Tunajaribiwa na kushawishiwa—lakini tunasaidiwa
Tunaweza kusaidiana kama watoto wa Baba yetu wa Mbinguni katika majaribu na vishawishi vyetu.
Wakati wa maisha yetu, tunajaribiwa na kushawishiwa. Pia tuna nafasi ya kutumia uhuru wetu wa kuchagua na kusaidiana. Kweli hizi ni sehemu ya mpango wa ajabu na mkamilifu wa Baba yetu wa Mbinguni.
Rais John Taylor alifundisha: “Nilimsikia Nabii Joseph akisema, akizungumza kwa wale Kumi na Wawili wakati mmoja: ’Mtakuwa na aina tofauti ya majaribu mtakayopitia. Na itakuwa muhimu kabisa kwenu kujaribiwa kama ilivyokuwa kwa Ibrahimu na watu wengine wa Mungu, na (Yeye alisema) Mungu atawahurumia, na atawashikeni na ataisokota mishipa ya mioyo yenu.’”1
Mara tunapofika umri wa uwajibikaji, majaribu na ushawishi ni mambo ya kawaida kabisa. Wakati mwingine yanakuwa mizigo mizito sana, lakini pia yanatuimarisha na kutusaidia kukua wakati tunapofanikiwa kuyashinda.
Kwa bahati nzuri, mizigo hii hauhitaji kuibeba peke yako. Alma alifundisha, “mnatamani kujiunga na zizi la Mungu, na kuitwa watu wake, na mko radhi kubeba mizigo ya mmoja na ya mwingine, ili iwe miepesi.”2 Maneno haya yanaonyesha kwamba tunawajibika kusaidiana. Jukumu hilo huja kutoka kwa wito wa Kanisa, uteuzi, urafiki, au kama sehemu ya wajibu mtakatifu kama wazazi, waume na wake, au wanafamilia—ama tu kwa kuwa sehemu ya familia ya Mungu.
Nitatoa mifano minne ya jinsi mizigo hufanywa miepesi tunaposaidiana.
1. Mwokozi alisema, “Yoyote yule atakaye kukulazimisha kwenda naye maili moja, Nenda naye mara mbili.”3 Kwa mfano, tunaombwa kuhudhuria hekaluni mara kwa mara, kama hali zetu binafsi zinavyo ruhusu. Kuhudhuria hekaluni kunahitaji kujitolea muda na uwezo, hususani kwa wale ambao ni lazima wasafiri umbali mkubwa. Hata hivyo, kujitolea huku kunaweza kufikiriwa kuwa sehemu ya maili ya kwanza.
Tunaanza kutembea maili ya pili wakati tunapoelewa maneno “ kupata, kupeleka, kufundisha,”4 tunapotafuta na kutayarisha majina ya mababu zetu kwa ibada za hekaluni, wakati tunaposaidia katika kuindeksi, tunapohudumu kama wafanya kazi hekaluni, na wakati tunapotafuta njia za kuwasaidia wengine kupata uzoefu wa maana wa hekalu.
Wakati nilipokuwa nahudumu kama Sabini wa Eneo, mojawapo ya vigingi katika baraza langu la uratibu kilishiriki katika msafara mkubwa wa kwenda hekaluni. Hekalu ambalo waumini walihudhuria ni ndogo, na kwa bahati mbaya kulikuwa na baadhi ya waumini ambao, licha ya kusafiri safari ndefu ya saa12, hawakuweza kuingia hekaluni kwa sababu lilikuwa tayari limepita kiwango change cha kila siku.
Siku chache baada ya safari hii, nilitembelea kigingi hiki na kumwuliza rais kama ningeweza kuzungumza na baadhi ya waumini ambao hawakuweza kuhudhuria hekaluni siku ile. Mmoja wa ndugu niliyezungumza naye aliniambia. Mzee, usiwe na wasiwasi. Nilikuwa katika nyumba ya Bwana. Nilikaa kwenye benchi katika bustani na nikatafakari akilini mwangu ibada. Kisha nilipewa nafasi kuingia, lakini badala yangu nilimruhusu ndugu mwingine kuingia, ambaye alikuja hekaluni kwa mara ya kwanza kuunganishwa na mke wake, kuchukua nafasi yangu. Kisha wakapata nafasi ya kuhudhuria vikao viwili siku hiyo. Bwana ananijua, na Yeye atanibariki, na sisi tuko sawa.”
2. Tabasamu. Kitendo hiki kidogo kinaweza kuwasaidia wale ambao wamezidiwa au wana mizigo mizito. Wakati wa kikao cha ukuhani cha mkutano mkuu huu uliopita wa Aprili, nilikaa kwenye jukwaa pamoja na Viongozi wakuu Wenye Mamlaka watano wapya walioitwa. Tulikuwa tumekaa pale akina dada wa urais wa makundi saidizi walipokaa sasa. Nilikuwa najisikia kuwa na wasiwasi sana na kuzidiwa na wito wangu mpya.
Wakati tulipokuwa tunaimba wimbo wa kati, nilihisi wazo lenye nguvu kwamba mtu fulani alikuwa ananiangalia. Nilifikiria mwenyewe: “Kulikuwa na zaidi ya watu 20,000 katika jumba hili, na karibu wote wanatazama mwelekeo huu. Kwa vyovyote, mtu fulani anakuangalia.”
Wakati nilipoendelea kuimba, nilijisikia tena wazo lenye nguvu kwamba mtu fulani ananiangalia. Niliangalia kule kwenye safu ambako wale Mitume Kumi na Wawili walikuwa wamekaa na niliona kwamba Rais Russell M. Nelson alikuwa amegeuka katika kiti chake, akiangalia kule tulikokaa. Tuliangaliana, na akanipa tabasamu kubwa. Tabasamu lile liliniletea amani kwenye moyo wangu uliokuwa umelemewa.
Baada ya ufufuko wake, Yesu Kristo aliwatembelea kondoo Wake wengine. Aliwaita na kuwatawaza wanafunzi kumi na wawili na kwa mamlaka yale, waliwahudumia watu. Bwana Yesu Kristo mwenyewe alisimama miongoni mwao. Bwana aliwaomba kupiga magoti na kusali. Sina hakika kama walioitwa wapya na kutawazwa wanafunzi kumi na wawili walikuwa wamelemewa na wito wao, lakini maandiko yanasema, “Ilitokea kwamba Yesu aliwabariki walipokuwa wanasali kwake: na sura yake ilitabasamu juu yao, na nuru ya sura yake iliangaza juu yao.”5 Wakati wa mkutano mkuu uliopita, tabasamu lilifanya rahisisha mizigo yangu kwa njia ya mara moja na ya ajabu.
3. Elezea hisia za huruma kwa wengine. Kama una ukuhani, tafadhali tumia uwezo wako kuwasaidia watoto wa Mungu, kuwapa baraka. Onyesha maneno ya kuliwaza na faraja kwa watu wanaosumbuliwa au wenye mateso.
4. Jiwe la msingi la mpango wa Mungu ni Upatanisho wa Bwana Yesu Kristo. Angalau mara moja kwa wiki, hatuna budi kutafakari sawa na Rais Joseph F. Smith alivyofanya kwenye “upendo mkubwa na wa ajabu uliowekwa wazi na baba na Mwana katika kuja kwa mkombozi katika ulimwengu.”6 Kuwaalika wengine kuja kanisani na kwa kustahili kushiriki sakramenti kutawaruhusu zaidi ya watoto wa Baba wa Mbinguni kutafakari juu ya Upatanisho. Na, kama hatustahili, tunaweza kutubu. Kumbuka kwamba Mwana wa Aliye juu kabisa aliteremka chini ya wote na kujichukulia makosa yetu, dhambi, uhalifu, magonjwa, maumivu, mateso, na ukiwa. Maandiko yanafundisha kwa Kristo “aliyepaa juu, vilevile pia alishuka chini ya vitu vyote, kwa hiyo alielewa vitu vyote.”7
Haijalishi ni matatizo ngani ya binafsi tuliyonayo—kama ni magonjwa au upweke wa muda mrefu au kuteseka na vishawishi na majaribu ya adui—Mchungaji Mwema yupo hapa. Anatuita kwa majina yetu na anasema, “Njooni kwangu, nyote mliolemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.”8
Nataka kujumuisha hizo pointi nne:
Kwanza—nenda maili ya pili.
Pili—tafadhali tabasamu. Tabasamu yako itawasaidia wengine.
Tatu—onyesha huruma
Nne—waalike wengine waje kanisani
Ninatoa ushuhuda wangu wa Mwokozi. Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, na Yeye yu hai. Ninajua kwamba anaidhinisha, kwa uwezo wake mkuu, na nguvu, mpango wa Baba. Ninajua kwamba Rais Thomas S. Monson ni nabii anayeishi. Anashikilia funguo zote kwa mafanikio kutimiza kazi ya Mungu hapa duniani. Ninajua kwamba tunaweza kusaidiana kama watoto wa Baba yetu wa Mbinguni katika majaribu na vishawishi vyetu. Katika jina la Yesu Kristo, amina.