Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93: “Kupokea Utimilifu Wake”


“Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93: ‘Kupokea Utimilifu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 23–29. Mafundisho na Maagano 93,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi

Picha
Stefano anamuona Mungu na Yesu Kristo

Namuona Mwana wa Mtu Amesimama Mkono wa Kuume wa Mungu, na Walter Rane

Agosti 23–29

Mafundisho na Maagano 93

“Kupokea Utimilifu Wake”

Watoto unaowafundisha ni wana na mabinti wa thamani wa Wazazi wa Mbinguni na waliishi pamoja Nao kabla ya kuja duniani. Baada ya kujifunza Mafundisho na Maagano 93, unahisi kupata mwongozo wa kiungu kufanya nini ili kuwasaidia watoto hawa kukua “katika nuru na kweli”? (mstari wa 40).

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha za Mwokozi (kama vile zile zilizo katika Kitabu cha Sanaa ya Injili, au magazeti ya Kanisa), na waombe watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu Yeye. Watoto wakubwa wanaweza kushiriki andiko kutoka Mafundisho na Maagano 93 ambalo limewasaidia wao kujifunza juu ya Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 93:2–21

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Ni muhimu kwamba watoto unaowafundisha wajifunze Yesu Kristo ni nani na kwa nini wanapaswa kumfuata Yeye. Kweli juu ya Yesu Kristo zinazopatikana katika sehemu ya 93 zinaweza kusaidia.

Picha
dirisha la kioo

Tunapokea nuru ya Kristo wakati tunaposhika amri Zake.

Shughuli Yamkini

  • Chagua kweli kadhaa ulizojifunza juu ya Mwokozi katika sehemu ya 93 ambazo zinakupa mwongozo wa kiungu. Kwa kila ukweli unaouchagua, wasomee watoto mstari huo pale unakopatikana, na wape neno kuu ili walisikilize wakati wewe ukisoma. Toa ushuhuda wako mfupi juu ya Mwokozi, na waruhusu watoto kutoa shuhuda zao. Orodha ifuatayo ya kweli hizo inaweza kukupa mawazo:

    Yesu Kristo alifanya kazi za Baba (mstari wa 5).

    Yesu Kristo ni Nuru ya Ulimwengu (mstari wa 9).

    Yesu Kristo ni Muumbaji wa ulimwengu (mstari wa 10).

    Yesu Kristo alipokea uwezo wote mbinguni na duniani (mstari wa 17).

    Hapo mwanzo Yesu Kristo alikuwa pamoja na Mungu (mstari wa 21).

  • Waombe watoto kusikiliza kitu ambacho wanajifunza juu ya Mwokozi wakati ukitoa muhtasari kwa maneno yako wa baadhi ya kweli zilizofundishwa katika sehemu ya 93. (Unaweza pia kutumia “Sura ya 33: Ufunuo Juu ya Yesu Kristo” [Hadithi za Mafundisho na Maagano, 126–27].)

Mafundisho na Maagano 93:23, 29

Niliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani.

Kwa nini ingekuwa muhimu kuwasaidia watoto unaowafundisha kufahamu kwamba wao waliishi pamoja na Baba wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa? Je, ni kwa namna gani ufahamu wa ukweli huu umekubariki wewe?

Shughuli Yamkini

  • Rudia pamoja na watoto maneno haya “Ninyi pia mlikuwepo mwanzoni pamoja na Baba” (Mafundisho na Maagano 93:23). Elezea kwamba kabla hatujazaliwa hapa duniani, tuliishi mbinguni na Baba yetu wa Mbinguni. Imbeni pamoja “Mimi Mwana wa Mungu” au “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3, 4).

  • Waalike watoto kupaka rangi ukurasa wa shughuli na kuchora picha za wao wenyewe wakiwa pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kabla ya kuzaliwa duniani. Toa ushuhuda wako kwamba Mungu anatupenda sisi sote na kwamba sisi sote ni watoto Wake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 93:2–21

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Kadiri tunavyozidi kumfahamu Yesu Kristo, ndivyo kwa kina na kwa dhati tunavyotaka kumwabudu Yeye na kuja kwa Baba kupitia Kwake (ona Mafundisho na Maagano 93:19).

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Mwokozi, na waulize watoto kwa nini ni muhimu kwetu sisi kujua juu ya Yesu Kristo. Waalike watafute majibu ya nyongeza katika Mafundisho na Maagano 93:19. Waalike kufikiria njia moja ya kujifunza zaidi juu ya Yesu Kristo wiki ijayo, na wape nafasi ya kushiriki mawazo yao.

  • Fikiria juu ya njia ya ubunifu ya kuwatia moyo watoto ili wasome juu ya Mwokozi katika sehemu ya 93. Ungeweza kuandika kwenye vipande vidogo vya karatasi mistari kadhaa ya marejeleo kutoka sehemu ya 93 ambayo hufundisha kweli juu ya Yesu Kristo (kwa mfano, ona mistari 5, 9–10, 17, 21). Weka vipande hivyo vya karatasi ndani ya chombo, na waambie watoto kufanya zamu ya kuchagua kimoja na kusoma kifungu cha andiko kwa darasa. Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye vifungu hivi vya maneno?

Mafundisho na Maagano 93:23, 29, 38

Niliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani.

Mwokozi amesisitiza mara tatu katika sehemu ya 93 kwamba sisi tuliishi pamoja na Mungu “hapo mwanzoni” (mstari wa 23, 29, 38). Ni kwa nini Yeye anataka sisi tujue hili? Ni kwa jinsi gani kujua ukweli huu kunawabariki watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Someni Mafundisho na Maagano 93:23, 29, 38 pamoja, na waalike watoto kutafuta kweli kuhusu wao wenyewe ambazo zinarudiwa katika mistari hii. Waombe watoto kushiriki chochote wanachojua kuhusu maisha yetu pamoja na Baba wa Mbinguni kabla ya kuzaliwa. Mpe kila mtoto moja ya marejeleo ya maandiko yafuatayo, na wasaidie kutafuta kitu ambacho maandiko haya yanakifundisha juu ya maisha kabla ya kuja duniani: Yeremia 1:5; Mafundisho na Maagano 138:53–56; Musa 3:5; Ibrahamu 3:22–26.

  • Imbeni pamoja “Mimi Mwana wa Mungu” au “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3, 4). Je, ni kweli zipi tunajifunza kutoka kwenye wimbo huu juu ya malengo yetu ya kuja duniani?

Mafundisho na Maagano 93:24

Ukweli ni maarifa ya mambo yaliyopita, ya sasa, na ya baadaye.

Ulimwengu una mitazamo mingi tofauti juu ya ukweli ni nini na jinsi ya kuupata. Je, unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kufahamu kwamba ukweli ni kweli bila kujali wengine wanasemaje na kwamba Baba wa Mbinguni anajua ukweli wote?

Shughuli Yamkini

  • Andika neno ukweli ubaoni, na waombe watoto kuandika maana yake pembeni yake. Someni kwa pamoja namna Bwana alivyotoa maana ya ukweli katika Mafundisho na Maagano 93:24. Imbeni wimbo kuhusu ukweli, kama vile “Oh Say, What Is Truth?” (Nyimbi za Kanisa, na. 272), na waalike watoto kutafuta katika wimbo njia nyingine za kuelezea ukweli.

  • Ili kuwasaidia watoto kuutumia ukweli uliomo katika Mafundisho na Maagano 93, andika marejeleo machache ya maandiko kutoka katika sehemu hii juu ya kipande cha karatasi. Kwenye vipande vingine vya karatasi, andika kweli ambazo kila moja ya mistari hii inafundisha. Waalike watoto kushirikiana kuisoma mistari na kuoanisha kweli kwenye mistari wanayoisoma. Kwa nini tunashukuru kuwa na ufahamu juu ya ukweli?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto waandike au wachore kitu kimoja walichojifunza darasani na kukishiriki pamoja na familia zao wakati watakapofika nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kumtambua Roho. Unapokuwa na uzoefu wa kiroho na watoto (kwa mfano, wakati unaposoma maandiko pamoja nao, unaposikiliza shuhuda zao, au kuimba pamoja nao), wasaidie kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Chapisha