“Agosti 16–22. Mafundisho na Maagano 89–92: ‘Kanuni yenye Ahadi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Agosti 16–22. Mafundisho na Maagano 89–92,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi
Agosti 16–22
Mafundisho na Maagano 89–92
“Kanuni yenye Ahadi”
Unapojifunza kweli katika Mafundisho na Maagano 89–92, tafakari njia mpya na zenye kujenga unazoweza kuwasaidia watoto kuzielewa.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Watake watoto wachore na kuzungumza kuhusu vitu vyema walivyovifanya wiki hii kutunza miili yao na nafsi.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Nitabarikiwa ninapotii Neno la Hekima.
Wafundishe watoto kwamba miili yetu ni zawadi kutoka kwa baba wa Mbinguni na anatutaka tuitunze miili yetu.
Shughuli Yamkini
-
Kuwasaidia watoto waelewe amri za Bwana katika Mafundisho na Maagano 89:10–17), chora au onyesha picha za vitu vizuri tunavyoweza kula au vitu vizuri tunavyoweza kufanya kuiweka miili yetu iwe yenye afya (ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Pia wasaidie watoto kuelewa kwamba pombe, tumbaku, chai, kahawa, na madawa mengine ya kudhuru yanaumiza miili yetu na Bwana ametuonya kutovitumia. Watake watoto kuchagua kitu fulani wanachoweza kufanya wiki hii kuweka miili yao iwe yenye afya.
-
Watake watoto kufanya zamu kuchora picha ubaoni ambayo inawakilisha kitu fulani kilichofundishwa katika Neno la Hekima. Acha watoto wengine kukisia kile ambacho kila mtu anakichora. Zungumza kuhusu amri ya Bwana katika sehemu ya 89 ambayo inahusiana na mchoro.
-
Tumia mfano ufuatao, au mingine unayofikiria, kuonyesha jinsi tulivyobarikiwa kwa kutii Neno la Hekima (ona Mafundisho na Maagano 89:18–21)). Fanyeni zoezi la kawaida pamoja, kama vile kutembea au kukimbia katika sehemu, na kisha kujifanya “kuwa wachovu” au “dhaifu” (mstari wa 20). Shuhudia juu ya ahadi za Bwana.
-
Onyesha picha ya hekalu, na watake watoto kuelezea nini wanakiona. Tumia wimbo kuhusu afya ya kimwili, kama vile “The Lord Gave Me a Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 153), kufundisha watoto kwamba miili yetu ni kama mahekalu kwa ajili ya nafsi zetu na Mungu anatutaka kuiweka miili yetu katika hali ya kiafya. Wasaidie watoto kufikiria juu ya njia tunazoweza kuitunza miili yetu, na waache watoto waigize hivyo.
Mungu hutupa sisi manabii kutuongoza na kutulinda.
Wasaidie watoto kuelewa jinsi manabii wa Bwana wanavyoweza kutusaidia kupata amani kutokana na dhoruba za maisha.
Shughuli Yamkini
-
Waonyeshe watoto picha za manabii wa kale, na wasimulie jinsi manabii hawa walivyowaonya watu wa wakati wao. (Kwa mawazo, ona ”Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11.
-
Kwa nini tunapaswa kuwasikiliza manabii wa Mungu? Onyesha picha ya nabii wa sasa, na shiriki baadhi ya vitu alivyovifundisha au kuonya kuvihusu hivi karibuni. Wasaidie watoto kufikiria njia tunazoweza kumfuata nabii. Shiriki ushuhuda wako wa kweli zilizofundishwa katika Mafundisho na Maagano 90:5. (Fahamu kwamba “Oracles” maana yake ni funuo au manabii waliozipokea.)
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Neno la Hekima linanisaidia kuwa mwenye afya katika mwili na nafsi.
Mzee Gary E. Stevenson aliwashauri vijana kupanga kabla kile watakachofanya wakati watakapojaribiwa na pombe au madawa. Kisha alifundisha, “Mtaona kwamba majaribu yana uwezo mdogo juu yenu. Utakuwa tayari umekwishafanya uamuzi jinsi utakavyojibu na kile utakachofanya. Hutahitaji kufanya uamuzi kila mara” (“Your Priesthood Playbook,” Ensign au Liahona, Mei 2019, 48). Watie moyo watoto unaowafundisha kuamua sasa—kwa muda wote wa maisha yao—kuishi Neno la Hekima.
Shughuli Yamkini
-
Wagawe watoto kwenye makundi mawili, na litake kundi moja lisome Mafundisho na Maagano 89:1–4 na kundi lingine lisome mistari 18–21. Watake kutafakari maswali kama yafuatayo: Kwa nini Bwana alitupatia Neno la Hekima? Jinsi gani kuishi Neno la Hekima kunaweza kunibariki kimwili na kiroho?
-
Tengeneza maelezo ya kujaza–katika–sehemu–tupu kwa kutumia vifungu vya mneno kutoka Mafundisho na Maagano 89, kama vile “ imewekwa wakfu kwa ajili ya matumizi ya binadamu na ya wanyama” au “Na wata na hawatazimia” (mistari 14, 20). Watake watoto kufanya kazi wawili wawili kupata majibu katika sehemu ya 89. Watoto wangeweza kuchambua maelezo kwenye makundi yafuatayo: vitu vizuri kwa ajili ya miili yetu, vitu vibaya kwa ajili ya miili yetu, na baraka.
-
Mtake mtoto mmoja asome Mafundisho na Maagano 89:4 na mwingine kusoma nukuu kutoka kwa Mzee Stevenson hapo juu. Kwa nini tunapaswa kuamua sasa kutii Neno la Hekima kuliko kungoja mpaka wakati wa majaribu? Wasaidie watoto kuigiza jinsi wanavyoweza kujibu kama mtu fulani, hata rafiki, akiwapa kitu fulani ambacho ni kinyume na Neno la Hekima. Jinsi gani kutii Neno la Hekima kunatulinda?
Mafundisho na Maagano 90:2, 335, 14–16.
Urais wa Kwanza unashikilia “funguo za ufalme.”
Maelekezo ya Bwana kuhusu Urais wa Kwanza katika mwaka wa 1833 (Joseph Smith, Sidney Rigdon, na Frederick G. Williams) yanaweza kuwasaidia watoto kuimarisha ushuhuda wao wa Urais wa Kwanza wa sasa.
Shughuli Yamkini
-
Watake watoto watafute Mafundisho na Maagano 90:14–16 na kuandika baadhi ya vitu Bwana alivyoutaka Urais wa Kwanza kufanya. Waonyeshe watoto picha ya Urais wa Kwanza wa sasa, na shiriki kitu fulani kuwahusu. (Unaweza kusoma wasifu wao chini ya “Living Prophets and Church Leaders” kwenye ChurchofJesusChrist.org.) Shiriki ushuhuda wako wa wito wao mtakatifu na baraka ulizopokea kutokana na kufuata ushauri wao.
-
Rejea na watoto kitu fulani ambacho mshiriki wa Urais wa Kwanza amefundisha. Kisha someni pamoja Mafundisho na Maagano 90:5. Onyesha kwamba “oracles” ni funuo au manabii ambao walioupokea. Inamaanisha nini “kupokea mafunuo … kama kitu chepesi”? Jinsi gani tunaweza kuonyesha kwamba manabii na vitu wanavyofundisha ni muhimu kwetu?
Roho anaweza kunisaidia kujua kipi ni kweli.
Unaposoma kile Bwana alichomwambia Joseph Smith kuhusu Apocrypha, fikiria kuhusu jinsi ambavyo ushauri huu ungeweza kuwasaidia watoto kutambua kati ya ukweli na makosa watakayokabiliana nayo maisha yao yote.
Shughuli Yamkini
-
Someni pamoja kichwa cha habari cha sehemu ya Mafundisho na Maagano 91 kuwasaidia watoto kuelewa Apocrypha ni nini (ona pia Mwongozo kwenye Maandiko, “Apocrypha,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Wasaidie watoto kufikiria sehemu zingine, kama vile katika vyombo vya habari, ambako tunaweza kupata “vitu vingi … ambavyo ni vya kweli” na “vitu vingi … ambavyo sio vya kweli” (mistari 1–2). Kisha watake watoto watafute Sehemu ya 91 kujifunza kile Bwana alichosema tunaweza kufanya kutambua kati ya ukweli na kosa.
-
Someni pamoja Mafundisho na Maagano 91:4, na waulize watoto ni nini mistari hii inafundisha kuhusu Roho Mtakatifu. Watake watoto washiriki uzoefu binafsi wakati “Roho [alipodhihirisha] ukweli” kwao. Pia shiriki uzoefu wako mwenyewe. Katika njia gani zingine Roho anaweza kutusaidia?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Watake watoto kushiriki pamoja na familia zao kile walichojifunza leo kuhusu kutunza miili yao na nafsi au malengo yao kwa ajili ya kutii Neno la Hekima.