Mafundisho na Maagano 2021
Agosti 2–8. Mafundisho na Maagano 85–87: “Simameni katika Mahali Patakatifu”


“Agosti 2–8. Mafundisho na Maagano 85–87: ‘Simameni katika Mahali Patakatifu”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Agosti 2–8. Mafundisho na Maagano 85–87,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
familia ikitembea kwenda hekaluni

Agosti 2–8

Mafundisho na Maagano 85–87

“Simameni katika Mahali Pakatifu”

Kwa sababu muda wenu pamoja na watoto ni mchache, tafuta mwongozo wa kiroho kujua ni kanuni gani kutoka kwenye maandiko unapaswa kusisitiza. Amini misukumo unayoipata.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waonyeshe watoto baadhi ya picha au kurasa za shughuli ulizozitumia katika masomo ya hivi karibuni, na watake watoto kushiriki kile wanachokumbuka kujifunza kuhusu wao, ama katika darasa au nyumbani.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 85:6

Roho huzungumza kwa “sauti ndogo, tulivu.”

Mzee Richard G. Scott alisema, “Kama hukamilishi chochote kingine katika uhusiano wako na wanafunzi wako zaidi ya kuwasaidia kutambua na kufuata misukumo ya Roho, utabariki maisha yao kwa kiasi kikubwa na milele” (“kujifunza na kufundisha kwa Matokeo mazuri Zaidi” [Brigham Young University Education Week devotional, Aug. 21, 2007, 5 speeches.byu.edu).

Shughuli Yamkini

  • Soma kwa watoto jinsi Joseph Smith alivyomwelezea Roho: “Ndiyo, sauti ndogo tulivu yasema hivi” (Mafundisho na Maagano 85:6). Watake watoto kutaja baadhi ya vitu ambavyo ni vidogo (onyesha picha kama wanahitaji msaada). Watake watoto kujikunja chini ya ardhi kuwa kama wadogo na watulivu kadiri wanavyoweza. Wasaidie kufikiria kuhusu jinsi sauti inavyoweza kuwa ndogo, na waache wafanye mazoezi ya kusikiliza na kusema katika sauti ndogo. Wasimulie kuhusu nyakati ambazo Roho alisema nawe katika sauti tulivu na ndogo.

  • Wafundishe watoto wimbo kuhusu Roho, kama vile “Roho Mtakatifu” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,105). Watake kuuimba pamoja nawe kwa kunong’ona. Wimbo huu unafundisha nini kuhusu Roho Mtakatifu? Wasaidie watoto kutambua wakati walipowahi kuhisi ushawishi Wake (kama vile wakati wanaposali, kuimba wimbo, au kusaidia wengine).

Mafundisho na Maagano 86:11

Ninaweza kuwa Nuru kwa Wengine

Sehemu ya 86 inaeleza kazi muhimu Bwana anayotaka watumishi wake kufanya katika siku za mwisho. Njia moja ambayo watoto wanaweza kusaidia katika kazi hii ni kwa kuwa nuru kwa watu wanaowazunguka.

Shughuli Yamkini

  • Soma kwa watoto kirai kifuatacho kutoka Mafundisho na Maagano 86:11.: “Heri ninyi kama katika wema wangu, na nuru ya kuwa mwangaza kwa wayunani [au watu wasio na injili].” Jinsi gani nuru inatubariki? Inakuwaje wakati hatuna nuru? Jinsi gani tunaweza kuwa nuru kwa watu wengine wasiojua kuhusu injili? Wasaidie watoto kufikiria njia tunazoweza kushiriki uzuri wa Yesu pamoja na wengine.

  • Waombe watoto wafikirie kwamba rafiki anajaribu kutembea katika giza (zima taa kama itasaidia). Kwa nini ni vigumu kutembea katika giza? Tufanye nini kumsaidia rafiki yetu? Eleza kwamba tunapomfuata Mwokozi, ni kama kuangaza nuru kuwaonyesha wengine njia ya kwenda.

  • Magazeti ya Liahona na Friend mara kwa mara yana hadithi kuhusu watoto ambao ni mifano mizuri. Tafuta moja ili kushiriki pamoja na watoto ambalo litawatia moyo kuwa mifano mizuri pia.

Mafundisho na Maagano 87

Nyumba zetu zinaweza kuwa “mahali patakatifu.”

Hakuna nyumba iliyo kamilifu, lakini kuna vitu wote tunaweza kufanya ili nyumba zetu ziwe mahali patakatifu.

Shughuli Yamkini

  • Eleza kwa watoto kwamba Joseph Smith alikuwa na wasiwasi kuhusu mambo ambayo yalikuwa yakitokea ulimwenguni. Fupisha kichwa cha habari kwenye sehemu ya 87, au soma “Sura ya 30: Ufunuo kuhusu Vita” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 117–18; ona pia video juu ya ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto kusikiliza vitu ambavyo vingeweza kumfanya Joseph kuwa na wasiwasi. Kufundisha kile Bwana alichosema tunapaswa kufanya kuhusu matatizo hayo, soma Mafundisho na Maagano 87:8.

  • Onyesha picha ya hekalu, na shiriki kwa nini hekalu ni mahali patakatifu. Onyesha picha nyumba, na wasaidie watoto kufikiria juu ya njia wanazoweza kufanya nyumba zao takatifu kama hekalu (ona ukurasa wa shughuli wa wiki hii). Kwa nini tunataka kuwa katika mahali patakatifu?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 85:6

Roho huzungumza kwa “sauti ndogo, tulivu.”

Ulimwengu una vivutio vingi ambavyo vinaweza kufanya iwe vigumu kumsikia Roho. Jinsi gani Utawasaidia watoto kusikiliza sauti ya Roho?

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto ni nini watasema kama mtu fulani angewauliza jinsi wanavyojua wakati Roho Mtakatifu anaposema nao. Watake kusoma kuhusu njia moja ambayo Joseph Smith alielezea sauti ya Roho katika Mafundisho na Maagano 85:6.

  • Cheza wimbo wa kanisa au wimbo wa watoto kimya kimya, na mwombe mmoja wa watoto kukisia ni wimbo gani wakati wengine wakipiga kelele za kuvuruga, kama vile kupiga makofi au kupiga miguu chini. Kisha watake watoto wengine waache, na jadili jinsi gani hii ni kama kumsikiliza Roho Mtakatifu wakati tunapotoa vurugu kutoka kwenye maisha yetu. Wasaidie watoto kufikiria juu ya vurugu wanazoweza kuzitoa ili kumhisi zaidi Roho mara kwa mara.

Mafundisho na Maagano 86

Ninaweza kuwakusanya watu wa Mungu.

Fumbo la ngano na magugu ni kuhusu “siku za mwisho, hata sasa” (Mafundisho na Maagano 86:4.). Tumia fumbo hili kuwasaidia watoto kuhisi kutiwa moyo kushiriki katika “mavuno ya ngano” (mstari wa 7).

Shughuli Yamkini

  • Wasimulie watoto fumbo la ngano na magugu, au mtake mtoto asimulie (ona Mathayo 13:24–30). Watake watoto kuchora picha ya kitu fulani kutoka kwenye fumbo. Kisha someni pamoja Mafundisho na Maagano 86: 1–7, na watake watoto kuandika juu ya michoro yao kile ambacho kitu walichokichora kinawakilisha.

  • Andaa picha ndogo kadhaa au michoro ya ngano, na zifiche kuzunguka chumba. Mtake kila mtoto asaidie kukusanya ngano na andika juu yake jina la mtu fulani wanayeweza “kumkusanya” kwa Yesu Kristo. Inamaanisha nini kuwakusanya watu kwa Yesu Kristo? Ni baadhi ya njia zipi tunaweza kufanya hivi? Inamaanisha nini “kuendelea katika uzuri wa [Mwokozi] na jinsi gani hiyo inatusaidia kukusanya watu Kwake? (Mafundisho na Maagano 86:11).

Mafundisho na Maagano 87

Ninaweza “Kusimama … katika mahali patakatifu.”

Watoto unaowafundisha watakabiliana na hatari za kimwili katika maisha yao yote. Unaweza kuwasaidia kujiandaa kukabiliana na hatari hizo kwa kuwafundisha kutafuta na kusimama katika mahali patakatifu.

Picha
Mwanamke na mtoto nje ya hekalu

Huduma ya hekaluni ni njia moja tunayoweza kusaidia kukusanya watu wa Mungu.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 87:6 kujifunza kuhusu mambo Bwana aliyosema yangetokea katika siku za mwisho. Waombe watoto kuzungumza kuhusu changamoto ambazo watoto wa umri wao wakati mwingine wanakumbana nazo. Watake kutafuta katika mstari wa 8 kile Bwana alichosema tunapaswa kufanya wakati wa nyakati ngumu. Waeleze watoto kuhusu sehemu takatifu katika maisha yako.

  • Wasaidie watoto kutengeneza orodha ya sehemu takatifu, mawazo matakatifu, na matendo matakatifu ambayo yanaweza kuwasaidia kukabiliana na hatari za kiroho (kwa mawazo, ona video “Standing in Holy Places” na “Stand Ye in Holy Places—Bloom Where You’re Planted,” ChurchofJesusChrist.org). Watake kuzitunza orodha zao pamoja nao ili kuzirejelea itakapohitajika.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Watake watoto kuchagua kitu kimoja watakachofanya kufanya nyumba zao au maisha yao “mahali patakatifu.”

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia ubunifu wako. Usijiwekee kikomo kwenye mawazo ya shughuli yaliyopendekezwa katika muhtasari huu. Acha mawazo haya yachochee ubunifu wako mwenyewe. Fikiria kuhusu nini watoto katika darasa lako watafurahia na nini kitawasaidia kujifunza.

Chapisha