundisho na Maagano 78:4). Ni nini ungesema ingekuwa “kazi” ya Kanisa? Tafakari hili unaposoma Mafundisho na Maagano 78:1–7. Pengine kufikiria kuhusu mistari hii kungeweza kushawishi jinsi unavyotimiza wito wa Kanisa au unavyoitumikia familia yako. Ni kwa jinsi gani huduma yako “inaendeleza kazi” ya Bwana? Ni kwa jinsi gani inakuandaa wewe kwa ajili ya “mahali katika ulimwengu wa selestia”? (mstari wa 7).

Mafundisho na Maagano 78:17–22

Bwana ataniongoza.

Je, umewahi kuhisi kuwa sawa na mtoto mdogo, pengine kwa sababu ya kitu ambacho “bado hujakielewa” au “hujakistahimili”? (Mafundisho na Maagano 78:17–18). Tafuta ushauri katika mistari hii ambao unaweza kukusaidia wewe “kuchangamka” (mstari wa 18) kwenye nyakati sawa na hizo. Kwa nini unadhani Bwana wakati mwingine huwaita wafuasi Wake “watoto wadogo”? (mstari wa 17). Ungeweza pia kutafakari jinsi ambavyo Bwana angeweza “kukuongoza” (mstari wa 18).

Mafundisho na Maagano 79–80

Wito wa kumtumikia Mungu unahusika zaidi kuliko wapi unapotumikia.

Kuhusu Mafundisho na Maagano 80, Mzee David A. Bednar alifundisha, “Pengine moja ya masomo Mwokozi anayotufundisha katika ufunuo huu ni kwamba jukumu la kutumikia katika mahala maalumu ni muhimu na la kipekee lakini si la pili kwenye wito kwenye kazi” (“Tumeitwa Kwenye Kazi,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 68). Fikiria kuhusu miito yako iliyopita na ya sasa ya Kanisa. Ni uzoefu gani umekusaidia kujifunza kwamba maneno ya Mzee Bednar ni ya kweli? Ni masomo yapi ya ziada unaweza kupata katika Mafundisho na Maagano 79–80 ambayo yangeweza kumsaidia mtu ambaye punde tu amepokea wito mpya?

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 77:2.Baada ya kusoma mstari huu, wanafamilia wangeweza kuchora picha za “wanyama, … vitu vitambaavyo, … [au] ndege wa angani” wanaowapenda walioumbwa na Mungu. Nini tunajifunza kuhusu uumbaji wa Mungu kutoka kwenye mstari huu? (Ona pia Mafundisho na Maagano 59:16–20). Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu uumbaji wa Mungu, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29), na kuonesha mchoro unaoambatana na muhtasari huu.

Mafundisho na Maagano 77:14.Mstari huu unaelezea kwamba Yohana alikula kitabu ambacho kiliwakilisha misheni yake ya kukusanya Israeli. Ni nini ishara ya kula inapendekeza kuhusu jinsi tunavyopaswa kuliendea jukumu letu katika kukusanya Israeli au kufanya mambo mengine ambayo Bwana anatutaka tufanye? Hapa ni baadhi ya maandiko mengine ambapo kula kumetumika kufundisha ukweli wa kiroho: Yohana 6:48–51; 2 Nefi 32:3; Moroni 4. Pengine ungeweza kuandaa chakula pendwa cha familia ili kula pamoja wakati wa mjadala huu.

Mafundisho na Maagano 78:17–19.Wanafamilia wangeweza kuchora picha za baraka kutoka kwa Mungu ambazo kwazo wana shukrani. Je, tunafanya nini ili kuelezea shukrani zetu kwa baraka hizi? Ungeweza pia kujadili jinsi familia yako inavyofuata ushauri wa kupokea “vitu vyote kwa shukrani” (mstari wa 19). Ni nini Bwana anaahidi kwa wale wanaofanya hivyo?

Mafundisho na Maagano 79:1.Shiriki ushuhuda wako juu ya “uwezo” uliopokea wakati ulipotawazwa au kutengwa kwenye miito ndani ya Kanisa. Ni vipawa gani na uvuvio maalumu Bwana alikubariki nao wakati ulipotumikia?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Count Your Blessings,” Nyimbo za Kanisa, na. 241.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Chora picha. Kama familia, mnaweza kusoma mistari michache na kisha toa muda kwa wanafamilia kuchora kitu kinachohusiana na kile mlichosoma. Weka picha kuzunguka nyumba yenu ili kuwakumbusha familia yako juu ya kanuni mlizojifunza.

Picha
bustani yenye wanyama

Bustani ya Mungu, na Sam Lawlor

Chapisha