2010–2019
“Mkinipenda, Mtazishika Amri Zangu”
Oktoba 2015


11:9

“Mkinipenda, Mtazishika Amri Zangu”

Amri za Mungu ni dhihirisho la upendo wake kwetu, na utiifu kwa amri zake in maonyesho ya upendo wetu kwake.

Wakati binti yetu wa Kwanza, Jen, alimpoleta binti yake wa tatu nyumbani kutoka hospitali, nilienda nyumbani kwake kumsaidia. Baada ya kumchukua mtoto wake mkubwa wa kike kutoka shule, tuliamua kwamba Jen alihitaji zaidi kupumzika. Kwa hiyo msaada mkubwa ambao ningeweza kumpa ni kumchukua mtoto wake mkubwa Chloe nyumbani kwangu ili mama na mtoto wake mchanga wawe na muda mtulivu.

Nilimfunga mkanda Chloe katika kiti cha gari, nikafunga mkanda wangu mwenyewe, na nikaendesha gari kutoka kwenye maegesho. Hata hivyo kabla ya kufika mtaani, Chloe alijifungua mkanda wake wa gari na alikuwa amesimama, akiangalia upande wangu wa bega, na kunizungumzia! Nilisimamisha gari pembeni mwa barabara, nikatoka, na kumfunga mkanda kwenye kiti chake.

Tulianza tena safari lakini si kwa umbali mrefu alikwa ametoka tena kwenye kiti chake tena. Nilirudia hatua zile zile, lakini kabla hata sijafunga mkanda wangu mwenyewe Chloe alikuwa amesimama tena!

Nilijukuta nimekaa kwenye gari, nimeegesha pembeni mwa barabara, nikishindana nguvu na mtoto wa miaka mitatu. Na alikuwa anashinda!.

Nilitumia kila njia ambayo niliifikiria kumshawishi kwamba kuendelea kubaki kwenye kiti huku akiwa amefunga mkanda ni jambo zuri. Hakushawishika! Mwishowe niliamua kujaribu njia ya kama/basi.

Nilisema, “Chloe, kama utabaki umefunga mkanda katika kiti chako, basi tukifika nyumbani kwa bibi, tutachezea kinyunya cha plastisini.

Hakujibu

Chloe, kama utabaki umefunga mkanda katika kiti chako, basi tukifika tu kwa bibi tutatengeneza mkate.”

Hakujibu

Nikajaribu tena. “Chloe, kama utabaki umefunga mkanda katika kiti chako, basi tutasimama dukani kwa ajili ya vitafunwa!

Baada ya majaribio matatu, niligundua kuwa lilikuwa si zoezi lenye kuzaa matunda. Alibaki na msimamo na hakuna kama/basi iliyotosha kumweka kwenye kiti akiwa amefunga mkanda.

Hatungeweza kutumia muda wote tukikaa pembezoni mwa barabara, lakini nilitaka niwe mtiifu kwa sheria na haikuwa salama kwa Chloe kwenda akiwa amesimama. Nilitoa sala fupi na kusikia Roho akininongoneza, “Mfundishe”.

Nilimgeukia na kuvuta mkanda wangu kutoka katika mwili wangu. Nikasema, “Chloe, Nimevaa mkanda huu kwa sababu unanilinda Lakini wewe hujavaa mkanda na hauko salama. Nitasikitika sana kama utadhurika.”

Alinitazama, nilikaribia kuona fikira za kina katika akili yake na nilisubiri kwa hamu jibu lake. Mwishiwe macho yake makubwa ya buluu yaliangaza, na akasema, “Bibi, unataka nivae mkanda kwa sababu unanipenda!”

Roho aliijaza gari nilipoonyesha upendo wangu kwake. Sikupenda kupoteza hisia hizo, lakini nilijua nilikuwa na fursa hivyo nilitoka na kumuweka vizuri kwenye kiti kwa kumfunga mkanda. Baadaye nikamwuliza, “Chloe utabaki kwenye kiti chako ? Alisema angefanya hivyo—kote mpaka sokoni kwenye vitafunwa. Na aliendelea kukaa akiwa kwenye mkanda njia nzima mpaka sokoni na nyumbani kwangu, ambako tulitengeneza mkate na kucheza na kinyunya cha plastisini kwa sababu Chloe hakusahau.

Nilipokuwa naendesha gari kurudi nyumbani siku hiyo, andiko liliijaza akili yangu. “Kama unanipenda zitii amri zangu.”1 Tuna sheria za kufundisha, kuongoza na kulinda watoto wetu. Kwa nini?” Kwa sababu ya upendo mkubwa tulio nao kwao. Lakini mpaka Chloe alipoelewa kuwa tamanio langu kwake ni kwamba aendelee kukaa kwenye kiti huku mkanda ukiwa umefungwa kwa sababu ya upendo wangu kwake, hakuwa tayari kujisalimisha kile alichokifiria kuwa ni kizuizi. Alihisi kwamba mkanda wake ulizuia uhuru wake.

Kama Chloe, tunaweza kuchagua kuziona amri kama vizuizi. Wakati mwingine tunaweza kuhisi kwamba sheria za Mungu zinazuia uhuru wa kibinafsi, zinaondoa uhuru wetu, na kuzuia fursa zetu na ukuaji wetu. Lakini tunapotafuta uelewa wa juu, tunaporuhusu Baba yetu kutufundisha tutaanza kuona kwamba amri zake ni dhihirisho la upendo wake kwetu, na utiifu kwa amri zake in maonyesho ya upendo wetu kwake.

Kama utajikuta kiistiari, umeegesha pembezoni mwa barabara acha nishauri kanuni chache ambazo kama zikifuatwa, zitakusaidia kurudi salama kwenye ”njia ya imani na utiifu”?2

Kwanza, mwamini Mungu. Amini katika mpango Wake wa milele. Kila mmoja wetu ni mwana au binti wa kiroho wa wazazi wa mbinguni” Upendo wao kwetu ni wazi kwenye amri. Amri ni maelekezo ya muhimu katika kufundisha, kuongoza na kutulinda ”tunapopata uzoefu wa duniani.”3

Katika “maisha kabla ya hapa duniani” tulitumia uhuru wetu wa kuchagua kukubali mpango wa Mungu,4 na tulijua kwamba utii katika sheria ya milele ya Mungu ilikuwa ni muhimu katika ufanisi wetu katika mpango wa Mungu. Maandiko yanatufundisha: “Kuna Sheria isiyotenguliwa mbinguni kabla ya misingi ya ulimwengu huu, ambapo juu yake baraka zote hutoka.5 Kama tutatii sheria, tutapokea baraka.

Hata kwa makosa yote, upinzani, na kujifunza ambako huambatana na uzoefu wa hapa duniani, Mungu hapotezi mwelekeo wa umuhimu wetu wa milele, hata pale tunapofanya hivyo. Tunaweza kumwamini “kwa sababu anawataka watoto Wake warudi.”6 Na ametupa njia kupitia Upatanisho wa Mwanawe, Yesu Kristo. Upatanisho ni “kiini cha mpango wa wokovu.”7

Pili, mwamini Yesu. Dhihirisho la juu zaidi la utii na upendo thabiti ni Upatanisho wa Yesu Kristo. Alijiweka Mwenyewe chini ya Mapenzi ya Baba, alitoa maisha Yake kwa ajili yetu. Alisema, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.”8

Yesu alifundisha:

“Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

“Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

“Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”9

Kila Jumapili tuna fursa ya kutafakari na kukumbuka upendo safi wa Mwokozi wetu tunapokea nembo za upatanisho Wake usiyo na mwisho. Wakati wa sakramenti, Ninaangalia wakati vidole na mikono inaponyooshwa katika kupitisha mkate na maji. Ninaponyosha mkono wangu na kupokea, ninaweka ahadi kwa hiari kwamba ninakubali kujichukulia jina Lake juu yangu daima kumkumbuka na kutii amri Zake. Na Yeye anaahidi “kwamba [sisi] tutakuwa na Roho Wake pamoja [nasi].10

Tatu, amini katika minong’ono ya Roho. Kumbuka kwenye uzoefu wangu na Chloe ambapo Roho alininong’oneza maandiko ndani yangu? Iko katika Yohana 14:15 ”Mkinipenda mtazishika amri zangu.” Na mistari hii muhimu kama ifuatavyo:

“Nami nitamwomba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele;

“Yeye ni Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua.Lakini ninyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.”11

Kila muumini mstahiki, aliyethibitishwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ana haki ya uenzi wa Roho Mtakatifu. Kufunga, sala, na kujifunza maandiko, na utii hukuza kwa kiasi cha juu uwezo wetu wa kusikia na kuhisi ushawishi wa Roho.

Wakati akili yako inapokuwa imejawa na shaka na kuchanganyikiwa, Baba na Wana watamtuma Roho Mtakatifu kukuonya na kukuongoza salama kapitia hatari zote katika maisha haya ya duniani. Yeye atakusaidia kukumbuka, kukufariji, na kukujaza “tumaini na upendo kamili.”12

Nne, amini ushauri wa mitume wanaoishi. Baba Yetu ametupa njia kwetu sisi kusikia neno Lake na kujua sheria Yake kupitia Mitume Wake. Bwana alisema, “Maneno yangu … yote yatatimizwa, iwe kwa sauti yangu mwenyewe au kwa sauti ya watumishi wangu, yote ni sawa.”13

Hivi majuzi manabii waishio walitushauri “tuikumbuka siku ya sabato, na kuitakasa.”14 na kuishi sheria ya mfungo. Utiifu wa ushauri huu wa kinabii unatupa njia ya kuwa watiifu kwa amri ya Mungu ya kupenda na kumpenda jirani yetu tunapoongeza imani yetu katika Kristo na kuunyoosha mkono wetu kuwapenda na kuwatunza wengine.15

Kuna usalama katika kufuata neno la Bwana kupitia kwa manabii wake. Mungu alimwita Rais Thomas S. Monson, washauri wa Urais wa Kwanza na washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi. Katika ulimwengu ambamo uoga unaongezeka, uadui, kupotoshwa na hasira tunaweza kuwatazama ili kuona jinsi wafuasi ya Yesu Kristo—wamejawa na upendo— wanavyoenekana, wanavyosikika, na wanavyojibu masuala inaweza kuleta mgawanyiko. Wanamshuhudia juu ya Yesu Kristo na wanatenda katika hisani, upendo halisi wa Yesu Kristo, ambao ndiyo mashihidi Wake.

Baada ya uzoefu wangu na Chloe, nilipekua maandiko kwa aya zinazotaja amri na upendo. Nilipata nyingi. Kila moja ya aya hizi hutukumbusha kwamba amri Zake ni dhihirisho la upendo wake kwetu, na utiifu kwa amri zake in maonyesho ya upendo wetu kwake.

Ninashuhudia kwamba tunapomwamini Mungu, Baba yetu wa Milele; Mwanawe, Yesu Kristo na kufanya imani katika Upatanisho Wake; kuamini katika minong’ono ya Roho; na kuamini katika ushauri ya manabii walio hai, tutaiona njia yetu kutoka kwenye kingo ya barabara na kuendelea salama—si kuvumilia tu bali kupata furaha katika safari yetu nyumbani. Katika jina la Yesu Kristo, amina.