Mafundisho na Maagano 2021
Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84: “Nguvu za Uchamungu”


“Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84: “Nguvu za Uchamungu”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Julai 26–Agosti 1. Mafundisho na Maagano 84,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Joseph Smith akipokea Ukuhani wa Melkizedeki

Urejesho, na Liz Lemon Swindle

Julai 26–Agosti 1

Mafundisho na Maagano 84

“Nguvu za Uchamungu”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 84, ni kweli gani unazohisi zimekushawishi kuzisisitiza kwa watoto unaowafundisha? Andika umaizi unaokujia kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Watake watoto kushiriki vitu wanavyojua kuhusu ukuhani. Ungeweza kuonyesha picha ya mtu fulani akibarikiwa na nguvu ya ukuhani, (kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 103–10, na waulize watoto jinsi gani ukuhani unabariki familia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 84:19–22; 26:–27

Ukuhani ni uwezo wa Mungu.

Je, watoto unaowafundisha wanajua azma ya ukuhani? Katika Mafundisho na Maagano 84, Bwana anafunua azma moja: kutusaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni. (Kujifunza zaidi, ona Mada za Injili, “Ukuhani,” topics.ChurchofJesusChrist.org

Shughuli Yamkini

  • Soma Mafundisho na Maagano 84:20, na watake watoto kusimama wakati wanaposikia neno “ibada.” Kuwasaidia kuelewa ibada ni nini, onyesha picha za ibada kadhaa za ukuhani, kama vile Kitabu cha sanaa ya Injili, na. 103–8, na waombe watoto waelezee nini kinatokea katika kila picha (ona pia Mwongozo kwenye Maandiko, “Ibada,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Elezea kwamba Baba wa Mbinguni ametupatia sisi ibada hizi kutusaidia kurudi na kuishi pamoja Naye.

  • Waache watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli. Wanapofanya hivyo, elezea ibada mbalimbali za ukuhani zilizooneshwa kwenye ukurasa na kwa nini una shukrani kwa ajili ya ibada hizo.

Mafundisho na Maagano 84:77

Mimi ni rafiki wa Yesu ninapomfuata Yeye.

Jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujua kwamba Mwokozi anatupenda sisi hata zaidi kuliko rafiki mpendwa anavyotupenda.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Mwokozi unaposoma Mafundisho na Maagano 84:77. Watake watoto kuonyesha kwenye picha ya Mwokozi kila wakati wanaposikia neno “marafiki.” Elezea kwamba wakati tunapojaribu kutii amri, tunamwonyesha Yesu kwamba tunampenda Yeye. Shiriki nini inamaanisha kwako kuwa na Yesu kama rafiki yako.

  • Wasaidie watoto kuorodhesha baadhi ya vitu wanavyoweza kufanya kuwaonyesha rafiki zao kwamba wanawapenda. Ni nini Yesu alifanya kutuonyesha kwamba Yeye ni rafiki yetu. Je, tunaweza kufanya nini kumwonyesha Mwokozi kwamba sisi ni rafiki Zake? Imbeni pamoja wimbo kuhusu Yesu, kama vile “Jesu is Our Loving Friend” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 58).

Mafundisho na Maagano 84:88

Baba wa Mbinguni anawasaidia wamisionari Wake.

Wazo la kuwa mmisionari siku moja linaweza kuwa la kusisimua lakini pia la kutisha kwa baadhi ya watoto. Mafundisho na Maagano 84:88 inaweza kuwafundisha jinsi Baba wa Mbinguni anavyowasaidia wale walio tayari kuhubiri injili Yake.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya wamisionari wanaowajua. Waambie kwamba Baba wa Mbinguni amefanya ahadi maalumu kwa wamisionari. Soma Mafundisho na Maagano 84:88, na wasaidie watoto kufikiria juu ya vitendo ambavyo vinakwenda pamoja na ahadi katika mstari huu. Simulia kuhusu wakati ulipokuwa unamhudumia Bwana na ukahisi kwamba Alikuwa pamoja nawe, kama ilivyosimuliwa katika mstari wa 88.

  • Shiriki hadithi ya mvulana mwenye umri wa miaka minne katika ujumbe wa Mzee Takashi Wada “Kula na Kusherehekea Maneno ya Kristo” (Ensign au Liahona, Mei 2019, 38–40). Msaidie kila mtoto kufikiria juu ya kitu fulani ambacho wangeweza kusema kushiriki ushuhuda wao pamoja na mtu fulani—kama vile kushiriki makala ya imani. Mtake kila mtoto kujifanya anashiriki injili pamoja na rafiki. Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anatusaidia kujua nini cha kusema wakati tunazungumza pamoja na wengine kuhusu injili.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 84:4–5, 18–28, 30

Ibada za ukuhani zinanisaidia kujiandaa kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

Wanapokuwa wakubwa, watoto unaowafundisha wataweza kushiriki katika ibada zaidi za ukuhani, pamoja na ubatizo na uthibitisho kwa ajili ya wafu katika hekalu. Unawezaje kuwasaidia waelewe azma na nguvu za ibada za ukuhani?

Shughuli Yamkini

  • Andika Ukuhani wa Haruni na Ukuhani wa Melkizedeki ubaoni. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 84:18, 26–28, 30, na wasaidie watoto kuorodhesha kweli wanazojifunza kuhusu Ukuhani wa Haruni kutoka mistari hii. Kisha someni pamoja Mafundisho na Maagano 84:18–25, na orodhesha kweli kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki.

  • Watake watoto kuorodhesha ibada za ukuhani walizozishiriki au kuzishuhudia, kama vile ubatizo, uthibitisho, baraka za ukuhani, au sakramenti. Waombe washiriki uzoefu wao wa ibada hizi. Someni Mafundisho na Maagano 84:20 Pamoja (wasaidie kuelewa maneno wasiyofahamika). Je, ni kwa nini Bwana anatutaka kushiriki katika ibada? Jinsi gani ukuhani unatusaidia kurudi kwa Baba wa Mbinguni?

    Picha
    watoto wakipokea sakramenti

    Ibada zinatusaidia kukumbuka ahadi zetu kwa Mungu.

  • Tengeneza fumbo kutoka kwenye picha ya hekalu. Soma pamoja na watoto Mafundisho na Maagano 84:5, na waombe kusikiliza kile Bwana alichowaamuru Watakatifu wajenge. Mpe kila mtoto kipande cha fumbo, na watake kushiriki kitu fulani wanachoweza kufanya kujiandaa kuingia hekaluni.

Mafundisho na Maagano 84:64–72; 81–88

Bwana anawalinda na kuwapa nguvu wamisionari.

Mistari hii ina ahadi Bwana alizozifanya kwa wale Aliowaita kuhubiri injili. Ahadi hizi zinaweza pia kuwatia moyo watoto wakati wanaposhiriki injili ya Yesu Kristo pamoja na wengine.

Shughuli Yamkini

  • Wagawanye watoto katika jozi, na toa kwa kila jozi mistari michache ya kusoma kutoka Mafundisho na Maagano 84:64–72; 81–88. Watake kutafuta ahadi Bwana anazozitoa kwa wale wanaoshiriki injili. Waombe kushiriki kile walichojifunza pamoja na darasa. Wasaidie watoto kufikiria juu ya watu wanaowajua, au watu katika maandiko, waliopokea msaada wa Bwana wakati wakihubiri injili (kama vile Samuel Mlamani [ona Helamani 13:2–4; 16:6–7] au Amoni [ona Alma 17:32–38]). Shiriki uzoefu wakati ulipohisi msaada wa Bwana wakati ulipokuwa unamhudumia Yeye.

  • Leta vikombe au vyombo vingine vinavyofanana darasani. Andika kwenye vipande vya karatasi njia ambazo watoto wanaweza kuwa wamisionari sasa, na weka kila kipande cha karatasi katika kikombe. Viweke vikombe pamoja vikiwa vimekaribiana, upande wa wazi juu, kwenye sakafu. Watake watoto kufanya zamu kutupa kitu kidogo ndani ya moja ya vikombe na kisha igiza kile kilichopo kwenye karatasi ndani ya kikombe kile. Jinsi gani Baba wa Mbinguni anatusaidia wakati tunaposhiriki injili pamoja na wengine, hata wakati inapokuwa vigumu au tunapohisi wasiwasi?

  • Wasaidie watoto waone kwamba sisi wote ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho kwa sababu ya kazi ya umisionari—wamisionari ama walifundisha injili kwetu, kwa wazazi wetu, au kwa mababu zetu. Waambie watoto kuhusu jinsi wamisionari walivyokusaidia wewe au mababu zako kupokea injili. Waache watoto washiriki uzoefu sawa na huo. Watie moyo wawaulize wazazi wao jinsi waumini wa kwanza wa Kanisa katika familia zao walivyojifunza kuhusu injili.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watake watoto kufanya kitu fulani wiki hii kushiriki injili pamoja na mtu fulani nyumbani kwao au pamoja na rafiki. Watie moyo kuomba msaada wa Baba wa Mbinguni na kutazamia kile Atakachofanya kuwasaidia.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Husisha milango ya fahamu. “Watoto wengi (na watu wazima) wanajifunza vyema zaidi wakati milango mingi ya fahamu inapohusishwa. Tafuta mbinu za kuwasaidia watoto kutumia milango yao ya fahamu ya kuona, kusikia, na kugusa wanapojifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Chapisha